Monday, May 31, 2010

BABA ANAMWANAMKE MWINGINE . ANAMTESA SANA MAMA YANGU, MIMI NI MTOTO TU! NIFANYE NINI?

Dada Violet, na wadau wote wa blog yako, nawaomba mmwombee baba yangu, maana amekuwa na tabia za ajabu sana kwa mama, zamani hakuwa hivyo ila tumefanya uchunguzi ni kwanini amebadilika gafla hivi, tumegundua ana mahusiano na mwanamke mwingine wa nje
Siku hizi haachi pesa ya chakula nyumbani yaani, matatizo kila kukicha, ugomvi kila siku ugomvi hauishi na siku nyingine hudiriki kuwafungia nje mama pamoja na wadogo zangu,
mama amejaribu kulipeleke kwa mkwe wake pamoja na mawifi zake ili wamsaidie lakini wanaonekana wako upande wa kaka yao (baba) sababu shangazi zangu hawampendi kabisa mama yangu, amekosa pa kukimbilia, amekosa msaada kabisa,
namshukuru Mungu nimesoma na ninafanya kazi ndio huwa kidogo namsapoti mama in short jamani naomba mumweke baba yangu kwenye maombi jamani ili abadilike sababu magonjwa ni mengi sana siku hizi najua wadau mnaosoma humu kila mtu ana imani ya lakini Mungu tunaemwabudu ni mmoja jamani nawaombeni.pili jamani kwenye ukoo wetu kuna kama kalaana ka ktoolewa sababu ndugu zangu wengi hawajaoa wala kuolewa

jamani sipendi niishie kama ndugu zangu napenda niolewe na niwe na familia yangu kama watu wengine,mimi ni msichana wa miaka 26 na nina degee kwa sasa ni mzuri sababu watu hawaishi kunisifia kila nipitapo lakini sijajua who is who jamani nimetulia sana mpaka mwenyewe kwa hilo huwa najisifu na najijua sababu mpaka sasa nimewai kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja then tukashindwa kuelewana,then nipo alone kwa sasa sijasubutu kuwa na uhusiano tena jamani naomba mniombee niweze pata mme wa maisha natamani kuolewa na kuwa na watoto,asanteni sana na imani mtaniombea.


9 comments:

 1. pole sana mdogo wangu,sisi tutawakumbuka katika maombi, tutawaombea kabisa, pole sana yani niwatoto wachache sana wanaopenda wazazi wao kama wewe, tena kwa umri wako huo, Mungu akujalie na huyo mume umpate mwenye tabia nzuri atakedumu na wewe, pole sana

  ReplyDelete
 2. pole sana mpendwa wangu,
  ninachoweza kukushauri kwa upande wangu ni kwamba, mama anawakati mgumu sana, na ukumbuke kuwa wewe ndie mkubwa na mfariji kwake, uwe karibu nae, muonyeshe mapenzi yote ili kumtolea ile hali ya upweke, mjali, mpe nafasi, hakuna kama mama dear! na hasa kipindi hiki ambacho yeye anawakati mgumu, ni lazima ummpe suport ya kutosha,
  najua mwanaume akishapata mwanamke nje, ni ngumu sana kumuacha, lakini pia kumbuka kuwa KWA MUNGU HAKUNA LISILOWEZEKANA, ni kuomba tu! baba atakaa sawa sawa, na atarudisha mapenzi kwa mama, kingine pia nafikiri ni nzuri sana kama utamtafutia mama biashara ya kufanya, ili imtoe katika upweke japo kwa asilimia fulani, mpe biashara itakayomkeep busy, na endelea kuomba tu, MUNGU ATAMSAIDIA, POLE SANA DEAR,
  NGOJA TUPATE USHAURI KWA WADAU WENGINE PIA.

  ReplyDelete
 3. NIKIJA KWA UPANDE WA WEWE KUOLEWA,
  kwanza hadi sasa nakuhesabu ni mshindi, maana umeshaikataa ile hali ya kutoolewa, unajua hakuna kitu kizuri kama kupinga/kukataa laana? lakini pia ni vizuri kama utaendelea kujiheshimu, nahakika utapata mume mzuri sana, wanaume siku hizi wanataka wanawake wanaofanya kazi, wasiwe tegemezi, wanataka wanawake wanaojiheshimu wasiwe malaya, hivyo wewe tulia tu! wala usikurupuke kukimbilia ndoa, unaweza kumpata mwanaume ambae atakupa stress hadi ujichukie,
  omba, mwamini mungu kuwa anaweza, na atakusaidia tu! wala usitie shaka mpenzi,
  nakupenda sana.

  ReplyDelete
 4. ASANTE SANA DADA NA MDAU NAMBA MOJA HAPO JUU NIMEFARIJIKA SANA NDUGU ZANGU MAMA ANA BIASHARA ANAYOIFANYA AMBAYO NAYO KIDOGO INAMSAIDIA.ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.

