Tuesday, May 31, 2011

NISAIDIENI JAMANI, MAMA MKWE WANGU AKIJA TU! AMANI NDANI INATOWEKA-NATAMANI HATA KUACHIKANisaidieni mwenzenu, niliolewa miaka 5 iliyiopita, ila mama mkwe wangu hakunipenda toka mwanzo, kwakuwa alikuwa ameshamuandalia mwanae mke wa kuoa, lakini mwanae akaforce kunioa mimi kwakuwa tulipenda sana, 

Sasa toka nimeolewa, mama hanipendi mimi wala kizazi changu, yani anachukia wanangu kiasi kwamba akifika watoto wananywea kabisa, na hawataki hata kulala nae, nilijaribu sana kujiweka karibu nae, lakini wapi!

Some times huwa anasusa hata kula,  anaweza  akashinda hata njaa, sasa mimi hali hii sijazowea, natamani kupatana na mkwe wangu kama ambavyo wengine wanapatana nao, lakini huyu wangu aliwahi kunitamkia kabisa kuwa sitakuja kukupenda mpaka nakufa,
Nilimueleza mume wangu, akasema wewe si unajua tatizo mama hakupendi toka mwanzo? ila mimi nakupenda sana, wewe tulia,  muache tu! Akae akichoka ataondoka, 
sasa nishaurini wapendwa, maisha  haya yananipa ugumu sana maana niko nyumbani muda mwingi, nashinda nae, nakosa raha kabisa, mara anitangaze nimemroga mwanae, wakati hata mganga simjui, mara mimi mchawi ndio maana mwanae haoni, wala haelewi, tena maneno haya anatamka kwa housegirl wangu, sasa kweli ni halali hii? na akija anakaa mwezi mzima, 

mwenyewe anadai amekuja kupumzika, lakini mbona hapumziki ila analeta matatizo tu! Nifanyaje??? Akifika tu! Amani ndani inatoweka. Sometimes huwa nahisi labda yeye ndio ana mambo ya kishirikina, maana kuna siku mwanae (mr wangu) alimlazimisha kulala na mwanangu wa kike ana umri wa miaka 4, 

mtoto usiku alilia sana, nilipoenda  kumchukuwa mama akawa mkali, cha ajabu hata kumbembeleza hambembelezi, anasema mmezowea kudekeza watoto, akilia tu mnambeba ukiangali ni usiku wa manane,  ilibidi nimchukuwe mtoto, nilivyomfikisha kwangu tu! Akalala, wakati siku zote huwa analala kule chumbani kwao pamoja na housegirl na wala hasumbuhi

Hali hii isikie kwa mwenzio tu! Ikikukuta unaweza kutamani hata kuacha mume ambae unampenda, nishaurini jamani

Monday, May 30, 2011

NIMERUDI DEARS- THIS TIME KIPAPER KIMENITESA KIDOGO LO!Wapendwa wangu, im back, mambo kama kawaida  sasa,  Maswali, ushauri hapa ndio mahala pake , ndio wakati muafaka kabisa, maana kidogo akili imetulia baada ya kumaliza mitihani yangu, ya 1st semester.
Karibuni sana

Monday, May 16, 2011

SITAMANI KUSHIRIKI TENDO LA NDOA- LAKINI NAHOFIA MUME WANGU ANAWEZA KUTOKA NJE?


habari yako violet, kwanza nakupongeza sana kwa kuwa na blog ambayo inatusaidia sana , mungu akubariki
mimi nina shida moja, ni miezi karibu sita sasa, nimechukia sana tendo la ndoa, sitamani hata kidogo, ila kwakuwa nimeolewa, inanibidi tu! kulifanya, sasa unakuta napata maumivu makali sana baada ya kumaliza tendo, naumia sana maeneo ya sehemu za juu,nafikiri ni kwakufanya pakiwa pakavu, 

zamani nilikuwa nikitoa ute sana, Nilikuwa nikishikwa tu! Nalowanisha hadi kitanda,  lakini siku hizi inabidi akitaka kuingiza apake mate kwanza,  yani hata nikijiforce kusikia raha, bado sisikii raha, sanasana naumia tu, na tunatumia muda mwingi tu! kuwekana sawa, lakini kwangu wapi
 
sasa hali hii nifanyaje iishe, nahisi mume wangu anaweza kuibiwa, na ninampenda, sijui sababu ni nini?? ni ugonjwa au ni hali ya kawaida inatoke, hali hii inatesa sana jamani, kiasi kwamba akitaka kunifanya tu! nahisi tumbo linaniuma, na jasho linatoka kabisa,