Wednesday, May 5, 2010

MUME WANGU ANANITEGEMEA KWA KILA KITU- LAKINI HAJATULIA HATA KIDOGO- NIMWACHE?

Du! jamani kuna wanawake wenzetu wanashida sana jamani, hebu soma hii, maana mimi imenisisimua sana, na imeniumiza pia, ametuma ndefu sana, nimejaribu kuedit kiasi, but soma kisha mshauri, yani nawaza kama ndio ningekuwa mimi sijui ingekuwaje, yani sipati majibu maana kichwani yanakuja mfururizo kama majibu kumi hivi but yote yana madhara at the end, inasikitisha sana
Nimeolewa, miaka mitatu iliyopita, lakini nilimkuta mume wangu anawatoto watatu, binti wa miaka 16, na  wa miaka 10 na miaka 6, mimi sikuwa na mtoto hata mmoja, mama wa watoto hawa alifariki.

Tumefunga ndoa ya kanisani, sikubahatika kuzaa mapema, ila kwa sasa ndio nina ujauzito wa miezi saba, Nilimpenda sana mume wangu,Mimi nafanya kazi nzuri tu, ila mume wangu hana kazi yeyote ile, maana alifukuzwa, hivyo nafanya dili zake tu za pembeni zinazofanya aishi hapa mjini, aliponioa alihamia kwangu, maana yeye alikuwa amepanga, mimi nimejenga, hivyo tulikubaliana aje kwangu na nilikubali aje yeye na familia yake,
 nilimtafutia biashara, mradi tu! Asiwe anakaakaa nyumbani , akafungua duka la nguo za kiume huko mjini, na bila hata uoga alimuweka girlfriend wake awe ndie msimamizi na muuzaji, yeye ndie controller wa kila kitu pale. nilipogundua niliifunga ile biashara. Toka siku ile niliapa kutomsadia lolote lile.

Ni Malaya kupita kiasi, nilishawahi kumfumania na wanawake zaidi ya watatu, kuna mwingine alimpangishia na chumba akawa anaishi nae kutwa nzima, na hivi hana kazi akawa anatoka asubuhi anaenda kushinda huko, jioni anarudi kulala kwangu, nilipogundua nililia sana violet mdogo wangu niliumia sijapata kuumia vile katika maisha yangu, nilimpokonya gari nililokuwa nimempa, nikawa simpatii hata pesa. sikuona maana ya kumjali mtu asieniheshimu, lakin kama mjuavyo mapenzi tena, nikaamua kumrudishia gari ili watu wasihis kitu kwa kuona limepaki nayeye anatembea kwa miguu.

Nashukuru Mungu watoto hawa wananiheshimu na kunipenda sana, watu wengi wanajua kuwa nimewazaa mimi mwenyewe, nami nawapenda sana, Nilimfumania kabla sijabeba hata mimba, sasa mwezi uliopita nimepigiwa simu na mwanamke mmoja akanitukana sana, isitoshe amenitishia kabisa maisha yangu, anasema ataniroga nitazaa mbuzi, na maneno mengine makali sana, yani hadi huwa najuta,

Violet, hapa nilipo mimi ndio kila kitu, najua ni ngumu sana kuamini kuwa mimi ndie ninaesomesha hadi watoto wake, nawalipia ada na kuna mmoja huyu wa kati, nimempeleka boarding namlipia mimi, huyu mkumbwa nae yuko private (secondary) nalipa mimi. huyu mdogo mimi pia nimempeleka Tusiime ( international) namllipia mimi, moyo wangu unaniuma sana, kwanini anitese hivyo? Inamaana hanithamini mimi wala wema wngu kwa wanawe?

