Friday, May 21, 2010

JE HUYU KWELI NI MUME WANGU


Wapenzi wa Blog hii nzuri.Mimi ni mwanamke wa miaka 33, nina watoto 2 wa kike na wakiume.

Ninaishi na mume /baba watoto wangu tangu mwaka 1996 january., nilipokutana nae alanieleza kuwa ananipenda sana na anataka kunioa. Mimi nilikuwa na boyfriend wangu na yeye alikuwa na girl friend wake, kwa kuwa tulipendana tukakubaliana kila mmoja wetu avunje mahusiano na mwenzie ili tuwe huru kufunga ndoa ambapo wote tulikubaliana na kuacha na hizo dates zetu na kuconcetrate na maamuzi yetu mapya.

Mwaka 1999 mwanzoni nikawa nimepata mimba ya mtoto wetu wa kwanza..Tukapanga taratibu zote za mahali na hatimaye akaja kwetu akatoa mahali kwa sherehe kubwa sana. Baada ya Mahali tulipanga siku ya harusi. lakini baada ya hapo, wakaleta kwetu barua ya kusogeza mbele harusi kidogo mpaka nitakapojifungua.. nilijuwa Mume wangu alikuwa na nia sana lakini nikagundua hilo lilikuwa ni shinikizo la baba yake mzazi, na kwamba yeye hakuachana na huyo girl friend wake, na ambaye na yeye alikuwa mjamzito kwa kipindi hicho ambacho mimi pia nilikuwa mjamzito

kwamaana hiyo huyu mume alikuwa anakula huku na huku..Basi mume huyu aliendelea kunihudumia kwa hali na mali na kusema kuwa nisijali ananipenda sana na ndio maana kanitolea mahali.(wakati huo wote sikuwa najua kama anaendelea na huyu girlfriend wake)

Tuliendelea hivyo mpaka tukaanza kuishi wote na kujenga pamoja. .kumbe na huku kwa girlfriend wake nako alikuwa anajenga. Mpaka hapa ninaongea na wewe bwana huyu anaishi kwa mitara. leo kalala kwangu kesho kwa huyo mama na anawatoto nae WANNE. Kitendo hichi kimekuwa kero sana kwangu kiasi naona kama siishi kwa amani. na magomvi yasiyoisha..Huyu bwana ananiregard mimi kama mke mdogo kwake cos nina 33 na yeye 43 huyo mama ana miaka 42years. Kwa hiyo mimi ndio nachukuliwa kama mke mdogo

Hayo ni machache sana nisiwachoshe.Wapendwa kwa busara zenu kama za mfalme Suleiman naomba mnishauri kama huyu ni mume wangu au ni wa mwenzangu? je nina haki nae gani??au nifanye nini?? Huwa nasikia wanakwenda kwenye baadhi ya sherehe pamoja, inaniuma sana sina furaha hata kidogo, kwani alivunja makubaliano yetu na kunidanganya, ila kwakuwa nilimpenda niliamini kuwa nae atavunja mahusiano ya nje kama nilivyofanya mimi.


NISHAURINI NILIYEVUNJIKA MOYO 


9 comments:

 1. hupendwi dada,
  na si mume wako huyo, ni kwamba mliharakisha tu bila kufikiria,huyo mumeo anaweza hata kukua huku anakutama machoni,
  kwanini mkubaliane halafu akugeuke, achana nae huyo miaka 33 wala sio mingi, utapata mume wa kweli atakuoa, watoto wako ondoka nao wala usiwaache,
  wanaume hawa lo! wakivaa suruali utadhani watu wamaana!!

  ReplyDelete
 2. Pole sana dada.Shukuru wewe kuwa unamjua mke mwenzio,waume zetu wanayofanya huko nnje ni hatari tupu,bora wewe umejua akitoka aut anatoka na nani.Mimi nakushauri kwavile hajakutamkia kuwa hakupendi usiondoke,lea watoto wako lakini usijibweteke,akili kichwani mwako ukae kwa akili huku ukijiwekea akiba,kuwa smart dada,yaani uvutie muda wote,nyumba yako iwe safi muda wote na kila mahali na watoto wako pia hakikisha wapo fresh,hakikisha sebule yako na chumbani kwako unakubadilisha angalau kila baada ya miezi mitatu,eg.mapambo ,makochi kama yalikuwa upande wa kulia baada ya muda unabadilisha kushoto, ongeza mapenzi kwa mumeo sio mpaka adai glasi ya juisi,hapana muulize anataka nini na wala usimuulizie habari za bi mkubwa,wewe ukiwa nae zungumzieni mambo yenu na watoto wenu,epuka kuanzisha ugomvi.hiyo itamfanya mumeo aone mabadiliko mazuri kila mara na atavutiwa kukaa kwako bila kuchoka.Na usishangae akakata mguu kwenda kwa mwenzio, kwanza wewe ndo mdogo shoga.Usiondoke ,kubanana hapo hapo,si alikudanganya mwenyewe.Ila haya yote yatafanya kazi haraka ukiongezea na maombi.

