Wednesday, February 17, 2010

NAJUTA KUPENDA, NA NASIKITIKA KWA USALITI ALIONIFANYIA MPENZI WANGU"(Hii ni ndefu kidogo, ila tumshauri mwenzetu)

Hellow Dada Violeth,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24,Mpare, Mkristo na nina boyfriend wangu mwenye umri wa miaka 30,Mkinga,Mkristo.Tumekuwa wapenzi kwa muda wa miaka mitatu (3).Lakini toka Christmas mwaka jana tumekuwa na migongano katika mapenzi yetu, yeye amepanga chumba kimoja, kwakuwa tulikuwa tunapenda sana nilikuwa huru kwenda kwake muda wowote ule, na funguo ninazo,
 
kazi zake yeye sometimes anaingia shift ya usiku kwa hiyo unakuta mimi nikienda anakuwa hayupo, au tunapishana, lakini mara nyingi tulikuwa tukionana nae juma mosi na juma pili.
 
siku zinavyozidi kwenda ndio akawa anazidi kubadilika, hana furaha na mimi hata nikienda kwake, hapo anapoka kuna mama wa makamo, ambae ndie mama mwenye nyumba,ambae ametokea kunipenda, na huwa ananishauri nimwambie boyfriend wangu kama kweli ananipenda basi anitambulishe kwa kwao,
 
wakati ndio tunaanza urafiki mimi na yeye, hakuwa na kazi yeyote ile, alikua akiishi na kaka yake, ila hali sikuipenda, mimi nilijitahidi nikamtafutia kazi ambayo ndio anaifanya hadi sasa, na badae kumsihi ahame akae kwake,
 
lakini yote hayo mchumba wangu huyu hakuwa ameyaona, siku moja aliingiza msichana mmoja ambae ni BARMAID(mfanyakazi wa baa) akalala nae, asubh wakati yle dada anatoka akakutana na mama mwenye nyumba, yule dada alistuka na kurudi ndani, yulekwakuwa ananipenda, siku nilipoamua kwenda kwa ajili ya kumfanyia mpenzi wangu usafi, yule mama aliniita na kunieleza lile tukio, nililia sana, niliumia na niliondoka bila kuuliza
 
lakini nilishindwa kuvumilia kabisa, usiku nikapiga simu kwa boyfrienda wangu ana kumuuliza, akakataa akasema sio mpenzi wake isipokuwa alikwenda kufata pesa yake, sikumuamni, toka pale mapenzi yangu kwake yakawa yamepungua sana,

Christmas 2009, ilikuwa ni majira ya usiku nilipigiwa simu na mtu ambae simjui, ilikuwa ni sauti ya mwanamke aliyenitolea maneno machafu na kuniambia tutabanana hapo hapo,haijalishi mimi na huyu mpenzi wangu tunamahusiano kwa muda gani ila kama nitakuwa nae mchana basi na yeye zamu yake ni usiku.Nilihisi maini yananitoka,kwanza nikajiuliza ni yule dada barmaid ameamua kunitusi hivyo au ni mtu mwingine tu katumwa??

Kumbe ni dada mwingine tena, ambae nae pia ni barmaid!, nliishiwa nguvu na kujiona nipo utupu kwani yule dada alinieleza kila nilichokuwa nafanyana na mpenzi wangu ikionyesha kuwa alikuwa pia ni mpenzi wake.Hadi mara ya mwisho tulipoenda kumsalimu wifi yangu yule dada alikuwa anajua kila kilichokuwa kinaendelea.Na matusi mengine ya kashfa kama"Wewe unanuka,unajipendekeza kwa ndugu zake, mwenyewe anasema hana muda na wewe, ameshanipata mimi ninamridhisha, hujui mapenzi mshamba tu!na isitoshe hapa nilipo ameshanivalisha pete na ni mjamzito.Akidai kuwa mimba yake ina miezi miwili!

Dada Violet,  nilichanganyikiwa wala sikulala, nikaamua kumpigia simu boyfriend wangu tena kujuwa kama ni kweli, matokeo yake simu ilipokelewa na yule mwanamke na kunijibu kwa jeuri, Anti!mbona lakini unakuwa sio muelewa?naomba uniachie mpenzi wangu na hatutaki usumbufu saizi, hapa tulipo tunajazia VIUNGO vya mtoto wetu, kama MIGUU na VIDOLE"

nililia sana, hadi mama yangu alishtuka na kuja kunigongea, niliogopa kumueleza mama ukweli kwakuwa ana pressure, hivyo nilidanganya kuwa nimeota nimepata ajali, basi mama aliniombea na kwenda kulala,
toka pale nikaamua kumsahau, nakuanza maisha mapya, nilichokifanya ni kwenda kupima afya yangu tu!
na nikaamua kuendelea na masomo yangu tu!,

baada ya muda akaanza kunisumbua tena ili turudiane, nilliona kero nikabadili namba ya simu, lakini aliitafuta kwa marafiki zangu na kuendelea kunisumbua kwamba turudiane nae,