  ReplyDelete
 5. Mimi nafikiri kama alivyosema dada violet, wewe kuwa karibu na mama tu! mfariji sana, mpende, mkumbatie,
  na ikiwezekana pia, mimi nakushauri hivi, sijui kama wengine watakubaliana na mawazo yangu lakini, ni bora niyawasilishe, halafu utaangali mwenyewe kama yatakusaidia yachukuwe

  WEWE HAPO ULIPO NI MTU MKUBWA SASA, kusanya wadogo zako wooote, mchukuwe na mama yako, muombeni Mungu kwanza kabla hamjafanya hili, muwekeni baba mbele za Mungu, Mungu afunge kiburi chake kabisa ili hata mnapokwenda kuongea nae akawaeleweni,

  tafuta siku ambayo wote mpo nyumbani, namaanisha mama, wewe, na wadogo zako wote, kisha mpe mdogo wako mdogo simu ambae anaweza kuongea vizuri, mpe simu aongee na baba yenu, na amsisitize kurudi nyumbani, ( huwa napenda kuwatumia watoto sana maana wanaaminika kuliko mtu yeyote yule) amuombe baba awahi kurudi nyumbani,
  naamini atakubali tu! maana Uwepo wa Mungu utakuwa umeshamfunika, na siku ya kutaka kufanya hivyo, mjulishe violet, ili nami niwe kwenye maombi pamoja nami nifunge nguvu za shetani zoote, nipo mbea, ni mbali, ila nitawaombea tu! baba akirudi
  wote kaeni sebuleni,
  muulizeni, kwanini anafanya anachokifanya? msiogope kumwambia kuwa tunajua kila kitu kuhusu wewe baba, kwanini unamtesa mama yetu? ulituzaa sisi ili tuje tuone jinsi gani mama anapata mateso? huna upendo hata na sisi wanoa? nani atakulea usipotupa misingi mizuri ya maisha kwa wakati huu? ongeeni kwa uchungu, na ikiwezekana mama asiseme lolote? muulizeni, baba ni maisha gani haya unataka kutufundisha? familia zetu na vizazi vyetu tutavifundisha nini? hebu ongeeni nae, natamani ningekuwepo. ila nakwambia lazima atabadilirka tu! wala msikurupuke,
  SIMAMA KWENYE MAOMBI TU!, IKIWEZEKANA SIKU YA KUMUITA KWA AJILI YA KIKAO, WOTE MSILE CHOCHOTE, MUWE NA MUNGU TU!
  (Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, ) ss mimi nakupa maarifa haya, fanya hivi uone mungu alivyo waajabu.
  NA AKITENDA TU! TUJULISHE ILI TUMRUDISHIE MUNGU UTUKUFU WAKE.
  Mtumishi

  ReplyDelete
 6. ASANTE MDAU HAPO JUU ULIETUSHAURI TUMWITE BABA YETU TUONGEE NAE ILA MIMI NIPO DAR KIKAZI NA FAMILIA YANGU IPO MOSHI MDOGO WANGU MDOGO YUPO FORM 3 NA ANAPATANA SANA NA BABA TUPO SITA WATANO TUPO UPANDE WA MAMA ILA YEYE YUPO UPANDE WA BABA,MIMI NI WA PILI KUZALIWA,ASANTE SANA NASHUKURU KWA USHAURI WAKO,SIJAKATAA KWENDA LIKIZO ILA MWEZI ULIOPITA WA TANO NILIKUWA NA MITIHANI NILICHUKUA LIKIZO SIWEZI CHUKUA TENA SI UNAJUA KAZI ZA WATU MPENDWA ILA ASANTE SANA NITAWASILIANA NAWE NIKIENDA NYUMBANI NAJUA MUNGU ANAWEZA YOTE NA ATATENDA SAWASAWA NA MAPENZI YAKE,YOTE YANAWEZEKANA,ASANTE SANA MUNGU AWABARIKI JAMANI.

  ReplyDelete
 7. pole nami nitaendelea kukuombea mwanangu, najua maumivu unayoyapata, lakini usijali,
  BWANA ATAFANYA NJIA MAHALI PASIPO NA NJIA, aliigawa bahari ya shamu na wana islael walipita, atashindwa kumrekebisha baba yako, wakati kamuumba yeye?
  JIPE MOYO UTASHINDA, NITAKUOMBE MWANGANGU, imeniuma na inaonyesha jinsi gani mtoto anaweza kuugua na mama yake.
  pole bi

  ReplyDelete
 8. pole sana mdogo wangu.mwambie mama aondoke hapo kwa baba. Na wote muombe mungu.Mimi pia nimekulia kwenye familia ya baba anayemtesa mama. ni ngumu kuelewa lakini isikutese wewe kwani siyo makosa yako wewe bali ni ya babayako. Na mama yako anatakiwa kuamka na kuondokana na mateso aombe mungu na kumuweka yesu mbele sio baba yako.Ishi maisha mema.

  ReplyDelete
 9. noun An open, shallow, usually round container used especially for holding liquids.
  While purchasing. Usually, a bassinet mattress is made from foam as it provides more softness.


  Here is my web page ... round crib

  ReplyDelete