Monday, February 1, 2010

MUME WANGU AMEOA KWA SIRI NA SHAHIDI YAKE SIKU YA HARUSI NI BINTI YANGU NILIYEMZAA MWENYEWE

Kwakweli akili yangu haitaki kuamini kilichotokea, lakini hata isipoamini, ukweli utabakia pale pale,
Mimi ni mama wa familia yenye watoto wanne, wakwanza ana mika 23 wapili miaka 18 watatu miaka 16 na wa mwisho anamiaka 7, kinachoniumiza sana na kuninyima raha na kunifanya nijishushe thamani, ni kitendo cha mume wangu kuoa katoto kadogo sawa na mwanae, tena kaoa kwa siri, na siku ya ndoa yao alienda na binti yangu wa miaka 18, Binti alishiriki katika harusi ya baba yake na hakumwambia mtu yeyote, alinificha hata mimi mama yake niliyemzaa kwa uchungu, alikaa kimya kabisa hadi nimekuja kugundua ndoa hiyo ina miezi minne sasa, nililia nakuumia sana baada ya kuona picha ambazo Binti yangu nae amepiga na huyo Bibi harusi siku ya harusi,
kabla ya ndoa hiyo mume wangu alikuwa ni mtu wa kero, mtu mwenye gubu, kitu kidogo tu kwake kinakuwa kikubwa sana, ila mara kwa mara alikuwa akinitishia kuoa mke wa pili, ukiangalia sisi tulichelewa sana kuzaa watoto wote hao tumewazaa tukiwa watu wazima kabisa, tumepitia maisha magumu sana, lakini baada ya kupata pesa ya kustaafu tu! ndipo alipoenda kuoa, tena huyo bibi harusi kwenye picha anaonekana ni mtoto kabisa, kinacho niuma ni kwanini amshirikishe mwanangu kwa siri? mtoto amechange sana, siku nilipoona zile picha kwenye laptop ya baba yake nililia sana, nilimuita binti yangu ambae yuko for four, nikamuuliza kwanini alifanya vile na baba yake na kuamua kunificha? ukizingatia ni mtoto wa kike?, nampenda sana mwanangu, lakini wakati namuuliza  mtoto alikaa kimya, kila ninapomsemesha juu ya suala hilo hajibu chochote, zaidi ya kusema mama muulize baba mwenyewe, mtoto pia amebadilika sana,
pia nahisi ushirikina kwa sehemu fulani, maana kuna siku binti yangu yule wakwanza alipiga kelele usiku na kuja kugonga chumbani kwangu, nilimuuliza kuna nini? akasema kuwa amemuona mdogo wake(yule alienificha) kuwa anataka kumchoma kisu, niliingia hadi chumani kwao, nikakuta anacheka kitandani, nilimuuliza ana nini? na kwanini anafanya hivyo akajibu kwa dharau mama usimsikilize huyo, kalale anaota tu! sasa kisu kiko wapi? toka siku hiyo binti mkubwa amehama chumbani analala na huyu mdogo wake wamwisho. yani kuna vitu vya ajabu ajabu ambavyo sivielewi kabisa.
siku nyingine tena nilikuta khanga yangu ina damu na pia imeandikwa kiarabu, ikiwa sandukuni, sikuivaa tena niliichukuwa na kuichoma moto, mume wangu sasa hivi ananiomba msamaha, wakati aliamua kuoa bila kuniambia, sasa hivi ndio anatubia na anaomba nimruhusu awe analala kwangu siku nne kule kwa mke mdogo alale siku tatu! nilimwambia akitaka hata ahamie huko sawa tu!
wengi wamenishauri, hata majirani zangu wengine wameniomba niondoke nisijekuuliwa bure, nikiangalia na utu uzima huu mimi naenda wapi? sina raha, nishaurini , najua nawapa wakati mgumu sana, lakini ndio limeshanitokea,

11 comments:

 1. Pole sana mamii, huo msalaba ni mzito. Kama unakipato unaweza kumudu maisha yako mwenyewe, please ondoka haraka, kama maisha ya ndoa umeshaishi sana sidhani kama unahamu nayo kiasi hicho. Usiogope kurogwa tu, je ukimwi! utaulimbiaje, hao vitoto wanaopenda wazee wengi si salama manake wanaruka huku na kule kutafuta hela, hakuna mapenzi. Chukua wanao anza mbele. Mwache ahangaike akichoka atarudi, ila mpime kwanza. Jaman wanawake tuna kazi sana.

