Monday, March 28, 2011

NIMECHOKA SANA, TUNAISHI KAMA MAADUI, HAKUNA MWENYE AMANI NA MWENZIE, NIFANYAJE

Jamani maisha yangu ya ndoa yamenishinda, adui yangu wa kwanza sasa hivi ni mume wangu,  hatuna amani, kitu kidogo tu anaweza kukukasirikia hata wiki nzima, haongei wala kushirikiana na wewe chohote, watoto wako boarding so nyumbani tuna house girl tu, unakuta hata kama nipo, hanitumi mimi anamwagiza housegirl wangu, hapa nilipo nawaza kumtimua, lakini kazi kwangu ni nyingi, namimi sina muda wa kufanya kazi zooote,

Yeye anabibi nje, naamini hivyo maana hata siku tukibahatisha kufanya mapenzi,  na unakuta tumekaa hata wiki mbili bila kugusana, siku tukikutana, anaweza nifanya mimi nikapiz hata mara tano, yeye akawa bado na kama akija kupiz basi ni kidogo sana, tofauti na mwanzo, tukikaa siku nne tu, akiweka ni dk 3 anapiz na anapizi za ukweli haswa, sasa huyo bibi yake wa nje ndio anipe tabu ndani??? 

Kwanini anipige pige hovyo??? kwanini ujinga wake asiufanyie nje na akarudi ndani na heshima?Kitu kidogo makofi, ananiaibisha kwa majirani zangu, dharau ndio usisem
Nisaidieni, au nikae nae mbali sana iwe kama rikizo kwetu, baada ya muda nirudi atakuwa amejirekebisha? Ah! Nimechoka jamani, nimechoka sana na huyu mwanaumeWednesday, March 23, 2011

NIMEZIJUA TABIA CHAFU ANAZOFANYA MUME WANGU- NIMEUMIASANA, SASA KUNA WATU BADO WANANIITA ILI WAKANIPE HABARI ZAKE ZINGINE- NIENDE AU NISIENDE??? USHAURI PLEASE

 
Naombeni ushauri please,
 kuna baadhi ya tabia  chafu za mume wangu ambazo sikuzijua before,  au sijui kwakuwa nilikuwa simchunguzi sana, sasa nimegundua baadhi ya tabia chafu anazofanya, nimelia sana na nimeumia vya kutosha kias kwamba huwa nawaza hata kumuua yeye na mimi mwenyewe nijiuwe, lakini nikiwaza watoto, moyo unaniuma kupita maelezo. Naumia sana, lakini kuondoka siwezi, na bado nampenda sana isitoshe nimezaa nae, nampenda sana.

Huwa najaribu kumuonya mimi kama mimi, na sometimes nimeshawafahamisha ndugu zake, wamemuonya, lakini sioni mabadiliko,
la kwanza,  kinachoniumiza zaidi ni kwamba, hataki kuonekana kama ana mke. Hivyo huwaambia wanawake zake kuwa sijaoa, wala sijazaa, utakuta hadi usiku tumekaa nae, wanamtumia sms za mapenzi, ukicomplain anakuuliza hiyo sms ina ubaya gani.  (hivi jamani, mtu asiempenzi wako anaweza kukuuliza- sweet umekula nini usiku huu, I wish ningekuwa karibu nawe)hii ni sms ya kawaida kweli?

Pili anapenda sana kusifia wanawake wa nje, kwenye website na sehemu zingine, mimi naumia sana, moyo unauma, hadi nimeamua kutaka ushauri, naelekea pabaya, NAMPENDA SANA, SANA TU! Nahisi siwezi kuishi bila yeye, kweli kabisa, nampenda mume wangu. Nahisi anajua ndio maana ananitesa namna hii.

Sasa nimepigiwa simu na mtu ambae mimi nayeye wote tunamfahamu, akaniuliza unayajua anayoyafanya mumeo? Njoo nikueleze, mimi nakupenda, na uthibitisho ninao. Sasa mimi najijuwa hali yangu, nahisi naweza kufa,
Roho moja inashauri nisiende, nyingine inasema niende nikayajuwe, bado nashindana na sauti hizi ndani ya moyo wangu. Pia najiuliza kama nikienda na nikayajua  je kifua cha kustahimili ninacho??? SINA, lakini mbona nataka kuyajua anayofanya?????

MAPENZI YANATESA JAMANI, YASIKIE KWA MWENZIO TU USIOMBE YAKUKUTE WEWE. NIMECHANGANYIKIWA NIFANYAJE MIMI, PLEASE NAOMBA USHAURI NAONA GIZA TU, Maana huwa nikipata habari zake akili zote huhama, kama ni kazi nitavuruga toka asubuhi hadi jioni, naweza hata kula nisile, nina mwaka wa sita kwenye ndoa yangu, tena ya kanisani. ah! some times naona bora hata nisingezaliwa.


