Thursday, February 18, 2010

NAMTAMANI MUME WA MAREHEMU RAFIKI YANGU KIPENZI

Violet pole na kukutwika mizigo mikubwa,

Mimi ni mama wa miaka 42, sijawahi kuolewa, ila nilibahatika kuzaa mototo mmoja wa kiume, nilizaa nikiwa mdogo maana mwanangu sasa hivi anamiaka 25, yuko Swaziland anasoma,
Nina maisha mazuri tu!, nina nyumba zangu nne, tatu nimepangisha na moja ninaishi mwenyewe, nina daladala nne, nina mifugo ya kutosha, nina kila kitu, lakini sijabahatika kupata mwanaume na kunitamkia kunioa, toka usichana wangu hadi sasa, sina ulemavu wowote wa kiungo, ila nafikiri sikuwa nimeandikiwa kuolewa labda,

Nimelia sana, pesa ninazo nina kila kitu lakini nimekosa kitu cha muhimu sana katika maisha yangu, na sitaki kufa kabla sijakipata, Unavyoonekana violet ni binti mdogo bado, lakini kwakuwa toka nimefatilia mambo ya humu ktk blog yako, na ushauri unaotolewa na watu, naamini UKUBWA WA PUA SI WINGI WA KAMASI, nahitaji ushauri toka kwako na wengine pia,

Nilikuwa na rafiki yangu mpenzi, nilimpenda sana, yeye aliolewa na mume wake tulikuwa tukiheshimiana sna, na walikuwa family friend wangu, mtoto wake mkubwa wa kiume, ni rafiki wa mwanangu sana, na wanasoma wote switsland, bahati mbaya mwaka juzi rafiki yangu alifariki ghafla tu!, alilala kichwa kinauma, akanywa dawa ya maumivu ili assubuhi awahi hsptl, ikawa bahati mbaya hakuamka tena,


Akawa amepoteza maisha, nililia sana, wakati huo hata shemeji yangu sikuwa nimeanza kumtamani, siku zinavyozidi kwenda, najikuta nampenda sana Yule baba, nae ni mtu mzima, nikimtumia sms za kumsalimia, anarespond vizuri, muda mwingine simu yangu inakuwa na salio la kutosha tu, lakini namjaribu kumuomba aniwekee salio kidogo, anaweka muda huo huo na na ananipigia kuniuliza kama nimeipata, yani akipiga siku mimi huwa akili zote zinahama, natamani asikate hata simu,

Kuna siku nilijifanya gari zangu zote mbovu ili anipe gari lake, akaniletea hadi kwangu, nikachukuwa nikalijaza mafuta full tank, sikwenda kokote, jioni nililirudisha, badae usiku akanitumia sms asante kwakuniwekea mafuta, usiku mwema, nilitamani kulia, inamaana hajui kama nampenda, na yote ile ni kutaka anizowee?

Yani ni mtu mwenye heshima zake, nikimualika aje mahali dinner, anakuja anakula namsindikiza anaondoka, ss sielewi je, hajajuwa bado kama namtamani? Inafikia kipindi hata nikilala namuota kabisa, yani hii imenitokea kama mara nne hivi, naota niko nae, naota nampikia anakula, naota nimelala nae , naweza chukuwa simu kumpigia ikiita tu! Nakata maana nakuwa sina hata la kusema, umri wake yeye mkewe aliwahi kuniambia ni miaka 50 ambapo hadi sasa ana miaka 53, anafanya kazi kwenye wizara moja hapa Dar es salaam, anacheo kizuri tu.

Violet naombeni mnishauri, kuna siku nilikuwa nikiongea na mwanangu, tumezoeana nae sana, nay eye ndio kila kitu kwangu, maana sina mtoto mwingine, niliwahi kumuuliza je nikipata mume niolewe utajisikiaje? Mtoto alichukia sana na kuniambia mama, futa hayo mawazo, sitakusuport kwa kitu chochote, umri huo unataka nini mama? Kwani umekosa nini wewe hadi uolewe sasa hivi

Mimi sitaki uolewe mama, sitaki, nilimshangaa sana, lakini yeye ni mtoto, hajui mateso ninayopata mimi, nimeamini kwama kuolewa ni bahati ya mtu, unaweza kuwa mzuri wa kila kitu na usiolewe,

Sasa huyu baba mimi nimempenda, ila najiuliza, je nikimwambia akikubali, jamii itanielewaje? Maana watu wote walikuwa wanajua mimi ni rafiki wa mkewe, mwanangu atanielewaje? Maana wototo wetu pia ni marafiki wa kufa na kuzikana, lakini pia nikikaa kimya moyo unauma sana, naogopa asije kupata mawazo ya kuoa mtu mwingine

{Najua kuna baadhi ya watu watanishangaa, lakini ukweli ni kwamba, nimempenda sana huyu baba}.

