Friday, January 29, 2010

MKE WANGU NI MCHAFU SANA, NISAIDIENI KUMSEMA

Bila shaka hujambo Violet, Mimi ninashida moja kubwa sana ambayo inaniumiza kicha na kuninyima raha, shida hii ni uchafu wa mke wangu jamani, nina mke mzuri sana, nampenda sana, tatizo ni uchafu alionao, tuna watoto wawili, na yeye anamiaka 29, si mtoto kusema kwamba ashindwe hata kuusafisha mwili wake, yani hadi sometimes naona kinyaa kula wala kulala nae,
 
anaweza asitandike chumbani hata siku tatu, kazi ni kukung'uta kitanda wakati wa kulala, nguo utakapoiacha ndipo utakapoikuta, yani hadi huwa nawaza labda na pepo, halafu cha ajabu huwa haoni hata aibu, nimesema sana, hadi tunaishia kugombana na kunijibu kama naujuwa usafi nifanye mwenyewe,

 
yani haoni aibu kabisa, huwa namtolea mifano nyumba za dada zake zilivyosafi, lakini wala hana hata mpango kabisa, nimewambia dada zake wamseme, lakini haijasaidia hata kidogo, yani mimi sielewi tatizo hasa nini nini

vyombo vinaweza kulala kwenye sink hata siku mbili na wala asishtuke, hadi huwa namuuliza pua zako zina matatizo? mbona husikii harufu ya vyakula vimeanza kuchacha, kunasiku niliamu kufanya usafi mwenyewe, nikaingia hadi jikoni, nikakuta kule stoo sufuria limefunikwa, ile nafunua, limejaa funza wengiii tena wazima,
aisee nilimtandika mabao kwa hasira, nikajuwa kuwa tumeshalishwa uchafu
niliacha kula nyumbani kwa muda wa mwezi mzima, lakini hajabadilika kabisa jamani
sikua aliyoniudhi kupita zote ni sikumoja ambayoalikuwa mwezini, imefika usiku wakati tunalala nikaona amechukuwa nepi ya mtoto kwenye beseni akavaa kama pad, sikusema chochote, asubuhi wakat naenda kazini nikamwachia pesa anunue pad, jioni wakat wa kulala akavaa matambara yake tena, nikamwambia pesa  ya pad nilikupa mke wangu, kwanini unavaa matambara? akajibu ile hela amelipia kwenye mchezo, kuna mchezo anacheza na rafiki zake, sasa violet hebu nisaidie dada yangu, kuna wanawake wa hivyo au ni huyu wangu tu???? mbona mwenzenu sina amani, sitting room utakuta nepi za mtoto hata zenye mavi zitazagaa masaa hapo, yani hadi huwa naona aibu kuja na rafiki zangu ghafla, 
kina dada, hebu nisaidieni ushauri, nampenda sana mke wangu, tatizo uchafu tu!

Thursday, January 28, 2010

NGUO IPI .....???????? IVALIWE WAPI?..................................

 
hebu leo tuongee kuhusu mavazi yetu hasa kina dada,
na hasa mavazi ya ofisini, na pia tuelimishane jamani, ni vazi gani la ofisini??? ni vazi gani la sherehe? ni vazi gani simple tu kwaajili ya nyumbani? na mavazi mengine meeeeeengi, TUTAKUWA TUKIANGALIA VAZI MOJA MOJA, NA LEO TUTAANGALIA JUU YA MAVAZI YA OFISINI TU!
Vazi gani hasa kwa wadada linafaa kuvaliwa ofisini???Tuambie uonavyo wewe
 
Unaweza kuvaa suti yeyote ile na ukapendeza,si lazima suti tu, unaweza kuvaa hata kiblauzi chako simple skirt or trouser  na ukanoga tukama hawa huyu kavaa simple na amenoga, huyu nae suti pia amenogabut naona kama vile suti zinapendwa sana ofisini,unaonaeeee, mrembo huyo nimependa sana alivyovaa, BELT linakwenda na SKIRT yake, blauzi inaignia kidogo kwenye hiyo rangi ya skirt, umeona kiatu kileeeeee, (nimekipenda sana) basi pale kwa pembeni unapiga pochi black, We  inanoga hiyo, usipime!!!!!mh! hapo sasa,!!!!!!!!!! si umeona tofauti iliyopo? si kwamba hajapendeza, kapendeza sana, lakini hii ni yakuvaa ofisini kweli?  sema na wewe, unaonaje? ofisini tuvae vipi wadada???