Wale watoto ni damu yake yeye, watamsaidia yeye sio mimi? Niliahidi kuwasaidia kwa moyo wangu, maana nilipoolewa mimi nilikuta watoto wana hali ngumu sana, waliona kama wamepata mkombozi wao, Sasa yeye nikimuuliza kwanini ameshindwa kufanya hata kwa siri tu umalaya wake, mimi nisijuwe, kwanini ananidharirisha, mimi nampa heshima zote, nampa matumizi yake binafsi, namlelea watoto wake, gari namtilia mafuta, lakini anakwenda kuwapakia wanawake wengine, wanapanda kwenye gari yangu,

hana cha maana anachonijibu ninapomuuliza, yeye anasema hawajui, mimi nakataa maana nilishawahi kukuta hata sms za mapenzi, anawatambua maana kuna mambo yangu mengi ya ndani tunayopanga mimi na yeye tu chubmani, cha ajabu huyo mschana  anayafahamu, hilo ndilo linalonipa hofu, wasije wakayatumia hayo kuniumizia kiumbe changu, sasa naomba mnishauri, nifanye nini? Nimfukuze?

Moyo wangu umechoka sana jamani, moyo unaniuma sana, kwanini iwe hivi? Hali hii hata kujifungua bado, nimeanza kutishiwa eti nitazaa mnyama(mbuzi) sina hata nilichowakosea,

Ananitia aibu kwa majirani, maana mtaa mzima wameshamjuwa kuwa yeye ni malaya, cha ajabu anachukuwa visichana vya ajabu ajabu, havina kazi wala pesa, vinamtegemea yeye kwa kila kitu. vikorofi, midomo imejaa matusi, na hata elimu havina, aibu hii mimi hadi lini? inaniuma, nimekuwa nikilia kila siku!

 18 comments:

 1. pole sana tena sana mpendwa... kweli unamzigo tena mzigo wa hatari... yaani huyo kaka ana aibu jamani? yaani mwanamke anakusomeshea watoto, gari na nyumbani kwake ndio unaishi lakini bado anakufanyia hivi dada? kweli huyo hana shukrani hata kidogo, yaani huyo angekuwa na pesa kukushinda usingemuona kabisaaa, angekuwa anakujia na wanawake mpaka nyumbani, hapo tu unampa kila kitu lakini bado yuko hivyo... mimi ninachokushauri funga moyo wako, mwacheeee kabisaaa huyo mtu mana ni mtu gani huyo asiyejua wema wako... hata kama mmefunga ndoa hiyo aijalishi mradi unakazi yako nzuri, nyumba unayo, gari na pesa pia, jitegemee mwenyewe utazaa mtoto wako na utamtunza vizuri sana mana una uwezo wa kufanya hivyo... huyo anakurudisha nyuma kimaendeleo na hata kimapenzi, mfukuze huyo, basi ata kama akikuachia watoto hao watakuwa ni thawabu kwako wewe kuwasomeasha, yawezekana hata mke wake alikufa na presha aliyoisababisha yeye wakati wa kujifungu... huyo ni malaya by nature hawezi acha hata umfanye nini atakudanganya tu mpaka mwisho... atakuuwa huyo angalia ndugu yangu, ni bora ukamfukuza mapema mana anaonekana hana shukrani, kashaona unampenda sana anajua ata afanye nini hutamwacha, sasa mwache ajue umuhimu wako... funga moyo mana utakuwa ushamzoea na utammisi sana... lakini jitahidi tu.... pole sana mwenzagu yaani natamani hata nikuone niongee na wewe private lakini mwombe sana mungu atakupa nguvu zaidi... lakini mfukuze huyooo...

  ReplyDelete
 2. habari yako imenigusa sana dada, nimeskia kutetemeka, wakati naiedit nilikuwa ni kama yamenitokea mimi vile, pole mpenzi wangu,najua inauma sana
  mimi ninachokiona hapa nikwamba huyo baba hakupendi, na hafadhiriki hata kidogo, ni mwanaume gani asiekaa na kufikiri yote unayofanya kwa ajili yake? akiruka ruka huko akuletee maradhi? aisee hakufai hata kidogo
  PLEASE! USIACHE KUSOMESHA HAO WATOTO, huwezi juwa, pengine baraka zitaongezeka kwako kutokana na moyo wako kwao, pia wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa sana kuliko hata unavyohisi,
  walipie ada, ila huyo kicheche huyo, m! sijui umfanyaje, nikisema mwache nitakuwa natenganisha ndoa yenu, but if ningekuwa mimi, we! nshamwacha siku nyingi? maana sababu inajionyesha, yani wala asingenisumbua kichwa.
  kwanini niishi kwa mateso, kwanini anipe stress, maisha yenyewe haya magonjwa kibao, lo! mh! ila huyo baba nae mpana jamani ka! hadi siri za ndani anazibwaga du!pole mwaya

