Wednesday, June 30, 2010

NIMEKUTA CHUPI YA KIKE KWA MCHUMBA WANGU, ANASEMA YEYE HAIJUI NIFANYAJE.


Wadau hapa nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni ushauri wenu, nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu Tanga(ndiko kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka nikiwa nimeshavishwa pete.

Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto wake wote tulio mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na kukuta kweli hali ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu kumuuliza yuko wapi, ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba amesafiri kikazi gafla kwa siku moja tu then kesho yake angegeuza, nikamuuliza inakuwaje huniambii, akasema nimesafiri gafla, hata hivyo nilitaka nikujulishe maana nimeondoka leo.Niliumia sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, mbona mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana? Nilijisikia huzuni sana ila nilijipa moyo

nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto wa mwenye nyumba, nikamuuliza kama kweli mchumba wangu amesafiri,(nikajua labda alikwenda supermarket kununua vitu vya safari) akasema mbona yupo? Na asubuhi nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo pale kwake, akasema atachelewa sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho ndio nije, nikamwambia namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni nimekaa namsubiri, aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na kuanza kunifokea kwanini nisingesubiri hadi kesho.

Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi mkubwa,

Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani, itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.

Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri wenu?


Monday, June 28, 2010

KARIBUNI KATIKA CLUB YA NDOA ZAKAYO NA WITNESS

This weekend tulisherehekea harusi ya mtoto wa wifi yangu, Zakayo aliemuoa bibie Witnes, ilipendeza kiukweli, tulienjoy sana, sasa hebu cheki pic hizi, waweza pata some styles

waliingia kwa style yao, walikuwa wenye furaha na kujiamini sana, ''niliipenda hii'', umeona eee, Bi harusi kambebea mumewe Koti

kati kati ya ukumbi akamvalisha,

anamfunga vishikizo, jamani raha sana, nilimpenda huyu Bi harusi, yani always alikuwa anatabasabu,
mie nae sikukosa, ninavyopenda shughuri we!

Mume wangu nae alikuwepo kumpongeza mjomba wake,


Abilia chunga mzigo wako wewe!!!!!!!!!!!!

Wasimamizi wao pia walikuwa wacheshi, wote walikuwa na furaha


shemeji yangu na mimi, Ba trace na mke mwenzangu, was fun sana tu!


hivi ndivyo ilivyoonekana keki kwa juu,

na hapo ndio full,

i like this style, badala ya kupeleka keki kwa wakwe mmezibeba, sasa hivi zinapelekwa na kigari kama hicyo, huku vile vitoto vya mbele vikiwa vinaendeshwa na matroni wao '' ubunifu wenye maana sana huu'' ni baraka tu!

Maids wa kike

wakiume nao hawa

enjoy dears

Thursday, June 24, 2010

NILIWAHI KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE, NIKIZAA MUME WANGU ATAJUA?

habari aunt violet hongera sana kwa kuanzisaha blog ambayo inasaidia watu wengi kwa ushauri mungu akuzidishie.mimi ni msichana mweye umri wa miaka 25 nimeolewa mwaka jana naweza kusema tangu nimeolewa karibu mwaka sasa na nashukuru tunaishi vizuri na mume wangu.

Tatizo langu ni moja aunt kabla sijaolewa niliwahi kuwa na boyfriend ambaye nilikuwa nae kwenye mahusiano karibu mwaka mmoja mwanzo alikuwa anaonyesha ni kijana mtaratibu na mstaarabu lakini baadae kama baada ya miezi sita ya mahusianao alianza tabia ya kuniomba tufanye mapenzi kinyume na maumbile, Sio siri nilipingana nalo sana hilo jambo baadae akaniambia alikuwa ananitania aone kama nitakubali yakaisha.