15 comments:

 1. usijali mama naomba nitafute mimi ntajaribu kukusaidia mawazo yako lakini kama uko serious nikutumie email yangu nitakwambia ufanye nini kama uko tayari nijibu ili nikutumie email yangu

  ReplyDelete
 2. WE MAMA
  HUJUI KAMA KUFA KUFAANA, ALIEKUFA KESHA KUFA, KAMA UMEMPENDA OLEWA NAE, HUYO MTOTO WAKO NAE AFUNGE KALOMO, ATULIE HUKO ASOME, MAPENZI YAKO YEYE YANAMUHUSU NINI, ULISHAMZAA INATOSHA]
  AKA! OLEWA MWAYA

  ReplyDelete
 3. wewe mama,
  umri huo unataka mume wanini jamani? mbona mie naona aibu? tena mbaya zaidi mume wa rafiki yako, japo ni marehemu jamani, loh!
  mimi wala sikushari uolewe, ushauri wangu ni huu
  hama mko unaoishi, hamia mkoa mwingine, ili umfute kabisa akilini mwako, ushajizeekea mama yangu, ukiolewa uanze tena kuzaa na umri huo ya kazi gani, mama tulia tu,
  usiolewe kabisa,

  ReplyDelete
 4. mi namtetea mama!sidhani kama anamaamisha akiolewa ndo azae, sidhan, ila anaona ni faraja akiishi na mzee mwenzie wachangie mawazo na afurahie maisha ya hapa duniani, mi sion kama kuna tatizo huyo mama akianza mahusiano na huyo baba. miaka 3 ishapaita tangia rafiki yake afariki ingekuwa miez hapo kweli, mwenzangu mama jiachie kwa raha zako, kwanini ufe na msongo wa mawazo wakti tatizo linatatulika? ila kupima muhimu,muite mzee mwenzio mweleze hisia zako nafikiri mtaelewana kama na yeye hana mwanamke. jali hisia zako mama, ukiogopa walimwengu hutafanya lolote, walimwengu tupo na kazi yetu ni kusema tu. wala usijali. take care

  ReplyDelete
 5. mimi kwa upande wangu nakushauri uolewe tu na huyo baba kama umempenda, unaweza ukamwambia ukweli ila kama unaona aibu jaribu kumsogeza karibu zaidi mwisho atajua nini haja ya moyo wako, kama rafiki yako kufa alishakufa na hata biblia inasema mjane anaruhusiwa kuowa tena mjane mwenzake lakini kwa kuwa wewe sio mjane ila tu ukuwahi kuolwa basi ni ruksa mbele za mungu pia.Ili mradi mfunge ndoa tu kanisani inaruhusiwa kufungia hata ofisini kwa mchungaji siyo lazima iwe na cherekoc hereko, ila kwa ushauri msizae tena watoto muwe mnaponda raha tu mana umri wenu umeshaenda. Ni bora ukafanya hivyo kuliko tamaa za mwili ziwe zinawaka mara kwa mara inaweza kukusababishia matatizo kiakili. Mimi nakutakia kila la kheri na mafanikio......

  ReplyDelete
 6. Dada yangu kwa Mungu yote yanawezekena, kama kweli unahitaji msaada mpe Violet namba yako ya simu anipe mimi then tutawasiliana.

  ReplyDelete
 7. WALA HUJAZEEKA UMRI WA KUWA MZEE NI FROM 60s WEWE KULA GOOD TIME NA HUYO BABA, NENDENI KWA KIONGOZI WA DINI HALALISHENI, UKIWEZE VAA HATA SHELA, HILO NI LAKO DADA, UKILALIA MASIKIO, UTAKUTA MWANA SI WAKO.

  ReplyDelete
 8. My mum pole kwa mtihani mimi ningekushauri umwambie tuu my dad uwe wazi kwake, kwani wewe sio mwanamke malaya wala nini unataka heshima usikie atakuambiaje? huo kijana wako achana naye hajui kama mapenzi yalianza toka adamu na ever, Wala usikiri eti hukuandikiwa ndoa, mwamini mungu tuu ukiona mambo yamekubali iteni watoto wenu wote wawili wakwako na wakwake muambie adhima yenu nyinyi ni watu na heshima zenu.Ni jambo la kawaida mama mimi nimeshaona ndoa za dizaini hiyo mara nyingi tuu mf ni mtu wa familia yangu mke kafa shemeji kaowa rafiki yake mke wake. walimwengu kusema ni lazima lakini watasema mchana usiku watalala.We mweleze na uwe wazi tuu.
  mpendwa

  ReplyDelete
 9. OMBA MUNGU UTAOLEWA,
  SIKUSHAURI UOLEWE NA MUME WA MTU, OMBA UPATE WA KWAKO, HUYO MUME WA RAFIKI YAKO WALA USITHUBUTU, KWANZA JAMII HAITAKUELEWA, WALA WATOTO WALA FAMILIA ZENU, KWANI WANAUME HAKUNA HADI UMTAMANI WA ALIYEKUWA RAFIKI YAKO?
  MMM. HAPANA KWELI

  ReplyDelete
 10. VIOLET,
  MBONA WEWE HAUCHANGII? TUNATAKA TUONE NA USHAURI WAKO, NAONA STORY NYINGI UNATUPATIA TU! ILA WEWE HAUKOMENT, KWANINI?

