Monday, May 17, 2010

MCHUMBA ALINIACHA MWENYEWE- SASA ANATAKA TURUDIANE TENA, NIFANYAJE


Napenda sana ushauri wa watu na naamini utanisaidia sana, mara nyingi huwa napita ktk blog yako japo huwa sichangii, lakini sasa kuna tatizo lililonikuta, na sina ufumbuzi, nahitaji msaada wa mawazo sana

Nilikuwa na girlfriend wangu tuliekuwa tukifanya kazi pamoja na tulikubaliana kuoana, badae nilimtafutia kazi yenye maslah mazuri zaidi kwa nafasi yake ofisi nyingine, basi akaacha pale na kwenda kule kwa nilipomuunganishia. Alieniunganisha katika ofisi hiyo ni rafiki yangu mimi anaefanya kazi pale

Nilimtambulisha mchumba wangu kwake, akamfahamu, na hata wakati tunapeleka mahali kwao, nae alitusindikiza, kinachonitatiza ni kwamba, huyu mchumba wangu amebadilika gafla sana, yani mapenzi yamekwisha kabisa, kitu kidogo tu anakasirika sana, inakuwa ugomvi mkubwa, wakati hakuwa hivyo hapo zamani, kuna mfanya kazi mwenzao mmoja pale aliwahi kunitumia sms na kusema kuwa mchumba wako sio mwaminifu anachukuliwa na rafiki yako. Nilipomuuliza alikasirika sana na kukimbilia kunijibu kuwa kama nasikiliza watu basi tuachane, kwakuwa nilimpenda sana, niliamua kuwa mpole tu

Sasa niezi kama mitatu hivi iliyopita nilikuwa nimelala usiku sana akanitumia sms kwamba anaenda kuwaambia kwao wanirudishie mahali, yeye hataki kuolewa tena, nilishangaa sana, usiku ule ule nilimpigia sim kutaka kujua sababu, akawa hapokei, sikulala hadi kunakucha, asubuhi nilimtafuta kwenye simu tena ili aniembie tatizo, safari hii alipokea ila akasema hataki hata kuonana na mimi, nilibembeleza sana lakini alikataa na badae kuanza kukata simu. basi nilifikisha kwa wazazi/washenga, wazee wangu walinishauri kuwa hata hiyo mahali niiache iwe kama nimeitoa sadaka,

Nikamtumia sms nikamwambia sawa, lakini juwa umenitesa sana, nami nikaamua kufata yangu, violet kila nilipokuwa nikikaa nilikuwa nikikumbuka mazuri mengi niliyomfanyia, muda niliopoteza kwake, bado kanilipa ubaya, da!

Niliamua kuanza maisha mapya, sasa juma pili kanipigia simu anataka aonane na mimi, mimi sikutaka kumlipa ubaya, nilikubali, tukakutana pale Santina restaurant, anachokiomba kwangu, anataka turudiane nae. Anasema toka ameniacha hana raha, ni mtu wa majonzi, mikosi na hana furaha hata kidogo, sasa hadi sasa sielewi cha kumjibu, ila mimi kwake mapenzi yamepungua sana.12 comments:

 1. Kwanza nianze kukupa pole kaka yangu! Huyo mwanamke hana msimamo hata kidogo, halafu inaonekana anatamaa sana. Hebu muulize ni nini kimlimfanya mpk kukuambia hakutaki ukachukue mahali yako?? kukufedhehesha kwa ndugu zako na hata rafiki zako nini?! Sitaweza kukushauri either umuache au muendelee kwasababu siwezi kujua moyo wako ila mchunguze kwanza huyo ni bendera anafuata upepo tu hana lolote huko alikokwenda kumemshinda. Wasichana ndivyo tulivyo tunaona mwanaume mwenye pesa ndio tulizo lakini hakuna lolote. Kaka yangu mchunguze ila usimkubalie mwambie muwe marafiki kwanza halafu muone siajabu amekuja kukujaribu.

