Monday, May 31, 2010

BABA ANAMWANAMKE MWINGINE . ANAMTESA SANA MAMA YANGU, MIMI NI MTOTO TU! NIFANYE NINI?

Dada Violet, na wadau wote wa blog yako, nawaomba mmwombee baba yangu, maana amekuwa na tabia za ajabu sana kwa mama, zamani hakuwa hivyo ila tumefanya uchunguzi ni kwanini amebadilika gafla hivi, tumegundua ana mahusiano na mwanamke mwingine wa nje
Siku hizi haachi pesa ya chakula nyumbani yaani, matatizo kila kukicha, ugomvi kila siku ugomvi hauishi na siku nyingine hudiriki kuwafungia nje mama pamoja na wadogo zangu,
mama amejaribu kulipeleke kwa mkwe wake pamoja na mawifi zake ili wamsaidie lakini wanaonekana wako upande wa kaka yao (baba) sababu shangazi zangu hawampendi kabisa mama yangu, amekosa pa kukimbilia, amekosa msaada kabisa,
namshukuru Mungu nimesoma na ninafanya kazi ndio huwa kidogo namsapoti mama in short jamani naomba mumweke baba yangu kwenye maombi jamani ili abadilike sababu magonjwa ni mengi sana siku hizi najua wadau mnaosoma humu kila mtu ana imani ya lakini Mungu tunaemwabudu ni mmoja jamani nawaombeni.pili jamani kwenye ukoo wetu kuna kama kalaana ka ktoolewa sababu ndugu zangu wengi hawajaoa wala kuolewa

jamani sipendi niishie kama ndugu zangu napenda niolewe na niwe na familia yangu kama watu wengine,mimi ni msichana wa miaka 26 na nina degee kwa sasa ni mzuri sababu watu hawaishi kunisifia kila nipitapo lakini sijajua who is who jamani nimetulia sana mpaka mwenyewe kwa hilo huwa najisifu na najijua sababu mpaka sasa nimewai kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja then tukashindwa kuelewana,then nipo alone kwa sasa sijasubutu kuwa na uhusiano tena jamani naomba mniombee niweze pata mme wa maisha natamani kuolewa na kuwa na watoto,asanteni sana na imani mtaniombea.


Saturday, May 29, 2010

KINA BABA MSIOKAA NA FAMILIA ZENU- HEBU JARIBUNI WEEK END HII TUONE MTAPUNGUKIWA NINI

(wapenzi wangu, nitajitahidi kila weekend tuwe tunaongelea mambo ya kifamilia hasa kwa upande wa malezi kwa watoto wetu, pia nitoe nafasi hii kwa yeyote yule mwenye kitu chochote cha kumfanya mtoto ajisikie vizuri, basi anitumie kwenye email yangu pale juu, ili aweze kushare nasi, tunajisahau sana juu ya suala zima la watoto wetu.)

Jamani kuna kitu kinasumbuwa familia nyingi sana, nakutana na watu wengi hasa wanawake nikiwa salon na sehemu zingine, wanalalamika sana kuhusu waume zao kutokutulia nyumbani siku za weekend, unakuta mtu yuko busy kuanzia jumatatu hadi jumapili, kazi na yeye, yeye nakazi, sasa sijui ndio kazi kweli au ndio kazzzzzziiiiiiiiiiiii


inapendeza kuona familia zikiwa na furaha kwa pamoja, sio kila siku, but hata weekend moja moja jamani
chukuwa mkeo, watoto wenu, nendeni sehemu ambazo mtabadirisha mazingira ya nyumbani kidogo, japo kwa masaa machache, hebu jaribuni weekend hii muone watoto watakavyofurahia,

si lazima beach tu jamani, nendeni hata sehemu yenye hewa nzuri, ukiwa na familia yako, na mkeo inanoga jamani, mtakaa mtacheza na watoto kidogo, mtawauliza maswali ya michezo michezo, yani inapendeza sana,
lakini unakuta mwanaume mwingine, unapita hata mwezi hajuwi kama mtoto shule anaenda, anaandika, anashida gani, hajui lolote, akitoka kumi na mbili akirudi saa tatu saanne, wakati mtoto amesha lala, sijui wanafikir sifa

watoto ni wepesi sana kuridhika, chukuwa kipesa chako kidogo, wapeleke hata super market tu! wakajichagulie wanachotaka, mkimaliza mnakaa mahali mnapata chakula au hata kinywaji, then warudishe nyumbani, kweli siku hiyo mtoto ataenjoy sana, sio mtoto ametoka sana, kaendashule, akirudi kucheza cheza nyumbani, wala hainogi, na hii huzidisha sana mapenzi kwa watoto wetu, sio unakuwa busy kiasi kwamba siku ukishinda nyumbani tu! watoto wanakushangaa na kumuuliza mama, ''baba anaumwa''
hebu jaribuni jamani, muone watoto watakavyojiskia vizuri,
Friday, May 28, 2010

