Wednesday, June 27, 2012

AMANI IMETOWEKA NDANI YA NDOA YANGU- TUNAISHI MRADI SIKU ZIENDE, SASA HALI HII HADI LINI?????


Naomba ushauri  kwako dada violet  na wadau wengine, Mimi ni mke halali wa mume mmoja na watoto wawili, ndoa yetu ina miaka kumi sasa,  ugomvi huwa haukosekani ndani ya nyumba, lakin naona kwangu imezidi, mume wangu amekuwa na dharau kupita kiasi, hanijali mimi wala familia (watoto)..  yani upendo wake ni wa kubeep
 
Ananichosha tunapokuwa kitandani, yani  imefika kipindi inapita hata wiki tatu au nne bila kugusana kimwili, na kama nikihitaji  inachukuwa muda sana hadi kukamilisha tendo, hisia zake zinakuwa mbali sana na mimi, yani in short simuelewi huyu mwanaume… watu wamenishauri nimdharau tu! Lakini mimi dharau siwezi, naumia mno jamani, bora ukose pesa uwe na amani, kuliko uwe na pesa ukose amani, nishaurini wapendwa wanguFriday, June 22, 2012

NIMEMFAHAMU MWANAUME ANAENICHUKULIA MUME WANGU-NIFANYAJE??????? MAANA NINA HASIRA ZILIZOPITA KIASIHabari yako violet, nahitaji msaada wako sana juu ya hili, kuna mwanamke nimeambiwa anatembea na mume wangu, huyo mwanamke namfahamu sana,  ila sina mazowea nae, sasa nimeambiwa ndio anaemzuzua mume wangu, hasikii wala haelewi chochote.

 Yani hataki kuambiwa lolote lile, maisha yetu ni ugomvi kila siku, kitandani hatuna ushirikiano wowote, kila mtu analala kivyake, nimejishusha kiasi cha kujion mjinga, nimezaa nae watoto watatu, wa mwisho ana miezi kumi.

 Naomba sana unisaidie mawazo, ushauri………


Thursday, June 14, 2012

HONGERA FAITH GERALD KWA KULETA NEW BABY BOY

HONGERA ZAKE  FAITH KWA KULETA MTOTO WA KIUME JANA...MUNGU AMKUZE KATIAK HEKIMA NA KIMO, ILI AMPENDEZE MUNGU NA WANADAMU,
WELCOME TO THE DUNIA NEW BABY BOY )BRIGHTON