Friday, July 29, 2011

VINYWELEO VIMEJAA MIGUUNI – NIVITOE NA NINI? VINAHARIBU MIGUU YANGU


Wapenzi, mnisamehe kwa kuwatupa kwa muda mrefu kidogo, jamani niko busy kupita kiasi, nimebanwa sana kazini, chuoni , na kuna issue nyingine nafanya inanikeep busy sana, ikikamilika hiyo issue ya tatu nitawajulisha wadau wangu, but tupo pamoja sana, 

Kuna mtu ameniomba ushauri jinsi ya kuondoa vinyweleo katika miguu yake, sasa je kwa wale ambao mnafahamu  njia za kutoa hivyo vinyweleo ni nini? 
atumie wembe, uzi, veet , au hairuhusiwi kuvitoa au kuna njia zingine tena za kutumia??


Jamani vinyweleo vinakera, vinaharibu uzuri wa miguu yetu kabisa yani, unakuta mguu mweupe halafu vinyweleo vimejazanaaaaaa vyeusi,  wala hainogi,  naamini kwa kumsaidia alieuliza, na wengine watapata msaada piaSaturday, July 16, 2011

NINA MIAKA 48 NATAKA NIISHI NA MTU MZIMA MWENZANGU, JE NITAWEZA KUSHIKA MIMBA??


Dada Beauty touch in Dar, napenda nikupongeze kwa blog yako nzuri sana, mungu akubariki maana inatusaidia sana,

Mimi ni mama mtu mzima tu! Nina watoto wakubwa, ila sikubahatika kupata elimu ya darasani, sasa hivi nina miaka 48 na nimeacha kuona siku zangu, huu ni mwaka wa sita na niliacha kuona nikiwa na miaka na 42, sasa nauliza hivi, je? Ninaweza kupata mimba?

Maana zamani nilitumia njia mbali mbali za kuzuia mimba, sasa nilipoachana na mzazi mwenzangu nikaamua kuachana  na hizo njia za kuzuia mimba, kwakuwa nilianza maisha ya kuishi peke yangu.

Lakini sasa nimepata mtu mzima mwenzangu na tunataka kuishi pamoja, je naweza kupata mimba wakati siku zangu sizioni? Mimi na mwenzangu wote hatutaki mtoto, maana kila mmoja ana watoto wake tena wakubwa ,
Naombeni ushauri wenu  jamani,Monday, July 4, 2011

NIMEPIMA NIMEAMBIWA NINA UKIMWI?? NDOTO ZANGU ZIMEPOTEA GAFLA NAHISI KAMA NIMESHAKUFA,

Habari yako dada Violet, tafadhali usinitaje jina langu, wala email yangu, nimepewa blog yako na mtu, nahisi naweza kusaidiwa shida yangu
Nilipitiliza siku zangu hivi karibuni nilipata ujauzito,  kwa bahati mbaya ulikuwa nje ya kizazi, kusema ukweli sijaolewa, ila kuna mtu nilikuwa na musiano nae, na ni mwanaume wangu wa kwanza, kwa sasa nina miaka 22,
Ninaishi na wazazi  wangu walezi, maana mama alifariki wakati ananizaa, baba amefariki mwaka jana, sasa nina wazazi wangu wa ubatizo ndio walinichukuwa ili kunisaidia,  basi baada ya mimba kuwa nje ya kizazi nilipelekwa hsptl nikahudumiwa, nilikuwa na maumivu makali sana, na nilikuwa sijielewi kabisa, baada ya hapo nilianza kuumwa sana, siku moja mama alinipeleka  hsptl, wakapima vipimo vyote, na aliwaambiwa wanipime hadi ukimwi bila mimi kujua,

Baada ya kurudi nyumbani mama akaniambia nimeathirika, dada violet, naandika huku nalia, maana ni wiki mbili sasa tangu nitambuwe hivyo, najiona nimeshakonda, nahisi nimeshakufa, ila ninahema,  nifanye nini? Mbona sina matumaini tena, au nijiuwe? Au niende nikakae wapi??  Ina maana ndoto zangu ndio basi tena?? Ina maana sitafanya mambo yangu ya msingi yote??? Au ndio nimeshakufa mimi?? mbona mimi bado mdogo sana, ndio kwanza naanza kuyajua maisha, kwanini nakufa mapema hivi??
 
Nilikutana na yule kaka kwenye harusi moja tulikuwa maids, akanitaka kimapenzi, nilimzungusha kama miezi hivi, badae nikasema namimi nijaribu, ndio tukawa wapenzi, sikujuwa kama naenda kufa, sikujua hata kidogo dada violet, nifanyaje sasa?  Nimelia hadi nimechoka na machozi hayatoki tena, nimeanza kuvimba miguu, nywele zangu zote nimekata , najihisi kama maiti inayotembea, nitafanyaje jamaani,