POLENI KWA KUWACHUNIA JAMANI, NILIKUWA NAUGULIWA
Jumapili hii nilikuwa hospitali, Twins wangu walikuwa wanaumwa,  walikutwa na malaria, 
but, many thanks to God, coz wamepona na wako shwari kabisa, kazi ya kuzaa wala sio kubwa
kiviiiiiileeee, issue iko kwenye kulea we! usipime,

tena hawa wawili ndio bonge la issue, maana kila nitakachofanya kwa huyu, basi na huyu nae lazima nimfanyie, nilijaribu siku moja kwa makusudi tu!  nikamnunulia Tymon nguo Trace nikamchunia, we! mbona nilijuta kuthubutu!

mtoto alinililia hadi nilijiskia vibaya, tena alivyo mpanaaa  mtoto huyu, akagoma kukaa na sisi ndani akatoka akaenda kukaa nje kwenye kona ya nyumba peke yake, nikamfata nambembeleza aingie ndani akagoma,

anasema ''mama wewe si haunipendi na mimi sikupendi' nikamwambia nakupenda sana mwanangu, ''wewe ndio dada mkubwa, akanibana tena ''mbona mimi hujaniletea nguo kama tyimo? nikamdanganya baba yako kasema anakuletea ndio maana sijanunua. ndio akakubali kuingia ndani, alipofikia tu kaanza kumchimba mkwara Tymo,'' usikae na mimi kakae na mama yako, namimi namsubiri baba yangu''.
 ila ilinibidi nimwambie baba, lete nguo ya Trace mwenzio nimeyakoroga huku.
akaletewa akawa na amani.

hata kuumwa, mara nyingi unakuta kidada kinaumwa, baada ya muda kidogo kaka nae anaanza vilevile, but all in all uzima wao ndio furaha yangu, wakofresh kabisa sasa hivi,
 tupo pamoja dears, nawapenda sanaaaaaa

weekend njema


Friday, May 21, 2010

JE HUYU KWELI NI MUME WANGU


Wapenzi wa Blog hii nzuri.Mimi ni mwanamke wa miaka 33, nina watoto 2 wa kike na wakiume.

Ninaishi na mume /baba watoto wangu tangu mwaka 1996 january., nilipokutana nae alanieleza kuwa ananipenda sana na anataka kunioa. Mimi nilikuwa na boyfriend wangu na yeye alikuwa na girl friend wake, kwa kuwa tulipendana tukakubaliana kila mmoja wetu avunje mahusiano na mwenzie ili tuwe huru kufunga ndoa ambapo wote tulikubaliana na kuacha na hizo dates zetu na kuconcetrate na maamuzi yetu mapya.

Mwaka 1999 mwanzoni nikawa nimepata mimba ya mtoto wetu wa kwanza..Tukapanga taratibu zote za mahali na hatimaye akaja kwetu akatoa mahali kwa sherehe kubwa sana. Baada ya Mahali tulipanga siku ya harusi. lakini baada ya hapo, wakaleta kwetu barua ya kusogeza mbele harusi kidogo mpaka nitakapojifungua.. nilijuwa Mume wangu alikuwa na nia sana lakini nikagundua hilo lilikuwa ni shinikizo la baba yake mzazi, na kwamba yeye hakuachana na huyo girl friend wake, na ambaye na yeye alikuwa mjamzito kwa kipindi hicho ambacho mimi pia nilikuwa mjamzito

kwamaana hiyo huyu mume alikuwa anakula huku na huku..Basi mume huyu aliendelea kunihudumia kwa hali na mali na kusema kuwa nisijali ananipenda sana na ndio maana kanitolea mahali.(wakati huo wote sikuwa najua kama anaendelea na huyu girlfriend wake)