lakini baada ya kama miezi kadhaa hivi akaanza tena kuniambia kuhusu jambo hilo tena nikakataa, siku moja tukiwa tunasex akaforce kuniingilia kinyume na kwakuwa alinistukiza akaniingilia tukawa tunagombana huku mimi nikijitoa nikafanikiwa kutoka huku nikiwa na maumivu sana kiasi kwamba kama muda wa siku tatu hivi niliumwa nikastop mawasiliano nae

akaanza kunifuata kwetu na kunipigia simu akiomba turudiane nimsamehe ni shetani alimpitia alinibembeleza sana kwakuwa nilimpenda nikakubali tukaendelea na mahusiano siku nyingine tena nikaenda kwake kumtembelea akanipa kinywaji kumbe sikujua aliniwekea dawa za usingizi nikalala akaniingilia nyuma tena akiwa ndio ananiingilia kwa mbali nikiwa na kizunguzungu nikahisi maumivu nikawa nalazimisha kuinuka huku sina nguvu na alivyoona nimeshituka akajitoa akaanza kuomba msamaha akasema yeye hawezi kuwa na mwanamke bila kufanya hivyo akasema kazoeshwa na mwanamke wake wa mwanzo ambae alishaachana nae mimi kuona vile nikaamua rasmi kuachana nae nikaona ataniharibia na isitoshe dini inakataza

nikawa naogopa kwakuwa nasikia wanawake wengi wenye mchezo huo wakati wa kuzaa wanapata shida na manesi wanawatukana sana. sasa aunt tatizo ni kwamba baada ya kukutana na mume wangu sikumwambia ukweli kama boyfriend wangua aliyepita aliwahi kunifanyia kitendo hicho ingawa anajua kama niliwahi kuwa na boyfriend kabla yake na kitu kingine aunt mimi sasa hivi nimeolewa na napenda na nahitaji sana kuzaa

lakini naogopa kitu kimoja nikija kuzaa haitojulikana kama niliwahi kufanyiwa hivyo?na pili. watu wengine wanasema kama umezoea ndio unajulikana lakini kwa mara moja au mbili sio rahisi jamani naombeni mnishauri kwani nina wasiwasi nikija kuzaa ikajulikana mume wangua ataniacha na nampenda sana mume wangu na naogopa sana aibu ikijakujulikana hakuna atakae niamini kama sikufanya kwa hiari yangu. please violet naomba msaada pamoja na wadau wote wa blog yako.JE NI KIZAA HAITOJULIKANA.


Tuesday, June 22, 2010

MUME WANGU ANANINYANYASA NA HATAKI KUNIPA TALAKA-NIFANYAJE

Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 40, niliolewa miaka 25 iliyopita, lakini hadi sasa na utu uzima huu sina mtoto hata mmoja, baada ya kujiona nina matatizo, nilimruhusu mume wangu azae na mwanamke mwingine, alizaa nae mtoto mmoja ambae sasa ana miaka tisa, lakini baada ya mtoto kufika miaka miwili Yule dada alipata ajali akafariki, hivyo mtoto akahamia kwangu na nikamlea hadi sasa, kama mwanangu na ananipenda sana.

Kuna siku nikiwa nyumbani kwangu  nilipigiwa simu niende buguruni, nikaambiwa wewe mtu mzima ni (dawa) jikaze, mumeo anaoa leo, unalijua hili? Nikawaambia hapana mume wangu ameniaga anasafiri kikazi, wakasema muongo, mumeo anaoa (wakanielekeza eneo la shuhuri ili niende) nilijikaza nikanyanyuka na kwenda, nilipofika hilo eneo nilikuta kweli harusi kubwa, vyakula na taarab inapigwa, nilijibanza pembeni nililia sana, na nilishuhudia kwa macho yangu na kumuona mume wangu,