Nipo kwenye mawazo sana, kwakuwa nilimpenda sana huyu kaka, na mafanikio yake mengi yametokana na juhudi zangu, amenitenda yasiyostahili, sasa hivi ndio anataka nimrudie tena, naombeni mnishauri maana sijui hadi sasa nifanye nini. 15 comments:

 1. shoga usirudiane nae huyo, kakutenda mwanzo na atakutenda tena, anataka kukutumia tu kwenye mafaniko yake, wanaume wako kibao, huyo hastahili penzi lako....

  ReplyDelete
 2. pole kwa matatizo yaliyokusibu mamii,

  pole kwa yote yaliyokupata ila usichoke kumuomba mungu wako akujalie yale yaliyo mema.

  Kwa hakika ulichokipata ni mtihani mkubwa ambao usijali tu naamini umeshaushinda. Wewe ulipata shida hiyo ila wapo wengine wanayo mengine yanayokuzidi, wengine wanaletewa hadi wanawake wengine ndani na kufanyia mapenzi katika kitanda mnacholala.
  Cha kukushauri ni kuwa huyo mwanaume tayari umeshakutia doa katika moyo wako. Kwa kuwa umeshakiri kuwa ulijitahidi kumsahau na kweli ukafanikisha achana nae kwani sio mwema,
  usiangalie mafanikio yake kuwa wewe ndo umeyasababisha bali mshukuru Mungu na fanya kama vile ulitoa sadaka kumsaidia.

  ReplyDelete
 3. Dada Pole!

  mimi ushauri wangu kwa kweli, sio ubavu wako hata kidogo tegemea wewe ni Mkristo, endelea kumwambia Mungu akupe mume mwema, achana na kutembea na wanaume kabla ya ndoa. ona sasa unavyoumia. hakufai hata kwa dagaa.

  Funguka ufahamu wako ujue kuwa kama uchumba umepata kuletewa kitandani na ndoa je? si utashushwa chini mwenzako alale kitandani? achana kuanglaia umemfanyia mema mangapi angalia je moyo wako una amani?

  ReplyDelete
 4. MH! WEWE MTOTO,
  UNACHOKITAKA HAPO NINI TENA? WEWE UNAONA KUNA MAPENZI HAPO? HATA NDOA BADO AMESHAANZA KUKUUMIZA, AKIKUOA SI ATAKUUA HUYO? HAFADHIRIKI HUYO MWANAUME, ACHANA NAE, KWANZA ANATEMBEA NA MABARMAID WEWE WA KAZI GANI, ANAKUSHUSHA HESHIMA TU! HAPO, ACHANA NAE DADA, UTAJIUMIZA BURE, CHAPA KZI, MAISHA YAENDE, MUNGUA AMEKUANDALIA
  ACHANA NAE, TENA MWAMBIE AKUACHE KABISA YANI, ASIKUTIE SHOMBO UKASHINDWA KUNUNULIKA, MUACHE NA MILAANA YAKE
  MH MIJANAUME YA SIKU HIZI? UPUUZI MTUPU

  ReplyDelete
 5. Pole dada
  mimi nakushauri usirudiane naye cz alishaonyesha dharau mwanzon atakuumiza hapo baadae jua mume mwema huletwa na Mungu ivo hayo mafanikio aliyoyapata kupitia wewe ucjali Mungu atakulipa kwa njia nyingine...sali utapata ubavu wako wala usiwe na haraka.kifupi huyo hakufai.

  ReplyDelete
 6. Mdogo wangu ingekuwa amekuowa ningekwambia heshimu ndoa, hajakuowa kero ni hizo. na kama anatembea na barmaid atakuuwa ukimwi nje nje, umri wako bado mdogo sana sana mtafute mungu akupe wa kufanana na wewe sio wa kukupa maudhi ndugu yanguSoma fanya mambo yako ya maendeleo, kwa wakati aliyoupanga mungu utaolewa. Muombe mungu umsahau na umwambie kabisa niache kwa uliyonitendea yanatosha ingekuwa wewe ndiyo unamtenda hivyo angejisikiaje?. Katika maisha yangu mimi nimesota sana katika usichana lakini mungu aliponifungulia mlango nimeolewa na miaka37 na mume wa rika langu na nina amani. sasa miaka 24 usiogope.
  Mama Dear

  ReplyDelete
 7. Mh pole sana data.huo sio mwisho wa maisha kwamba ukimkosa ndo hutapata mwingine?Dada ukiingia hapo inakula kwako kwani kama aliweza kumpa mwanamke mwingine simu yake akutukane eti unanuka na hujui mapenzi?unadhani ukimrudia ndo utanukia au ndo kwanza utazidi kunuka.Wanaume wapo wengi tu mwombe Mungu akupe ubavu wako tena mwenye hofu ya Mungu tofauti na hapo utajeruhuka zaidi na hutaona raha ya maisha.Na kumbuka wanaumenhuwa hawajali.