  ReplyDelete
 3. Pole dada yangu, cha msingi wewe jihesabu kama vile hauna mume, yani mdelete kichwani kwako kabisa, maana ni mpumbavu, piga kazikwa bidii,(kama unayo) na kama huna basi tafuta biashara ya kufanya ya kukuweka busy tu!, pole dada,
  mimi naogopa hata huko kuolewa

  ReplyDelete
 4. usiache nyumba mliyojenga pamoja mdogo wangu, wewe kaa hapo kwakuwa ni haki yako na watoto wako, ila yeye usiwe karibu nae kabisa, ikiwezekana mpe na chumba chake, nimeexperience hicho kitu ndio maana nakwambia hivyo, utakufa na ukimwi uche wanao wanateseka, na pengine huyo bi mkubwa ni wasikunyinga na usikute hata ndoa wamefunga, nakuhurumia sana ndugu yangu, wanaume waone tu wamevaa suruali, lakini ni mashetwani namba moja
  pole sana

  ReplyDelete
 5. pole sana dada usijilaumu sana kwani wewe una tamaa kilicjokufanya mpaka umsaliti mpenzi wako wa mwanzo ni nini? malipo ya tamaa ndio hayo huyo mwanaume kakuona bwege mbona wakwake hajaachananae huo ni ujinga nanifundisho usirudie tena. Miaka 33 siomingi usikate tamaa achana kama bado anakupenda na anakuhudumia vumilia mitala kama anakuzingua achana nae pengine mwanaume wako wa kwanza ndiye angekuwa mwanaume mwema kwako pole sana kwahilo tulia

  ReplyDelete
 6. hivi kwani nyumba ni kitu gani? hadi mumshauri eti asiondoke akae kwa ajili ya nyumba. anyanyasike kisa nyumba, hakuna kitu kizuri duniani kama kupata amani ya nafsi, mimi nakushauri kama unafanya kazi, mwache huyo mwanaume, ondoka na wanao, piga maisha huko, wala usikubali kuwekwa mitara, kwanza utaonewa, pia ulishatenda kosa mwanzo la kumkataa mchumba wako wa mwanzo, lakini hilo lilishatokea no need to complain, coz it has arleady happen, but what i advice you, is to leave that place, how many girls wanaishi peke yao na wanamaisha mazuri, tatizo lililop kwa wanawake wengi ni kwamba, siwezi ishi bila man, kitu ambacho sio sahihi, ondoka dada, tena usimfiche, unamwambia bwana, nimeamua hivi kwa sababu hizi, kama wanao ni wadogo ondoka nao, asikubabaishe, ila nawachukia sana wanawake waoga ambao wanaona bila wanaume maisha hayaendi, napata hasira sana, dada ondoka hapo hapakufai, unless otherwise ukubaliane na hali hiyo.

  ReplyDelete
 7. kazi ipo,
  nakushauri ondoka, nenda kaishi kwingine, achana nae huyo kaka, japo dada ulishakosea toka mwanzo kumkataa mchumba wako, pengine mungu alimuweka yule kwa ajili yako,. but pole dada, nakushauri tu uondoke

  ReplyDelete
 8. dada ondoka mpenzi,unachosubiri hapo ni nini zaidi ya ukimwi?utakufa uwaache wanao,nyumba kitu gani,33bado mdogo anza maisha upya

  ReplyDelete
 9. Tatizo wasichana wa siku hizi tamaa, ukiweka tamaa mbele mauti nyuma hilo lazima utambue kilichokufanya umuache boyfriend wako wa wazamani ni nini. mtu uko commited na mtu mwingine unaanza kuwa na mikataba na mtu mwingine hayo ndiyo matokeo yake. Na jinsi ulivyoongea hapo toka mwanzo huyo dada hakuwa girl friend wake alikuwa ni Mke wake kabisa sio girl friend wewe ndiye umeingilia ndoa ya watu sio wewe umeingiliwa, huyo kaka alishaoa siku nyingi hivyo alikudanganya makusudi tu aone msimamo wako na kweli kumbe huna msimamo Huyo ni mume wa mtu tu ukiweza wewe ondoka tu, alikwishaoa huyo longtime alitaka tu kukuharibia kwa mchumba wako wa zamani so hayo ndiyo malipo yako na iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama hiyo. inavyoonyesha hata akitokea mwingine akakuambia anakupenda achana na huyo pia utakubali.....

  ReplyDelete