Tuesday, November 30, 2010

MUME WANGU HANISHIRIKISHI KWENYE MAAMUZI YAKE-NIFANYAJE

Mume wangu hanishirikishi kwenye maamuzi ya familia, naona tu mabadiliko yanafanyika ndani, lakini siambiwi chochote, kazi yangu kupokea tu! Sasa nimesikia tetesi kuwa anajenga huko kwao, lakini mimi mkewe wa ndoa sijui chochote, cha ajabu mama yake mzazi ndio anajua kila kitu, na huyu ni mume wangu wa ndoa, tuna miaka nane kwenye ndoa yetu, ukimuuliza anakuwa mkali sana,  tumezaa watoto wawili mpaka sasa.
Mimi nina kazi nzuri tu na nina mshahara mkubwa Ambao naweza kufanya vitu vya maana, nilivyokwisha vifanya hadi sasa nimejenga nyumba 2, moja ndio hii tunayoishi na mume wangu, sasa mwenzangu ndio kanibadilikia sana, hata simuelewi, je namimi nianze kufanya mambo kivyangu??? Lakini naona kushare Ideas ni nzuri zaid, wadau nisaidieni naona nimetegwa  sana, na pia kwanini asinihusishe mimi mkewe?? Kajenga baa kubwa tu kwao! Lakini mimi Nimejua nilipokwenda kwenye msiba wa kaka yake,  nilipomuuliza ilikuwa ugomvi sana.na hadi sasa hata sielewi nilichomkosea


Tuesday, November 23, 2010

MUME WANGU AMEOTA ANAFANYA MAPENZI NA MWANAMKE MWINGINE NINAEMFAHAMU- IMENICHANGANYA SANA HII, NAOMBA USHAURI WENU

Habari,
Mume wangu amenichanganya sana, siwezi hata kuwaza mambo mengine ya msingi, namuwaza yeye tu, nawaza nafika mwisho bila kupata suluhu, ndio maana ninaomba ushauri wenu
Hivi karibuni tukiwa njiani kwenda kazini, akaniambia kuwa ameota anafanya mapenzi na mwanamke mwingine, (alinitajia jina la huyo mwanamke, ni mtu ninaemfahamu vizuri sana, tena mimi na huyo mwanamke wala hatuivi, kutokana na kuwa na mdomo mchafu sana,
Sasa nashangaa na kujiuliza
1. Kwanini amuote yeye na asiniote mimi???
2. Kwanini aniambie ndoto ya kipuuzi kama hii?
3. Aliniambia ili iweje
4. Ingekuwa mimi ndio nimwambie yey enimeota nafanya mapenzi na mtu anemfahamu ingekuwaje?

Wadau naombeni ushauri wenu, ni jambo dogo bila kutafakari, ila ukilitafakari … inauma sana, ushauri please!!!!


Sunday, November 14, 2010

NIMEMZIDI UMRI MCHUMBA WANGU NAONA AIBU KUFUNGA NAE NDOA


 Habari ya kazi, mimi ni mpenzi sana wa blog yako, Inatusaidia sana mungu akubariki, mimi ni mama wa mtoto mmoja , nilitokea kuchukia wanaume wote pale nilipotendwa na nilikaa miaka mitatu bila ya kuwa na uhusiano na mwanaume yeyote. Mwaka huu january niliingia kwenye uhusiano na kaka mmoja ambaye kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya harusi.

Kinachonifanya niombe ushauri ni kuhusu umri ninamzidi huyu mwanaume miaka miwili na ninaumbo kubwa sana naonekana mkubwa sana nimejalibu kujipunguza lakini wapi, ninakosa amani na ninapozungumza nae kumweleza mimi ni mkubwa kwake yeye hajali na anaona sawa tu.

Ninaogopa sana mwanzo wa uchumba alikuwa hataki kuniambia miaka yake sasa juzi nilipokuwa kwao ndio mama akawa anaelezea jinsi mwanae alivyomzaa mpaka kukuwa kwake. Niliumia sana dada natamani kusitisha maandalizi ya harusi lkn nashindwa maana next thursday ndio send off yangu. Jamani nifanyeje ninaumia sana moyoni.naombeni ushauri wenu wadau.

 
 
 
 

MAELEKEZO - JINSI YA KUTUMA MIKASA YENU KWENYE BLOG

Wapenzi wa blog yangu, kipindi cha nyuma niliwahi kuelekeza namna ya kutuma mikasa yenu ili kupata ushauri,(kwa wale wanaohitaji ushauri) sasa naona wengi mnatuma mikasa kwenye comments, ili inifikie kwa urahisi na niweze kuiedit, fanyeni hivi
1. andika mkasa wako woote, ila ni vizuri kufupisha kidogo (kuandika yale ya muhimu tu)
2. then tuma kwenye email yangu mimi, na sio kwenye comment, email yangu ni violet.gerald@yahoo.com
mkasa wako utanifikia, then mimi nitaurusha, ili upate kushauriwa, 

PAMOJA SANA!

