Sunday, October 31, 2010

MWANANGU ALIWAONA HOUSEGIRL NA MUME WANGU WAKIFANYA MAPENZI- WAO WANAKATAA KABISA, NIFANYAJE?


nisaidieni wapendwa,
nilikuwa safarini Arusha kikazi, kwa muda wa wiki mbili, nyumbani nilimuacha mdogo wangu ambae ni mwanafunzi wa form three,  mume wangu , housegirl wangu na mtoto wangu mwenye umri wa miaka minne na nusu.

 niliporudi safari nikakuta amani kama kawaida,  na wala sijaona mabadiliko yeyote kwa housegirl wangu, kesho yake mume wangu nae alisafikir kikazi, yeye ni dereva wa Bank Fulani hapa Dar es salaam, sasa baada ya kusafiri, usiku niliamua kulala na mwanangu,
nilishangaa  sana mtoto akaniambia mama basi ulipoondoka dada alikuwa analala  na baba huku chumbani kwakowananichukuwa na mimi, Violet, nilishtuka sana, nikamwambia unasemaje? 

Akasema kweli mama, baba alikuwa anavua nguo na dada anavua halafu wanalaliana, nikamuuliza mama mdogo alikuwa wapi? (nikimaanisha Yule mdogo wangu) akasema sijui mwenyew, basi nikaamka usiku huo huo nikamuamsha mdogo wangu nikamuuliza kama aliwahi kulala nje ya nyumbani wakati sipo, akasema ni kweli rafiki yake alifiwa, hivyo alitakiwa kuwa kwenye msiba kwa siku mbili,..........

 Mschana nimembana sana, amekataa kata kata yeye hajawahi kulala na mume wangu, mume wangu nae  amekana kabisa, sasa sielewi, huyu mtoto hata leo hii umuulize nilipoondoka baba alikuwa analala na nani, anasema na dada, niambieni nahisi kichwa changu kimeruka kabisa, nifanyaje? Friday, October 29, 2010

TAREHE 31 OCTOBER - CHAGUA CHADEMA - CHAGUA SLAA


Mtanzania, wakati umefika sasa wa kufanya maamuzi sahihi, maamuzi yatakayobadilisha maisha yetu, maamuzi yatakayokuwa faida tosha kwa vizazi vyetuMsiogope mabadiliko, tumpe nafasi Dr Willibroad Slaa,IT IS A TIME!


Time 4 changes!

Time 4 liberation!

Time 4 revolution!

Time 4removal of corruption! Eradication of poverty!

Time 4 all Tanzanians 2 enjoy our resources!

Time 4 CHADEMA!

Time 4 DR.SLAA!

It is you & I 2 bring changes.

VOTE 4 CHADEMA,

VOTE 4 DR.SLAA on 31 oct 2010.

 Thursday, October 28, 2010

USIMWAMINI RAFIKI KUPITA KIASI, (KIKULACHO KI NGUONI MWAKO)

Napenda niwakumbushe wadada wenzangu, jamani, hata ukiwa na rafiki yako, ukampenda vipi, usithubutu kumueleza kila kitu kuhus wewe, wengine huthubutu kueleza hadi madhaifu ya waume zao kwa marafiki zao, hi ni mbaya sana. maana kikulacho kiko nguoni mwako, huyo rafiki yako siku mkitibuana tu! anaweza bwaga mambo yako yoote, sometimes husema hata ya uongo mradi akuchafue tu! unaweza shindwa kufanya hata kazi zako kwa kufikira maneno machafu alosema rafiki yako.

Too much of anything is harmful, unaweza kuvumilia kidogo lakini kadri yanavyozidi huwezi kuvumilia tena na kujikuta mnaaibishana kama hivi, sasa yote haya ya nini? sijamaanisha ni marafiki woote, but kati ya marafiki 100, wanaoweza kukaa kunyamaza zikitokea miss understanding ni watatu tu! wengine hakuna kitu, ni aibu tupu

unaweza kusikia maneno ambayo ukiyatafakari unapoteza furaha kabisa, unatamani kulia kila ukimuona, but you cant change the situation hata ufanyaje, mbaya zaidi umpate rafiki ANEBORESHA TAARIFA LO! Utajuta kuzaliwa, maana hata usiyoyajua, anakutupia wewe,  (inakera sana hii, zamani mimi nilikuwaga najua mtu akisoma, basi hata behaviour yake inabadilika, kama alikuwa mmbea basi ataapunguza au kuacha kabisa, kama muongo, basi atadanganya kidogo, but i was wrong, hakuna cha msomi wala nini, (kuweni makini jamani,  mashosti hawafai hata kidogo,