Kilichoniumiza kwanini mume wangu anifiche kitu kama kile? Kwanini asiniambie tu kama anataka kuoa, kwanini afanye siri? Basi sikufanya lolote, nilikubali matokeo nakurudi kwetu Kisarawe, baba yangu alinisihi nirudi nyumbani kwa mume wangu, hadi anipe talaka ili tugawane mali tulizochuma pamojan, nikarudi. baada ya wiki moja mume wangu akarudi, hakujua kama hata kwenye hiyo harudi nilienda na kushuhudia nikiwa nimejitanda vitenge na nikaondoka, , cha ajabu hataki kunipa talaka, anasema kama unaenda wewe nenda, ila mimi najua kuoa tu! Sijui kuacha

Mimi sikumuuliza kitu, ila hakuwa na amani, nilipoona yupo kimya niliamua kuanza kumuuliza, mwanzoni alikataaa, nilipomshikia kisu na kumtishia, ndio akakubali kuwa ameoa na akaomba msamaha, tokea pale sikumwamini tena,, na chuki zikazidi, mbaya zaidi huyo bi mdogo ni mtoto mdogo sana, ni sawa na mwanawe wa kuzaa,

Huwa anakuja kwangu, eti kumsalimia Yule mtoto ninaekaa nae, kuna siku alikuja na kutaka kuondoka nae, nilimkunja, nilimpiga sana, nilimuumiza, toka siku ile, mumewangu nae hanipendi,

Sasahivi Napata tetesi kutoka kwa watu kuwa anataka kuuza nyumba hii tunayoishi, na isitoshe analeta vitu ndani bila hata kunitaarifu, mimi nayeye tunazaidi ya miaka 25 ya ndoa, yani ananibagua sana, hanishirikishi kwenye chochote kile, sasa na utu uzima huu akiuza nyumba ahamie kwa huyo bi mdogo mimi nitaishi vipi? Na hataki mimi nifanye kazi yeyote ile, toka aliponioa, hataki nitoke,

Tumejenga nyumba mbili pamoja, tumenunua magari mawili na daladala moja, lakini hata mahesabu ya daladala sikuhizi sipewi mimi, yanapelekwa kwa bi mdogo, sina amani wala furaha hata kidogo, nifanyaje?

Monday, June 21, 2010

NILIKUWA NAUMWA JAMANI - NILILAZWA, BUT NOW IM GUD
Sijawatupa, tena niliwamisi vibaya mno wapenzi wangu, but nilikuwa mgonjwa, vidonda vya tumbo vinanisumbua sana, nililazwa pale Dar Group, but now namshukuru Mungu niko safi kabisa, na ninaendelea vizuri, Im back dears.


kwenye ward yetu tulikuwa wawili, nikapata na shost humo humo, kitoto hiki kinaitwa Rachel au Nyambura, kilitokea kunipenda sana, hadi kulala kikawa kinataka kulala na mimi hakimtaki mama yake, nikichomwa sindano nikikunja uso, kinaanza kulia chenyewe, huku kinanipapasa,


kwakuwa chakula kilikuwa hakikai tumboni basi, nilipopata nafuu nilikuwa nasikia njaa hadi miguuni, nilikunywa juice kama maji, coz ndio iliyokuwepo kwa kipindi hicho, jamani vidonda vinatesa lo! halafu vinatokeaga gafla tu jamani,


at the end of the day, nilipata discharge na kumuacha shost wangu hospitali, wakati natoka mtoto alinililia sana, mama yake akaniomba nimsubiri ambembeleze alale ndio niondoke, yeye shost alikuwa ana malaria, hata hivyo ni kajasiri sana, yani kalijikaza kweli, basi nilimbembeleza mwenyewe, hadi akalala kabisa ndio nikaondoka, nashukuru Mungu after two days mama yake akaniambia nao wameruhusiwa,

all in all narudisha sifa na utukufu na shukrani za pekee kwa Mungu wangu, kwa kunitetea na kunipa nguvu, uponyaji na afya,Sunday, June 13, 2010

HAPPY BIRTHDAY TO MEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!