  ReplyDelete
 11. utaolewaje na mume wa rafiki yako, si utaambiwa umemuua wewe na hivi kafa ghafla. sio kwamba umepitiliza sana umti kuolewa, lakini ungepata mwingine huko it would be poa. mimi nadhani angekua na interest na wewe katika miaka hiyo mitatu angeshakutamkia, ukianza wewe italeta aibu ukizingatia na umri wako. mambo ya kutongoza wanaume wanafanya watoto wadogo wa kike, sio mtu wa umri wako. utajidhalilisha, kwani mwanamke hutafutwa, hatafuti. wewe tulia, kama imepangwa utaolewa tu hata ufikishe miaka 60.

  ReplyDelete
 12. Umri ulokuwa nao wala hujazeeka nawe ni binaadamu unapenda unatamani mi nakuombea mungu kwamba huyo baba aelewe naye awe anakupenda wenyewe mmalize maisha yenu kwa raha eeeh kwani mapenzi yana umri kwa raha zako anti huna uzee wowote usiniudh ukisema eti we mzee nani kasema!

  ReplyDelete
 13. Hallo
  Mbona umri wako ni mdogo sana miaka 42 ni michache sana hata hivyo wazungu wanasema life starts at forty. We huoni hata Ulaya wanamitindo wengi wanaolewa wakiwa na kuanzia 35 mpaka 40 na kitu.
  Pia mi naona ungeanza kwa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na huyo baba kwanza ambapo itakuwa ni mwanzo mzuri wa ndoa swala la namna ya kuanza ni rahisi tu maana inaonekana katika maisha yako ulikuwa mwenye aibu sana hadi kuanzisha mahusiano kwako inakuwa ngumu ukishindwa omba hata msaada kwa wazoefu.
  Kingine ni kwamba mimi ninaweza kukuagizia cosmetics za time reversing ambazo ni natural zinatoka Sweden na zina quality ya hali ya juu pia ni asilia hivyo hazina matatizo yoyote kama zilivyokuwa hizi cosmetics za chemicals zinazounguza.
  Zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kuondoa mikunjo na dalili zote za uzee usoni ambapo miaka 45 inaweza kuonekana kama 25 na kuna watu wameshazitumia hapa hapa Tanzania na wameweza kupata mabadiliko kabisa yaani bila kukuonyesha cheti cha kuzaliwa huwezi kuamini kama umri anaokwambia ni wake kabisa.
  Yoyote unaweza kunicontact kwa 0717452790.
  Nakutakia kila la heri na mafanikio mema katika mahsiano yako.

  ReplyDelete
 14. Jamani mimi sioni huo uzee wa huyo mama watu bwana miaka 42 mbona bado sister tu hivi nyie siku hizi miaka 42 mnaijua mtu akikuambia ana miaka hiyo unaweza ukakataa mpaka asubuhi. wanaonekana ni wadogo sana. Huyo mama bado anahitaji sana mume kwa umri wake acheni kumkatisha tamaa si bora yeye kasema na hao masugar mummy wanaobaka watoto wa kiume au vijana wetu siku hizi tusemeje, mama mimi nakuunga mkono olewa tena na huyohuyo mume wa rafiki yako maana wewe ndio unaemfahamu kuliko mwingine, sioni tatizo maadamu huyo mama kafariki hamna shida olewa. huyo mtoto ni utoto unamsumbua hajui how much you are suffering. HAMNA KITU KIBAYA KAMA UPWEKE, Tena mimi nimekupenda sana mama kwa kuwa muwazi yaani unahitaji mume ili uendelee kutulia maana nina imani umetulia tena kama ni mapenzi ya Mungu ninakuombea kabisa maana ni haki yako kuwa na mwenzio.

  ReplyDelete
 15. Mmmh Mummy mbona wewe bado kabisa? Dada yangu kaolewa na miaka 45 sembuse ww!Ningeweza kupata mawasiliani ningekupa steps za kukusaidia na amini ndani ya mwezi mmja angeekutamkia mwenyewe mfunge ndoa. Na huyo mwanao ningemfanyia counselling ya kutosha na angekuwa wa kwanza kukuchagulia shela. Keep praying utafanikiwa,ila naomba mawasiliano!

  ReplyDelete