Sunday, January 6, 2013

SIJUI JINSI YA KUMBEMBELEZA MPENZI WANGU, NISAIDIENI

Habari ya kazi Voiet. Mimi ni kijana wa kiume, i have 18yrs, hadi sasa naishi Zanzibar katika wilaya ya Mjini. Nilikua nikitembelea kwa siku nyingi katika blogi zako zinazohusiana na suala zima la MAPENZI, katika utafiti wangu juu ya suala hilo, nimefaidika na mambo mengi sana yanayohusu MAPENZI, kwa mfano, jinsi ya kumpata mwanamke akupendae, pia vipi utaweza kuishi kuishi nae, na vipi munaweza kuboresha na kudumisha mapenzi yenu na mengineyo. Nashkuru sana nimefaidika kwa kiasi kikubwa sana kupitia BLOG zakoAnt Voilet.
              Ila lakini, pamoja na yote hayo, niliyoyapata kupitia BLOG zako bado mimi nina tatizo moja tu ambalo linanikwaza katika MAPENZI yote kwa ujumla, kwa kutumia TAALUMA ambayo nimeipata kupitia BLOG zako, nahisi nikitu MUHIMU sana katika MAPENZI pia inaweza ikapelekea kuachana na MPENZI wangu na ni kitu ambacho mimi sijakipanga maishani mwangu kumsaliti yeye kwani NAMPENDA.
              Tatizo langu Ant Voilet ni kwamba mimi hadi sasa bado sijajua jinsi gani ya KUMBEMBELEZA MPENZI wangu, kwani yeye kila siku ananmbia NIMBEMBELEZE wakati wa usku asa na mimi sijui kwa sababu mimi nilitaka kuyajua MAPENZI kabla ya kumpata MPENZI,aidha naliyasoma kwanza yakoje halafu ndo nikaingia,bali yeye anambia nimwambie MANENO MAZURI YA MAPENZI YENYE KUMLIWAZA WAKATI WA USIKU ANAPOTAKA KULALA, husema yeye hapati usingizi na mimi pia nimeshachoka kumdanganya, kwaiyo nakuomba Ant Voilet kwa ROHO YA UNYONGE na nainamisha kichwa changu chini na napinda magoti yangu chini na nainua mikono yangu juu kupokea MSAADA wako kwani nakuomba unisadie juu ya hilo kwani NAMPENDA ZAIDI YA ANAVYOFIKRIA na sitaki nimpoteze. Pia nimeshamuahidi Mungu ikiwa hatochukua roho ztu nitakuja kufunga nae NDOA.

                                                          Ni matumaini yangu yakua ombi limefanikiwa
na litajibiwa.
                                                                                        Ant Voilet ndio tumaini langu la pekee.

Thursday, January 3, 2013

MNISAMEHE KWA UKIMYA TAKRIBAN MWEZI MMOJA WAPENDWA

HAPPY NEW YEAR WAPENDWA WANGU WOOOTE, mnisamehe kwa ukimywa wangu jamani, nilisafiri nilienda dodoma kusheherekea sikukuu zangu zoote huko,, nimerudi salama,, poleni kwa kuwasahau jaman,,, mlionitumia post za kuomba ushauri nimeziona wapendwa, nitapost moja baada ya ingine, ila zooote zitapostiwa wapenzi...... thawa eee, MISS YOU SANAAAAA YANI SANAAAAAA