  ReplyDelete
 2. Pole sana, mimi yaliwahi kunikuta na kwa bahati mbaya nadhani sikua makini nikamkubalia na tukaoana, lakini leo hii najuta, imani yangu hainiruhusu kumuacha(hatuna kitu kinachoitwa talaka katika imani yangu) hivyo nakushauri fikiria mara mbili, huyo ni mtu hatari sana, hawa watu wanaoshawishika kirahisi hivyo huwa hawajifunzi, kila siku wana jipya litakalokuudhi, mi nadhani maana ulishalipeleka kwa ndugu na wakakupa ushauri wa kukubali kumuacha na kusamehe mahari, basi achana nae kabisa huyo. hao waliomdanganya wako wengi na wataendelea kuwepo hivyo ataendelea kudanganywa. nakupa pole sana ila kazi kwako, sitaki yalionipata mimi yatokee na kwako.

  ReplyDelete
 3. Pole kaka,inaonekana ulimpenda sana Mchumba wako ingawaje yeye alikuwa athamini penzi lako kwako,au alikuwa hana uhakika na anachokitaka kutoka kwako.Mchumba wako amechezea penzi lako na kulitupa bila woga wala huruma,mimi nisingefurahi kusikia umerudiana nae,kwanza unapaswa uangalie mbali,hebu fikiria kakugeuka na kukueleza ukachukue mahari uliyotoa...then unampigia simu hapokei...unamtumia message anasema hataki hata kukuona..mimi naona hakufai.Inawezekana kweli alidanganywa na rafiki yako,penzi la rafiki yako likamchanganya sasa wameshazoeana anaona hamna jipya ndio akakukumbuka...ila hujatueleza mlivyokutana Santina Restaurant alikueleza nini..ni sababu zipi zilimfanya akusaliti?unapaswa kuzipima ili utoe maamuzi...kama ni kweli alitembea na rafiki yako?are ready to take her back?na je mkiwa mmetoka ukakutana na rafiki yako...utajisikiaje?na je wazazi/ washenga wako hawatakuona mume bwege?kumbuka uliwaendea wakakujibu hata hiyo mahari usiifwate iwe kama umetoa sadaka.,je ukimrudia watakuelewa?
  Vilevile ujumbe wako nimeusoma kwa makini nimejaribu kutafuta baadhi ya maneno lakini nimepata maneno haya:"umekumbuka mazuri uliyomtendea,muda uliyopoteza na kwamba mapenzi yako kwake yamepungua" siwezi kusema kama humpendi inaonekana unampenda sana tena sana ndio maana ukaamua kwenda kumsikiliza...kama unaona huwezi kuishi bila yeye msamehe lakini inabidi ufanye kazi ya ziada sana..
  1. kurudisha heshima yako kwa rafiki yako na kwa wazazi wako? (je hili unaweza?unadhani litafutika moyoni mwa wazazi/washenga wako?
  2.je unaweza kurudisha mapenzi yote kwake?na yeye yupo tayari kwa hilo

  Ushauri wangu ni kwamba ukimuacha heshima yako itarudi na utapata mwingine mtaelewana tu 90%

  Ukimrudia,utapata msongo wa mawazo,maisha yako hayatakuwa ya furaha kama mwanzo,mkigombana hata kama ni ugomvi mdogo,utakumbuka ya nyuma yote..majuto yatakuwa mengi kuliko furaha
  majuto yatakuwa 90% furaha 10%
  hayo ni mawazo tu..ila MUNGU akuongoze katika maamuzi utakayochukua..

  NN/Nighty Naughty.

  ReplyDelete
 4. DAH KAKUABISHA SANA HASA KWA FAMILIA YAKO...ukirudiana nae...UTAIABISHA FAMILIA YAKO NA WATAKUSHANGAA....SANA .....hana msimamo ukiona hivyo ujue kule kwa rafiki ako kimempata kitu ndo anataka aje apozee kwako...daah pole san akaka amekuabisha sana jamani....eeh dunian kuna mambo watu wanatafuta ndo ana kupendwa kumbe kuna watu wana chezea bahati....kaka usirudi coz ukimuoa...akipata mwingine ataomba talaka halafu akuue kwa mawazo....this am tellin huamni nenda kajionee.....then ndo ujute tena plz endelea na life lako.....atakutesa tena tuu huyo han amsimamo....mi nakwambia usirudi...utaiambia nini familia utaonekana na wewe huna msimamo unapelekwa tuu na demu....

