Thursday, May 13, 2010

AMESEMA HANIOI HADI NIZAE, NA WALA SISHIKI MIMBA, NAWEZA KUWA TASA??


Hello Dada Violet,

Pole na kazi za nchi hii pamoja na kutusaidia sisi.
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 24 na ninaishi na mchumba wangu. Tumeishi kwa miaka miwili sasa, sijabahatika kupata mimba. Ila dada Violet nina tatizo moja ambalo linaninyima raha kabisa. Huwa sizioni siku zangu naweza kukaa mwaka mzima nisizione.je inawezekana kuwa mimi ni tasa?? Na mchumba niliyenaye yupo tayari kunioa lakini ndio anataka nipate mimba kwanza je kuna uwezekanano wa mimi kupata mimba kweli??

Nipo njia panda sitaki kuteseka baadae nikiingia kwenye ndoa.
Hali hii inaniumuza sana, naombeni ushauri wenu


7 comments:

 1. pole sana mdogo wangu
  but unaniudhi,
  ''KWANINI UNAFIKIRIA NEGATIVE'' hilo ni tatizo la kutoona siku zako sio lako peke yako, na haimaniishi kuwa wewe ni TASA, ndugu yangu, hebu kemea hayo mawazo ya UTASA, unajua kama ulimi UNAUMBA, Futa hayo mawazo kabisa, pia miaka miwili kutokupata mimba wala sio issue, watu wanakaa zai ya miaka hiyo,
  Umewahi kwenda hsptl? nenda na ueleze tatizo lako, mm nina mdogo wangu nae alikuwa na tatizo kama hili, yeye anapitiliza hadi miezi nane, ndio anaingia tena. na tumbo lilikuwa likimuuma sana, tulimpeleka Aghakhan wakamsaidia, ss hiv anapata kama kawaida, ss mm sio mtaalamu sana, la zaidi ni kwamba nakushauri nenda hospitali na utasaidiwa tu!
  KUHUSU MCHUMBA WAKO,
  sidhani kama yuko sahihi kwa kutaka ubebe mimba ndio akuoe, ukweli ni kwamba anakukosea sana, yawezeka tatizo likawa kwake, (hii ya kuzaa ndio uolewe) naona kama haiko sawa vile, mmmmmmmmmmmm sijui lakini ngoja tuone wengine wanakushauri nn, but mimi nakuomba uende hospitali, onana na Specialist wa matatizo ya uzazi ya kina mama, then atakusaidia, kwa ushauri zaidi kama uko Dar, Nenda Muhimbili hsptl (kule private) omba kumuona Dr. Kamugisha, atakusaidia sana. na akikusaidia please let me know.
  nakupenda sana mpenzi, basi usiwaze HASI always try to think POSITIVE

  ReplyDelete
 2. Dada Violeth nashukuru sana kwa ushauri wako na nitaufanyia kazi pindi tu nitakapokwenda kumwona Dr. Kamugisha nitakupa taarifa.Asante na Mungu akubariki sana....

  ReplyDelete
 3. pole sana rafiki yangu,
  ila nachowezakusema ni kwamba
  huyo mchumba wako hakupendi
  angekuwa anakupenda lazima angekujali
  lazima tatizo lako lingekuwa lake, sasa eti hadi uzae, kwani yeye mungu hadi ajuwe uzazi wako? fikiria hili rafiki yangu. nyota njema huonekana asubhi dear.
  tia akilini

  ReplyDelete
 4. shost mchumbako wala hakupendi.
  hata biblia inasema chukulianeni mizigo daima, tatizo lako alibebe kama lake, na lake ulibebe kama lako, kwanini akwambie uzae kwanza? fikiria mata tatu. kabla hujaolewa, hebu muombe mungu akwambie kama huyu ni sahihi kwako.
  pia kama alivosema violet
  nenda hospitali haraka, huyo dr alomsema mimi nasikia ni mzuri sana, nenda kule fast track
  (private) watakusaidia, na ukifika sema namtaka Prof. kamugisha,
  pole mdogo wetu

  ReplyDelete
 5. mmmhh nianze kwa kuguna kwanza pole sana ndugu yangu tatizo ilo sio lako peke yako hata mie navoandika hapa nina tatizo kama,na story yangu kama yako,nilikua na boyfriend wangu uko bongo ilikuwa kama wewe tunatiana miaka nenda rudi mimba sijashika miaka saba nilikua naee,nikasafiri nilikaa sweden miaka miwili sijapata period nikaja uk nimekaa miezi sita sijapa period nikaenda kwa doctor nikamwelezea akanipa vidonge nikaona siku zangu basi zikawa zinakuja mwezi unapita sipati,nikapata bwana mwingine huku kumbe yule bwana target yake ilikuwa anitie mimba namie mimba sishiki natiwa tuu lakini mimba haiingii basiii kumbe naona mungu alikua ananipenda huyo mwanaume navokwambia na na barua kanitolea ila hamu sina tena alinitukana etii miee mwanamke ama galasaa mwanamke nisie concieve nililiaa wallah sitakaa nisahau,basii hayo niyangu tuu maana nisikuchoshe na sipendi nikuone unapata tabu ama uje udharauliwe baada na sitakushauri pia uzae nje ya ndoa huyo mwanaume atakua ana nia na wewe na sikwambii umuache ila nachotaka kukwambia miee nitakusaidiaa maana dawa napewa bure sasa nitakachofanya nakuachia contact zangu hapa,unipigie simu ama unitumie email na details zako ikiwezekana nikutumiee dawa popote ulipo kwa gharama yangu nasitakutoza chochote ndugu najua ukipona wewe na mie kesho ntapona Inshaallah basi ni hayo hayooo mengine tutaongea number yangu ya simu ni 00447591311670 na email yangu ni aysha_moh@hotmail.com,samahani kwakukuchosha na maneno sema uende kwa doctor piaa na usije ukakubali kusafishwa maana ma doctor wa bongo wanakimbilia kusafisha watakulegeza kizazi,ok then hope to hear from you soon.take care mungu atakusaidia

  ReplyDelete
 6. Nashukuru kwa kujitolea kunisaidia, usijali nitakutafuta kwa uwezo wangu wote ili uweze kuniambia wewe umeponaje. Yani kwa jinsi ninavyotamani kuzaa naona wivu pindi nionapo wanawake/wasichana wenzangu wana mimba au watoto. Ahsanteni sana kwa ushauri. Na Dada Violet nakushukuru kwa mara ingine tena Mungu akubariki kwa kupost tatizo langu..na wote Mungu awabariki sana!!

  ReplyDelete
 7. Pole dada ila muweke Mungu mbele kwa yote ambayo yanakukuta yeye ndio mpangaji wa yote. Sali sana pia kwa ajili ya huyo mpenzi wako..

  ReplyDelete