Tuesday, May 4, 2010

NATAMANI KUOLEWA ILA SIJAWAHI KUMPATA HATA WA KUTAMKA TU!

(mnisamehe jamani, wiki iliyopita nilikuwa busy kupita kiasi, nikawa naona masaa yanayoyoma tu hata blog sijaigusa, lakini nshamaliza nilichokuwa nakifanya, im back wapenzi)

msaada wa mawazo yenu ni muhimu sana kwangu,
mimi ni mschana, sijaolewa bado, na nina umri wa miaka 32, nina kazi nzuri tu ambayo inaniwezesha mimi kuishi vizuri, ila nina shida moja, ambayo sijui kama dada violet na wengine mnaweza kunisaidia au hata kuniambia ni kwanini inanitokea hivi,
  
  mimi ni mzuri, nikijitazama, na pia sina ulemavu wowote,  nafanya kazi nzuri, na naishi nyumbani kwangu,
wazazi wangu wako Nairobi, ndiko nilikokulia, ila kazi nafanya hapa Dar es salaam,

katika maisha yangu sijawahi kupata mwanaume wa kuniambia anataka kunioa hata siku moja, hata nikimpata tu! tunakuwa marafiki kwa muda, then wanakimbia, ukimpigia simu anakata, sometimes hata kupokea hapokei, hadi nachoka na hatimae kuachana, naweza ingia gharama ya kumuhudumia mwanaume nitakae kuwa nae, kwa kila kitu, lakini nikishajiweka karibu yake, na kumuuliza lini tutafunga ndoa,  huwa  ni kama nimemwonyesha bomu,

niliwahi kwenda kanisa moja hivi, nikaombewa maana walisema ni laana ambayo inabidi ivunjwe, niliombewa sana, lakini since there, no any changes, nimechoka kuhudhuria na kuchangia harusi za wenzangu, wakati mimi nazeeka tu!, staki kuzaa nje ya ndoa, na staki kuishi na mwanaume nje ya ndoa,

natamani na mimi niitwe Mrs. fulani, huwa nakaa nalia sana peke yangu, najiona kama mwenye mkosi fulani.unakuta mwanaume natokea kumpenda sana, nitaonyesha njia zote za kumtamani kimapenzi, lakini tutaishia out tu!na hakuna kitakachofatia hapo. sasa sielewi, kama ndio nimeumbiwa kupata shida hii, unakuta natamani kumwambia mtu kuwa nampenda, ila nakuwa nashindwa kwa kuhofia jamii itanichukuliaje, lakini hali hii inanitesa sana, kwa msichana wa umri wangu, ninaeelekea kwenye umama, bila kuwa na mtoto wala mume

16 comments:

 1. pole sana dada yangu, i can feel jinsi unavyoumia. napenda nikutie moyo kwamba biblia inasema ivi "kwa kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu kuna wakati wa kilia, wakati wa kucheka............" Muhubiri 3.1-8. Mungu amempa kila mtu jaribu lake kulingana na uwezo wake, kuna wengine jaribu lao ni kupata mtoto, wengine kupata kazi (kuajiriwa) nafikiri umeshawahi kusikia watu wanalalamika katika nyanja tofauti tofauti. hata mimi pia nina jaribu langu ambalo kila siku namlilia Mungu anisaidie. ninachoamini ni kwamba ipo siku nami nitalishinda hilo jaribu tu!!. ninachokuomba wala usilie au kukata tamaa, we kaza msuli na uombe sana (ng'ang'ania)utaona milango inafunguka na unapata mume mzuri mpaka utashangaa.maombi ndo siri pekee ya kupata. huo umri usikutishe, wapo wanaoolewa mpaka miaka 35-40. so dont worry, God is there to help you.

  ReplyDelete
 2. polee sana dada yangu ila usijione una mkosi haya yote ni majaribio mungu anatupima imani zetuu..mimi nilikua na family friend wangu hakuwai kuolewa mpaka alikata tamaa lkn mungu si athumani alipata mchumba ambae hakuwai kuoa na akamuoa huyo family friend wangu akiwa katika miaka ya 40 na sasa anaishi maisha mazuri..muweke mungu mbele anakupima imani akuone je utachoka kumlilia yeye??usife moyo mpenz na kama unaona vipi jaribu kuingia mitandaoni kwenye arrange marriage au dating sites watu hupata waume kutokana na izo sites na pia endelea na msimamo wako ukishaanza kuishi na mwanaume kama hajakuona basi kukuoa ukishaishi nae ni ngumu sana pole kwa yote mungu atakusaidia

