Thursday, February 25, 2010

MSIONE NIMEDODA- MWENZENU NINA ''TEST'' CHUONI,

Kusoma ukubwani kazi kweli jamani, ah! ukirudi nyumbani shida tupu, tracy anataka kuandika nayeye, timo nae anataka umfundishe kusoma
mara mgeni huyu kaja unaitwa, mara usingizi, yani taflani tupu, basi muda wangu mwingi nasoma nikiwa kazini ninapopata kinafasi tu! basi mimi na daftari hivyo msione kimya sanaaaaaa mkajua nimedorola, namalizia test chuoni, then tutakuwa pamoja,

mlionitumia mikasa yenu, pia wala msikonde wapenzi wangu, tupo pamoja, nikimaliza test tu!  nairusha, iko mingi, na mirefu, so i hv to edit, msijisikie vibaya jamani, karibu namalizia then tutakwenda sawa.
nawapenda wooooooooote

10 comments:

 1. Dada Violet upo juu hujadorora wala nini shost. Wanawake na maendeleo,unajitahidi dada siku hiZi ni ulimwengu wa wanawake na maendeleo,tunakua sambamba na wanaume.Ile point ya kua mama wa Home now days hakuna kabisa.Wanawake tusaidiane ili tuzidi kuwa juu kama kawa.

  ReplyDelete
 2. nakupenda pia Violet,
  pole na mitihani mdogo wangu, ndio hivyo tena, hakuna maisha mazuri bila elimu, soma tu! ndio muda wenyewe huu,
  mitihani mema

  ReplyDelete
 3. SIO UTUAMBIE UNASOMA, HALAFU UFELI,
  TUNATAKA TUIONE MITIHANI YAKO YOTE HAPA,
  SAWA

  ReplyDelete
 4. hahaha! mdau hapo juu umenichekesha, mitihani mema dada Violeth, elimu ndio msingi wa maisha, acha wanawake tusonge mbele bwana, hatutaki kuwa wa mama wanyumbani, dada violeth mimi sina watoto wala sijaolewa lkn ninamajukumu mengi shule na kazi alafu niko kwenye nchi za watu basi bill kibao zakulipa yani kila siku nalala hoi wa acha tu,Mungu atusaidie tu jamani.

  ReplyDelete
 5. Pole dada na best wishes na mitihani yako.
  NB>Picha zimetoka vizuri,ila uso una madoa doa, jitahidi kuondoa hayo madoa. Hata ndimu au limao ikipaka usoni madoa yanaondoka.

  ReplyDelete
 6. pole mpenzi wangu,
  nakutakia mitihani mema, na nakupenda pia,
  jitahidi usome ufanye vizuri na mtihani wako wa mwisho ufaulu vizur, napenda sana wanawake wanaotambua umuhimu wa elimu, tunakoelekea nchi yetu itakuwa na wasomi wengi sana,
  nakupenda sana violet, na naona kabisa, una vitu vingi vizur mbele yako, jitahdi utavifikia tu!

  ReplyDelete
 7. mh! uliesema nijitahidi uso una madoa doa, wala hujakosea, yani uso huu naona kama umeshindikana vile, ah! lakini NO, bwana, utapona tu! you know what, kuna harusi nilisimamia, basi tulirembwa tukapakwa mavitu vitu mengi sana, baada ya kutoka pale tu! nilitokwa na chunusi za ajabu, hadi hivi ninavyokujibu ni kwamba niko kwenye dose, nilikwenda hospitali nikaonana na dr. wa ngozi, kanipatia dawa ndio naitumia, yeye dr. kasema sio chunusi ni alarge,
  so najitahidi mwaya, but hadi sasa naona kuna mabadiliko kidogo,
  MWANAMKE RECEPTION BWANA, ukiwa na madoa wala haunogi, ndio najitahidi tahidi, viishe.

  ReplyDelete
 8. hahaaaaaaaaaaaa
  eti unataka uone matokea yangu,
  hii kali, usijali, siwezi anika matokea hapa, ukitaka uje chuoni then utayona huko,
  asanteni, wote

  ReplyDelete
 9. POLE SANA NA MITIHANI USHAURI WANGU KWAKO NI KUWA NA MPANGILIO MZURI WA RATIBA YAKO.NAJUA KAMA MAMA,MFANYAKAZI,MWANAFUNZI NA UNASHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII,MUDA KWAKO NI KITU ADIMU SANA.HIVYO BASI YAKUPASA KUTUMIA KILA WAKATI KWA MPANGILIO ULIO BORA NA FASAHA.JARIBU KUWA NA AT LEAST A MINIMUM OF 45MINITES TO 1 HOUR KILA SIKU KUFANYA REVIEW YA ULICHOSOMA NYUMA.NAAMINI KUWA UNA UWEZO,UNA NIA,NA UNASABABU YA KUAMUA KUSOMA KEEP IT UP MAMA.

  ReplyDelete
 10. Good dada v nakupenda sana unapenda sana kukosolewa hivyo ndiyo inavyotakiwa utafika tuu dada yangu.sasa itabidi ufungue office ya kusimamia harusi watu wakodishe au unasemaje?

  ReplyDelete