Monday, February 8, 2010

MUME WANGU HANA HAMU NA MIMI- SIMUELEWI

nahitaji msaada wenu jamani
mume wangu hana hamu namimi kabisa, nakuwa nashindwa kumuelewa kabisa, yani huwa najitahidi sana kuwa karibu nae, huwa naonyesha kabisa kuwa namuhitaji na sio kunyesha tu! bali huwa namuhitaji toka moyoni kikweli kabisa, lakini mwenzangu huwa haonyeshi kabisa kama yuko namimi, mara nyingi sana imetokea hii, na kabla hatujafunga ndoa hakuwa hivi, kilichozidi sana ni pombe anazo kunywa, alikuwa akinywa toka zamani, lakini hivi karibuni amekuwa mlevi wa kupindukia, akirudi nyumbani ni kuanzia saa tano usiku, napo amelewa sana, 
 
alishawahi kupata ajali shauri ya ulevi, aliumia sana, Lakini Mungu alimsadia akapona ,alilpunguza kidogo kunywa pombe, baada ya muda akarudi kule kule, mbaya zaidi akaanza kunifundisha na mimi, mimi sikupenda kabisa maana sikuona wala kuhisi utamu, nikaacha wala sikuendelea kujifunza,
unakuta akirudi kama hajalewa sana basi anakuwa busy na shughuri zake zingine tu, ataangalia Tv hadi usiku sana, au ataanza kucheza game, yani hana hamu na mimi kabisa,
sikuwahi kusikia kuwa labda ana mwanamke mwingine, ila kwa jinsi alivyo sasa naanza kuhisi hivyo, ila nahisi vitu viwili, kama sio mwanamke mwingine, basi nahisi ni pombe anazokunywa.
kuna siku aliporudi nilimwambia kuwa namuhitaji, maana tulikuwa teyari tumefika wiki tatu bila kufanya kitu chcohote kile, siku hiyo aliwahi kurudi kwakuwa nilimdanganya mtoto wetu anaumwa, akarudi saa mbili, alipokuta mtoto mzima nilimuita chumani nikamwambia shida yangu, nikamueleza kwanini ananitesa hivi,
akauliza kwani nakupiga, au sikupi hela ya kula? nikamwambia hata kuwa mbali na wewe ni mateso kwangu,
akanifokea sana kwanini nimesingizia mtoto anaumwa na kunipa baadhi ya mifano kwamba inaweza kutokea kweli akaumwa, niliomba msamaha na kumwambia sitarudia tena ila kwa usiku huo anipe haki yangu, nilikuwa nikimuitaji sana, cha ajabu wala hakujali hisia zangu, ndio kwanza akapanda kitandani tena siku hiyo hakuoga wala kula, akalala, nikamwambia nimekuandalia chakula kizuri akasema anajisikia kuumwa nimuache apumzike, nilisononeka sana, kesho yake nikamdamsha ili twende hospitali akasema atanda mwenyewe, imefika usiku karudi kalewa sana, namuuliza kama alienda hospitali akasema alikunywa panadol akapona kabisa, sasa mimi sielewi jamani,
hali hii inanitesa sana mimi, niliwahi kumuita best man wetu na aliongea nae namimi nikiwepo, akatubu na kuahidi kubadilika, basi siku mshenga alipoondoka niliinjoy sana, kwani nilipata kile nilichokuwa nakihitaji kwa nafasi, niliona kama nimepelekwa mahali pazuri sana, nilijua hali ile itaendelea,
baada ya wiki kama mbili kupita, ikarudia pale pale, yani kumkuta nyumbani, hadi uweke apoint ment, hadi weekend yeye ni safari tu! hajui kanisa wala msikiti, tangu tutoke kushukuru kanisani ni baada ya harusi hakwenda tena, siku ya ubatizo wa mtoto alikwenda tena baada ya kumsema sana maana alisema yeye hatoenda, since that day, hajaenda hadi leo.