Tuliendelea hivyo mpaka tukaanza kuishi wote na kujenga pamoja. .kumbe na huku kwa girlfriend wake nako alikuwa anajenga. Mpaka hapa ninaongea na wewe bwana huyu anaishi kwa mitara. leo kalala kwangu kesho kwa huyo mama na anawatoto nae WANNE. Kitendo hichi kimekuwa kero sana kwangu kiasi naona kama siishi kwa amani. na magomvi yasiyoisha..Huyu bwana ananiregard mimi kama mke mdogo kwake cos nina 33 na yeye 43 huyo mama ana miaka 42years. Kwa hiyo mimi ndio nachukuliwa kama mke mdogo

Hayo ni machache sana nisiwachoshe.Wapendwa kwa busara zenu kama za mfalme Suleiman naomba mnishauri kama huyu ni mume wangu au ni wa mwenzangu? je nina haki nae gani??au nifanye nini?? Huwa nasikia wanakwenda kwenye baadhi ya sherehe pamoja, inaniuma sana sina furaha hata kidogo, kwani alivunja makubaliano yetu na kunidanganya, ila kwakuwa nilimpenda niliamini kuwa nae atavunja mahusiano ya nje kama nilivyofanya mimi.


NISHAURINI NILIYEVUNJIKA MOYO 


Wednesday, May 19, 2010

KILA NIKIFANYA NAE MAPENZI- NAPATA MAUMIVU MAKALI SANA


Dada violet, pole na kazi, nahitji msaada wako kama utaweza kunisaidia nitakushukuru sana, pia kama inawezekana weka kwenye blog yako (ila usinitaje jina) ili niweze kupata ushauri zaidi,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22, niko Zanzibar, tangu niwe mwali hadi leo nimekutana na wanaume wawili, mmoja aliniacha, kwa sababu ambazo hata sizielewi Mpaka leo hii na alinitamkia kabisa sina sababu ila tu sikutaki tena, iliniuma sana nilitamani hata kujiua, ukizingatia niliweka nadhiri kuwa atakaenibikiri ndie atakaenioa, lakini akawa ameshapotosha ndoto zangu,

Baada ya muda nikiwa chuo, nilipata boyfriend mwingine, ambae niko nae hadi sasa, cha ajabu kila ninapokutana nae, tukimaliza tu! Huwa naumwa sana hadi nameza dawa, yani akishaniambia kesho tutafanya mimi nitalala nawaza usiku kucha, Napata maumivu makali sana huku chini na maeneo ya kwenye kinena panauma sana, huwa naumia hata saa zima na jasho linanitoka kabisa

Huyu boyfriend wangu hadi anaogopa kunigusa, sasa nawasiwasi asije akashawishika kuwa na mwanamke mwingine, nampenda sana, na hata kwetu wameshamjua bado kuja rasmi tu!,

Aliwahi kunichukuwa kunipeleka hospitali moja huku huku Zanzibar, dada violet nilipimwa kila kitu, lakini hakukuwa na tatizo, hata daktari alishangaa, yani alichukuwa vipimo vyote, lakini hakukuwa na tatizo, siku ingine tena tulisafiri nae kwenda Kigoma, tulipofika tulilala pamoja hotelini, alivyonifanya tu! Sikulala hadi kunakucha, kiuno kinauma hadi miguu, asubuhi alinipeleka hospitali kule kule kigoma, napo wakaniambia kuwa sina shida

Tukakaa kama wiki mbili baada ya kutoka hsptl tukafanya tena, maumivu pale pale, nikaenda hospitali ingine tena kwa mara ya tatu, napo wakasema kuwa mimi sina tatizo lolote, wakampima hata na boyfriend wangu wakasema pia hana tatizo,

Hadi sasa sijielewi, maana nakosa kitendo cha muhumu kuliko vyote, naumia sana na hasa wasi wasi wangu ni kwamba huyu boyfriend wangu atanikimbia, Napata taabu sana naombeni mnisaidie nifanye nini? nawaza labda tatizo linaweza kuwa kwangu ndio maana hata mwanaume wa kwanza alinikimbia bila sababuMonday, May 17, 2010

MCHUMBA ALINIACHA MWENYEWE- SASA ANATAKA TURUDIANE TENA, NIFANYAJE


Napenda sana ushauri wa watu na naamini utanisaidia sana, mara nyingi huwa napita ktk blog yako japo huwa sichangii, lakini sasa kuna tatizo lililonikuta, na sina ufumbuzi, nahitaji msaada wa mawazo sana