Rafiki anaweza kupata ujasiri hata wa kuweza kuwagombanisha wewe na mumeo, kwa maneno ya uongo, kwa taarifa TATA, mradi tu mkose amani ndani ya ndoa, mbaya zaidi mumeo ayapate, lo! aibu mno, unaweza pata hasira ukatamani kutoa nywele kichwani, ukahisi miguu yote inatetemeka, meno yanajisugua kwa hasira, kila ukimuona unapata hasira kali sana, (marafiki msiwaamini sana jamani, wanatesa )

sio wote, but hata hao unaoona kwao ndio umefika, hakuna atakaewagombanisha, mh!
mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, msikubali kuwa wapumbavu, MUWE MAKINI WEPENDWA, NAWAPENDA SANAAA
Monday, October 25, 2010

MCHUMBA WANGU YUKO SOUTH AFRICA- HAJISIKII KUWASILIANA NAMIMI, NAMI NAMPENDA SANA, NIFANYAJE


habari mpendwa,

mimi ni msichana wa miaka 25, naomba mnishauri maana niko njia panda,nilikuwa na boyfriend wangu ambaye anafanya kazi south africa sasa huu ni mwaka wa tano hajarudi na kila nikimuuliza anasema anakuja kesho na kesho kama unavyojua huwa haifiki,nyumbani kwao wananijua kuna siku mama yake alimuuliza anarudi lini ili aanze kufanya maandalizi ya harusi lakini akamjibu bado baada ya hapo akanipigia simu na kuanza kunilaumu kuwa nimeenda kumwambia mama yake kuwa ye hataki kurudi, yaan nimechanganyikiwa maana zamani alikuwa ananiambia mambo yake yote lakini sasa hivi hata nikituma sms inaweza ikajibiwa baada ya wiki au isijibiwe kabisa, naombeni ushauri wenu jaman maana maji yamenifika shingoni.
Friday, October 22, 2010

TEAM BUILDING - ILIFANYIKA GIRRAFE HOTEL

Tulikuwa na Team Building ya wafanyakazi, namna ya kufanya kazi as a Team, na mambo mengine mazuuuuri sana, ikiwemo michezo na MISOSI, Lo! tulienjoy sana, nilitamani sana kung'ang'ania pale maana lo! kula ni kila baada ya masaa mawili,Hapa tukiwa ndani ya chumba cha mkutano, tulienjoy sana kiasi kwamba hata wale wa kusinzia hawakusinzia tena, it was fun kiukweli kuanzia wale ma TRAINER wetu, huduma za pale, haswa upande wa msosi we! nilitamani kung'ang'ania huko huko nisirudi, Hapo sasa, naona  raha nikiyatizama maji, but lo! kuogelea ni isue, staki hata kujaribu  kuogelea kuna wenyewe bwana, acha tu sisi tupige picha

Mandhari yenyewe ndio kama hivyooo, lo! raha jamani

Kitengo nilichokuwa nikikisuburi kuliko vitengo vyooote ni hiki, yani i wish ningekaa siku tano hivi, but tulilala siku moja tu! unakula kama hutakula tena lo!
Michezo ya maputo, tulicheza sana, tukahisi ni mchezo tu, kumbe kuna somo ndani yake, TUMEENJOY SANA
(Nawe enjoy kupitia this pictures)
I LOVE YOUUUUUUU

Saturday, October 16, 2010

ANAPENDA KUFANYA MAPENZI NA MIMI NIKIWA KWENYE PERIOD, SIKU ZA KAWAIDA HAISIMAMI, NIFANYAJE NISAIDIENI.

(Wewe unaweza kuwa na tatizo, ukaliona lakwako ni kuuubwa saaana, kumbe kuna wengine wanayo zaidi ya kwako,hebu soma hii ya huyu dada, kisha mshauri wewe unaona afanyaje maana mh! )
Hi dada Violet
Ninatatizo na naitaji msaada wenu. Hapa najiona nipo njia panda sijui pa kuelekea. Nimeolewa juzi juzi tu, ila kinacho nichanganya mume wangu tunapo jamiiana huwacha kusimamisha uume wake katikati ya tendo la ndoa, hii ndo tabia yake kila siku. Wakati mwingine hasimamishi kabisa hata wiki, na akisimamisha basi haichukuwi dakika moja inalala tena,, Hii inanikera sana na kuniumiza. Na sasa imesababisha nisijiskie tena kujamiana nae, ingawa nampenda sana na sitaki kumsaliti.

