Monday, August 30, 2010

INAHUSU, WEWE UNASAFIRI UNAMWACHA MUMEO NA HOUSEGIRL PEKE YAKE?? SOMA HIYO, NAIMANI UTAJIFUNZA KITU!

(nimerudi rasimi wapendwa wangu, nimejaa tele,  namshukuru Mungu nimerudi salama, na niko mzigoni kama kawa,  mikasa ni mingi kimtindo, but tutakwenda nayo taratiibu hadi tutaimaliza, niliwamiss sana,)

tuanze na mkasa wa huyu dada, maana umenigusa sana, coz mimi mwenyewe ni mama, na pia ndani ya story hii naimani unaweza pata kitu cha kukusaidia, 
soma hiyoMimi nina miaka kumi saba, nilikuja Dar kufanya kazi za ndani, nilifanya kwa mama mmoja polisi, na mumewe siijui kazi yake, ni watu wazima, hawakuwa na mtoto watotot wao wapo kenya wanasoma, isipokuwa walikuwa wakichelewa kurudi sana hasa mama, na mimi nikawa nawapikia na kufanya usafi, maana wao walikuwa busy,

Niliishi kwa miezi sita, nilipofika pale kwanza baba akaanza kunitaka kimapenzi, nilimueleza rafiki yake na mama, Yule rafiki yake akaenda kumwambia mama, nilipigwa sana siku hiyo, akaniambia mumewe hawezi kunitamani mimi ni mchafu sana na wala silingani nae ila nataka kumdharirisha tu mumewe,

Nikasema basi sitasema lolote, hali iliendelea vilevile, na Yule baba hakukoma kunifatilia, kuna kipindi Yule mama alisafiri alienda course, kusema ukweli Yule baba aliendelea kunifatilia sana, ilifika siku nikashawishika, nikamkubali, maana aliniahidi vitu vingi sana, baada ya kuishi hivyo kwa muda wa miezi mitatu, Yule mama alirudi, na rafiki yake  ambae ni jirani yetu akamwambia kuwa mimi natembea na mumewe, alinipiga sana na kunifukuza usiku,

Nilirudi Singida nikiwa teyari mjamzito, baada ya mama kugundua alifunga safari tukaja hadi kwa huyu baba, alituzuia na kusema nikutane nae mahali, alitufata, mama akamwamueleza hali halisi, Yule baba akatupa masharti, akasema kama nikienda kwake mkewe akijua tu! Basi hatanihudumia chochote, ila nikitulia, basi atanihudumia kwa siri,

Tukakubari kurudi Singida akanipa na laki moja ya kutumia akaninunulia na simu ili tuwe tunawasiliana ila alinipa masharit ya muda wa kumpigia, nikipata shida alikuwa ananisaidia sana hadi nilipojifungua ndio huduma zikasitishwa, tukimtafuta kwenye simu hatumpati, tukaja dar tena na mtoto akiwa na mwaka mmoja na miezi mitatu, tukaenda hadi kwake, tukaambiwa alishahama,

Nipo nyumbani hadi sasa, sina mbele wala nyuma na hata sijui nitampata wapi, maana wanasema alihamia Zanzibar na mkewe, sasa hata nikienda nitaanzia wapi na sijawahi kufika huko?

Kwa kifupi maisha yangu ni ya shida sana, mama amekuwa kipofu aliumwa macho hadi yakapofuka, haoni, baba alikwisha kufa, nimebakia mimi, ndio kila kitu. Mama ananitegemea mimi, na wadogo zangu wananiangalia mimi. namtaka huyu baba ili amsaidie mtoto maana anahali ngumu, siku zingine analala njaa, siku nikipata ndio anakula(( violet, huyu dada nimeona nitumie blog yako kumsadia, naomba kama inawezekana nikupe picha ya huyo baba, ili uirushe, ajione, aje amuone mtoto wake, anateseka sana, hata asipomchukuwa alete tu matunzo, please violet))

Tuesday, August 24, 2010

RAMADHAN KAREEM WADAU

Nilikuwa na Likizo mbili:-
1 Masomo/Mitihani
2 Pia likizo yangu ya kawaida kwa kila mfanyakazi
Sasa inakaribia ukingoni kabisa, nitarudi FULL.