  ReplyDelete
 3. mtimue huyo mwanaume anakuumiza tuu atakuzeesha tuuuu..nachokushauri usiache kuwapa msaada hao watoto huwezi jua watakuja kukuangalia na wewe hapo baadae..ila huyo mwanaume hafai

  ReplyDelete
 4. Pole dada kwa yaliyo kukuta ni kweli inauma lakini napenda tu nikushauri kuwa angalia MSINGI AMA MZIZI wa mahusiano yenu mpaka mkaoana ulikua nini ndo utajua nini ufanye.

  You knw wat MAFANIKIO KTK NYANJA YOYOTE ILE HUJA KWA WALE AMBAO WANAJUA NINI WANAKITAKA NA WAKITAKA KWA MOYO WAO WOTE.

  Je kabla ya kula kiapo ulijiridhisha KWAMBA HICHO NDO ULICHOKUA UNAKITAKA au ulijidhulumu nafsi yako kwa kukubali labda ulikua DESPERATE kuolewa.....sio kwamba nakusema vibaya hapana.

  Ubajua unapokua na kiu kali na ukakosa uvumilivu usipokua makini unaweza ukanywa maji yoyote tu ilimradi maji kwa sababu umekabwa na kiu afu ukitulia ndo unawaza hee kumbe kulikua na maji ya chupa masafi, hapo ushakunywa ya mtaroni au bombani yasiyochemshwa.MAJI NI MAJI TU LAKINI SI TOTE YANAFAA KUNYWA.Hata ya Chupa kila mtu ana chaguo lake mwingine KILIMANJARO mwingine DASANI n.k n.k

  Kwa iyo me wakati mwingine huwa napenda kusema angalia MISINGI ndo utajua namna gani utatue tatizo.WANASEMA KUJUA CHANZO CHA TATIZO NI NUSU YA KULITATUA.Yawezekana ulimdekeza sana au ulikua wazi sana kwake kiasi kwamba akajua hiki ndo KISIMA CHA KUCHIMA MAFUTA.Na kama ni mwanaume asiye na tumaini basi akaona hapa ndo pa kujiweka.

  Kwa kumalizia kama umeshajikagua na ukajua ni wapi ulipokosea na bado unampenda Sali kwa Mungu wako kama ni mkristo omba rehema kwa Mungu kwamba Mungu nilifanya makosa hapa na hapa nirehemu.Mungu aonae sirini atakujazi.Other wise I wish you all the best.WENGI TUNAKOSEA LAKINI MUNGU BADO ANASAMEHE.NI WA REHEMA MNO MUNGU WETU.