  ReplyDelete
 2. kama nguvu za giza zimeanza kuhusishwa hapo, basi ujuwe uko hatarini sana, mimi nakushauri wewe mtegemee Mungu tu! usiamini huo ushirikina, Hata ningekuwa mimi, yani mwanangu wa nimembeba tumboni miezi tisa aje anisaliti hata mimi? anifiche kama baba yake ameoa? inauma sana, inauma, lakini usikute nae amehusishwa kwenye ushirikina ili asikuthamini wewe
  mh! hizi ndoa hizi??? tuolewe tu! lakini, hamna cha vijana wala wazee, wote ni walewale, yani ni kama laana vile
  MUNGU TUHURUMIE WAJA WAKO

  ReplyDelete
 3. SWALA LA HUYO BABA KUOA MIMI WALA SISHANGAI, UNADHANI WANAUME WANA UBINADAMU? MIMI MUME WANGU AMEOA KWA SIRI KAMA WAKO, YAKAMSHINDA AKARUDI MDOGO KAMA PIRITONI,
  KINACHONISHANGAZA NI HUYO MWANAO, NAE YAMEMSIBU YEPI? MTOTO WA KIKE NA MAMA YAKE, YEYE VIPI AFICHE MADHAMBI YA BABA???
  UTUUZIMA KITU GANI, ONDOKA UKAISHI PEKE YAKO, HAPA WATAKUTUPIA HATA MAJINI MAMA YANGU
  POLE

  ReplyDelete
 4. MAMA pole sana maji yameshamwagika hayazoleki kitu kimeshatokea kukimbia tatizo sio kulisolve cha msingi ongea na mume wako vizuri...km ameamua kujirudi mwnyewe basi amejua kosa lake ukiwa km mtu mzima maliza hilo swala kiutu wanaume hawana utu lkn hyo baba kwanza amekuheshimu sana kuoa kwa siri coz wengne na sherehe wanfanyiaga hapo hapo nyumbn huyo mtoto wako wa kike ametengenezwa wala usimpe laana mama mana akikua ataona kwa sababu wanawake sisi wote kilio chatu ni kimoja siku zote...rudisha moyo mama as long as huyo baba amemua kupanga siku mshukuru maana wengne wanahamaga kimya..sema ndo kajipime mama kaah kumuacha hy baba ni sawasaw na kumpa faida hyo mtoto alieolewa sasa pigana vita kiutu uzima huo uchawi wke wla usiuogope wala kuukimbia km unatumia mungu m2mie sana na km unatka kuutumia nguvu za giza YANI NENDA KAFANYE WALA SIO KOSA COZ UNAJILINDA NAFSI YAKO USIJE KUFA HUMLOGI M2 UNAJILINDA...MAMA NAKUSHAURI MI CJAOLEWA BADO ILA KISIKUSHINDE HCHO KISHAWISHI FIGHT FOR WHAT IS UAZ..Y UMFAIDISHE HUYO MTOMTO WA JUZI KWA KUMUACHIA MUME JUMLA MAMA KM ULIKULA KIAPO KWA SHIDA NA RAHA....BASI SHIDA NDO HIZO SIMAMA KIDETE IWE KWA UPANDA AU SIME USIMWACHE HUYO BABA KISA....MMMH MHHH NAKATAA HUYO MTOTO WAKO WA KIKE MPE SOMO ATALIELEWA NA ATARUDI UPANDE WAKO SIUMEMZAA MWENYEWE BWANA HATAKI SISI WALIMWENGU TUTAMFUNZA...MAMA KAZA UZI MAPAMBANO NDO YAMEANZA..CHAGUA MOJA MUNGU AU KWA WENZETU HUYOOO MKE WA PILI ANAPOENDA...AAH IMEZIDI HOA WAKE WA PILI WATATUTESA MPAKA LINI....JAMANI MAMA NARUDIA RUDISHA MOYO NYUMA THEN PAMBANA KM ULIVYOWAZAA HOA WATOTO WANNE....

  ReplyDelete
 5. pole na matatizo mama, nakushauri tulia anza kufanya maombi kwa uaminifu ukimwambia Mungu shida yako Mungu wetu ni mwaminifu. kwanini nasema hivi ndoa ya wanawake wawili tegemea mengi mama.Mimi nimeshuhudia vurugu nimetoka katika familia hiyo.
  Nasikia uchungu sana najua uko katika wakati mgumu sana sikushauri kuondoka sababu bado mnapendana.