Dada violet, ananipa wakati mgumu sana mume wangu, kujali familia yake anatujali sana, tunakula, anampenda mtoto sana, hanipigi, ila hivi vitendo ambavyo anafanya simuelewi? je pombe imemaliza hamu yake??? kuna mwanaume kweli ambae ni kamili akaacha kumpa haki mkewe kwa takribani wiki tatu? nimempekuwa na kumpeleleza sana labda ana mwanamke mwingine, anasema hana, sasa mbona hanitamani??mbona haonyeshi kama anahamu namimi, mimi ni mzuri, najijuwa kabisa hilo halina ubishi, nimeridhika na mungu alivyoniumba. ninajiheshimu sana.
ananifanya nitamani sana ndoa za wenzangu, ananifanya nitamani hata kuwa na mwanaume mwingine ambae atautambua uthamani wangu, lakini naogopa sana, maana maradhi ni mengi, pia namuogopa sana Mungu,
unakuta hadi napoteza hamu yakula. na siku nikibahatika kula nae basi huwa nakula hadi najishangaa, nafurahi siku nzima, ila ujuwe siku akishinda nyumani anaumwa.hii imekuwa too much maana hata wazazi wake wakija anakuwa hivyo hivyo kunasiku alikuja mama yake mzazi kutusalimia, nikafurahi nikajua siku hiyo atawahi kurudi, lakini alirudi saa 6 na kukuta mama amekwisha lala, nilimsema sana, akalala bila hata kuoga, asubuhi akataka kutoka bila hata kumsalimia mama, nikafata nikamuuliza huyu ni mama yako mzazi au wa kukulea tu! akajitetea eti anaogopa kumsumbua nimuache alale, nikamvuta hadi kwa mama yake ndio kwa aibu akaenda kumsalimia, nilimuweka mama wazi,juu ya hali ile, mama alichukia sana alimsubiri hadi aliporudi na alimsema sana, akamwambia kama ananiona kero aniache nirudi kwetu asinifanye mlinzi, maana alikuwa hataki hata nifanye kazi anataka nikae nyumbani tu!
kama kawaida yake, aliomba msamaha tena, tukaka siku mbili hali ikarudi pale pele, nikitafuta mtu mwanaume mwingine nitakuwa nimekosea sana, sasa nifanyaje jamani?
ushauri wenu ni wamuhimu sana kwangu

15 comments:

 1. mh!pole sana kwa matatizo unayoyapata, ni bora mtu akunyime hata pesa asikunyime penzi pindi unapolihitaji, maana hapo mtu anaweza hata kuamua maamuzi yasiyo sahaihi,huyo mumeo anahitaji maombi tu! au anakufanyia makusudi kwakuwa ameshajuwa unampenda sana,, sikushauri kuwa na mtu mwingine, maana yake waaminifu ni wachache, wanaume wetu siku hizi vicheche kama nini, utakufa na ukimwi bure, wewe vumilia tu mpendwa wangu, usichoke kusema nae, huyo ni wwako, hilo ni jipu lako, tembea nalo wweeeee, hangaika naloweeeeee itafikia kipindi litapasuka tu
  pole sana

  ReplyDelete
 2. MPEGE CHINI HUYO, HAFAI WALA NINI.
  MAISHA YENYEWE HAYA MAFUPI.