  ReplyDelete
 5. MMMMMMMMMH, sijui nianzaje jamani dah,kweli fadhila mfadhili mbuzi biandamu atakuudhi jamani....kha.....Dada unathamani kubwa sana hapa duniani....ndo mana mpaka leo upo...mshukuru mungu kwa hilo....HUYO MUMEO HAKUPENDI....KABISAAAA....KAKUPENDEA PESA JAMANI.....KWANZA NAKUPONGEZA DADANGU....miaka ya leo UMLELEE MTU WATOTO WATATU......ni watuwachache sana wenye moyo huo.......MWANAUME HANA SHUKURANI JAMANI.....TENA YANI NAMLAANI.....sikia mama ACHANA NA HUYO BABA....mwambie achukue kilicho chake...ATAMBAE KABISAAAAA....mwambie watoto wake utawasomesha....coz hawezi kuwapa huduma yoyote huyo mbwaaa...ILA YEYE ATOKE ATOKE YANI ATOKE ATOKE MUUAJI HUYO...ATOKE ....kama hataki ukae na watoto wake andoke nao.....yani hivi we dada kwa nini lakini jamani eeeh KWA NINI UNATESEKA HIVYO MUNGU WANGU JAMANI DAAAH....CHUKUA HILO GARI UPAKI AU KALIFANYE TAX.....KWAKO ATOKE DADA WACHANGIAJA HAPA SIO WAJINGA WANAYOYAONGEA YATAKUKUTA KAMA UTAKAA NA HUYO BWANA HAKYAMUNGU ROHO INANIUMA KAMA NIJE NIMTOE MIMI HUYO MUME ASO SHUKURANI WALA HURUMA....basi asikuurumie wewe awahurumie hao watoto wak ewasio na kitu chochote jamani eeeh kwa nini lakin huyo baba yuko hivo......yani nachukia na hasira jamani mi sielewi yani hapap tumbo linaniumaduuuh ama kweli....mmmmh YANI ATOKE HAPO BILA HIVO UTAJUTA ZAIDI YA HAPO ULIPO FIKIA HAKYAMUNGU....JAMANI LOOOH...

  ReplyDelete
 6. wewe dada una roho ya peke yako,
  tena una roho ya paka? yani hadi sasa uko nae na unataka ushauri? da!ningekuwa Tanzania ningekutafuta nikupe gud time hata kidogo ili ufeel, but anavyofanya mshkaji wetu sio kabisa yani.

  ReplyDelete
 7. mam pole naoba uendelee kuwalea watoto jamaa mpe kibuti ucjali walimwengu watakuonaje kama anakudhalilisha mpaka mtaani hana faida ya kumlea chukua kilicho chake aende kwa hao anaoona wana mfaa. Mungu na akusaidie hutaweza kuzaa mbuzi huyo aliekupigia cm ya kukutisha na laana imrudie nae ni mwanamke ipo cku yatamkuta atajuta.. Sali ukimaanisha kwa Mungu wako utakacho kwani humjalia kila aombae kwa kadri ya mapenzi yake.. naweka novena kwa ajili yako mpenzi. kiukweli wote tutakushauri hapa viatu umevivaa unajua wapi panabana na kuumiza kwann ucvue uvae sandals upate hewa na kupunguza maumivu... pole wangu katika maana halic ya pole.

  ReplyDelete
 8. pole sana, huyo mume akufai, atakuletea maladhi we achana nae endelea na maisha yako, watoto watunze tu mungu hatakubariki kwani watoto hawana kosa lolote.

  ReplyDelete
 9. Pole sana dada kwa mkasa ulionao, ni majaribu makubwa sana hata ss wanaume anatudhalilisha labda anapepo la ngono huwezi jua,ila usiwaache hao watoto watatabika sana. Nakupa pole tena sana mno. Usilifmbie macho hebu jaribu kuwaeleza hata wazazi wake.

  ReplyDelete
 10. Hana adabu huyo ndugu yangu, nikweli hakuna mwanaume perfect, ila cha msingi heshima ndo inayohitajika hapo. Wewe achana naye na hao watoto wake wake mwache akawalee wenyewe, ukipenda msaidie tuu kwa ajili ya upendo wa hao watoto wakiwa mikononi mwake. Duh, pole sana mwenzetu.

  ReplyDelete
 11. Wema usizidi uwezo,

  samtaims siwaelewi wanawake wa namna hii, jitu halina kipato, jitu lina watoto watatu, jitu lina umalaya uliokubuhu... Mtu bado unaomba ushauri, ushauri gani kama sio ujinga kung'ang'ania ukimwi tu!!!

  ReplyDelete
 12. Pole sana dada yangu!

  Huhitaji ushahidi mwingine uliokusanya unatosha!

  Wewe ni wa thamani mno na hukumbwa usononeke maishani!

  Uamuzi uko ndani ya moyo wako! Usikilize moyo wako unakumbia nini cha kufanya!

  Alaaniwe huyo mumeo kwa mateso anayokupa na kwa kutudhalilisha akina Baba wote duniani!

