Thursday, July 22, 2010

MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI - (BINADAMU HATUNA HURUMA HATA KIDOGO)

Imenisikitisha sana hii, lakini ndio hivyo tena, hawa wenzetu wakikukamata wala hawakuachi na wala hawana huruma.
hii imetokea huko gongolamboto, usiku wa kuamkia leo, mwizi huyu ameuwawa kwa kuchomwa moto, lo!
 story nilizopata jujuu ni kwamba, watu walikuwa wakikimbiza mwizi, mwingine tu! bahat mbaya yule mwizi aliwachenga  na kukimbilia sehemu zingine, (akawapotea) sasa wakat wale watu wamekata tamaa wanarudi, wakasikia kelele mtu analia, anaomba msaada, kama mtu anaekabwa hivi, wakafata kelele zilipo wakamkuta huyu (kwenye picha) akimkaba dereva wa piki piki na wamekuta amemchoma bisi bisi, ila huyo dereva nae alikuwa na ubavu kidgogo, basi walichokifanya waliwahi kumkamata mwizi huyu na hasira za yule mwizi wao wa kwanza zikaishia kwake,
inasemekana baada ya hapo walimwambia aseme ametumwa na nani, (kabla hawajamkaanga) akasema bosi wao anaishi bagamoyo, akawapa na namba za simu, basi wale watu wa hasira kali, walimkamata, wakampa kichapo, haikutosha wakaamua kumkaanga Binadamu mwenzao kama kama hivyo,
nimeona asubuhi hii, du! jamaa kaiva ile mbaya, (binadamu sio kitu jamani lo!) ila ndio waache jamani mbona hawajifunzi??????? ss sijui nae tuseme akalale pema wapi ah!
lakini sasa, kuua kwa kujichukulia sheri mkononi hakufai, kwanza ni dhambi, ss kama walipata namba za huyo tajiri si ni bora wangembananisha awapeleke ili wakamjuwe anaefanya hivyo? inasikitisha sana,
yani mtu unamwagia mwenzio mafuta, unachukuwa kiberiti, unamuwasha, da! mi naona bora wangemtandika mbakora za kufa mtu, wamjeruhi tu! ili yale maumivu yamfundishe, kuliko kuua,Tuesday, July 20, 2010

NAWAAGA WAPENZI WANGU - NINA MITIHANI


Wapendwa, kusoma ukubwani shida! ah! lakini tutabanana humo humo, hadi kieleweke,
nitawaacha kwa muda, coz nina mitihani ya kumaliza semester hii, tunaanza juma tatu.
so nitakuwa busy kwa muda,
si mwajua tena, akili inabidi niiweke na kuituliza mahala mapoja tu!, but i beleave in God, to be back soon!!!,
nitawamiss sana,  ngoja nikavune nilichokipanda.
BYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEMonday, July 12, 2010

RAFIKI YANGU ANAAMBUKIZA WATU UKIMWI KWA MAKUSUDI, NIMFANYAJE? AU NIWAAMBIE UKWELI?

Habari dada, nina rafiki yangu (msichna kama mimi) ambae tumedumu nae kwa muda mrefu sana, ni rafiki yangu wa muda mrefu, ila tunatofautiana kwenye tabia, yeye anapenda sana wanaume, na hawezi kuwa na mwanaume mmoja, hawezi kabisa, nimeongea nae hadi nimekata tamaa,

Tunaishi nae hostel, sote ni wanachuo, sasa kuna siku watu wa ushauri nasaha walikuja hostel kwetu, wakatupa semina sana, hadi tukashawishika kupima, na tukakubali kupata majibu, yangu yalikuwa safi, ila ya mwenzangu hayakuwa mazuri,

Lakini alipotoka kuchukuwa majibu yake akaniambia mazuri, kumbe alikuwa ananificha, sasa kuna siku aliamua kuniweka wazi juu ya afya yake, na kuniambia kuwa ameathirika, niliumia sana as if ni mimi, lakini niliendelea kumsihi inabidi atulie, ikiwezekana aweke akili yake kwenye kusoma zaidi aachane na mambo ya wanume, na haimaanishi kuwa nao ni kufa, mwanzoni alinisikia,

Sasa kinachonishangaza, baada ya miezi sita tabia yake ikarudia, tena naona this time imekuwa mara tano zaidi, haingii darasani, na ana wanaume wengi sana. Mbaya zaidi anasema yeye hatumiagi kinga. Na ananishangaa mimi nilie na mwanaume mmoja

Kinachoniumiza zaidi, amempata kaka mmoja tunasoma nae, na ameniambia bado hawajatembea nae, na atahakikisha anatembea nae, sasa mimi inaniuma sana, asijekumuua kaka wa watu bure, sasa hivi ni nusu ya changu doa, pombe anakunywa sana, ametoa mimba sana, na anasema yey e hataki kinga yeyote,

Nimuwahi Yule kaka nimuweke wazi juu ya hili? Na uhakika asilimia 90% kuwa hajatembea nae, maana anatabia yakunieleza kila kitu

Wednesday, July 7, 2010

NIMEOA MKE MCHAFU SANA- NITAVUMILIA UCHAFUU HUU HADI LINI??

Mke wangu ni mchafu kupindukia, nimesema sana hadi nimechoka, imefika kipindi namsusia hata chakula, maana mazingira anayopikia tu! Unaweza kutapika, lakini wala hajali, na anafuraha kabisa, hali ambayo imenifanya nishindwe kuelewa nimuweke kwenye kundi gani,

Kabla sijamuoa hakuwa hivi, alikuwa akijitahidi sana usafi, baada ya kumuoa tu! Akaanza kudai housegirl, nikamuuliza, housegirl wa nini wakati huna kazi, upo nyumbani tu! Wala mtoto huna? Akawa mtu wa hasira sana, akaagiziwa huko kwao akamleta, nilishindwa kuzuia, nikawa namlipa tu!, alipojifungua ndio kabisaaaaa, uchafu umezidi, housegirl ndio amekuwa kama mama wa mtoto, yeye ni usingizi na kuangalia TV tu,
Jaribuni kumsema nyie wanawake wenzake labda ataelewa, na kweli kwakuwa bado yuko nyumbani, nitaprint comments zoote nitampelekea asome, labda itasaidia, wala sishawishiki kumtafutia biashara, maana hajawahi hata kuniambia nimfungulie hata biashara, yeye ni wakudai mafuta ya gari, ashinde anazungukaa, jioni anarudi, hadi nahisi sijui nimeoa changu doa, mwanamke gani safari haziishi? Hata siku za weekend mimi nipo nyumbani, yeye anaondoka.

Blog hii nimepewa na dada yangu, ndio nimeona bara niombe msaada wa mawazo yenu,

Wakati mwingine mtoto anaweza vikwa pampas akajisaidia, hadi choo kikaganda, bila kusafishwa, kuna siku nilipata hasira sana ,nikamuwasha vi bao, mtoto alinyea shuka asubuhi wakati natoka, nimerudi jioni nakuta vile vile, namuuliza kwanini hujasafisha, eti anajibu alipata safari gafla akatoka nae amerudi jioni, kwanza hajaaga, pia hata usafi tu! Safari gani hiyo hadi usahau usafi wa familia yako,

Huwa najuta kwanini nimeoa, ndio kwanza ndoa ina miaka miwili tu! Ila nimechoka sana utadhani nimeoa mika kumi iliyopita, nilimshtaki kwao, wakasema ndio alivyo, hadi dada zangu wamemsema lakini habadiliki, sijui anashetani gani la uchafu,

Violet na wanawake wenzie, hebu mshaurini huyu kiumbe abadirike.