TATIZO KUU:
Tukienda kulala ananijia na kuanza kunishika shika na anasimamisha sana, ila akisema aingize tu, kitu kinagoma. Hii inanichanganya sana na naumia sana ingawa simwambii. Maana nampenda mno.
Nikimuliza, anasema yeye pia anaumia kwa hili,. Hata yeye anashangaa, maana haijawai kumgomea hivi kwa wanawake wengine wa mwanzoni. Ananiomba nimvumilie, anasema hili tatizo ni la mda mfupi, litaisha. anachosisitiza ni kuwa ananipenda na nisimkimbie

Sasa najiuliza au mie simrizishi, hajiski chochote tunapojamiana na anaogopa kusema anachopenda.
cha ajabu kila tukienda kwa wazazi wake, tukirudi tu, siku hiyo atafanya kazi tam sana kitandani, sote mimi na yeye tutajiskia raha hadi basi. Ikitoka hapo basi,,hasimamishi, hadi nikiwa ktk period ataniganda kama luba, anataka ajamiane na mimi hivo hivo kila siku, sipumui. Hata kama mie naumia anasema pole mke wangu, anapenda zaidi nikiwa ktk hali hiyo. akimaliza ananicheka na kunibusu na kunikumbatia hadi asubuhi, yaani anaonesha upendo zaidi. Na period ikimalizika yeye hanitamani tena, anageukia huko.au husubiria kipindi ambacho sijiski kufanya tendo la ndoa, ndio husimamisha usiku wote kama chizi wa mapenzi. Hajui mie nateseka moyoni ingawa sisemi. Alafu naona kama vile mie ninapo umia yeye anapata raha na kuridhika.

Natumaini kupitia blog hii ya Violet, nitashauriwa,, mie nimejingiza tu ktk ndoa sijui A wala Z. Mie na mume wangu tunaumri sawa, tumefikisha miana 30, sio watoto tena sasa.

Naombeni mnishauri jamani. ASANTENI
Monday, October 11, 2010

OFISINI LEO,

Kikazi zaidi,

Lo, unaweza kuwa busy sanaaaaa, but sometimes lazima ulifresh mind jamani oh!, 
Mh! tunapenda kupiga picha, tatizo mapozi ya picha ndio yamekaa kushoto kweli, ah! tutabanana humu humu, hadi pozi zieleweke, I LOVE YOU ALL!!!!!!!!!!!!!
Wednesday, October 6, 2010

NAMCHUKIA SANA MUME WANGU- NATAMANI HATA KUACHANA NAE, NIFANYE NINI


Habari, mimi ni mama, nina miaka 12 kwenye ndoa yangu, na nimejaaliwa kuwa na watoto watatu,
Mimi na mume wangu ndoa yetu ni ya kanisani, isipokuwa bamiaka minne iliyopita, mume wangu alianza vituko vya ajabu ajabu, akawa ananichukia hadi watoto wakajua hilo, ananipigiga, kuna kipindi alitoa hadi nguo zangu nje ili niondoke na kudai namng’ang’ania kwanini, hali hii iliniumiza sana, baada ya kuchunguza nikajua amepata mwanamke mwingine. na ameshazaa nae na mtoto wao ana umri wa miaka mitatu sasa

 Niliumia sana, maana hata huduma nyumbani zilisitishwa. tukaanza kuishi maisha ya shida sana na wanangu. nikajitahidi kuwasomesha, nashukuru mungu wanangu wanaendelea vizuri. sasa juzi juzi hapa nimepata taarifa kuwa wameachana na yule msichana waliezaa nae, tena kwa ugomvi mkubwa, cha ajabu eti ndio mume wangu anahamishia mapenzi yote kwangu. 

 lakini kwa upande wangu sasa hivi nimetokea kumchukia kupita maelezo, yani nimemshiba kabisa, sijiskii kushirikiana nae jambo lolote, namuona kama ananuka vile, najitahidi kuicontrol sana hali hii, lakini nashindwa kabisa, unakuta akija tu! Natamani hata nikajifiche mahali na staki hata anisemeshe, nimejaribu kwenda kuombewa, lakini wapi, hali ipo pale pale, sijui kwa kuwa alinitesa sana, yani sasa hivi hata kutoka nae kwenda nae kwenye sherehe siwezi, akienda yeye mimi bora nibakie, na akibakia yeye bora mimi nitoke,


tena sasa hivi hata nisikie yuko baa gani sijui anakunywa na wanawake, sishituki wala kuumia naona afadhali aendelee kunywa huko akirudi amelewa anafikia kulala, kiufupi simpi huduma yeyote ile, mimi sijisikii kufanya chochote kile, sasa naona kama vile ninaishi maisha ya mateso, nifanyaje wamama wenzangu?  na kikubwa ni kuhusu huyo mtoto, jamani inauma sana, isikieni tu kwa wenzenu, mimi yamenikuta naumia nateseka sana, hata kama wameachana mtoto si atawaunganisha tu???

Naombeni mawazo yenu.