  ReplyDelete
 3. Hi dada pole na matatizo kitu cha kwanza kabla ya yote hebu mkabidhi bwana shida yako unajua kwa mungu hakuna lisilowezekana, Yaani zama kwa yesu kwa kumaanisha kabisa, kabisa, mwambie mungu naomba uondoe kiu ya pombe kwa mume wangu na kitu chochote kile kinachomfanya mpaka asiwe na hamu na wewe, Mungu hashindwi na jambo lolote lile mpendwa wangu, hakuna dawa wala mganga, mganga ni yesu, vyakula hali na maji ya kunywa je ombea hayo maji yawe damu ya yesu akinywa yakate kiu ya aina yeyote ile mwilini mwake, haswa ulevi na ufahamu wake ufunguke. Ukiamini na ukifanya kwa kumaanisha utamshanga mungu.ikibidi kufunga pia funga hata kwa wiki mara mbili mwambie mungu nataka kukuona kwa mume wangu, huo ni ubavu wako mwambie mungu nataka mume wangu abadilike,Soma zaburi hizi ya 91: 9-13.Soma zaburi 31:1-24. soma zaburi:30 10-12 soma isaya 54:1-17 ukiomba kwa kusimamia neno usikubali shetani acheze ndoa yake mpenzi na kuiba amani yako mwambie mungu najua hushindwi kumbadilisha mume wangu. usimpe shetani nafasi mwambie shetani umeshindwa na hauna mamlaka na mume wangu kiu ya pombe sasa ni mwisho.

  Mama Dear

  ReplyDelete
 4. sio wewe peke yako, mie mume wangu sijui ana nini, tikifanya kile kitendo tu! hata sekunde haifiki anakuwa amesha maliza na amelegea sana, hawezi kufanya kwa mara ya pili, sasa bora wewe unaekosa kabisa, kuliko mimi ambae naonjeshwa kisha napokonywa, yani yeye akiingia tu! hazipiti hata dakika mbili, hapo mimi sijafika kokote yeye anamwaga, na akimaliza usingizi hadi anakoroma, hata umfanye nini hastuki ng'o na wala haoni kama shida,
  yani ninashida kama nini mwenzio

  ReplyDelete
 5. poleni
  wanawake wenzangu, waombeeni tu! watabadilika
  MAMA LILI

  ReplyDelete
 6. mh! atakuwa na mwanamke huy, wewe kaa tu ndani endelea kupika na kupakua akuletee ukimwi.

  ReplyDelete
 7. Huyo kaka mwenye kumtesa hivyo mke wake hafai kabisa. Ila pia tunajadili kesi kwa kusikia upande mmoja. na mtu huvutia kamba kwake. Ni wachache sana huzungumza kweli iliyopo ili kupata uhauri sahihi. Lazima kuna kitu ambacho ni chanzo cha huyo jamaa. Sio kirahisi tu mtu awe hivyo. Inawezekana kuna jambo ambalo mwanamke hataki kuliacha na anajua kuwa mume linamkela sana. So mwanaume kaamua na yeye kuwa na style yake ingawa ni mbaya, kwa yeye anaona ni nzuri tu kutokana na maumivu aliyoyapata kwa mke. Mtu uliyekuwa unampenda huwezi fikia hivyo bila sababu yoyote ile. Watu tuwe wakweli tunapowasilisha mada kwa huyu dada na kuzipost hapa. Achani kujionesha mnateseka wakati ninyi wenyewe mnaleta mateso ndani. Aaaa tabia hizi si nzuri.

  ReplyDelete
 8. mm sikushauri kuachana nae,
  kwanini uachane nae wakati ni mume wako huyo????
  usimuache, wewe muombee, kama ni mkristo, fungua biblia kwenye hiyo mistari aliyokupa mama dear, soma kwa kumaanisha,
  MWANAMKE MPUMBAVU HUBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE, usikubali kuwa mpumbavu,
  usifate ushauri wa huyo anesema UMPIGE CHINI,
  ili iweje? usikute yeye hata kuolewa hajaolewa,
  ndoa tamu rafiki yangu asikwambie mtu! japo milima milima ipo, lakini pambana tu! wala usimuache mume wako
  huyo ni wako umetoka ubavuni mwake

  ReplyDelete
 9. NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOOOOOTE,
  sasa nyie mnaomshauri amuache mume wake mnapingana na maagizo ya Mungu
  MIKOSI IWE JUU YENU WOTE MNAOSHAUR HIVYO

  ReplyDelete
 10. bwana we hebu achana nae, ndoa ndoa, siku hizi nako kuna ndoa???
  kimbia bwana kwanini ujitese hivyo???