Nimeongeza mwaka jamani, nimekua, tunafurahia kuufikia utu uzima, namshukuru sana Mungu, kwa kuniongezea mwaka mwingine tena!
also many thanks to my Mom, Coz bila yeye mimi nisingekuwa hapa nilipo, amenipa malezi yapasayo hadi sasa nami naitwa mama kama yeye na nina familia yangu sasa, hakika misingi yake imara aliyoijenga alipokuwa ananilea, ndio hiyo imesimama hadi sasa, nafurahi kuwa na mama kama huyu! Mungu akubariki mama yangu, wewe ndiwe nguzo ya maisha yangu, zaidi ya mama wewe ni rafiki na mshauri wanguDad too, thanks for your support to mother, umetusomesha, umetuongoza, umetufundisha maisha, umetusaidia kwa mengi, kwa niaba ya watoto wako woooote watano, nawawakirisha kwa kusema MUNGU AWABARIKI WAZAZI WETU!

mwingine ni dada yangu (mama Godluv) Joy, coz ndie alieniandalia this small function, but ilinoga kusema ukweli, nilikata keki, nilikula, nikaimbiwa, we! raha jamani, mwenyewe nilikuwa sina hata mpango, lakini akasema no! ill do it 4 you, '' be under blesses of God dada! wengine ni wanangu, japo siku ya party walinitoroka, walienda kusimamia birthday ingine ya rafiki yao,nawapenda sana wanangu, coz wao ndio wanaonipa heshima ya kuitwa mama, wao ndio wananifanya niwe na furaha every minute


Pia namshukuru Mume wangu, thanks baba ''T'', coz yeye ndie alikuwa wa kwanza kuniwish happy birthday, na ameninunulia gift nzuri ambazo wala sikuwa nimetegemea kwa sasa, ameninunulia handbag nyekundu, kigauni chekundu na Belt lake, na viatu vyekundu, we! nimenoga kama nini? asante sweet heart!
namuomba Mungu, anipe afya njema, amani, furaha, abariki kila ninachokifanya,
AMEN!

Friday, June 11, 2010

NIMEMFUMANIA MCHUMBA WANGU, AMETUBU NA ANATAKA TUFUNGE NDOA, NIKUBALI?

Watanzania wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu,

Katika maisha yangu yote hadi sasa nina miaka 24, sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine, zaidi ya huyu mchumba wangu nilie nae, nampenda kuliko kitu chochote

Tumeanza urafiki wetu nikiwa na miaka 21 ila mchumba wangu amebadirika sana, alisema atanioa, amejitambulisha na kwetu, lakini gafla, ameahirisha, anasema kwa sasa mambo yamekuwa mengi sana, na hata maongezi yake si ya kawaida, yani anaongea as if amekasirika, sasa ile hali mimi siipendi, kila nikijaribu kupeleleza ili nijuwe labda nimemkosea, sipati jawabu lolote,


Baada ya kuchunguza sana, nikagundua anatembea na secretary wao, na ninasikia tu kwa watu kuwa anataka kumchumbia, nimelia sana na moyo wangu wala hautaki kuamini hili, nilishawahi taka kunywa vidonge nife, dada alinikuta, na kunisema sana, lakini bado akili haijakaa sawa,

Mwezi uliopita rafiki wa mchumba wangu, alikuja yeye na dada yake, wakaomba kuongea na mimi, I thought kwamba wametumwa na Rick (mchumba wangu), kumbe walikuja kwa mengine,

Kilichomleta ni kwamba, anataka kunioa yeye, anadai alikuwa akiichunguza tabia yangu toka siku nyingi na kudai kuwa mchumba wangu si mwaminifu, lakini kwakuwa hatujafunga ndoa, basi yeye anataka kunioa, na dada yake ni mtumzima amethibitisha hilo, mimi nilikataa kata kata, nikawafukuza kwa hasira,

Nilimpigia sim mchumba wangu kumwambia, alichukia sana, akachukuwa company yake, wakalewa wakaenda kumpiga, walimpiga sana, Yule kaka alinitumia sms hii, ‘’ iko siku utanikumbuka’’ dada, sikuamini siku ambayo nilitoka safari, na kupitiliza kwa mchumba wangu nikamkuta na yule secretary wao, nilikwenda moja kwamoja kwakuwa sikumpata kwenye simu kumjulisha kuwa nakwenda. Na ni wiki ile ile ambayo rafiki yake alipigwa,