  ReplyDelete
 13. Hivi ulishapima kama huyo jamaa hajakuambukiza HIV kweli?? Maana kama hauko salama halafu anakula vyako na mademu wengine ni wazi wengi mko katika hako ka-chain. Subiri ujifungue ukishakuwa sawa mmwage tu..NIna imani utapata mtu mwenye akili iliyotulia. Otherwise unaweza kuni-PM tukazungumza.....Unahitaji mapenzi wewe sio kuvurugwa vurugwa!!

  ReplyDelete
 14. Pole Sana na mkasawako. Kwa ushauri wangu lakufanya fukuzia mbali huyo gasia na wewe ukibaki na hao watoto italeta shida sana afathali uwatafute wazazi wa mume na uwakabithi kwao lakini kwaa sababu ni malaika wa mungu basi wapatie elimu lakini wasikae na wewe.

  Hiyo mimba yako baki nayo na mtunze mtoto wako mwenyewe. inaelekea uko poa sana kimshiko utapata mume mwingine atakaye kupena inavyo stahili...

  ReplyDelete
 15. Huu ndio upuuzi mwingine usiohitaji ushauri. Kwa nini abebe mzigo wa mtu ambaye ameshindwa hata kumuheshimu tu??? Huyu Bwana ni yatima? hana dada zake? hana ndugu zake? hana shangazi na wajomba zake? Mtimue na watoto wake apeleke mizigo yake inakohusika! Usijifanye Mother Theresa wa kubeba mizigo ya dume linajiweza lakini akili limeweka kwenye mguu wa tatu badala ya kichwani!! Anatutia aibu wanaume wenzake! Wee mdada, stop this sentimentality fnonsense! Mpe Rambo yake na watoto wake achape lapa akawaweke kwa hao anaowaona bora kuliko wewe!!

  ReplyDelete
 16. ukiuliza nini? ndoa????? ndoa kitu gani wewe! fukuzilia mbali malaya huyo asiye na haya wala kujua vibaya. kwanini unyanyasike, ndo kupenda sana ama? mwenzako anakula gud time tene kwa pesa yako wewe unazeeka. acha ujinga. mungu akutie nguvu katika kuwalea watoto wake, hilo malaya fukuza haraka iwezekanavyo. atakuua! m uwa nawashaangaaga sana wanawake, wanateseka ukiuliza ndoa. hiyo ndoa ndo imebeba pumzi yakoooooo?

  ReplyDelete
 17. POLE SANA DADA WANAUME WAKIBONGO HAWANA SHUKRANI MIMI WAKWANGU NAMSHOMESHA NAMLISHA NAMSOMESHEA NA MTOTO WAKE LAKINI WAPI SIJUI TUFANYE NINI CHA MUHIMU NI KUMUOMBA MUNGU. SASA SITAKI KUWAZA NAWAZA WANANGU BAHATI NZURI TUMEZAA WATOTO WATATU NA WAKWAKE WANNE KIKUBWA UNACHOTAKIWA KUKIFANYA NI KUANGALIA MAISHA YAKO NA KUTUMIA MPIRA BASI, NDIO TUNAVYOISHI HAPA MJINI SIKU HIZI KWENE NDOA CONDOM KWA KWENDA MBELE UTAFANYAJE NA LI MTU HALIELEWEKI. MIMI BILA CONDOM HAKIJAELEWEKA NA NUNUA MWENYEWE KWENYE MADUKA NAMVISHA TU MWANZONI ALIKUWA ANAKASILIKA LAKINI SASA KAZOEA CAUSE ANAJIJUA YEYE MALAYA. NATEGEMEWA KWETU MIYE. POLE SANA MUATHIRIKA MWEZANGU BORA WEWE UMEONGEA UMETUPA NA MOYO WENGINE TULIZANI TUKO PEKE YETU KUMBE WENGI TUNATESWA NA MIJANAUME SURUALI.
  MAMA P

  ReplyDelete
 18. lea watoto wake ni mungu amekupa ,mimi sina mtoto wakuzaa alikufa waklea sina lea hao nao watamjali huyo watumboni

  ReplyDelete