Wednesday, August 29, 2012

NIMEMPATA NINAE MPENDA SANA- TATIZO DINI ZETU ZINATOFAUTIANA, NA NDUGU HAWATAKI HILO,, NIFANYAJE???
Hello miss violet
Nimekua nikifuatilia sana matukio yenu na jinsi watu wanavyotoa uashauri nimeguswaa maana na me nina langu lanitatiza na sijui nifanyaje yaaani sina jinsi ya kufikiria tena.
Nilikua na bwana ambae alikua ananipenda sana ila mimi sikuampenda kiiivyo nkaamua kuachana nae maana ntamuumiza tu maana sikua muaminifu kwake na nkawa najisikia vibaya, kwa ilo nkaamua kumuacha aendelee na maisha yake.


 


Nilipoachana nae nkapata mkaka mwingine ambae kanionesha maisha ambayo sijawai kua nayo ninampenda sana uyu kaka na yeye ananipenda saaana ila ni anawivu na hasira mbayaa ila sababu namuelewa namchukulia kama alivyo najua jinsi ya kumuhandle kama anahasira ilaaa tatizo kubwa ni lililopo ni DINI,
Yeye ni muislam na mimi ni mkristo, ndugu zangu  washaanza kunijia juu kua hawataki niolewe na muislam, kifupi hawataki mausiano yangu nae na me nampenda sana jamani nina furaha  kuwa nae, tuna amani na niko huru saaana kwake!  Mbaya zaidi mama yangu anasema anatambua ndoa moja tu ya kikristo nyingine hazitambui  nisaidieni jamani nifanyaje?? Na hatuko tayari kuachana!!!


Tuesday, August 28, 2012

MPENZI WANGU AMENICHUKIA KISA.. NIMENUNUA KIWANJA NA KUFUNGUA DUKA LA COSMETICS, KWA JINA LANGU-- JE NILIKOSEA????

( MNAIKUMBUKA STORY HII?) Huyu dada aliwahi kuomba ushauri kwamba mchumba wake anamuignore sana, sometimes anamzimia hata simu akimuuliza why, anasema some times yuko buzy hataki usumbufu........ tukamshauri jinsi ya kufanya,,, amenijibu hivi,,,,

Aunt nashukuru kwa ushauri wako kweli mpenzi wangu alibadilika nakunipenda na iyo tabia yakuzima cm kaacha
 ila saivi lime jitokeza tatizo lingine ananipenda ila nahisi km yuko na mwanamke mwingine na saivi anasema kuwa nimemkera kisa nilifungua cosmetcs na nilinunua kiwanja na vyote hivyo nimeandika jina langu na lake hivyo kakasirika eti ckumshirikisha ila mimi niliona nisawa kuandika hivyo kwani nampenda km mchumba wangu ila kanibadilikia hataki kuongea na mimi nimejaribu kumuuliza km umefika mwisho wa penzi letu aniambie ila hataki kuwa muwazi nimeongea na dada yake amuulize km tatizo nini hataki kuongelea hayo mambo akiulizwa anae mwanamke mwingine anadai hana hebu nisaidie kuwa ananipenda kweli kwasababu nampenda sana isitoshe nimtu tumekaa nae myaka mingi na hatujawahi kugombana 
NISAIDIENI USHAURI  MWENZENU


 

Friday, August 24, 2012

NIFANYE NINI ILI KUONDOA VINYWELEO MWILINI MWANGU????

Dada samahan ningependa kufahamu dawa ya kuondoa vinyweleo mwilin
nisaidie napata shida na aman sina naitwa mary nipo dodoma niliona
uliwahi kumshaur mtu pia tatizo kama langu sa sijui alifanikiwa?
Wednesday, August 22, 2012

HIVI KATI YA MKE NA MUME--- NANI MWENYE MAPENZI YA KWELI???

Ni swali ambalo huwa najiuliza sana, sipati majibu,,,, KATI YA MKE NA MUME, Ni nani anaekuwa chanzo cha kuvunja uaminifu ndani ya nyumba,  Ni nani sio mkweli???,

Baada yakujibu hayo, hebu tuzungumze jamani,,,,,, UTAJUAJE KAMA UPO WEWE PEKE YAKO… kwa huyo uliye nae??? Kuna njia zozote za kufanya ili kuprove kwamba uko peke yako??? 
Tuesday, August 7, 2012

INAWEZEKANA KUURUDISHA UPENDO ULIOPOTEA??????

Ni swali ambalo wapenzi wengi hujiuliza, pindi linapotokea tatizo kubwa la kutereresha  Mapenzi yao,,, inafiki kipindi kila mtu anajuta kwanini nilianzisha au kwanini nilikubali kuwa na uhusiano na huyu mtu,,, pamoja na yoote hayo.. watu wale wanaendelea kuwa wapenzi na mikikimiki yooote hiyo,, ila mapenzi yao yanakuwa ya kawaida, yanakuwa mapenzi ya mazowea tu,,, ,,, sasa kuna kipindi kinafika mmoja wao anatakuwa anatamani kurudisha mapenzi ya zamani,, unakuta upande wa pili, haukubali kabisa kurudisha mapenzi, hapa ndipo mmoja wapo anapoweza kupata shida,,,,, NA KUJIULIZA,, NIFANYE NINI KURUDISHA UPENDO WANGU WA AWALI????  WEWE MSOMAJI WANGU,,, UNASHAURI NINI INAPOFIKIA KIPINDI KAMA HIKI???? FUNGUKA..................