Tuesday, February 2, 2010

INAKUWAJE MWANAMKE UNAKUWA NA KUCHA CHAFU?????

Jamani urembo sio usoni tu au mavazi kama ambavyo wengi wanafikiria,
tujajisahau sana kuangalia kucha zetu, unakuta mtu amependeza kweli, lakini muangalie kucha zake, unaweza kuona hata kinyaa kula nae chochote
Inapendeza sana kama mwanamke ukiwa na kucha safi, kwanza kucha chafu zinaficha uchafu mwingi
Kucha safi sio lazima upake rangi, waweza kata tu zikawa fupi zikapendeza au ukapaka corouless, 
Mh! hii iko kwa watu wengi sana, mtu unakuta anakata kucha na meno, vikucha vikitoka pale vinakuwa vifupiiiii? vinapoteza mvuto kabisa, yani tukucha tunakuwa na sura mbaya sana.

kama unakuwa unaona uvivu unaweza mwambia hata mpenzi wako akukate, kulikoni kuwa na kucha chafu, mwingine unakuta kucha chafuuu, halafu anapiga bonge ya sandols miguuni, inakuwa hainogi jamani
wa kurahisisha ukataji wa kucha kama huyu mrembo hapa wapo kibao, mm huwa nikiwakuta nawatoa mkono mdomoni, mwenyewe unakuta ametulia kabisa,
unaweza kuwa na kucha ndefu tu! lakini ukijua jinsi ya kuzitunza wala hazina shida, lakini utakuta mtu amefuga kucha, halafu full kujikuna, akitoka hapo mikucha myeusiii, na wala haoni noma, anakuwa MPANAAA, yani haoini hata aibu, mimi nikiona mtu anakucha chafu tu huwa naona hata kinyaa kushea nae chakula chochote kile, na hii si kwangu tu hata kwa familia yangu, Mr. kucha zikiwa ndefu tu! zinakatwa, waototo wangu ni kila baada ya wiki, hadi wao huwa wanakumbusha, mama leo tukate kucha,  tena kwa watoto ndio tunajisahau kabisa yani,
Vifaa vya kukatia kucha viko kibao, tena wala havina bei, simple tu! unaweza kuwa na Tsh 5000/= tu ukapata seti nzima yenye vikorokoro kibao, weekend uko home, basi unajisafisha wewe mwenyewe,
Nail Cut kama hii ikiwa peke yake ni Tshs 1500/= tu! unaitumia hadi unachoka, na kucha zinapendeza kabisa, kariakoo vimejaa kibao,
Machine nyingine ni Mkasi mdogo na ni special kwa ajili ya kucha tu! sio uchukuwe mkasi wa nguo ukatie kucha, utatoa vidole, mkasi mdogo kama huu bei yake ni 1000/= hadi 1500/= kucha zinakuwa zinapendeza ,
sasa hivi kuvaa sanviatu vya wazi (simple tu) ni fassion, basi bora uwe na kucha safi ndio uvae, huduma zote hizi waweza jifanyia wewe mwenyewe gharama yako ni kununua vifaa tu! ukiona uvivu, basi toa pesa upeleke kwa wataalam wa kucha wakusafishe, wewe upumzike tu!, wale wa huku kwetu Gongolamboto (GOMS) ukiona uvivu njoo pale DOUBLE 'T' HAIR DRESING SALON, huduma hii inapatikana
hebu jiangalie hapo ulipo, kucha zako, ni safi??? wewe unalo jibu.
mimi najaribu tu kuwakumbusha jamani, kucha zikiwa safi zina raha yake,

4 comments:

 1. umejuaje?
  wanawake tunatia haya jamani, yani unakuta limdada lina kucha chafuuuu, halafu unamtembelea kwake, unakuta anatengeneza juice, mikucha imetangulia myeusiii, hapo utakuwa unakunywa juice au miuchafu yake? mm nina shoga yuko hivyo, nimemsema hadi alibadilika, ni tabia mbaya, kucha zinaficha mengi hata ukienda msalani uchafu hubaki kwenye kucha, na huku kusalimiana kiTZ hadi tushikane mikono, we! tunapeana uchafu kila siku,
  kwani kiwembe kina garimu shilingi ngapi? na ukinunua unatumia kwa siku ngapi? tuache kina dada, inatia aibu, lo! kwani lazima ufuge kucha kama huwezi kuzihudumia? au unakuta mwingine kama unavyosema violet, anakata kucha na mdomo, wewe unaefanya hivyo unajua unakula uchafu kiasi gani? ndio maana magonjwa ya tumbo huwa hayatuishi, kazi ya uchafu
  JOYS

  ReplyDelete
 2. WABONGO TUMEZIDI KUJISAHAU JAMANI,
  TUJIWEKE SAFI,

  ReplyDelete
 3. NI KWELI KABISA, INASHAURIWA KILA MWANAMKE AJIANGALIE MARA MBILI MBILI NI AIBU SANA KUWA NA KUCHA CHAFU UKIZINGATIA MWANAMKE SIKU ZOTE NI MTU WA KAZI ZA NYUMBANI HATA KAMA UNAFANYA KAZI BADO UKIRUDI UNATAKIWA KUSHUGHULIKA PIA NA MAMBO YA NYUMBANI KAMA MAPISHI NK SASA UKIWA NA KUCHA CHAFU ITAKUWAJE KWA WENGINE WANAOTAKIWA KULA CHAKULA CHAKO???????? TUWA WASAFI JAMANI....

  ReplyDelete
 4. Kweli jamani kuna baadhi ya watu hupenda urembo lakini kujihudumia km ipasavyo hawawezi,mi naona bora uwe na kucha zako fupi tu km vp c unaweka za bandia tena zmejaa kibao,co kukaa na makucha alafu unashindwa hata kufanya usafi vizuri,kufua tabu,kujichamba tabu,unakuwa km unafunza vidoleni,haipendezi jamani bora kucha za bandia ukirudi zako hom wazichomoa tu!ASIA ALAWI

  ReplyDelete