Monday, March 21, 2011

NIKIMWAMBIA NIKAMTAMBULISHE KWETU ANASEMA NIMWACHE KWANZA- NIFANYAJE

mambo dada v mimi kijana mwenye miaka 22 nnamchumba wangu ambae nampenda sana, chaajabu anasikiliza sana maneno ya watu,

na pia kila nikimwambia kwenda kwetu nikamtambulishe analeta sababu mi nashindwa kumuelewa kabisa na nnampenda sana jamani

tuna mwaka mmoja na miezi sita sasa na kila nikimwambia kwenda home ana jibu ucjali home tutaenda lakini kuna mambo nakamilisha na ukijaribu kufatilia mambo anayosema anayakamilisha hakuna lamaana  hata moja yani jamani mi cmuelewi kabisaaaaaaaaa, hebu jamani dada angu nisaidie nimueleweje huyu mtu?Friday, March 18, 2011

ANASEMA NIACHE KAZI - NA KAMA SITAKI BASI TUACHANE NAE- HELP ME PLEASE


Habari yako Violet, mimi huwa ni mpitaji mzuri kwenye blogu yako, japo huwa sichangii kutokana na ubusy nilionao . lakini leo yamenikuta naomba msaada wa mawazo,

Mimi ni muhasibu Company moja hivi ya clearing and forwading hapa Dar es salaam,  nimeolewa na mfanya biashara , ndoa yetu ya kiislamu ilifanyika mwaka jana  mwanzoni na tunamtoto mmoja wa kiume,

Mume wangu alinikuta nafanya kazi, sasa baada ya kujifungua mkwe wangu (mama yake ) aliniletea housegirl, nikawa namwachia mtoto, siku moja baba yake akaniambia yeye hataki mwanae alelewe na housegirl, nikamwambia mbona namuacha mtoto katika hali nzuri na nikirudi jioni huwa namuhudumia vizuri, akakataa,

Nikawa naenda kazini kwa kuforce, kuna siku asubuhi mimi naoga, akachukuwa nguo zangu nilizoaandaa akazificha pamoja na pochi yenye pesa zangu , nikamuuliza akasema hataki nifanye kazi, tukazozana sana, hata kazini sikwenda

Sasa nisaidieni wapendwa nimepewa mwezi huu tu! Nikishapokea mshahara niache kazi, anadai atakuwa ananilipa hiyo hela kila mwezi kama haiwezekani basi nirudi kwetu nimuache mwanae

KINACHONIUMA
1.   Mimi ndie msaada nyumbani kwetu, wazazi wangu wananitegemea mimi katika baadhi ya mambo
2.   Nikikaa nyumbani nitasahau ujuzi wangu, kwa wale maacountant wanaelewa namaanisha nini
3.   Kazini kuna posho nyingi, not only that lakini pia tunapata huduma ya hospitali mimi na familia yangu, so baadhi ya gharama zinapungua,
Nisaidieni mwenzenu, kazi naitaka na mume namtaka

Monday, March 14, 2011

HAPPY BIRTHDAY MY LOVELY TWINS - FIVE YEARS NOW

 alieshinda alipewa zawadi ya saa ya mkononi lo! tracy aliwapa watoto wakike
Tymon nae akawapa watoto wa kiume, was fun kwakweli
tracy nae alitembea kimiss.
A happy day kwa kweli, nilikuwa na furah ya pekee,

A HAPPY FAMILY
Friends pia walitupa gift
michezo mbali mbali ilikuwepo,
kalikuwa kasherehe kadogo tu! but was fun kwakweli, tulifurahi kupita kiasi, 
NAWATAKIA MAISHA MEME NA MAREFU WATOTO WANGU

MUME KANIZUIA URAFIKI NA MKEWE- CHA AJABU MKEWE ANANIPENDA NA NAMUHURUMIA KUMTENGA, NISHAURINI JAMANI


Dears, hii ni ndefu kidogo, hata hivyo nimejaribu kuiedit ili isitupe uvivu kusoma, lakini itakuwa na fundisho ndani yake, hebu tumshauri mwanamke mwenzetu maana mh!! soma mwenyeweMimi ni mama nimejenga, naishi kwangu na mume wangu na watoto watatu, Juzi juzi hapa kahamia mama mmoja hivi, alipofika mimi ndio nilimpokea, ni jirani yangu kabisa, basi tukatokea kuelewana sana, 

Ila kwa kumuangalia tu! Utagundua ni msemaji semaji sana, lakini mimi naweza kuishi na watu wa hivyo so sikuona tabu kuzoweana nae, mumewe hatuna mazowea, na kwanza si tabia nzuri kumzowea mume wa mtu, ila huwa tukionana mara moja moja mtaani au barabarani, husalimia tu! Inshort ni watu tunaoheshimiana sana

