Tuesday, May 11, 2010

NINAISHI KWA KAKA YANGU, ILA SINA FURAHA HATA KIDOGO SABABU YA WIFI


Dada violet habari za kazi?Nashukuru sana kwa blog yako maana tunapata ushauri wa
kutujenga sisi wanajamii.
Mimi ni Mischana mwenye umri wa miaka 26 nipo Tabora.Mkasa wangu ni kwamba naishi na kaka yangu pamoja na wifi yangu.Kaka yangu ana uwezo mzuri tu na amejenga nyumba kubwa na nzuri.

Sasa dada violet pale kwa kaka tunaishi na mdogo wake wifi yangu wa kike na tunalingana kiumri. Kwa sababu sis ni wasichana tunakaa chumba kimoja ila cha ajabu Yule huyu mdogo wake wifi yangu nafanyiwa vitimbi vya ajabu ajabu sana ambavyo sijui vinatokea wapi, ananichukia kupita kiasi.

Yani hataki kabisa kuniona pale, wakati yeye ni kwa dada yake na mimi ni kwa kaka yangu, hanipendi hata kidogo. Akiona nimevaa vizuri ananiangalia vibaya ila mimi sijui hili wala lile.na ameanza kutengeneza chuki kwa wote tunaoishi nao pale ndani mradi wanichukie tu, hata msichana wa kazi amemwambia asiniheshimu asiongee na mimi na kunisema mengi sana kwa msichana huyo ambayo yananichafua mimi.

Nikiwa nyumbani huwa siku nzima ananuna na haongei na mimi anaweka nyimbo za taarabu tu, mafumbo mafumbo mengi sana. Na tunaweza kuwa chumbani hakuna anaeongea na mwenzake.

Jamani nimechoka niliwahi kumwambia kaka nataka kutoka nikapange akasema bado sina uwezo wa kujitegemea na ananipenda sana. Kugombanisha ndoa ya watu sitaki na nawaza nikiondoka kwa nguvu kaka hatanisaidia tena ataona nimemdharau.

Dada zangu/Ndugu zangu naombeni ushauri wa wenu wapenzi wangu.Dada Violet naomba usinibanie ili nipate mawazo kutoka kwa wadau wenzangu. Hii blog nilipewa na rafiki yangu na namshukuru sana maana inanifundisha mengi. Dada nina huzuni moyoni hadi basi sina raha hata kidogo.



 

6 comments:

  1. pole sana mdogo wangu,lakini pia nikwambie kuwa katika maisha huwezi kupendwa na watu wote, hata kama utaamua kuhama hOME kwa bro, bado utakakoenda si porini, utaishi na watu na lazima wawepo watakaokuchukia tu! so kinachokiwa hapa ni kumuignore tu huyo mwenzio,
    wote nyie wapita njia pale, ungekuwa unachukiwa nawifi mwenyewe mwenye mume, ingekuwa issue ingine, lakini anaekuchukia ni mpitaji kama wewe, kila mtu atapata kwake, wala asikusumbuwe kichwa kabisa huyo,
    pia nikuulize, umeshawahi kumueleza wifi yako na kaka yako kuhusu hili tatizo?
    kama bado hebu fanya hivyo, waeleze na wao pia
    kuchukiana wasichana kwa wasichana mbona ni kitu cha kawaida sana, dawa yake kujifanya kama kipofu + kiziwi, wewe dharau, waswahili wanapenda kusema kuwa mbwa ukimjua jina wala hakupi tabu, halafu kwa umri wako wewe una uwezo kabisa wa kukaa peke yako, wala si mtoto wewe, labda uwe huna kibarua cha kufanya kitakachokusaidia, lakini kama una kazi na unajua unachokifanya, basi kwa miaka 26 una uwezo wa kukaa mwenyewe na kupiga maisha. but kama kaka hataki uondoke, basi mwambie the way unavyopata tabu hapo, naimani atakusaida kabisa

    pia kumbuka kumuomba Mungu akupe amani,
    UBINADAMU KAZI MDOGO WANGU

    ReplyDelete
  2. kwanza nianze na wewe violet, wewe unachagua mikasa ya kushauri?? mbona mikasa mingine hushauri? haya bwana.
    Umenifurahisha sana mimi, ETI MBWA UKIMJUWA JINA WALA HAKUPI SHIDA, hahahahahah,
    Ww dada unaetaka ushauri, nakushauri hivi, chiki za nini wakati nyie wote WAJA? kama akikupigia taarabu, wewe anza kucheza na kuiimba kama unaijua, yani kama alivyosema dada violet kwamba wewe umdharau tu,
    kama vipi hapa nyumbani kwa kaka yako bwana, wewe mkubwa, hama bwana kaka akuachie ukajifunze maisha, umri huo bado unalelewa tu!, kama una kazi bora uondoke,

    ReplyDelete
  3. Sikia nkwambie dada mtu mkweli siku zote ndo mzuri umeelewa....mimi huwa siezi vumilia mambo kama hayo.....lazima ntareact...nkiona yamezidi....yeye hapo kwa dada yake....wewe hapo kwa kaka yako sasa kila mtu hapo sio kwa mama yakke mzazi NKWAMBIE MWITE HUYO MSICHANA MWAMBIE....hivi wewe shida yako nini....nimekukosea nini....unataka nini....eeh....atakacho kujibu....ndo kitadetermine mbele kutakuwaje?kama atadundwa au yataisha kwa amani.....yani unamkawiza nini jitu lina wivu.usio na maana...mbaya zaidi unakaa nae chumba kimoja...atakuwekea sumu huyo shauri lako..MUULIZE BIBI WE WALA USIOGOPE...MANA ATAKUHARIBIA HADI KWA KAA YAKO MWENZANGU....AKUONE HUNA MAANA KUMBE HILO WIFI TEN AWIFI MANATI....NDO MCHOKOZI....MPE LIVE....MWAMBIE AM WATCHIN U...TKE CARE....

    ReplyDelete
  4. chapa vibao huyo hafai hata kwa kurumagia,
    au anamtaka shemeji yake nini??
    hovyo???
    mkiulizana nyie kama nyie, mtaishia kugombana zaidi, kama alivyosema dada violet, washirikisheni wenye nyumba wenu, kila mtu atoe duku duku lake,
    tena nikwambie eee, siku ya kikao kaanae huyo wifi mwehu karibu, akileta upumbafu pale pale unamtandika kibao mbele ya dada yake, atakuheshimu hadi mwisho,
    mijitu mingine sijui ikoje

    ReplyDelete
  5. wala usija mdogo wangu umweleze kaka yako wakiwa pamoja na wifi yako mkae chini mzungumze kwa nini akujime raha msicha mwenzako kwa amekuwa mke mwenza? usijali yataisha tu kilicho na mwanzo hakikosi kuwa na mwisho huyo ni bwege tu hajatembea akaona dunia take care

    ReplyDelete
  6. yaelekea kwao wana maisha ya shida kupita kiasi,
    kwanini akupe shida KUPE huyo,
    achana nae, wewe fatilia mambo yako, huyo bwege kama unaweza mwonyeshe kazi siku moja, mtandike vibao vya kumtia adabu, tena mwambie kabisa kwamba ukirudia ntakupa mara kumi ya hivi, atakaa sawa, pole sana, na kama alivyosema violet, wewe ukiweza muignore tu! atatulia,

    ReplyDelete