Wednesday, September 29, 2010

MUME WANGU AMENIACHA, NA SASA ANATAKA KUMUOA BEST FRIEND WANGU TENA KWA NDOA YA KANISANI- NIFANYAJE?

Mashost wamechachamaa jamani na waume za watu, kuweni makini nao, haya mambo ya shemeji yako huyu!, chukuwa namba yake hii!  sijui leo tunatoka twende utupe company, mh! shauri yenu,
soma hii ya huyu dada! imenigusa sana
(ni ndefu mno, but nimejitahidi kuedit na kubakisha points tu!)
Habari yako dada,


Nimepewa jina la blog hii na Arafa, anasema mlisoma nae, nahitaji sana msaada wako dada yangu, mimi nilikuwa na kijana mmoja tuliependana kupita maelezo tulikutana chuo cha ufundi, mimi nilikuwa nasoma kozi ingine na yeye ingine, baada ya kumaliza akaamua kunichukuwa na kuishi na mimi, tumeishi nae kwa muda wa miaka mitatu kama mke na mume japo mwenzangu umri wake umeenda kidogo,  tumefanikiwa kujenga nyumba mbili, baa mbili, yani hatukuwa na maisha ya shida, na nimezaanae mtoto mmoja,

Niliwahi mtambulisha rafiki yangu kwa mume wangu, hadi sasa naandika ujumbe huu ni miezi mitano nimetengana na mume wangu, alinifukuza kwake, nikamuuliza kosa langu ni nini? Akasema eti dini hazifanani yeye mkristo na mimi muislam, nikamuuliza sababu ni hiyo tu?? Hukuliona hili tokea mwanzo hadi kunichukuwa na kunizalisha? badae Nikakubali mimi kubadili dini ili niendelee kuwa nae, sikufichi violet huyu ndie mwanaume wangu wa kwanza tangu nizaliwe, wazazi walinikatalia kubadili dini, lakini mimi kama mimi nilikuwa teyari, nilijihisi kumkosa huyu ni kama kupoteza uhai wangu,

Sasa nimeshangaa kusikia baada ya yeye kuniacha, wazazi wangu waliniita kijijini kwetu, nikakaa huko miezi miitatu, siku moja akanitumia sms kuwa nimlete mwanae,(anamtaka) nikaona afadhali, ndio njia ya mimi kurudi kwake, nilikubali na kuja  tena dar, wazazi waliniambia nisifikie kwakwe niende kwa ant yangu ,  alinifata huko na kusema anamtaka mwanae ampleke mwanae machame (akalelewe na wazazi wake) pia bila aibu wala uoga, akatuambia anataka kuoa.,  hata ant yangu hakuwa akijua hili,

kumuuliza sana akasema anamuoa best friend wangu, na harusi ni mwezi wa kumi kati kati, vikao vimeshaanza. Mwenzenu natamani nijiuwe kabisa, najiona nina mkosi sana, kwanini rafiki yangu anifanyie hivyo? Kwanini itokee kwangu? Kwanini mimi tu? Amechachamaa anamtaka mwanae, sasa mimi nitabaki na nini? Kuna siku nilishika vidonge nimeze nife tu! But nikamuangalia baby wangu alikuwa amelala, nilimuhurumia sana nikaacha, but mawazo ya kujiua bado yananiandama sana jamani nisaidieni, naweza kuivuruga ndoa yao? Lakini kwa haki ipi niliyo nayo? Msaada wenu tafadhali siwezi kula wala kufanya chochote,

nina hali ngumu sana kichwani kwangu

Wednesday, September 22, 2010

NINA TATIZO LA UZAZI, MGANGA AMESEMA NIMEROGWA, MCHUNGAJI AMESEMA NIMEFUNGWA, SASA NIFATE LIPI? NISAIDIENI

Kuna kipindi niliwahi kurusha mkasa wa huyu dada, kwamba anatatizo la kutoona siku zake, na anahofia linaweza sababisha asiweze kuzaa, sasa watu walimshauri , wengine waliahidi kumsaidia, but hakuna mafanikio, hebu naomba tusome anachokisema, na ninaomba kwa mwenye uwezo wa kumshauri/kumsaidia afanye hivyo ili nae aitwe mama jamani, kuitwa mama  kuna raha yake! tena ni sifa. tumsaidie mwenzetu!
 

Hello Dada Violeth,

Natumaini wewe ni mzima wa afya pamoja na familia, nadhani utakumbuka kuwa nilishawahi kuja kuomba msaada kwako na kupost tatizo langu na watu pia walichangia na kupata mawazo tofauti tofauti.

Inshort sijafanikiwa mpk sasa ila nataka kukujulisha yaliyojiri katika tatizo langu hili nililonalo mpk sasa na nimepata mawazo mengi sana.. Nikianza na yule aliyesema atanitumia dawa ni muongo nilijaribu kufanya mawasiliano na yeye na nikampa na anuani yangu lkn hakuna kitu matokeo yake aliingia mitini.

Dada Violeth nimejaribu kwenda hospital mbalimbali kujaribu kwa mara nyingine nilienda kwa Kairuki, Muhimbili, Sinza pale MICO kwa madaktari bingwa wa akina mama, Aga Khan bila ya mafanikio nikipewa dawa natumia na nitapata kwa mwezi mmoja lkn kwa miezi inayofuata hakuna kitu mpk madokta huwa wanabaki kunishangaa coz nikipiga ultra sound hakuna tatizo lolote linaloonekana. Basi ikabidi nijaribu tiba mbadala...