Wednesday, January 27, 2010

NISAIDIENI NDUGU ZANGU NAHISI KUCHANGANYIKIWA
MUME WANGU ANATAKA KUNIINGILIA KINYUME NA MAUMBILE

Habari dada violet, naamini u mzima kabisa, kwa upande wangu mimi si mzima kimwili lakini nahisi kiakili naelekea kuchanganyikiwa, tangu niolewe ni miezi sita sasa, lakini sina amani kabisa ndani ya nyumba yangu, kwakuwa mume wangu anataka kuniingilia kinyume na maumbile, hali ambayo mimi binafsi siipendi na naona ni dhambi kubwa sana. Mume wangu aliponioa hakuniambia kuwa anapenda kufanya kitendo kile, hakusema kabisa, ila nilishangaa siku ile ya ndoa usiku akaanza kuniambia uchafu huo, nilikasirika sana na nilimlilia na kumwambia kama ni ndoa na ife, mimi siwezi kufanya kitendo kile, kwa kipindi cha mwanzo alinielewa kabisa, kadri siku zinavyoenda hali inabadilika kila siku, ugomvi hauishi, matatizo kila kukicha,
Kuna siku ilikuwa usiku sana, aliniamsha kwa hasira na kusema kuwa yeye ameshindwa kulala na hakuta kucha kama sitampa anachokitaka, na kujisifia kuwa mbona wake wa marafiki zake wanawapa waume zao na hawajaharibikiwa? kwanini namimi nisimpe? msimamo wangu ulibaki pale pale,gafla alishuka kitandani na kuchukuwa mkanda wa suruali yake, akaanza kunipiga, niliumia sana, badae niliishiwa nguvu kabisa nikaanguka, alinigeuza na kuniingilia kinyume na maumbile, niliumia sana, nililia sana, na kulipokucha akaniambia taratibu tu utazowea, na kama ukikubali mimi nitakupa kila unachotaka, akaondoka
nililia sana, lakini kitendo kile niliona cha aibu sana kuwashirikisha watu, nikaona nitamdhalilisha mume wangu, niliamua kukaa kimya, ila mwili ulima sana nikatumia dawa za maumivu, aliporudi jioni akataka tena ili nizowee, nilikataa nikamwambia basi niache, nipe taraka yangu niondoke, alichokifanya akanipokonya mtaji wa biashara niliyokuwa nafanya (nina duka la nguo za kike) akachukuwa nguo zote dukani ambazo hadi leo sijui zilipo, akaniambia sikupi taraka, ukitaka uishi kwa amani nipe ninachokitaka, nililia sana, niliamua kumwacha na kuendela na msimamo wangu,
kuna siku niliumwa sana usiku tumbo, akanipeleka hospitali, waliponipima waliniambia nina uvimbe kwenye kizazi inabidi operation, basi tuliporudi nyumbani nikamwambia anipe pesa akasema utakufa, ukitaka pesa yangu nipe ninachokitaka kwanza, nilimgomea, basi tukawa tunaishi hivyo hivyo, hakuna tunachoshirikiana nae, nikipika anasusa kula, nguo anapeleka kwa dobi afue, apasi, kitandani hata shuka alibadilisha kila mtu na shuka lake, nilimsihi anipe taraka niondoke, akakataa, akasema ole wako uvujishe siri hii, nilikaa kwa mwezi tena, kurudi hospitali daktar akasema uvime unazidi kukua na maumivu yanaendelea kwa kasi, niliporudi nilimsihi sana akakataaa, niliamua kurudi kwetu, mama alifariki, nipo na baba tu, na baba hana uwezo wa kulipia operation hiyo, kesho yake mume wangu akanifata kwa baba na kutaka nirudi, hadi hapo baba hakua akijuwa lolote, nilirudi kwa mume wangu, lakini hali ikabaki pale pale, kuna siku usiku alinikandamiza kwa nguvu na kuniingilia tena, niliumia na kulia sana, kesho yake akanipa hela ya upasuaji, Mungu alinisaidia nikapona haraka, niliporudi nyumbani hali ni ile ile, ananiuliza hadi leo hujazowea tu? nikamwambia sahau huo uchafu, na kama nitarudia tena nitakuwa kichaa, basi toka siku ile hadi sasa sijui cha kufanya, nawaza nimwambie baba yangu? baba ni mgonjwa mgonjwa maana toka mama afariki mwaka juzi hali ya baba imekuwa si nzuri nahisi na umri nao, naogopa nikimstua anaweza hata kupoteza maisha, kwao amenipiga marufuku kusema. niliwahi kumuita rafiki yake kumuomba aongee na mwenzie, nilishangaa yule baba nae akanilaum mimi akasema kwanini unamkatili mwenzio hivi? mimi mwenyewe mke wangu anafanya hivyo? na tuna raha kabisa, unakosea sana, alipotoka pale akaenda kwa mume wangu kumwambia, jamani nilipigwa siku hiyo kama mwizi, na mapenzi yangu kwake yamepungua sana, talaka hataki kutoa, na hataki niondoke
Naombeni msaada wa mawazo ndugu zangu, naona ninakoelekea ni kuwa mwehu kabisa, sina furaha wala amani kwenye ndoa yangu, naamini nitashauriwa vizuri na ushauri huo nitaufanyia kazi,
asanteni sana

