Wednesday, February 24, 2010

NI KWANINI UNATOA HARUFU MBAYA MDOMONI? UNAIJUA SABABU?




Inapofikia kuzungumzia usafi/urembo wa mtu mmoja mmoja wengi wanasahau kinywa kama ni sahemu muhimu sana. Inatakiwa kujali sana kinywa wakati wote ili kisiweze kutoa hewa mbaya. Imetokea mara nyingi sana, mtu anatoa hewa mbaya akiongea au ukimsogelea. Utasikia watu wanaambiza "Mh yule kaka mdomo wake unanuka au yule dada mdomo wake unanuka". Sasa hii ni aibu kwa mtu ambae unaonekana msafi nadhifu nywere mpaka viatu.


Sasa basi sio kwamba hupigi mswaki vyema ingawa wakati mwingine ni kweli watu wanarashia rashia tu kusafisha kinywa, hawa si wengi. Ila kama unasafisha kinywa vyema asubuhi na jioni na bado kinywa kinatoa harufu (KINATEMA) basi fanya jambo hili mara kwa mara ukiwa kwenye kazi zako. Kunywa maji mara kwa mara. Tafadhari sana usinywe maji kama vile unakiu! aaah sio hivyo. Chukua chupa yako ya maji ama glasi weka mezani kwako ili uwe unakunywa funda moja kila baada ya muda fulani. Ukifanya hivyo itakusaidia sana kusafisha kinywa na kuzuia kinywa kutoa hewa chafu. Wengine wanapendelea sana kutafuna vitu kama ChewGum ni sawa lakini hii inakusababishia tabia ya kutafunatafuna wakati wote. na hewa chafu haitolewi kwa kutafuna BIG G kama wanavyofanya wengi, urembo kuanzia kinywani jamani, ndio inanoga, ukiongea mtu anaskia raha kukusikiliza, na hatamani umalize









kuna mtaalamu wa afya mmoja, niliwahi kumdadisi dadizi akashauri watu kutumia zaid maji ya kunywa kwa wingi, sio kwa ajili ya mdomo tu, lakini maji yana kazi nyinig mwilini, mwingine kwake maji ni kama kituo cha polisi,  maji yanaondoa chunusi usoni, na kazi nyingine nyingi sana, maji yanazuia kuumwa kichwa mara kwa mara. yanakutia nguvu, ndio maana hata ukiharisha ukienda hospitali, wanakutundikia maji kwanza. Nafikiri kunawataalam zaidi watatusaidia kwenye tatizo hili la kutoa harufu mbaya kinywani. Na pia watatupa mawazo namna ya kuondoa harufu mbaya zaidi ya hizo mbili nilizosema hapo juu. au hata wewe kama unajua dawa ya kutoa harufu, unaruhusiwa kutushaur zaidi



7 comments:

  1. ni kweli dada violet, hapa ofisini kwetu kuna jirani yangu tumepakana meza, jamani ananuka mdomo vibaya sana, halafu mwenyewe sijui hajijui, anapenda kuongea ongea, basi akiongea ile harufu, utasema tundu la cchoo, ila mkorofi sana, naogopa hta kumwambia kama ananuka,
    ila rear dada violet, yani ananuka sana mdomo wake ss nimempa hii blog yako asome, makusudi, mm huwa sinuki mdomo, napiga mswaki sana asubuhi, nasugua ulimi sana, ila ni mvivu kunywa maji, inabidi nianze,
    asante

    ReplyDelete
  2. naomba ushauri dada violet, nimetuma muda mrefu sana, au hujaipaata? nisadieni jamani, maana sijui cha kufanya, nilijuwa itapostiwa leo, naona umepost kitu kingine
    dada, mdogo wako nina shida na mawazo sana, sina raha
    nisaidie jamani

    ReplyDelete
  3. UMEANZA KUDOROLA VIOLET,
    MBONA KIMYA?
    ULIANZA VIZURI...
    SASA HIVI UNACHEMSHA

    ReplyDelete
  4. lete mambo mengine bwana, mbona kimya sister V?
    napenda kusoma mambo ya mapenzi, maana inatufundisha sana sisi ambao hatuko kwenye ndoa, inatujenga, sasa kila nikiingia nakuta yaleyale
    inabore bwana

    ReplyDelete
  5. Ney a.k.a Mamie BrendaMarch 1, 2010 at 12:19 AM

    ok my sis tunashukuru kwa blog yako maana in myself najifunza vitu vingi sana kutokana na matatizo ya wenzangu inakuwa pia challenge kwangu ila dada Vai mbona unachukua muda mrefu sana kuweka mkasa mpya ili tuuotolee maoni kama wa huyu dada tokea ijumaa uko hapo ilihali najua unamikasa mingi tu watu wanakodolea macho kila siku wanakuta uja update pls najua una soma ila usitukwaze wanablog wenzako. Have a nice day!!!

    ReplyDelete
  6. Nimejaribu ushauri wenu wote lakini hakuna nafuu,nimeenda hospital kwa mtaalamu wa kinywa kasema sina tatizo,meno nasugua hadi yana nyufa,sasa nifanyeje?

    ReplyDelete
  7. sugua sana ulimi, pitisha mswaki wako hadi karibia na koo. kinachonuka sio meno bali ni ulimi.

    ReplyDelete