Monday, May 10, 2010

WAKWE WALIMTAFUTIA MKE MUME WANGU, KISA SIZAI, SASA NIMEZAA BADO HAWANITAKI, NIFANYAJE?

yamenikuta mwenzenu
nakupongeza dada violet kwa blog yako ambayo inatufanya tupate mawazo tofauti tofauti ya kutusadia wenye shida, nakuombea Kheri ndugu yangu.
Niliolewa miaka 8 iliyopita huku Njombe, nilipoolewa nilikaa miaka mitano bila kukamata mimba, nilihangaiika sana, nilienda kwa waganga wa kienyeji, nikatumia mitishamba lakini haikusaidia, ndugu wa mume wangu walianza kunichukia sana na hata mume wangu pia,
miaka mitatu iliopita, mume wangu aliniomba msamaha kwa kusema kuwa amezaa na rafiki yangu, rafiki ambae alikuwa akinificha sana kila nimuulizapo mimba ya nani, hakuwa akiniambia ansema mwenye mimba yuko nje, alipoenda kujifungua kwao singida aliporudi hakufikia pale, nikasikia amefikia kwa wakwe zangu,
nilishangaa sana, hao wakwe mimi wamenipiga marufuku hata kwao nisikanyage

wifi yangu mmoja akaja kuniambia yule rafiki yangu amepangishiwa chumba mahali, nililia kupita kiasi, lakini nilijipa moyo, huyu kaka tulichukuana tu hatukufunga ndoa, mume wangu alianza chuki na maneno ya kashfa kwangu, nilivumilia tu!,
mwaka jana nilipata ujauzito, namshukur mungu nilijifungua salama, na mtoto alikuwa amefanana sana na baba yake, badala ya kufurahi, nilishangaa mume wangu hakuwa na mapenzi na huyu mtoto hata kidogo,
ss mwaka huu mwanzoni nikaambiwa kuwa wameachana na yule mwanamke, na mtoto kaamua kumpeleka kwao, baada kama ya wiki, nikaletewa mtoto nyumbani, mimi nilikubali nikawa namlea
ss nimeletewa taarifa kuwa wamerudiana na yule msichana, mapenzi moto moto na wanataka kufunga ndoa,
yani kila nikiwaza hata sipati jibu mwenzenu, sielewi pa kuanzia wala pa kuishia,
huyo mtoto hadi sasa niko nae hapa nyumbani kwangu, na habari hizi ni zaukweli kabisa, maana niliambiwa na mshenga, kwamba nijiandae kama nina pa kwenda niende, maana huyo rafiki yangu (mke mwenza) atakuja kuishi hapa hapa na mimi
inaniuma sana

4 comments:

  1. dada polee sana kwa hayo ila vumilia tuu ndoa ni kuvumilia usikubali kuacha ndoa na hata kama utaona umeshindwa usimuache mtoto wako nenda naye umlee mwenyewe..pole sana mungu atakusaidia..

    ReplyDelete
  2. daaaah wanaume siwawezi....duh.....mungu akusaidie...jamani mimi hivi ndoa ntaiweza kweli...daah....mungu akusaidie dada.....

    ReplyDelete
  3. mh pole sana jamani na kwa uvumilivu huo sijapata ona kwanini usianze maisha yako mapya na mwanao kuliko kuumia kiasi hicho tena hata hajali huyo mume??usizekee kwake huku ukipata mateso na umri pia unakwenda na baadae pia utakuwa umechelewa fanya uanze maisha yako maana haina haja ya kuteseka na mwisho wake haijulikani itakuwaje,pole sana mungu atakupigania.

    ReplyDelete