Friday, November 12, 2010

SHEMEJI ANANITAKA, NAOGOPA KUMWAMBIA DADA, NI MKOROFI NA PIA HATANIAMINI

Dada, nakupongeza sana kwa kuwa na blog nzuri, inatusaidia sana, mungu akubariki, mimi nina shida, ninaishi na dada yangu ambae tumechangia baba, ila mama zetu ni tofauti, baba yetu alikufa, ndugu wakamuomba dada anichukuwe anisomeshe kozi yoyote ile,

Nikahamia kwa dada , sasa toka nimefika hapa, shemeji yangu ananifata sana, ananitaka kimapenzi, kwa nguvu na kunitishia kuwa anaenisomesha ni yeye na sio dada yangu, hivyo nimkubalie tufanye siri, Ananifata hadi chuoni, ananinyima raha kabisa, mchana ananifata anitoe luch, yani ah! ananisumbuwa sana na namshangaa amekuwa na wivu hata kwangu, hataki nipigiwe simu na mwanaume, anapekuwa simu yangu, sana, nimejitahidi kumkwepa lakini wapi

Dada yangu ana asili ya kiburi sana, ni mkali kias kwamba hata mama yake anamuogopa, na yeye ndie ameolewa na mwenye uwezo kidogo, hivyo wote wanamtegemea yeye, sasa naogopa kumwambia tabia za mumewe,  maana najua kabisa hatoniamini, na atanifukuza nitashindwa kusoma,,

Ninawaza niwaambie watu wazima wamwambie dada, lakini nina uhakika 100% dada hatoniamini, maana hupenda kusemasema kuwa, akiskia mtu yuko na mumewe, yeye hatadili na mumewe atadili na yule anaemchukulia mumewe, sasa mimi nahofia kukosa masomo yangu, maan shemeji mwenyewe anamjua mkewe alivyo, na kuna siku aliniambia unafikiri ukimwambia dada yako ndio atanifanya nini? Acha ujinga wewe, hutamani maisha ya dada yako, wewe nipe uone ntakavyokupa maisha mazuri,
nakosa raha kabisa, nisaidieni kwa ushauri wadau

nifanye nini mimi??? Dada usiirushe email yangu please!!!

Tuesday, November 9, 2010

NILIBADILI DINI NIKAOLEWA NA MUISLAM, BAADA YA NDOA NILIRUDI KWENYE UKRISTO, MUME WANGU AMEFARIKI, JE NATAKIWA KUKAA EDA???????


Habari ya kazi dada , mimi ni mpenzi mzuri sana wa blog yako, Dada nataka unisaidie mimi ni mkristo, nilibadili dini na kuolewa na muuislam  mwaka 2006 nina watoto 2 katika muda wote huo amani  kwenye ndoa yangu ilikuwepo

Lakini  mwaka 2008 mume wangu alianza  mahusiano na mwanamke mwingine  na kuamua kuzaa nje ya ndoa,  na hapo ndipo amani, na mapenzi vilikwisha,.

Sikuyapenda maisha yale hivyo nikaona bora nitafute njia ya kumrudisha  mume  wangu katika hali ya furaha na amani kama mwanzo,  nilirudi kwenye imani yangu ya ukristo na nilianza kwenda katika maombi kwa ajili ya kumuombea mume wangu, na kwakweli niliona mabadiliko na alianza kurekebishika

Lakini baada ya muda mume wangu alifarik. Kwa kweli niliumia sana  kumpoteza  mume wangu,  Sasa je  natakiwa kukaa eda? Hiyo eda ikoje? Au kwakuwa nilirudi kwenye ukristo haina haja tena ya kukaa eda,

Nisaidieni wadauTuesday, November 2, 2010

NINA MAKOVU SANA KWENYE MIGUU YANGU- YANANINYIMA RAHA, NIFANYE NINI?

Tunapozungumzia urembo, hatuwezi kuacha kugusia suala zima la mvuto kwanza, haswa kwa kina dada, na hasa hasa kwa upande wa ngozi, iwe nyororo, ing'are ivutie zaidi bila kujali wewe ni mweusi au mweupe, mpango mzima ni MVUTO,  sasa hebu tumsaidie mwenzetu huyu. 


mimi ni mdada mzuri na mungu kanijalia kwa kweli namshukuru mungu kwa kuniumba hivi. Lakini nina tatizo moja tu linalonisumbua...nina makovu sana miguuuni, yani mengi sana, na yananinyima raha kabisa...nimeshajaribu vitu vingi lakini wapi, hayapungui wala kuisha. nimetumia beauty cosmetics lakini yanashine tu!

naomba msaada.  lakini nilivyokuwa mdogo nilikuwa mtundu kupindukia sasa utundu unanicost na vidonda na makovu naomba msaada wako na wengine mnaosoma blog hii kama mnajua dawa naomba mnisaidie.

ASANTENI