Nilikuwa na girlfriend wangu tuliekuwa tukifanya kazi pamoja na tulikubaliana kuoana, badae nilimtafutia kazi yenye maslah mazuri zaidi kwa nafasi yake ofisi nyingine, basi akaacha pale na kwenda kule kwa nilipomuunganishia. Alieniunganisha katika ofisi hiyo ni rafiki yangu mimi anaefanya kazi pale

Nilimtambulisha mchumba wangu kwake, akamfahamu, na hata wakati tunapeleka mahali kwao, nae alitusindikiza, kinachonitatiza ni kwamba, huyu mchumba wangu amebadilika gafla sana, yani mapenzi yamekwisha kabisa, kitu kidogo tu anakasirika sana, inakuwa ugomvi mkubwa, wakati hakuwa hivyo hapo zamani, kuna mfanya kazi mwenzao mmoja pale aliwahi kunitumia sms na kusema kuwa mchumba wako sio mwaminifu anachukuliwa na rafiki yako. Nilipomuuliza alikasirika sana na kukimbilia kunijibu kuwa kama nasikiliza watu basi tuachane, kwakuwa nilimpenda sana, niliamua kuwa mpole tu

Sasa niezi kama mitatu hivi iliyopita nilikuwa nimelala usiku sana akanitumia sms kwamba anaenda kuwaambia kwao wanirudishie mahali, yeye hataki kuolewa tena, nilishangaa sana, usiku ule ule nilimpigia sim kutaka kujua sababu, akawa hapokei, sikulala hadi kunakucha, asubuhi nilimtafuta kwenye simu tena ili aniembie tatizo, safari hii alipokea ila akasema hataki hata kuonana na mimi, nilibembeleza sana lakini alikataa na badae kuanza kukata simu. basi nilifikisha kwa wazazi/washenga, wazee wangu walinishauri kuwa hata hiyo mahali niiache iwe kama nimeitoa sadaka,

Nikamtumia sms nikamwambia sawa, lakini juwa umenitesa sana, nami nikaamua kufata yangu, violet kila nilipokuwa nikikaa nilikuwa nikikumbuka mazuri mengi niliyomfanyia, muda niliopoteza kwake, bado kanilipa ubaya, da!

Niliamua kuanza maisha mapya, sasa juma pili kanipigia simu anataka aonane na mimi, mimi sikutaka kumlipa ubaya, nilikubali, tukakutana pale Santina restaurant, anachokiomba kwangu, anataka turudiane nae. Anasema toka ameniacha hana raha, ni mtu wa majonzi, mikosi na hana furaha hata kidogo, sasa hadi sasa sielewi cha kumjibu, ila mimi kwake mapenzi yamepungua sana.Saturday, May 15, 2010

WEEK END NJEMA JAMANI


jamani nawatakieni wooooote weekend njema wapenzi wangu, tukumbukane katika maombi jamani, maana hali ya sasa inatisha, tukumbuke familia zetu, waume zetu, watoto wetu, marafiki, na majirani pia,
 mie leo nina Mtoko mwenzenu,
tunaenda hukoooooo kumfundisha mwali jinsi ya kuishi na mume, asiende kutuabisha huko!!!!
hahahahahaaaaaahaaaaaaaaaahaaaaaaaaaaaaa, kazi  kwel kwel,
nawapenda wooooote


Thursday, May 13, 2010

AMESEMA HANIOI HADI NIZAE, NA WALA SISHIKI MIMBA, NAWEZA KUWA TASA??


Hello Dada Violet,

Pole na kazi za nchi hii pamoja na kutusaidia sisi.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 na ninaishi na mchumba wangu. Tumeishi kwa miaka miwili sasa, sijabahatika kupata mimba. Ila dada Violet nina tatizo moja ambalo linaninyima raha kabisa. Huwa sizioni siku zangu naweza kukaa mwaka mzima nisizione.je inawezekana kuwa mimi ni tasa?? Na mchumba niliyenaye yupo tayari kunioa lakini ndio anataka nipate mimba kwanza je kuna uwezekanano wa mimi kupata mimba kweli??