Nikaenda kwa mama mmoja anakaa Tanga aliniangalia akasema haya ni mambo ya kishirikina kwamba kuna mtu tena jirani yangu alichukua unyayo wangu na kunifunga.... Mmh ilinipa wakati mgumu sana kuamini nikapewa dawa za miti shamba na nikanywa kwa wiki kadhaa lkn mama yangu akanishauri nijaribu kwenda kanisani kumwomba mungu nilienda kwa mama yangu kitunda na nikaenda kumwona mchungaji.

Nilimuelezea mchungaji A - Z kuhusu maisha yangu tangu utoto wangu na sikumficha kitu basi nikaombewa pale na mchungaji akaniambia atafunga kwa ajili mpk aonyeshwe matatizo yangu na mwenyezi mungu. Kusema ukweli nami nikaamini hivyi wiki lililofuata nikaenda kanisani kama kawaida mwisho wa misa mchungaji akniita na kuniambia ameoteshwa kuhusu mimi kuwa kuna mtu amechungua nguo zangu na kwenda kutundika kwenye mti mkavu usiotoa maji wala majani( kwa maana mti usiozalisha) sio siri nipo njia panda hata sielewi pa kuanzia.

sielewi  chakufanya nizidi kumwomba mungu au nianze mambo ya kiswahili.... Nipo njia panda.

Ni mimi mdogo wako,


Thursday, September 16, 2010

MUME WANGU ANAWACHUKIA SANA WATOTO WETUHabari wadau wote kwa ujumla,
Mimi nina shida moja ambayo pia hata sielewi imetokea wapi, maana zamani haikuwepo kabisa,

Mume wanguAmekuwa ni mtu mwenye hasira kila akirudi nyumbani, sijui kama na kazini kwake huwa yupo hivyo,Hanywi pombe, na kipindi cha nyuma alikuwa ni mstaarabu sana, Mungu ametujalia kuwa na watoto wawili waliopishana kidogo, lakin baba huyu amekuwa akiwachukia sana, hadi watoto wamejua kama wanachukiwa, yani akirudi watoto hata kama walikuwa wanacheza wanakaa kama wamemwagiwa maji, nikijaribu kumuuliza ni ugomvi, anasema acheke cheke amekuwa mgonjwa wa akili?, yani ana majibu ya karaha sana, hadi tunaona bora awe anakaa kazini muda woote
Hata kutoka nao siku hizi hafanyi kama alivyokuwa akifanya zamani, kwa mwezi mara mbili, anawapeleka beach, au sehemu nzuri nzur za kupumzika, lakini siku hizi, mh! Hataki hata umgusie suala hilo, sasa mimi linanishangaza sana, na pia naona kabisa linavyotesa watoto, hivi violet, ni hii ni hali ya kawaida kweli? Yani mzazi mzima ukachukie watoto wako mwenyewe? Maana ile ni damu yake,

Nishaurini kwa wale yaliyowatokea kama mimi, au hata kama mna idea zozote mnishauri ili nijuwe cha kufanya kitakachorudisha furaha ya zamani
Wednesday, September 8, 2010

HONGERENI KWA KUMALIZA MFUNGO SALAMAKutokula mwezi mzima sio masihara we!, hongerni mwaya, na nawatakia maandalizi mema ya Eid!

NAHISI RAFIKI YANGU ANATEMBEA NA MUME WANGU - NIFANYAJE
 Habari za mapumziko Violet,
mimi ni imeolewa na nina mtoto mmoja wa kike, lakini sina furaha ya ndoa kama ilivyokuwa zamani, mume wangu ni mtu wa ugomvi sana, kitu kidogo tu! Anakibeba kinakuwa kikubwa, chuki zake kwangu hadi kwa mtoto wetu, basi nilijaribu kumuhadithia rafiki yangu mmoja, na nikamwambia kuwa ikiwezekana akaongee nae mume wangu maana naona wanaelewana, (nilitumia heshima)

Basi sikumoja nilimualika rafiki yangu aje mahali tukutane, nikamuomba ampigie sim mume wangu ili nae aje, nilimwambia atumie  namba yake maana imefika kipindi nikimpigia kwa namba yangu hapokei, basi nikampa rafiki yangu ampigie,

Alipokuja akanikuta namimi nipo alichukia na kuondoka, violet, hadi sasa sijui nilichokosea, but yeye amekuwa ni mlevi sana, akirudi wakati mwingine huwa analala na viatu na nguo kama alivyokuja hadi asubuhi, kuna baadhi ya siku huwa ananyea hadi chupi zake, ukimsema tu! Inakuwa ugomvi,

Rafiki yangu aliahidi kuongea nae, kweli baada ya siku tatu akampigia simu wakakutana kwenda kuongea, nilimwamini sana rafiki yangu na sikuhisi kama angenichukulia mume wangu, baada ya hapo rafiki yangu nae akaana kuonyesha kiburi kwangu, hanijali, wala kushauriana nami akawa hataki tena

Sasa siku moja rafiki wa mume wangu ndio akaniambia, shemeji chunguza mwenendo wa mumeo na rafiki yako nahisi si mzuri, nikamwambia sawa shemeji, ssasa kuna siku moja nikiwa naipekuwa simu ya mume wangu, nikakuta picha ya huyo rafiki yangu kwenye simu ya mume wangu, tena inaonyesha wamepiga bar, usiku, maana kulikuwa na chupa za bia, naogopa hata kuuliza,  maana kauli zake sasa hivi ni ''kama umechoka fungasha nenda kwenu, kwani ndoa kitu gani'' yani inshort hataki discusion za family

nishaurini nifanye nini?