UNAJUA KAMA LIMAO /NDIMU NI DAWA YA KUKATA HARUFU KWENYE KWAPA?


Wakisema watamke mwanamke mrembo hawataacha kutamka usafi ndani yake, usafi na usafi unahitajika kwa mwili wote, sasa leo tuone hiki kisehemu kidogo, lakini kikiamua kutoa harufu, kinakufukuzia mpaka marafiki, (KWAPA) Wanawake wengi tumekuwa tukioga, tunapulizia perfume kwenye makwapa kwa wale wenye uwezo, ili mwakwapa yasitoe harufu, lakini utakuta pamoja na kupulizia perfum bado sehemu ya kwapa inaacha alama ya njano, teyari inapunguza urembo wako, mtu akikuona atajua kabisa wewe ni mchafu.


wengine wansema kuwa ni Ugonjwa, uende hospitali, lakini kuna rafiki yangu anaitwa BETTY ameniomba niwafahamishe dawa simpe na ni nzuri kwa kukata harufu, ni dawa ambayo hata mtu mwenye uwezo wa chini anaweza kununua, ni LIMAO AU NDIMU,
(Nanukuu)
Mambo dear, nimeona kwenye blog yako umeelezea kuwa tutakuwa tukifundishana urembo, n.k sasa leo mimi ninafahamu jinsi ya kutoa harufu ya kwapani bila kutumia perfumu,
1. unaoga unajikausha na taulo safi hasa makwapani,
2. unachukuwa Ndimu au Limao unakamulia kwenye mkono
3. unachukuwa yale majimaji ya ndimu unaanza kupaka kwenye kwapa,
kipingi cha kutumia limao /Ndimu pekeyake, huruhusiwi kutumia perfumu yeyote ile
unafanya hivyo kutwa mara mbili, asubuhi na jioni, na kwa wale wanaotoa harufu sana, basi wafanye hata mara tatu,
USISUGUE, itakuchubua, unapaka taratibu tu! wajaribu kwa muda wa siku tatu mfurulizo wataona mabadiliko na mashati hayataweka alama ya njano tena.
tupo wote, tutazidi kushaurina sana, tuzidi kuwa warembo.
kazi njema.
(Mwisho wa kunukuu)
 
hapa hatumaanishi kwamba tusitumie perfume, maana nazo zina raha yake, zinafanya unukie vizuri sana,
ila kuna wale wenzetu ambao wanatoa jasho sana, kiasi kwamba imekuwa kero hata kwao, waweza tumia malimao kukata harufu hiyo,  then ukishajiona uko okey, basi utaendelea kutumia perfumu,
many thanks to BETTY