Nipo njia panda sitaki kuteseka baadae nikiingia kwenye ndoa.
Hali hii inaniumuza sana, naombeni ushauri wenu


Tuesday, May 11, 2010

NINAISHI KWA KAKA YANGU, ILA SINA FURAHA HATA KIDOGO SABABU YA WIFI


Dada violet habari za kazi?Nashukuru sana kwa blog yako maana tunapata ushauri wa
kutujenga sisi wanajamii.
Mimi ni Mischana mwenye umri wa miaka 26 nipo Tabora.Mkasa wangu ni kwamba naishi na kaka yangu pamoja na wifi yangu.Kaka yangu ana uwezo mzuri tu na amejenga nyumba kubwa na nzuri.

Sasa dada violet pale kwa kaka tunaishi na mdogo wake wifi yangu wa kike na tunalingana kiumri. Kwa sababu sis ni wasichana tunakaa chumba kimoja ila cha ajabu Yule huyu mdogo wake wifi yangu nafanyiwa vitimbi vya ajabu ajabu sana ambavyo sijui vinatokea wapi, ananichukia kupita kiasi.

Yani hataki kabisa kuniona pale, wakati yeye ni kwa dada yake na mimi ni kwa kaka yangu, hanipendi hata kidogo. Akiona nimevaa vizuri ananiangalia vibaya ila mimi sijui hili wala lile.na ameanza kutengeneza chuki kwa wote tunaoishi nao pale ndani mradi wanichukie tu, hata msichana wa kazi amemwambia asiniheshimu asiongee na mimi na kunisema mengi sana kwa msichana huyo ambayo yananichafua mimi.

Nikiwa nyumbani huwa siku nzima ananuna na haongei na mimi anaweka nyimbo za taarabu tu, mafumbo mafumbo mengi sana. Na tunaweza kuwa chumbani hakuna anaeongea na mwenzake.

Jamani nimechoka niliwahi kumwambia kaka nataka kutoka nikapange akasema bado sina uwezo wa kujitegemea na ananipenda sana. Kugombanisha ndoa ya watu sitaki na nawaza nikiondoka kwa nguvu kaka hatanisaidia tena ataona nimemdharau.

Dada zangu/Ndugu zangu naombeni ushauri wa wenu wapenzi wangu.Dada Violet naomba usinibanie ili nipate mawazo kutoka kwa wadau wenzangu. Hii blog nilipewa na rafiki yangu na namshukuru sana maana inanifundisha mengi. Dada nina huzuni moyoni hadi basi sina raha hata kidogo. 

Monday, May 10, 2010

WAKWE WALIMTAFUTIA MKE MUME WANGU, KISA SIZAI, SASA NIMEZAA BADO HAWANITAKI, NIFANYAJE?

yamenikuta mwenzenu
nakupongeza dada violet kwa blog yako ambayo inatufanya tupate mawazo tofauti tofauti ya kutusadia wenye shida, nakuombea Kheri ndugu yangu.
Niliolewa miaka 8 iliyopita huku Njombe, nilipoolewa nilikaa miaka mitano bila kukamata mimba, nilihangaiika sana, nilienda kwa waganga wa kienyeji, nikatumia mitishamba lakini haikusaidia, ndugu wa mume wangu walianza kunichukia sana na hata mume wangu pia,
miaka mitatu iliopita, mume wangu aliniomba msamaha kwa kusema kuwa amezaa na rafiki yangu, rafiki ambae alikuwa akinificha sana kila nimuulizapo mimba ya nani, hakuwa akiniambia ansema mwenye mimba yuko nje, alipoenda kujifungua kwao singida aliporudi hakufikia pale, nikasikia amefikia kwa wakwe zangu,
nilishangaa sana, hao wakwe mimi wamenipiga marufuku hata kwao nisikanyage

wifi yangu mmoja akaja kuniambia yule rafiki yangu amepangishiwa chumba mahali, nililia kupita kiasi, lakini nilijipa moyo, huyu kaka tulichukuana tu hatukufunga ndoa, mume wangu alianza chuki na maneno ya kashfa kwangu, nilivumilia tu!,
mwaka jana nilipata ujauzito, namshukur mungu nilijifungua salama, na mtoto alikuwa amefanana sana na baba yake, badala ya kufurahi, nilishangaa mume wangu hakuwa na mapenzi na huyu mtoto hata kidogo,
ss mwaka huu mwanzoni nikaambiwa kuwa wameachana na yule mwanamke, na mtoto kaamua kumpeleka kwao, baada kama ya wiki, nikaletewa mtoto nyumbani, mimi nilikubali nikawa namlea
ss nimeletewa taarifa kuwa wamerudiana na yule msichana, mapenzi moto moto na wanataka kufunga ndoa,
yani kila nikiwaza hata sipati jibu mwenzenu, sielewi pa kuanzia wala pa kuishia,
huyo mtoto hadi sasa niko nae hapa nyumbani kwangu, na habari hizi ni zaukweli kabisa, maana niliambiwa na mshenga, kwamba nijiandae kama nina pa kwenda niende, maana huyo rafiki yangu (mke mwenza) atakuja kuishi hapa hapa na mimi
inaniuma sana