  ReplyDelete
 3. hi binti mzuri uliyekataa tamaa amini liko tumaini. jione wewe ni wa thamani sana mbele za mungu na wanadamu. Kumbuka kwa mungu hakuna kuchelewa wala kuwahi,mungu ni mungu wa majira hawahi wala hachelewi, ila anajibu maombi. hali unayoipitia naijua ni ngumu mno na mimi nilipitia hiyo hali, ilikuwa kila mwanamme anayekuja naishia kuchezewa halafu kesho anaowa mtu mwingine, hakuna kitu kibaya kama roho ya kukataliwa, laana za vizazi majini mahaba, kuota unafanya mapenzi na mtu unayemjua au humjui hivyo vyote ni vifungo. na kama kwenu kuna vitu kama hivyo au kwako wewe hebu mtafute mungu acha kulia kumbuka kwa yesu kuna majibu yote usijipe strees mpenzi wangu. kaa chini mtafute mungu kwa kumaanisha kabisa usilie kabisa ikibidi tafute sehemu za maombi ufanyiwe derivarence kama kuna kitu mwilini mwako kitadhihirika tuu, na utafunguka soma mwanzo 2: 18-25 USICHOKE KUOMBA NAOMBA tuwasiliane kwa mail yangu ni kadinari4@yahoo.co.uk nitaongea na wewe mengi zaidi na maelekezo acha kulia mpenzi wangu.Shetani mwizi asikukatishe tamaa. mungu akubariki sana.

  ReplyDelete
 4. pole dada, hiyo hali inawakuta watu wengi huku nchi za nje, kumbe hata nyumbani pia, mi nakushauri usiogope kumwambia mtu unampenda najua nyumbani kuna watu bado wana mawazo mabaya mwanamke akitongoza wanadhani ni malaya lkn si kweli,najua umri wako umeenda,wewe mwombe mungu na ukipenda mtu mwambie na upe mda,wanaume wengu hawapendi kuambiwa ambiwa mambo kuona kila wakati wanaona kama unwapush,naamini utapata mtu na utaolewa tu,sina mengi nakuonbea upate mume mwema.

  ReplyDelete
 5. Nashukuru kwa ujumbe wako mzuri,

  Nakusalimu katika jina la yesu,

  mimi nilipita katika njia yako lakini nilifanya mambo yafuatayo:

  1. Baada ya kugundua wanaume hawasemi kuwa wananioa nilimwapia Mungu kuwa sitataka mwanamme aniombe tufanye mapenzi mpaka siku ya ndoa haijalishi hapo nyuma nilifanya dhambi hiyo.

  2.Nikaingia kwenye maombi ya kufunga nakuomba, na pia kuwashirikisha wanamaombi wa karibu ila sikushirikisha kila mtu, nilimwendea mama mmoja mama mchungaji nikamwambia na mahitaji mengi lakini niombee nipate mume mwema anayemwishilia Mungu.

  3. ikatokea siku namwona kaka mmoja ambaye ndie mume wangu sasa mfupi ila mimi nilitaka mrefu, nikaona nampenda nikaanza kushangaa itakuwaje nitamwambiaje halafu mi mlokole nitaanzaia wapi? ile hali ilinisumbua huwezi amini nilikaa siku saba siwezi kula wala kufanya kazi, nikaanza kuomba yeye anianze wala hakunianza, nikateseka mwezi nikapungua kilo tatu, nikashindwa nikamwambia kweupeee mi nakupenda na ningefurahi uwe mume wangu. akakataa. weeeeeeeeeeee lakini hapo furaha ya moyo wangu ikarudi.

  sikumfuata tena mpaka baada ya miezi miwili ananiletea ua kadi na ujumbe wa Mungu kuwa yeye ndie mume wangu ila alishindwa kunijua.

  nimeandika mengi ili uelewe, pia katika maombi yako unatakiwa kutamka kuwa Popote mume wako alipo unamamsha maana kalala hataki kuja kukuoa, sema nakuamsha katika jina la Yesu, nipo tayari Mkeo kama uko mbali au karibu nakuita nina haja nawe sasa.

  ukimpenda mtu mwambie Mungu, huu ni ubavu wangu? naomba niambie Mungu mwaminifu atakuambia na utamwambia nimekupenda naye atajibu.

  usikate tamaaa

  nisamehe kwa urefu wa ujumbe

  ReplyDelete
 6. Pole sana rafiki yangu, usikate tamaa mungu atakusaidia
  nakuombea