Sasa wiki iliyopita weekend nilikuwa natoka, ile natoka nje tu! Nikakutana na huyo mama (jirani yangu) getini, akanambia nimekuja kupiga story, nikamwambia mie natoka, akasema nikusindikize maana nyumbani niko mchov sana nikiwa pekeyangu, nikamwambia, umeaga kwa mumeo? Akasema ngoja nimusms, maana yuko uwanjani kwenye mpiria nikipiga hatutaelewana,
Baada ya muda akaniambia ameruhusiwa kwenda,

basi akaunga tela safari ikaanza, mishale ya saa 2:30 usiku tukarudi, nikamshusha kwake, nami nikaingia kwangu, ile nafika tu hata sijakoga geti likagongwa, kutoka namkuta Yule jirani yangu na mumewe, keshadundwa na macho yote yamekuwa mekundu sana kwa kulia.
Mumewe akaniambia shem mimi nakusheshimu sana, akaniambia nataka uniambie ulimpeleka wapi mke wangu, nikawambia ha! Si huyu hapo muulize tulikuwa wapi?

Akasema nimekuuliza wewe, aliongea kwa ukali hadi alinichefua  ananiliza as if ni mtoto wake, nami nikaja juu, nikamwambia bwana, haya wewe na mkeo wote out, mko kwangu leteni heshima, kama kwenu hamuheshimiani wala kuaminiana basi nikwenu, naomba mtoke nje sasa hivi, ikabidi awe mpole,

Akaniambia naomba niambie, nikamuleza ukweli wote kwamba kuna shemeji yangu huko tegeta alipata ajali, ndio nilikuwa nakwenda kumuona, akaniambia kwanini uliondoka na mke wangu bila ruhusa yangu, nikamwambia wa kuomba ruhusa ni mkeo sio mimi, na alikuomba na ukamkubalia,

Akamuuliza eti uliniomba ruhusa mimi? Kabla hajajibu akalambwa vibao mbele yangu, nikasema jamani, kwani nyie mnaishije??? Yule baba akaniambia hivi,

NAPENDA UENDELEE KUHESHIMIKA , NAOMBA ACHA URAFIKI NA MKE WANGU, HUYU MIMI NDIO NAMJUA, TABIA ZAKE HUZIWEZI, NAOMBA ACHA- UKIENDELEZA URAFIKI NAE YATAKAYOKUJA KUKUPATA USINIHUSISHE,

Akamgeukia mkewe na kumuwasha vibao kadhaa mbele yangu na akamvuta kuelekea nje
Kinachonitatiza, huyu dada haishi kuja kwangu, yani nikiwepo tu! Basi anakuja, nilimwambia bwana, hebu tulia kwako wewe, akasema mume wangu namjua mimi, wala usisikilize maneno yake, yani  ametokea kunipenda sana huyu binti (maana nimemzidi umri kidogo)

Sasa nifanyaje maana huyu mkewe nishamwambia mara kibao bwana wewe mumeo hataki uongee na mimi kaa tulia kwako, lakini hakomi na wala haachi, sometimes huwa najificha kabisa akija namwamiba mschana wangu mwambieni hayupo, hivi ninavyokwambia Violet hata jana alikuwepo kwangu. Nisaidieni,

Sunday, March 6, 2011

ANAFANYA UMALAYA HADHARANI BILA HATA KUNIOGOPA-NIMFANYAJE AACHENisaidieni mwenzenu jamani, nina watoto wawili, miaka 6 na miaka 4, wote wanasoma.

sikuhizi mume wangu amebadilika sana, kiasi kwamba hata ada za watoto wake hatoi, hadi tugombane sana ndio anatoa ada, mapenzi pia yamekwisha, anafanya mambo ya aibu hadharani huku watu wakiona,

Kuna siku moja alikuwa na wanawake bar, amewanunulia pombe, huku wanamshika shika, dada mmoja akiwa pale bar ananifahamu akanipigia simu niende nikamuone, nikaenda nikajionea, wanamnyonya, wanamshikashika sana, ndio maana akirudi nyumbani anakuwa hana hamu na mimi,

basi siku hiyo nilipata ujasiri nikamfata pale pale, nikawambia jamani, tafuteni nyumba ya wageni, msitie aibu hapa, wale wadada walikimbia, mume wangu nae akaanza kunikimbiza nipige huku kashika chupa mkononi, 

nikajificha mahali, nilipoona amerudi bar, nikarudi nyumbani nikachukuwa nguo nikaondoka, nikakaa kwetu mwezi mzima, badae akaja kuomba msamaha, nikarudi, sasa ujinga ule umeanza tena, anaweza hata kunitukana mbele ya watoto wangu, naumia sana
Mimi sina kazi, nikiondoka tu hata watoto hatawasomesha tena, sasa nifanyaje jamani, niliwahi kufungua biashara ya salon, akanifanyia fujo na kunifanya nifunge, hataki nifanye chochote kile,

Naomba ushauri please, sijielewi kabisa, ukizingatia mtaa mzima wameshajua tabia yake, naona hata aibu kutoka ndani