Thursday, February 11, 2010

KINA MAMA TUSIWE BUSY SANA KIASI CHA KUACHIA MAHOUSEGIRL KAZI ZOTE!

Kweli tuko busy na kutafuta maisha (pesa), kiasi kwamba lazima uweke house maid nyumbani ili aangalie watoto wako na kukusaidia baadhi ya kazi pale unapokuwa haupo.
Lakini tunajisahau sana na kuacha kila kitu kwa house maid, yani wewe ukishaitwa bosi, basi ndio kila kitu afanye mfanyakazi wako, unakuta hata kutandika kitanda chako na mumeo housegirl ndio anaetandika, 
maana wewe ndio uko busy, lakini ubusy wako usizidi kipimo,
mahousemaid wengine mabosi wao wakiwa hawapo, wanafurahi sana, wanafanya vituko vya kila aina, ukirudi wananyweaaa, wanakuwa wadogo kama piriton! wewe hujiulizi ni kwanini?
mwingine akimaliza kutandika ndio anapumzika kabisa anasoma na vitabu chumbani kwako
bora anaesoma kitabu utasema hakina shida, mahouse maid wengi wanaingia katika vishawishi kutokana na position aliyopewa ndani ya nyumba yako,
house girl atenge chakula kwa baba, tena sio atenge dinning room
anapeleka hadi chumbani alipo mumeo, kweli hii si tunawatega waume zetu??
hapo mama uko busy, nyumbani mwenyewe umemuacha DADA, aangalie familia
mh!


.
sasa, hapa analaumiwa nani?? house girl ndio anakusaidia hadi kunywa au kula na mumeo tena chumbani kwako, unafikiri mumeo mawazo yake yatakuwa kwenye hicho kinywaji au chakula alichopelekewa??

umeona matokeo yake eeeeeeee, baba ameshategwa, MDADA nae ndio anawajibika
mwenyewe ukiulizwa watoto umewaacha nanani, bila hata aibu, nimewaacha na DADA
haya sasa DADA anaacha kulea watoto anamlea DAD
HAPATOSHI........

hadi uje ushtuke ni TOO LATE, kama ndio una kitoto unakiacha na dada, basi kinaona mambo mengi, lakini ndio hakiwezi kusema, kwanza hadi urudi labda kitakuwa kimeshasahau kila kitu! kinaangalia tu!
LAKINI NANI ANASABABISHA HAYA YATOKEE??
Kweli kuna baadhi ya wanaume ambao hawaoni kichaka.......... lakini pia kwa sehemu kubwa tunachangia sisi wenyewe kina mama, si kwamba tusifanye kazi zetu,
kazi tufanye, lakini na housegirl nae umpe majukumu yake, yasipitilize, chumbani kwako akutandikie kitanda labda uwe unaumwa huwezi hata kunyoosha shuka,  mwingine ukimpata mstaarabu atakwambia, mama leo baba kaniambia hivi, lakini wa hivyo wachache, wachache sana, wengi wanakuja macho miamoja, anasubiri ategwe tu! ategeke, sasa kama unaweza zuia asitegwe kwanini usizuie?
anza na mume wako, bwanaeee chakula , kinywaji, vyote viliwe dining room, ukitaka chumbani usubiri hadi mimi niwepo!, unakuta mtu unaacha hadi nguo za ndani za mumeo unamrundikia housegirl afuwe, sasa ni nani mama hapo?? hiii nimeiskia kwenye  familia nyingi sana
mtu analalamika tu! housegirl wangu yuko hivi, yuko vile, sikuhizi anakiburi, unajibu nayeye anajibu, anakujibu si anaona mko sawa nae, kwani una nini ulichomzidi, kama ni baba nae anamjuwa kuliko hata wewe! kama  chupi za baba nae anafua, kitanda kile unachoamka wewe nae analala, sasa mnapishana nini?
MPANGIE HOUSEGIRL WAKO MAJUKUMU, kwamba dada, hakuna kuingia chumbani kwangu wakati baba yako yupo huku, ikiwezekana hakuna kuingia kabisa awepo, au asiwepo,  chumba chako na watoto ni hiki, unakuwa umezuia kitu, umemnyima sheteni nafasi, mengine ya kumshawishi baba wewe unaayajua
NI KWELI YAPO, NA YANATOKEA, TUSIJISAHAU SANA JAMANI


