Friday, November 25, 2011

NIPUNGUZAJE UZITO NILIONAO????Hope uko sawa wewe pamoja na familia yako, naomba ushauri mimi ni mama mwenye mtoto mmoja  baada ya uzazi nimeongezeka sana  naomba unishauri nitumie njia gani ili niweze kupungua kwani hata mazoezi nimefanya lakini sipungui naomba kama kuna dawa za kupunguza uzito uniambie na wadau wengine wanipe ushauri nifanyaje ili niweze kupungua sipendi kupoteza mwonekano wangu wa zamani

(Mwenzangu, hebu tushaurini, naana sio huyo tu! hata mimi nimo, toka nijifunguwe tumbo limegoma kupungua, the days goes on utafikiri nakaribia kujifungua, tupeni mbinu za kutoa matumbo, kupunguza uzito, ili turejee maumbile yetu mazuri ya zamani, )


 

MSITUME COMMENT ZA MATUSI KWENYE BLOGU YANGU


Tafadhari, naomba msitume comment za matusi kwenye Blog yangu, kama unamshauri mtu, basi tumia lugha nzuri, kata ukali wa maneno,

Kuna wengine the way mnavyocomment, ni kama mnabifu na aliyoomba ushauri, sasa kwa wale ambao mlituma comment za matusi, basi hamtaziona, nitazidelete faster na hata kwenye dustbin yangu nitazitoa kabisa,

Blog yangu ni ya watu wastaarabu, wenye comment za kujenga lakini sio kutoa lugha chafu, kama mtu una hamu ya kutukana fungua blogu yako halafu waambie watukanaji wenzio  msaidiane kutukana humo, lakini sio hapa.

Ushauri huu sio kwa ajili ya aliyehitaji tu! Bali wengi sana wanafaidika hata kwa kusoma comment zilizopostiwa, nikiwemo mwenyewe, sasa wewe unaetukana, nakuona bado mshamba tu! Na huna kazi ya kufanya coz mtu aliye busy hana muda wa kucomment matusi,

USAMEHEWE BURE!

Monday, November 21, 2011

MUME WANGU AMEZAA NJE YA NDOA, AMEOMBA MSAMAHA NISIONDOKE NIENDELEE KUWA NAE, NIFANYAJE


Habari dada Violet, naomba unipe ushauri, mimi ni mama wa mtoto mmoja mwenye miaka 5 sasa hivi, nilibadilisha dini toka kwenye ukristo na niliolewa kwa ndoa ya kiislamu, ndani ya maisha ya ndoa, kuna mikwaruzano mikubwa sana baina yangu mimi na mume wangu ikiwemo kupigwa sana,  kudharirishwa mbele za watu, maana wakat mwingine huwa ananipiga mbele za watu, yani mikwaruzano tu!  Na nikitaka kuondoka huniomba msamaha, kwakuwa naona nitashindwa kulea mtoto peke yangu
Juzi kati hapa nimepata taarifa kuwa amezaa nje, nilipomuuliza alikataaa, lakini baada ya kutishia nakwenda kufanya fujo kwa Yule mwanamke ndio akakiri kuwa ni kweli,  nimeamua kuondoka, lakini yeye anasema nimsamehe ilikuwa bahat mbaya, nishaurini nifanyaje jamani, mbona sijielewi mwenzenu , sasa hivi hayupo amesafiri, ila nataka akirudi akute nimeshafikia maamuzi, 
 

Thursday, November 17, 2011

ELIMU HAINA MWISHO - MAMA YANGU AMEGRADUATE

Hakika hakuna kama mama Duniani, mama ni kila kitu kwa mtoto, maisha bora, yenye heshima, furaha, na msimamo yanajengwa na mama zaidi,  na hata mtoto anapokuwa na tabia mbaya,  wa kwanza kulaumiwa ni mama.


Namshukuru Mungu sana sana, kwa kunipa mama Mzuri, mama mwenye hekima, mama alienilea katika maadili ya kumuheshimu na kumuogopa Mungu, mama alinifundisha mengi wakati natoka nyumbani kwenda kuanza familia yangu mwenyewe kwa mume wangu, mama ambaye ni zaidi ya rafiki na mshauri wa kweli katika maisha yangu hadi leo

Huyu ni dada yangu pekee aliyebakia, baada ya yeye kuachia ziwa, ndio nikaingia kunyonya mwenyewe,  anaitwa Joyce.


And this is my lovely Dad, Rev. Gerald Mhinga, wote kwa pamoja wametupa malezi mazuri, nawaombea maisha mema na marefu, ili hata watoto wetu waje kuwatunza watakapokuwa wazee

Amepata Bachelor ya Bible Theology mjini Dododoma, it was fun kwakweli tunamshukuru Mungu sana kwa hilo,wamesoma wanafunzi 17 lakini mwanamke alikuwa peke yake, (nimejifunza kitu kwa hilo)

Walikwenda kutembelea bungeni, wanafunzi, nae akaona sio mbaya akipata picha moja ya kumbukumbu, maana sie wengine pamoja nakukulia Dom, lakini bunge tunaliona kwa nje tu! Ndani tukatafute nini ah!
Kiufupi, mama ni kila kitu kwangu