  ReplyDelete
 7. Ndugu mliochangia,asanteni sana,mimi ni msichana wa umri kama wa huyu dada na nina tatizo linafanana sana na la huyu,asanteni sana kwa mawazo kwakweli nimepata ujasiri

  ReplyDelete
 8. dada ulienitumia email hii kutaka ushauri, naomba nipatie namba yako yasimu, tuma kupitia violet.gerald@ yahoo.com, mkasa wako uliutuma kwenye comments, sasa sina hata contact zako. naomba nipatie kupitia email yangu hapo. nina kitu nataka kuongea na wewe kwa urefu zaidi
  please!!!! nitumie
  pole na yatakwisha tu! utaolewa na mume mzuri mwenye upendo wa dhati kwako, huwezi jua, pengine hao hawataki kukuoa labda Mungu ameona ya mbele zaidi, ndio maana anazuia.
  please send your no.

  ReplyDelete
 9. dadaaaa
  nitumie namba yako pleaseeeeeeeeeeeeeee

  ReplyDelete
 10. Ahsanteni sana mliochangia mimi ni msichana wa umri kama wa huyu dada tatizo langu linafanana sana la lake nimepata mawazo kweli nilidhani ni me peke yangu ndio na tatizo ili asanteni.

  ReplyDelete
 11. Pole sana dada. usikate tamaa zidi kumuomba M/mungu. Atakisikia kilio chako sikumoja.

  ReplyDelete
 12. msikate tamaa jamani,
  bado waume wenu wanatengenezwa, msijisikie vibaya kabisa, haya nia maisha tu, mtauona utukufu wa mungu ukiwashukia na kutenda maajabu kwenu. msiogope kabisa

  ReplyDelete
 13. Nakuombea kwa Mungu awezaye kukupa mume mwema akupe sawasawa na kusudio lake kwako

  ReplyDelete
 14. Dada Mwenye tatizo pole sana. Pili kama inawezekana naomba unitumie e-mail tmajaliwa@yahoo.co.uk.
  Vile vile dada uliyteota ushuhuda mrefu kwa dada mwenye tatizo MUNGU AKUBARIKI SANA.
  Mtanzania

  ReplyDelete
 15. Asanteni ndugu zangu,

  maana hata mimi ninatatizo kama hilo ila langu ni tofauti kidogo:-

  Mimi nlikuwa na mchumba wangu wa kwanza kabisa, nikazaa nae mtoto wakike na kufuata taratibu zote kabla ya ndoa yeye alienda kwanza kusoma (Mastes) baada ya kumaliza Mungu mwingi wa rehema alimchukua:

  Baada ya kuishi kwa muda nikapata mtu mwingine ila yeye sasa ndio aliyenitenda hadi sitamaani kitu kinachoitwa mwanaume.

  Tuliishi kwa muda wa mwaka mmoja ndipo tulipata mtoto (tukazaa) ingawa kila mmoja alikuwa anishi kwake ingawa yeye alikuwa anaishi kwangu muda mwingi na kwenda kuona watoto na mimi nilikuwa naenda kwake week ends tu, wakati tupo wote yeye hali kidogo haikuwa nzuri kwani alikuwa na kazi ila ilikuwa haieleweki (Dereva) nikamsaidia kulea watoto aliokuwa anishi nao kwani mkewe alimuacha na watoto wawili wa kike na wakati huo alikuwa na muda wa miaka mmoja toka wameachana.

  Baadaye alipata kazi nzuri sehemu nyingine tena kwa ushauri wangu mimi, na alivyoona mambo mazuri akakutana na msichana mwingine akaamua kumleta nyumbani kwake alikokuwa anaishi na watoto wake bila mimi kuwa na taarifa na wakati huo nikiwa na ujauzito wa miezi mitatu. Nashukuru mungu nilijifungua salama mtoto wa kiume ingawa baadae alimkataa mtoto na kudai nimtafutie babake.

  Nashukuru mungu kuwa maisha yanaendelea vizuri. Namuomba Mungu kila siku sichoki anipatie MUME MWEMA atakeye nikubali mimi na Watoto wangu ambao nimezaa tayari.

  "NINA IMANI MUNGU YU MWEMA IPO SIKU ATASIKI KILIO CHANGU KWANI SIWEZI KUJIZUIA KUPENDA NI KITU AMBACHO TUMEUMBWA NACHO"

  ReplyDelete