6 comments:

 1. Kweli co vzuri na haipendezi,yn hadi kitanda atandke housegirl,nguo za mmeo afue yy,usafi yy,we mama mwenye nyumba ndo upo bize,asa hapo nani anapaswa aitwe mama mwenye nyumba?yn km mimi ndo ningekuwa house girl na mama mwenye nyumba yupo hivyo,alafu na baba ndo anajilengesha kwangu,namkubalia huyo baba maksudi ili mama apate fundisho.ASIA ALAWI

  ReplyDelete
 2. hahahaaaaaaaaaaaaaa
  ASIA ALAWI umenichekesha sana, yani nimecheka kwa sauti sana,
  hata hivyo nikupongeze dada Violet kwa kutukumbusha majukumu yetu, kwani tumekuwa tunajisahau sana, mm kuanzia hivi sasa hivi naanza kupanga majukumu ya housegil rasmi,
  kusema ukweli chumbani kwangu alikuwa anaingia na anafanya usafi, ila hizi picha zimenifanya nikonde, nahisi kama ndio mdada wangu na mume wangu vile, EEE MUNGU WANGU, mh! mie nikijuwa sijui ntakufa! ha!!!
  yani leo ndio mwisho wake kuingia chumbani
  Mama Winie

  ReplyDelete
 3. NA TUNATEGWA ASIKWAMBIE MTU,
  KAMA MIMI MKE WANGU SIJUI YUKOJE YANI, ETI MAMA YAKE MDOGO KAMLETEA HOUSEGIL KAMTOA SINGIDA, ANA HIPSI ASIKWAMBIE MTU, MKE WANGU HAONI NDANI, YANI ANAMAKALIO, YANI HATA RAFIKI ZANGU WAKIJA HUWA WANANIULIZA KUNA USALAMA HAPA? MWENYEWE BADO MSHAMBA MSHAMBA? HILO NALO MUWE MNALIANGALIA, NYIE WAKE ZETU NDIO MTATUFANYA TUCHOMWE MOTO NYIE,
  SIO KWAMBA NIMESHAMMWAGIA, BADO, HUWA NAJIKAUSHA, NIKITOKA KAZINI INABIDI NIKAE MAHALI NAMSUBIRI WIFE NDIO TURUDI NAE, NIKIRUDI PEKE YANGU SIPONI KWAKWELI, Na yule ant hivi anamtafutia mwanae nini?? kuleta housgirl mrembo hivi, halafu mwenyewe ananiita shemeji, mh! YANI DADA VIOLET, NATEGWA KWELI SIO MASIHARA,
  NO NAME

  ReplyDelete
 4. Mh! sitaki hosegirl??

  ReplyDelete
 5. Sitaki hause girl tunagawana kazi na mume wangu mpaka basi kazi inayonisumbua na huwa namwambia naomba tufanye wote kila jumamosi kufua tuu pasi napiga mwenyewe, maadamu mtoto asubuhi namtia katika basi anaenda shule, ndiyo na mimi naenda ktk mihangaiko yangu wakati mume wangu kaenda kazini, maana mimi ninashughuli zangu binafsi. Naogopa jamani Ukishi ughaibuni ukirudi Tz wala huitaji House girl hiyo imenishaidia sana sana.
  Mpendwa

  ReplyDelete
 6. Mpendwa,
  unawezaje kuzigawa kazi zako? na kama una mtoto mdogo utafanyaje?maana mimi nilikuwa sipendi sana kuwa na houegilr, kipindi ambacho sijazaa, lakini nilipozaa nilimtafuta mwenyewe, na kama haitoshi vile, miezi miwili tu! nikaitwa kurudi kazini, mtoto nitamuacha na nani? huyo mume wangu ni mvivu asikwambie mtu, anaweza kuvua chupi na nguo akaacha chini, nisipoitoa tu! basi itakaa hapo hapo, anairuka tu! nimeongea hadi nimechoka, kwahiyo
  kwa suala kama hili, ni lazima uwe na housegirl, kwa ajili ya mtoto, sema ni kama anavyosema dada violet kwamba tuweke mipaka ya kazi tu!

  ReplyDelete