Friday, February 19, 2010

WAZAZI WA MPENZI WANGU HAWANITAKI, WAKATI MTOTO WAO ANANIPENDA NA NIMEZAA NAE.

Habari dada violet, umri wangu ni miaka 30, nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kaka mwenye umri wa miaka 36, huyu kaka alikuwa na madhaifu mengi lakini nilimvumilia kwa kila hali, kutokana na kumvumilia magumu yake yote na tunajuana vilivyo tukaona bora tuoane, akawa anajiandaa kuleta barua, nami nikawambia wazazi wangu, chakushangaza yeye wazazi wake wakakataa kabisa hasa mama mama yake, akadai huwezi kumuoa huyo msichana, sababu hana elimu,
halafu tupo majirani, ila vikwazo vikawa vingi kiasi ambacho yule mchumba wangu alichanaganyikiwa sana. huyo kaka amemaliza chuo kikuu na mimi nilisomea usekretari baada ya kumaliza form 4,

tulipoona wamekataa tukashauliana na mpenzi wangu na tukatafuta njia nyingine, tukashauriana mi na mchumba nikabeba mimba, loh ndo tuliaharibu kabisa, ikawa uhasama juu ya uhasama, mchumba wangu akaitwa na wazazi wangu akaulizwa mambo mengi na yote akakubali, shughuli ikawa kwa wazazi wake,

wazazi wangu wakaenda kwa wazazi wa mwanaume, majibu waliyotoka nayo huko ilibidi wasinambie mana ningeweza kutoa hata hiyo mimba wakati huo mimba ina miez 7,ilikuwa mwaka 2008 mwezi wa kwanza, nikawaambia mniambie tu, siku moja mama wazazi wangu waliniita na kuniambia kuwa wazazi wa mwenzio wamesema hivi "kwanini ubebe mimba wakati wao hawakutaki?


kwa hiyo hiyo mimba si ya mtoto wao, tena marufuku kumshirikisha mtoto wetu kwenye huo ujauzito",na maneno mengi ya kejeli, nililia sana, niliumia sana sitaki hata kukumbuka, basi nikashukuru mungu lakini yule mchumba wangu hakuniacha kwa kweli alinipa matumizi yote mpaka nikajifungua mtoto wa kike.

walichohadhirika mtoto katoka kafanana na huyo mama mzazi wa mchumba. waliona aibu sana, mchumba wangu akawa anamtunza mtoto,vizuri tu, mtoto alipofikisha miezi saba, mchumba akaanza vituko, mara haleti hela mara ana mwanamke na huyo mwanamke ananipigia simu na kunitukana na kunitamkia maneno makali makali tu!

nilikuwa nakaa kwetu sina kazi wala nini, ndo nasubiri mpaka huyo mchumba alete hela. nikaona bora nitafute kazi, nikapata kazi wakati huo mtoto ana miezi 9, nikaanza kazi, nikashukuru mungu kazi nilipata nzuri, nikahama nyumbani nikaamua kupanga chumba changu, lakini motto wangu nilimwacha kwa mama yangu maana alisema anataka akae na mjuu wake
Nashukuru Mungu kwakuwa mtoto wangu anaafya nzuri tu, na nikaona huyu mzazi mwenzangu amepoteza malengo yote juu yang anafanya mambo yake kivyake na tangia muda ule tukawa hatuna mawasiliano ya karibu akijiskia kuleta matumizi anapeleka kwa mama. ila dada Violet mimi nilipenda na nilitaka sana awe mume wangu, si kwa sababu ya elimu au vipi,

hapa ndipo panaponipa shida, maana hadi sasa nimejikuta sioni mwanaume yoyote ambae nampenda kama yule, halafu naogopa kwa sababu wanaume wenyewe wamekuwa waongo wote nawaona wa tabia moja,

hadi sasa hatuna ule ukaribu kama mtu na mpenzi wake. nasema hivyo kwa sababu alikuja anataka turudiane na miadi kibao ya kushi pamoja moyo wangu unasita sana japo nampenda, sijui nifanyaje naombeni ushauri wenu? Je kama nikikubali kumrudia wazazi wake watanipenda?

7 comments:

 1. achana na huyo mtu, hana mapenzi ya dhati na wewe,
  achana nae kabisa, kuzaa sio sababu, huyo mama atakusumbua na kukufatilia sana anaweza kukunyima hata raha ya ndoa, achana nae, mwache mtoto wako alelewe na bibi, wewe fanya kazi zingine, huyo kaka achana nae

  ReplyDelete
 2. mwenzangu, mm nashauri hivi, kama unampenda na yeye anakupenda ukweli, basi wewe wala usimsikilize mama yako, wewe achana nae, kaeni mapange maisha yenu, wala haina haja ya kuachana sababu ya mama, au huyo mama yeye anataka aolewe na mwanae? elimu inahusiana vipi na mapenzi?

  ReplyDelete
 3. huyo mama atakuwa mgonjwa wa akili
  hivi dunia hii ya leo bado kuna watu wanachakulia watoto wao mchumba?

  ReplyDelete
 4. Sister V, mbona wewe huchangii?

  ReplyDelete
 5. pole sana dada, jamani inabidi kuwa makini sana,kama kweli anakupenda kwanini alikufanyia hivyo, basi atasema shetani alimpitia lol! wanaume hawa, mi kwakweli sikushauri urudi huko na hata kama utarudi kuwa makini nendeni mkapime kwanza, muombe sana mungu hakusaidie ktk hilo swala ndio watu wengi watakushauri lkn mungu ndiye muweza wa yote.

  ReplyDelete
 6. mmh yani story yako ni kama yangu mi tulikuwa tunaishi pamoja nikaja fanyiwa fuja na dada yake tena kasoma huyo dada ungesema labda mswahili hajasoma, ndo nikaamini kusoma si kipimo cha ustarabu wa mtu, basi ikabidi tuachane akamtafutia mwanamke mwingine wakamuoza kisa mi sijasoma nami nilikuwa nimemaliza form IV but nilikuwa nimejirndeleza na nashukuru now nimefikia mbali kielimu. Kusema kweli sijui kama nahitaji kuolewa bora nife hivi hivi tu ilinikatisha tamaa sana na iliniumiza sana kiasi nikikumbuka hulia ingawa ni miaka 5 now! Fikiria mtu ukimpenda with all ur heart! Love Hurt so badly sitaki tena! but pole!hapa naandika na machozi yananitoka sijui why nashindwa kusahau jamani nisaidieni nami!

  ReplyDelete
 7. sidhani kama angekuwa anakupenda kwa dhati angeyasikiliza maneno ya mama yake. kwani anamuolea mama yake au anakuoa kwa sababu anakupenda na anahitaji kuishi na wewe. huyo atakuwa anamsikiliza sana mama yake hata akikuoa atakusumbua sana dada yangu atapangiwa kila kitu na huyo mama yake.

  ReplyDelete