Monday, November 19, 2012

ANATAFUTA MUME..... ALIE SERIOUS KUOA AITIKE ASEME HAPA

Habari dada. 

Mimi ni mdada wa miaka 35 nimependa kukuandikia ujumbe ili unisaidie kuuweka kwenye blog yako ili yule atakayekuwa tayari kua mume wangu tuwasiliane na mimi.   Nimefikia kuandika ujumbe huu sababu nimeona kuna baadhi ya walioandika wamefanikiwa. kwa ufupi mimi nina mtoto mmoja na ningependa mume nitakayekuwa naye hata kama akiwa na mtoto nitamkubali na kumpokea mtoto. Awe anafanya kazi au biashara ya maana. awe anamcha Mungu. awe mwenye kujali familia.Asiyevuta sigara.  Yeyote atakayekuwa tayari awasiliana na mimi kwenye email yangu hii.

email ya huyu dada siiweki hapa, maana nanjua kuna mtakaoamua kumsumbua dada wa watu, wewe kama uko serios, niinbox mimi, halafu mimi nitamforwadia huyo dada email yako.


Saturday, November 3, 2012

MPENZI WANGU ALINIACHA, AKAAMUA KUISHI NA MWANAMKE MWINGINE, SASA ANAOMBA NISAMEHE TURUDIANE, NAOMBENI USHAURI


mambo vai
mm ni msichana mwenye umri wa miaka 28, cjaolewa ila nimebahatika kupata mtoto mmoja ambaye tangu amezaliwa ckuwahi kuishi na baba yake na kumlea inshort, tulishaachana

Baadae nilibahatika kumpata kijana mwingine ambaye tulipendana sana Nilijisikia furaha sana kuwa nae matokeo yake bila mm kujua kumbe alikuwa na mahusiano mengine na mwanamke ambaye alimpa ujauzito na baadae kujifungua ambapo mm nilipokuja kujua na niliumia sana, ckuumia kwa sbb ya yy kupata mtoto niliumia kwa sbb alinificha hakuwa mkweli kwangu.
 
Siku tuliyokutana alinipokea vzuri na kuomba msamaha sana kwa sbb aligundua kuwa amenikatisha tamaa na ckuwa najisikia vzuri, katika mazungumzo yetu nikamuuliza swali moja tu una mpango gani ss na huyo dada, akanijib hawezi ishi nae ktk maisha yake,jibu lake lilinipa amani tukarudiana,.

kadri siku zilivyozid kwenda nikaona anaanza kubadilika nikimpigia hapokei, msg hajib kumbe yule dada alishahamia kwake nilipojarib kumuuliza akasema ndio kwani ni dhambi yy kukaa na mwanae ? niliumia sana nikasema ngoja niachane nae na siitaji kuwasiliana nae awe free na familia yake

 juzi nimebadili cm ambayo naitumia nikaona ananzaa kunisumbua na kuomba msamaha kuwa anataka kuendelea na mm, na c mara moja kwa kuhesabu ni zaidi hata ya mara ishirini anaomba msamaha, nimekuwa cimuelewi kwa sbb kama anaishi na mtu iweje aendelee kuomba msamaha na anasubutu kusema hawezi kbs kuishi bila mm kwa yale niliyomfanyia na nilivyokuwa namjali na kumyenyekea, ameona mm ni mwanamke ambaye alikuwa naniitaji ktk maisha yake, naomba ushauri hv huyu kijana anamaanisha au ni msanii tu, ingawa bado nampenda ila nimekuwa muoga sana