Tuesday, January 26, 2010

TUPO PAMOJA SIJAWATUPA WAPENZI WANGU

jamani, kwenye email yangu kuna mikasa mingi hadi sielewi niuanze upi, mpenzi,  lakini nafikiri ni vizuri kutoa mkasa mmojammoja, ili tukimaliza tumemaliza, wapenzi miliotuma mikasa yenu, nawaahidi yote nitaituma, kwakuwa lengo letu ni kusaidiana, kushauriana, basi wala msijali, tutasaidiana tu, sijawatupa
Nawapenda wote na nawapa pole kwa mikasa  iliyowapata, pia niwakumbushe kuwa  matatizo hakuumbiwa mnyama, matatizo kaumbiwa binadamu, hivyo ni kama challenges tu katika maisha, msikate tamaa,

Monday, January 25, 2010

SIELEWI NINI KINAENDELEA KATI YA MCHUMBA WANGU NA RAFIKI YANGU, NAOMBENI USHAURI


 Dada Violet, kwanza nashukuru kwa kufungua blog ambayo naamini itatusaidia sana katika mambo mengi, na hata ushauri pia, mkasa huu ulionipata naomba uuweke ili nishauriwe kwani hadi sasa sijui la kufanya.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27, nafanya kazi katika Company moja ya simu, nina mchumba wangu ambae tumekuwa na uhusiano wa miaka minne sasa, nateyari ameshanivalisha pete, kwao nafahamika nae kwetu anafahamika, lakini siku za hapa karibuni nimekuwa siwaelewi yeye na rafiki yangu mimi, nina huyu rafiki yangu ambae nampenda sana, na namshirikisha mambo mengi, hadi kwa mchumba wangu nimemtambulisha na anamfahamu vizuri, miezi miwili iliyo pita mchumba wangu alikuwa na graduation, Basi kwakuwa aliniambia baada ya kutoka chuoni kutakuwa na part ya kumpongeza mahali fulani, basi nami sikusita kumfata rafiki yangu kumualika, cha ajabu nilipokuwa nikimuelezea alidakia na kunieleza kila kitu, kwamba mbona shem alishaniambia, siku nyinigi? wakat mimi ndio nimetoka kuambiwa, iliniuma lakini nilitake easy, basi ikafika siku ya tukio, nikampitia rafiki yangu kwao, sikumkuta isipokuwa nilikuta wadogo zake na nikakuta box kubwa sana la zawadi, nilipouliza wakasema amefunga zawadi ametoka kidogo, wewe tangulia tu! tukafika ukumbini, tumekaa kidogo nae rafiki yangu akaingia akiwa na box lake la zawadi, kitu nilichonote pale nikwamba rafiki yangu na mchumba wangu walikuwa wamebadilika sana, kila mtu ananijibu dry kwa chochote nitakachouliza, nikawa nimekosa amani kabisa, kabla ya party kuisha nilitangulia kwenye gari ya mchumba wangu, nikaanza kulia, sababu sikuwa nikijisikia vizuri, party ilipoisha walikuja hadi kwenye gari, mchumba wangu na rafiki yangu, akaniambia, kwanini uko huku? nikamwambia najisikia vibaya, wala hakuonyesha kujali, akaniuliza tunaenda wote nyumbani? nikamwambia ndio, akasema ngoja tukamshushe kwanza rafiki yako kwao ndio twende, nikamwambia sawa, bas hata wakati tuko kwenye gari, walikuwa wakipiga story wao, mimi wamenitenga kabisa, hata wakiongea nikichangia wanapotezea ile mada na kuleta ingine, inaniuma sana, kwani nampenda sana mchumba wangu, tulipomfikisha kwao tukarudi kwa mchumba wangu, tukaanza kufungua zawadi, nilikuwa nina hamu ya kujua ndani ya box la rafiki yangu kuna nini, nilipofungua sikutaka kuamini nilichokiona, nikakuta amemuwekea chupi za dazani moja, boxer dazani moja, kondom box zima, vest, viwembe, tauro,na mashuka, na picha yake, nikamuuliza mchumba wangu, imekuwaje? akasema unaniuliza mimi? muulize rafiki yako, nililia sana, nikampigia rafiki yangu simu, cha ajabu hakuonyesha kushtuka kabisa, ndio kwanza akaanza kucheka akasema mimi nilifikiri umekuta bastola au bomu, kumbe umekuta zawadi za kawaida tu! niache nilale bwana, akakata simu,
nilitoka usiku uleule hadi nyumbani, nilililia sana, kesho yake nikawanampigia simu mchumba wangu akawa hapokei na hata rafiki yangu pia akawa hapokei,  nikaenda nyumbani kwa wazazi wa mchumba wangu nikawaeleza wakakasirika sana, wakamuita, walimsema na pale pale baba yake akamuuliza unampango gani na binti wa watu, jibu hapahapa, yeye akasema ananipenda na bado anataka kunioa, lakini toka tutoke kwenye kikao kile, nimekuwa simuelewi kabisa, ananishushua hovyo, ananikaripia tu hata mbele za watu, hataki kutoka na mimi kama zamani,
hali hii inanipa shida sana, nashindwa hata kufanya kazi zangu kwa ufanisi, inaniuma sana yani. naomba mnisaidie dada violet na wadau wengine, nimepoteza muelekeo wa maisha kabisa,
bado nampenda sana mchumba wangu,