  ReplyDelete
 6. Mama Pole,

  Mi nakushauri kwa imani ya Mkristo yeyote ziko ahadi za Mungu nyingi, kama uliteleza kwenye nafasi yako kama mke bado muda upo, ngangana, tumia Jina la Yesu, Tumia Damu ya Yesu kuikomboa Ndoa yako.

  Mama nafasi yako ipo bado, pindua aliyekalia kiti chako kama Yesu alivyopindua meza kule Hekaluni, Mungu amekupa mamlaka ya kungoa na kuharibu na kuangamiza, huyo aliye chukua nafasi mngo`e mama usikubadili. Dai ndoa yako sasa kwa Mungu, shetani amenyanyuka lakini mtangazie umejitambua, waone wamama wanaomfaahamu Mungu wakufundishe jinsi ya Kukomboa ndoa mama inaniuma sana.

  simama kwenye sehemu yako. Mungu anatambua mke wa ujanani.
  hayo tu mama. MAMA HAKUNA KUONDOKA SOMA EZEKIEL 20:45-48

  ANZA VITA MAMA WASHA MOTO MPAKA KIELEWEKE,

  ReplyDelete
 7. pole kwa yaliyokupata, lakini tumesikia upande mmoja tu, sijui upande wa pili una yapi ya kusema, hivyo tungesikia na upande wa pili tungejua ni yupi wa kumpa pole, maana kuna uwezekano ukawa umechangia mumeo kufikiria kutafita mke mwingine.

  ReplyDelete
 8. pole mama wanawake tunateseka sana ila mtetezi wetu yu hai, yawezekana mtoto wako huyo amefundishwa mambo ya kichawi ila itia damu ya yesu itafanya na iko siku ndoa yako itatengamaa WEWE SIMAMA TU.

  ReplyDelete
 9. Pole sana mama, Mungu Mkubwa sana Hebu mwambie Mungu shida zako zote nae atafanya muujiza wake.
  USIACHE KUMCHA MUNGU ATATENDA MUUJIZA KWAKO!!! POLE SANA.

  ReplyDelete
 10. POLE SANA MPENDWA, MM NAKUSHAURI KWAMBA KAPIME, KAMA U SALAMA BASI USIKIMBIE KWA SABABU HAPO NI KWAKO ILA NDO UNYUMBA USIMPE KWANI MWILI HAUUZWI SUPER MARKET KUSEMA UTANUNUA MWINGINE.PILI FANYA MAMBO YAKO USIMPE ATTENTION YOYOTE,KAMA UNA KAZI KAMATA OVERTIME,KAMA NI UJASIRIAMALI BUNI ZAIDI ILI UWE BUSY DIA.TATU,KAA NA WANAO WOTE MFANYE MAOMBI HALAFU MSEMEZANE KWA UWAZI KUHUSU HILO MAANA NAONA NI WAKUBWA ILI WAMUWEKE KATIKA MAOMBI.VILEVILE,UTAFUTE MARAFIKI WAZURI WA KUWA MNABADILISHANA MAWAZO NA KUFANYA NAO MAOMBI,HATA KUTOKA MARA MOJAMOJA(LADY'S OUT) KUTEMBEA,KULA NJE YA NYUMBANI PAMOJA,VIKAO VYA AKINAMAMA N.K. MAANA UKIKAA PEKE YAKO WAWEZA KUPATA MATATIZO MENGINE DIA MAANA MUME ANAUMA,ILA TAMBUA KWAMBA WEWE SIO WAKWANZA NA YANA MWISHO HAYO,KWANI HUYO BINTI UNAFIKIRI PENSION IKIISHA ATALITAKA LIZEE HILO!CHA MSINGI UWE NA MSIMAMO WAKO,"NO MUST MEAN NO"MWISHO USIKATE TAMAA KWANI MUNGU NI MUWEZA NA HAWEZI KAMWE KUKUACHA,ATAKUFUTA MACHOZI YAKO MPENDWA WANGU. POLEEE

  ReplyDelete
 11. Pole mamii,hayo ni mapito ya dunia.Ushauri wangu mimi ni kwamba, endelea kuishi hapo nyumbani kwako,muombe akupe mahitaji yako ya hapo nyumbani,mwambie asigawe hizo siku nne,siku zote saba ampe huyo bi mdogo na usishirikiane naye katika tendo la ndoa.Kwani nina uhakika kabisaa bi mdogo huyo hampendi kwa dhati bali kapenda pesa yake,hivyo atakuwa na dogodogo wenzake ambao anawapenda kwa dhati,hivyo kuweza kuleta maradhi katika familia yenu.Kujitenga kwako katika tendo la ndoa ndo salama yako.

  ReplyDelete