  ReplyDelete
 11. MAMA DEAR UMEOKOKA NINI?
  Mistari uliyompa huyo dada nimeisoma hata mimi
  imenifariji sana,
  asante mama Dear,
  pia nikushauri dada mlengwa,
  usimuache mume wako

  ReplyDelete
 12. mi nakuashauri muombe mungu, ila lazima kutakuwa na chanzo, haiwezekani mtu from no where akaanza hayo mambo. mi nimetafiti sana nimegundua wanawake tuna matatizo sana, hasa ukishaolewa, sasa hapo tumekusikiliza wewe, mmeo akisema aseme yake utakuta mambo mazito. hakuna jinsi simama na maombi mungu atafanya njia. alichokiunganisha mungu mwanadamu hawezi kukitengua. simama mama na yesu. ukisema utoke nje uatakutana na balaa lingine. ndoa hizi mungu azisimamie sana. mana mh

  ReplyDelete
 13. Mama Dear nimeokoka nampenda yesu sana amenitoa mbali mno mno mpaka hapa nilipo kama si yesu sijui ningekuwa wapi Nimeokoka kwa kumaanisha. Mume wangu ananiita mchungaji. Mume wangu hajaokoka ila hanywi pombe hanizui kwenda kwenye mikutano ya injili maadamu naangalia familia vizuri na kujali na yeye kama My first bony, Usisikilize ushauri wa wanakwambia uachane na mumeo Ndoa iheshimiwe na watu wote na pia kumbukeni maneno ya siku ulipofungishwa ndoa padre alisema alichokiunganisha mungu mwanadamu asikitenganishe.usivunje ndoa hayo ni mapito tuu huwezi kuwa Testimony bila kupitia Test
  Mama Dear

  ReplyDelete
 14. Jamani kweli hata mimi nina hilo tatizo kumbe tuko wengi ila naomba Mungu nikiamini iko siku atabadilika tu. Maana kila siku anasema amechoka wewe bora hata ni wiki tatu mimi hata miezi inaisha hata hana mda na mimi. Ukizingatia tuna mtoto mmoja tu anakaribia miaka minne. Nitapataje mwingine mtu hana mda na mimi ukimuuliza anakwambia nina mawazo. Yani kero tupu ila I DO BELEAVE HE WILL CHANGE HIS BEHAVIOUR. ila sina mpango wa kumuacha. MWENYE SHIDA KAMA HIZI SISI TUENDELEE KUNG'ANG'ANA NA YESU TU.

  ReplyDelete
 15. Mpendwa asikudanganye mtu,jitafutie mtu wa kukukeep busy. Hapo ulipo tayari una msongo wa mawazo na usipoangalia na vingine vinafuata!! Pia jitahidi kujikwatua hata kama waenda dukani na ukirudi kiatu kivulie mlangoni ili akiridi ajiulize kulikoni? Pia kuanzia sasa usimwonyeshe kama unakasirika na hivyo vitendo vyake maana wanaume wanapenda attention na hilo unalolifanya ndo starehe yake hivyo hataacha kukutocha.Cha msingi,akirudi ndo kwaanza upo busy na msg hata kama ni kwa shosti wako na tabasamu juu mwenyewe atatia akili.Uigombane nae wala kuwa mjeuri,sauti ya ukarimu mkubwa ila tu usimpe attention yoyote.Mm hili lishawahi kunitokea nikapewa ushauri na rafiki yangu,hivi sasa mume wangu ananionea wivu ni balaa na hawezi kutoka jioni bila mm unless ni vikao vya kazi. Pia tafuta movie ya CHEATER'S CLUB uiangalie utaona mambo hayoo! Pole sana dia

  ReplyDelete