Wednesday, May 5, 2010

MUME WANGU ANANITEGEMEA KWA KILA KITU- LAKINI HAJATULIA HATA KIDOGO- NIMWACHE?

Du! jamani kuna wanawake wenzetu wanashida sana jamani, hebu soma hii, maana mimi imenisisimua sana, na imeniumiza pia, ametuma ndefu sana, nimejaribu kuedit kiasi, but soma kisha mshauri, yani nawaza kama ndio ningekuwa mimi sijui ingekuwaje, yani sipati majibu maana kichwani yanakuja mfururizo kama majibu kumi hivi but yote yana madhara at the end, inasikitisha sana
Nimeolewa, miaka mitatu iliyopita, lakini nilimkuta mume wangu anawatoto watatu, binti wa miaka 16, na  wa miaka 10 na miaka 6, mimi sikuwa na mtoto hata mmoja, mama wa watoto hawa alifariki.

Tumefunga ndoa ya kanisani, sikubahatika kuzaa mapema, ila kwa sasa ndio nina ujauzito wa miezi saba, Nilimpenda sana mume wangu,Mimi nafanya kazi nzuri tu, ila mume wangu hana kazi yeyote ile, maana alifukuzwa, hivyo nafanya dili zake tu za pembeni zinazofanya aishi hapa mjini, aliponioa alihamia kwangu, maana yeye alikuwa amepanga, mimi nimejenga, hivyo tulikubaliana aje kwangu na nilikubali aje yeye na familia yake,
 nilimtafutia biashara, mradi tu! Asiwe anakaakaa nyumbani , akafungua duka la nguo za kiume huko mjini, na bila hata uoga alimuweka girlfriend wake awe ndie msimamizi na muuzaji, yeye ndie controller wa kila kitu pale. nilipogundua niliifunga ile biashara. Toka siku ile niliapa kutomsadia lolote lile.

Ni Malaya kupita kiasi, nilishawahi kumfumania na wanawake zaidi ya watatu, kuna mwingine alimpangishia na chumba akawa anaishi nae kutwa nzima, na hivi hana kazi akawa anatoka asubuhi anaenda kushinda huko, jioni anarudi kulala kwangu, nilipogundua nililia sana violet mdogo wangu niliumia sijapata kuumia vile katika maisha yangu, nilimpokonya gari nililokuwa nimempa, nikawa simpatii hata pesa. sikuona maana ya kumjali mtu asieniheshimu, lakin kama mjuavyo mapenzi tena, nikaamua kumrudishia gari ili watu wasihis kitu kwa kuona limepaki nayeye anatembea kwa miguu.

Nashukuru Mungu watoto hawa wananiheshimu na kunipenda sana, watu wengi wanajua kuwa nimewazaa mimi mwenyewe, nami nawapenda sana, Nilimfumania kabla sijabeba hata mimba, sasa mwezi uliopita nimepigiwa simu na mwanamke mmoja akanitukana sana, isitoshe amenitishia kabisa maisha yangu, anasema ataniroga nitazaa mbuzi, na maneno mengine makali sana, yani hadi huwa najuta,

Violet, hapa nilipo mimi ndio kila kitu, najua ni ngumu sana kuamini kuwa mimi ndie ninaesomesha hadi watoto wake, nawalipia ada na kuna mmoja huyu wa kati, nimempeleka boarding namlipia mimi, huyu mkumbwa nae yuko private (secondary) nalipa mimi. huyu mdogo mimi pia nimempeleka Tusiime ( international) namllipia mimi, moyo wangu unaniuma sana, kwanini anitese hivyo? Inamaana hanithamini mimi wala wema wngu kwa wanawe?