Toka siku ile moyo wangu umekufa ganzi nilimchukia gafla na nikaona siwezi kuishi bila yeye. alipoitwa na baadhi ya jamaa zangu, alisema kuwa nibahati mbaya tu shetani alimpitia! Ila Bado ananipenda, na anataka anitolee mahari kabisa ili tufunge ndoa, lakini dada yangu ananikatalia maana ndie alienilea toka mdogo. Sasa nishaurini mdogo wenu nifanyaje? Sijielewi, nimsamehe, au nimkubali Yule rafiki yake


Friday, June 4, 2010

WATOTO WA MUME WANGU, WANATAKA NIACHWE, MAMA YAO ARUDIWE

Nilikuwa na uhusiano na baba mmoja huku kondoa ambae ni mtu mzima sana kwangu, lakini kwakuwa mapenzi hayachagui umri, basi tulipendana sana, na nilipomuuliza kwa umri ule alionao aniweke wazi kama ameoa, alisema walishaachana na mkewe, ila anawatoto watatu mabinti wakubwa wawili wa umri kama wangu, na wakiume mmoja.

alinipeleka kwao mwanza, akanitambulisha kwao, na ni kweli kwamba waliachana na mkewe, basi tukaanza maisha ya pamoja, yeye ni mfanya biashara! Na mm nina grocery yangu. baada ya miaka miwili nikajaliwa kupata mtoto wa kiume, nilimwambia tumeshachunguzana vya kutosha, sasa tufunge ndoa tuishi kiharari, akakubali, wakati tuko kwenye maandalizi ya ndoa alipigiwa simu huko kwao, kwamba watoto wake wanataka kuja, mimi sikuwa na hofu yeyote, nilimkubalia waje tu!

Violet, toka hao watoto wamefika, ndani hatuna amani hata kidogo, tunaishi kama mtu na wake wenzie, mimi kawaida huwa sipendi kuongea ongea lakini watoto hawa wamefanya niongee, Ugomvi kila siku, na kuna siku nilikuwa nafua nguo zangu, mtoto wa mume wangu wa kiume anamiaka 27, akatoa nguo zake zote mimi nifue, nilikataa kwakweli, ukizingatia hakuwa mgonjwa kusema anahitaji msaada, wale wa kike hawataki kufanya kazi yeyote ile, kukicha tu, sitting room kuangalia CD, kupika nipike mimi, au msichana wangu wa kazi wao wanataka kula tu, mbaya zaidi wanasema umemng’oa mama yetu nawewe jiandae tutakutoa, wakati mimi nilikuta wameshaachana kabisa. Na hapa tunapokaa ni nyumba yangu mimi. Baba yao kanikuta nayo

Kingine Hawampendi mwanangu kabisa, kuna siku nilirudi toka kazini, nikakuta mtoto kavimba mdomo wote, hawezi kuongea, nikamuuliza mschana, imekuwaje, akasema Regina (mtoto wa mwsho)wa mume wangu alimsukuma toka mlangoni hadi chini, akaangukia tofali, mdomo ukachanika kwa chini, nililia sana, nilichukia, nikawafata walikuwa chumbani kwao, alichonijibu akasema mwanao mjeuri, nilimuuliza wewe binti mkubwa miaka 24 utagombana na mtoto wa miaka mine kweli? wakati naongea nao walinirukia walinipiga sana,

Wakat yanatokea haya mume angu alikuwa safari, nilimpigia simu aliporudi nikamueleza, aliwasema sana, ila mimi nilimwambia hawa watoto wameshakuwa wakubwa, miaka 24 na 27 na huyo mkubwa 30. Wajitegemee, kwanini wakae kwangu ? nilimshauri awape mtaji wakafanye biashara, watoto walichukuwa pesa, na kuondoka hawakuondoka, na wamesema hawatoki pale, hadi mimi niondoke aje mama yao, sina amani wala raha hata kidogo, nisaidieni mwenzenu.