Sunday, January 24, 2010

MACHOZI NI SULUHISHO LA MATATIZO YA MWANAMKE????


Wanawake wengi sana tumekuwa tukilia pindi tunapopata matatizo, tumeshindwa kuvumilia yale yanayotupata, mfano hai ni mimi mwenyewe, hadi wengine huniambia nina machozi ya promotion, hii pia nimeiona kwa wanawake wengi, unalia weeeeeeee, ukinyamaza unaona kama umeshatua mzigo kwa kiasi fulani, kama ni hasira basi unaona imepungua kwa sehemu,


utakuta mtu anatafuta na private place, anajifungia kama ni chumbani peke yake, analia kwa uchungu sana, na anaweza kuchukuwa muda mrefu sana kwa kulia,


but problem inabaki pale pale


hali hii humfanya mwanamke kuwa mpweke sana kwa muda mrefu,

mwingine hataki kubembelezwa hata kidogo, yani ukimbembeleza ni kama umemwambia azidi kulia


Mwingine akitoka kulia huwa na hasira sana, atapiga watoto, usimsemeshe, anaweza kukupa jibu moja tu, ukanyanyua mikono juu. Lakini tatizo linakuwa palepale, sasa hebu tusaidiane kushauriana juu ya hili, je inawezekana mtu kuiacha hali hii??? na utaiachaje? ili ukipata tatizo usilie tena???

Thursday, January 21, 2010

Nisahihi kufunga ndoa na ujauzito kwa madai mtoto akizaliwa atakuwa ndani ya ndoa??

Hebu tuwekane sawa kwa hili jamani, siku hizi imekuwa kama fassion,
mtu kufunga ndoa huku mjamzito,

Pia tuelezane ukweli kabisa, je ni kweli kwamba mtoto huyo atakuwa ndani ya ndoa??


Wewe kama wewe, unaona ni sawa?? na kuna ukweli juu ya hili. .........
                                                             

Happy Birthday Furahaa

it was simple but goodFuraha akiwa na Dadiiiiiiiiiihapa akiwa na kaka na babaHapa napo  akitupa poziTracy nae hakuwa nyuma, akipata keki ilipendeza sana kiukweli, but sijamuona mama jamani, namtafuta.

Wednesday, January 20, 2010

mwanamke akisuka nywele anatakiwa kukaanazo kichwani siku ngapi


Kuna wengine hadi miezi miwili au mitatu nywele ziko kichwani, zingine hadi zinatoa na harufu,

halafu pia tufahamishane je kukaa na nyweli muda mrefu kichwani hakuchangii kukatika kwa nywele kweli??
japo zinapendeza sana, na waweza kubana style yeyote ile,