Wale watoto ni damu yake yeye, watamsaidia yeye sio mimi? Niliahidi kuwasaidia kwa moyo wangu, maana nilipoolewa mimi nilikuta watoto wana hali ngumu sana, waliona kama wamepata mkombozi wao, Sasa yeye nikimuuliza kwanini ameshindwa kufanya hata kwa siri tu umalaya wake, mimi nisijuwe, kwanini ananidharirisha, mimi nampa heshima zote, nampa matumizi yake binafsi, namlelea watoto wake, gari namtilia mafuta, lakini anakwenda kuwapakia wanawake wengine, wanapanda kwenye gari yangu,

hana cha maana anachonijibu ninapomuuliza, yeye anasema hawajui, mimi nakataa maana nilishawahi kukuta hata sms za mapenzi, anawatambua maana kuna mambo yangu mengi ya ndani tunayopanga mimi na yeye tu chubmani, cha ajabu huyo mschana  anayafahamu, hilo ndilo linalonipa hofu, wasije wakayatumia hayo kuniumizia kiumbe changu, sasa naomba mnishauri, nifanye nini? Nimfukuze?

Moyo wangu umechoka sana jamani, moyo unaniuma sana, kwanini iwe hivi? Hali hii hata kujifungua bado, nimeanza kutishiwa eti nitazaa mnyama(mbuzi) sina hata nilichowakosea,

Ananitia aibu kwa majirani, maana mtaa mzima wameshamjuwa kuwa yeye ni malaya, cha ajabu anachukuwa visichana vya ajabu ajabu, havina kazi wala pesa, vinamtegemea yeye kwa kila kitu. vikorofi, midomo imejaa matusi, na hata elimu havina, aibu hii mimi hadi lini? inaniuma, nimekuwa nikilia kila siku!

 Tuesday, May 4, 2010

NATAMANI KUOLEWA ILA SIJAWAHI KUMPATA HATA WA KUTAMKA TU!

(mnisamehe jamani, wiki iliyopita nilikuwa busy kupita kiasi, nikawa naona masaa yanayoyoma tu hata blog sijaigusa, lakini nshamaliza nilichokuwa nakifanya, im back wapenzi)

msaada wa mawazo yenu ni muhimu sana kwangu,
mimi ni mschana, sijaolewa bado, na nina umri wa miaka 32, nina kazi nzuri tu ambayo inaniwezesha mimi kuishi vizuri, ila nina shida moja, ambayo sijui kama dada violet na wengine mnaweza kunisaidia au hata kuniambia ni kwanini inanitokea hivi,
  
  mimi ni mzuri, nikijitazama, na pia sina ulemavu wowote,  nafanya kazi nzuri, na naishi nyumbani kwangu,
wazazi wangu wako Nairobi, ndiko nilikokulia, ila kazi nafanya hapa Dar es salaam,

katika maisha yangu sijawahi kupata mwanaume wa kuniambia anataka kunioa hata siku moja, hata nikimpata tu! tunakuwa marafiki kwa muda, then wanakimbia, ukimpigia simu anakata, sometimes hata kupokea hapokei, hadi nachoka na hatimae kuachana, naweza ingia gharama ya kumuhudumia mwanaume nitakae kuwa nae, kwa kila kitu, lakini nikishajiweka karibu yake, na kumuuliza lini tutafunga ndoa,  huwa  ni kama nimemwonyesha bomu,

niliwahi kwenda kanisa moja hivi, nikaombewa maana walisema ni laana ambayo inabidi ivunjwe, niliombewa sana, lakini since there, no any changes, nimechoka kuhudhuria na kuchangia harusi za wenzangu, wakati mimi nazeeka tu!, staki kuzaa nje ya ndoa, na staki kuishi na mwanaume nje ya ndoa,

natamani na mimi niitwe Mrs. fulani, huwa nakaa nalia sana peke yangu, najiona kama mwenye mkosi fulani.unakuta mwanaume natokea kumpenda sana, nitaonyesha njia zote za kumtamani kimapenzi, lakini tutaishia out tu!na hakuna kitakachofatia hapo. sasa sielewi, kama ndio nimeumbiwa kupata shida hii, unakuta natamani kumwambia mtu kuwa nampenda, ila nakuwa nashindwa kwa kuhofia jamii itanichukuliaje, lakini hali hii inanitesa sana, kwa msichana wa umri wangu, ninaeelekea kwenye umama, bila kuwa na mtoto wala mume