Tuesday, June 1, 2010

MUMEO NI MLEVI SANA? NA AKIRUDI TU ANAFIKIA KUKUTWANGA? JARIBU DAWA HII INAWEZA KUMSAIDIA

Nimepata rafiki mpya wadau, kama mjuavyo, wanawake tukikutana tu! Basi katika maongezi yetu lazima tufikie sehemu ya kuongelea waume zetu, iwe kwa mazuri au mabaya, lazima tuwaongelee tu! Basi jana akawa ananieleza matatizo ya mumewe, na jinsi alivyofanya hadi mumewe kuamua kutulia, nikamuomba niitoe ktk blog ili iwasaidie na wengine, amekubali. Na ndio naawapa kama ifuatavyo.

Mm nilimpenda sana mume wangu, kupita maelezo, na tangu anioe sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya ndoa,Ila alibadirika gafla sana, akawa na Company ya ajabu ajabu, akachukia hadi watoto wake,

Halipi ada ya shule, mm hanipendi hata kidogo, nimelia sanasana sana. Nimeshtaki kila mahali, hadi nikaona kama Mungu hanipendi vile, Akirudi ni usiku sana, amelewa chakari, akifika tu mimi naanza kulia kabla sijapigwa, labda atanihurumia, alkini wapi, nikifungua mlango tu! Ninae, yani ananipiga bila hata sababu

Siku moja nilichukuwa picha za harusi yangu, nikazitazama, machozi yalinitoka sana, nililia sana, nikapata wazo ambalo hata sijui ni Mungu alinipa au ni akili zangu tu, Ilikuwa siku ya juma mosi, niliamua kwenda salon, nikawaambie wanipambe mimi ni bibi harusi ila kuvaa nitavalia nyumbani, basi walikubali, wakanipamba vizuri sana, na usoni wakaniremba, nilipendeza kupita siku yangu ya harusi,

Nikarudi nyumbani nikachukuwa shera langu, nikalivaa, na kila kitu, na viatu nikashika na ua langu, nikakaa chumbani kitandani, kusema kweli nilikumbuka mbali sana, nililia sana huku nikiwa na ua langu, ni mwanaume niliempenda kwa moyo wangu woote,

Aliporudi akafungua mlango, akaingia ndani, kapitiliza hadi chumbani huku akitukana, basi kufika tu pale, alipigwa na butwaa sana, na pombe zilimwisha, akaniuliza wewe nani? Nikamwambia mimi ni mke wako? Najaribu kufanya kama bado sijaolewa vile, ni kama ndio najiandaa kwenda kanisani kukabidhiwa mume wangu,  maana haya unayonifanyia si ya mume kumfanyia mke, nahisi kama sikuwa nimeolewa, (nililia kwa uchungu sana)
Mume wangu alipiga magoti huku analia nayeye, akasema mke wangu naomba unisamehe, wewe umeolewa, na mimi nimke wako, nisamehe mke wangu , alilia sana, basi hapo hapo nami nikamuleza ninavyojisikia, nini nataka anifanyie ili nijihisi niko kwenye ndoa, nina mume,

Nashukuru alinielewa, toka siku ile hadi sasa tuna raha, kipigo kimekoma, mikwaruzano iliyopo sasa hivi ni ile ya kawaida tu, ambayo huisha bila hata kipigo.(kiukweli jana wakati ananisimulia, nilisisimkwa, na hivi nina machozi ya promotion, we! Yakaanza kulenga lenga, ni akili ya aina yake jamani, amewaza sana, nimependa na nyie wapendwa mjifunze kitu kupitia hili, hata kama hutovaa shela kama yeye, unaweza kutumia njia ingine tu itakayomvuta karibu yako, )