  ReplyDelete
 8. Shukuru mungu hukufunga nae ndoa laiti mngefunga ndoa ndio ungekuwa na wakati mgumu sana maana mkristo ndoa ni 1 tu lakini mungu amekuonesha mapema kama huyo sio chaguo sahihi anamapungufu sana ya usaliti inabidi umshukuru kwakukuonesha huo ukweli kwamaana iyo ndio tabia yake akuanza leo wala jana,sasa basi kwanza kaachini ujifikirie jee alikuwa anakupenda?na kama anakupenda mbona alikuwa analeta wanawake kwenye chumba ambacho uliweza mtafutia na ww unafunguo wa icho chumba inamaana alikuwa tayari ata ukija ukamkuta ndani na mwanamke asingejali ilo na pia asingeweza mwachia mwanamke sm yake akwambie huo upuuzi wao wanaoufanya,kifupi mama naona hana mapenzi na ww ila anataka kuwa na ww kwa maslahi yake kuwa makini sana na uyu mtu lamwisho ili usiweze kupata taarifa zake wala asiweze kukupata jaribu kubadilisha lina ya sm ambayo mlikuwa mnawasiliana ili asikupate na akafanyikiwa kukudanganya tena na jiepushe na watu ambao ww na yeye mlizoeana ilo litakusaidia zaidi,Pole sana Shostiiii

  ReplyDelete
 9. pole sana dia haya ndiyo maisha tunapaswa tusali sana ila Mungu ni mwema atakupa wa kufanana nawe umri bado mdogo una nafasi ya kuanza upya wazungu wanasema EVERYTHING HAPPEN WITH A REASON.mdogo wangu chagua njia iliyobora.magonjwa mengi tna na MABAAMEDI kweli hii ni hatari nafuu angechukua mtaani.sali sana dada utaona njia ya kutokea.GLORY

  ReplyDelete
 10. pole sana mdogo yangu!! kumbuka Mungu anakupenda sana na anakuwazia mema siku zote, maisha yako yote toka mwanzo hadi mwisho anayafahamu. kuna wakati Mungu anatupa majaribu ili kututoa katika ujinga tulionao na kutupeleka katika nuru. ninachokuomba mdogo wangu ebu FUNGUKA sasa na umtazame Mungu wako, huyo sio mume wako, kaa chini na umlilie Mungu akupe alie wa kwako na mwenye hofu ya Mungu. isitoshe umri wako bado mdogo TULIA.Maisha ya ndoa si lele mama na haipaswi kuyaendea kwa pupa. kila kitu kina wakati wake. Mshukuru Mungu sana kwa kuwa amekuonyesha jinsi huyo mwanaume alivyo kabla hajakuoa. kama utadanganyika ukakubali akuoe, am telling you hiyo ndoa yako hutaifurahia na utakuwa mtu wa kulia siku zote.

  ReplyDelete
 11. jaman my dia nakushauri usifanye kosa kabisa kurudiana na huyo mwanaume atakuumiza sanaa

  ReplyDelete
 12. Achana na mjinga huyo, atakusumbua utaona dunia pembenne na si duara.Yalinikuta kama yako na nikajifanya mama huruma na siwezi kuishi bila yeye (eti the love of my love) nikamsamehe,niliyoyapata ni bora uchemshwe kwenye mafuta kuliko machungu na maumivu aliyonipa kwa kunitenda. Songa mbele, utapata anayekupenda kwa dhati, nimeolewa sasa na mtu mwingine, mume wangu ananipenda na kunijali na nampenda pia saaaaaaaaaana.

  ReplyDelete
 13. Kwanza nakupa hongera kwa msimamo ulionao mpaka kumbadilishia laini mimi naona huyo mwanaume hakufai endelea namsimamo wako usikubali akuchezee atakuumiza tena kwakua hajakuoa nakushauri usimrudie

  ReplyDelete
 14. achana na huyo laana atakuuwa bure!!
  fanya mambo yako mwaya Mungu yupo na yeye ndo ameumba ndoa basi atakupa mme wa ukweli kabisa.

  ReplyDelete
 15. Usithubutu kurudiana nae, mwamini Mungu yeye hawahi wala hachelewi, atakupa wakufanana nawe.ni ngumu kumsamehe mtu aliyecheat kuliko hata unavyoweza kufikiria, maana kilio unacholia ni afadhali uone amekufa kuliko akiwa na mtu mwingine, maumivu yake yasikie kwa mwingine.

  ReplyDelete