Thursday, February 23, 2012


Wote twajua jinsi gani mama alivyo mtamu, hakuna kama mama jamani, ukiondokewa na mama yako, utalia na hutosahau ktk maisha yako, maana yeye ni kila kitu kwa mwana, kuna mdau mwenzetu aliondokewa na mama, na leo amemkumbuka san asana sana,
MIMI  VIOLET, NAKUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AKUPE USHINDI, NGUVU, NA UJASIRI WA KUWEZA KULEA FAMILIA YENU THOUGH HUTOFIKIA KIWANGO CHAKE,
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE


KUMBU KUMBU

Ni miaka 23 sasa tangu umetutoka lakini sisi kama watoto wako pamoja na baba ulietuacha huku tunaona ni kama jana tu umeondoka maana umeenda kimwili lakini kiroho bado tupo nawe, na kamwe hatutaacha kukumbuka malezi yako bora!
Tukiwa kama familia (watoto wako pamoja na mumeo (baba)) daima hatuishi kukuombea DUA njema kila kukicha upate kupumzika kwa kwa amani huko uliko.
Ni matumaini yetu mungu anasikia dua zetu MAMA
Ni sis wanao wapendwa Mariam, Hussein, Salum, Mariam Hawa pamoja na Baba yetu (mumeo) Sheikh Suleiman haatuna la zaidi ila ni dua tunakuombea
INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAAJIUN.


Monday, February 20, 2012

NAWASHWA SEHEMU ZA SIRI, NA KUTOA MAJI MAJI YASIYOTOA HARUFU, NIFANYAJE?

Habari yako Vio, mimi nasumbuliwa na tatizo la kuwashwa sehemu za siri na ninavimba hii sehemu ya kukojolea  na nashindwa kuelewa nifanye nini dada yangu,,kwani ninawashwa mpaka natoa majimaji na ute visivyokuwa na harufu na nilishaenda kwa dr akaniambia ni ugonjwa unaotibika akanipa dawa nikazitumia bikaa muda ila tatizo limejirudia tena na nakosa amani sijui nifanyaje mwenzako nisaidie

Friday, February 17, 2012

HAJISIKII KUFANYA MAPENZI NA MIMI, ANADAI HAPATI RADHA, NIFANYAJE


Aunt mm ni  msichana mwenye umri wa miaka 27,nimeolewa na nina mtoto 1,nina matatizo 2 ambayo yanaisumbua akili yangu,tatizo la kwanza

1)niliolewa miaka 5 iliyopita,siku ya ndoa nilikaa na mume wng siku 3 akasafiri kwenda uk kutafuta maisha kwa bahati nzuri nilishika mimba ndani ya siku 3 hizo,so nikaa peke yng na bila yakuuingiliwa mpk kujifungua,kwa bahati mume wangu akarudi tz baada ya mtoto wetu kua na mwaka 1 na nusu,hiyo ikawa mara yangu ya 2 kuingiliwa coz aliniowa na bikra na niliamua kujitunza pia katika ndoa yng,lkn tatizo likaja alipokua akiniingia alikua akinambia natowa maji sana chini so hajiskii raha ya kusex,nilipooanda vile nikenda kwa gynocologist km wawili hivi tofauti tofauti ili wanianglie km nina tatizo kwa bahati nzuri wote wakanambia nipo ok sina tatizo kama wanawake wenzaangu,yaani nipo normal.

Baada ya hapo mume wangu akasafiri tena mpk hii leo mwaka wa 3 tena sijaonana nae kimwili wala mwanamme yoyote yule na yote kwa kujituliza na kujiheshimu katika ndoa yangu,juzi juzi km miezi 2 hivi nimepata tatizo jengine ambalo nina ukosefu wakupata choo kikubwa so nikenda chooni nikijikamuua kidogo 2 napata maumivu makali kuanzia anus mpk kwenye virgina,ss aunt naomba ushauri wako katika matatizo yng haya 2?na pia sijawahi kuingiliwa kinyume na maumbile.