  ReplyDelete
 5. SIKILIZA KAKA ANGU NIKWAMBIE HUYO MWANAMKE NI MNAFKI HANA LOLOTE USIKUBALI KURUDIANA NAE KWANI KAMA NIMAUMIVU USHAYAPATA KWANINI UTAKE KUUMIA TENA JUA UKIRUDIANA NAYE TENA LAZIMA AKIPATA MWINGINE MWENYE PESA ATAKUSAHAU NAPIA KAMA MTAKUA KWENYE NDOA ATATOKA. WASWAHILI WANASEMA DALILI YA MVUA NI MAWINGU KAMA WEWE USHAYAONA MAWINGU KWANINI UTAKE MVUA IKUNYESHEE USIWEMJINGA KAKA TAFUTA MWANAMKE ALIE TULIA HUYO HAKUFAI HATAKIDOGO

  ReplyDelete
 6. kaka yangu ushauri wangu nikiwa kama mzoefu wa hiyo hali maana mimi ilinikuta japo kuwa ni msichana, mwanaume alinifanyia kama hiyo yako then akarudi akitaka turudiane nami kwa wakati ule nilikuwa bado sijajitambua vizuri nikakubali. unajua kilichofata akatembea na mwanamke wa jirani na nyumba yao wakati tumeshatangaza na ndoa kabisa. sikuona shida na ndoa yenyewe sikuitaka na mji nilihama. so nakushauri usirudiane nae maana hatakuja kukutendac kubwa kuliko hili hukakosa kwa kwenda kuomba ushauri. na pia sidhani kama ndugu zako wataridhia jambo hili tena. Sarah

  ReplyDelete
 7. Pole kaka,kiukweli huyo mwanamke hakufai kabisa,kwanza hana heshima,yaani kweli na rafiki yako amediriki kuwa na masiano naye,huyo si mwaminifu atakuja kukusumbua hadi huko mbele ya maisha.Achana naye huyo sio lastborn wa wanawake,wanawake wapo wengi wazuri,ukitulia na kumwomba mungu atakupa mke mzuri tu.Kitendo cha kurudiana nae utaifedhehesha hata familia yako kwakuwa tayari amekutia doa,ila hiyo yote ni mipango ya mungu huwezi kujua huenda asingeonyesha makucha yake mapema ukamjua angekuumiza zaidi maishani,usimsamehe hata huyo hajabadilika ana pretend tu,hapo kilichomrusha ni ndoa,manake wasichana wengi sikuhizi tunapenda ndoa utadhani ndo zinaongeza CV,mwache kabisa si mwaminifu atakuumiza na kingine zaidi ya hiki ukimkaribisha tena.

  ReplyDelete
 8. Pole sana kaka kwa yaliyokukuta, huyo dada hakufai hata kidogo inaonyesha anatamaa za mwili, me ninachokuomba muombe mwenyezi mungu akuleteee mke mwema na mwenye hekima na mwenye kumcha mungu, lakini kuhusu huyo mdada ni malaya atakusumbua tu huko mbele ya safari

  ReplyDelete
 9. pole sana kaka yangu nimesikitika sana nayaliyokukuta hayo tunaita mapito yata pita tu.Mimi kama mimi ninachokushauri huyo mwanamke akufai kabisa atakuwa na ukimwi maana sio mwaminifu kabisa hii tu mko ktk uchumba na ikshakuwa ndoa si ndio itakuwa balaa tena mungu anakupenda sana amekuonyesha mapema usijali wema uliyomtendea fanya kama umetoa sadaka mungu atakulipa mara mia najua kwa kiasi gani umeumia lakini usija kk hauko peke yako huwa inawatokea wengi.Jipe moyo utashinda utashinda majaribu usiache kusali omba mungu akuchagulie mwanamke wamaisha yako huyo hakupagwa kuwa wako kwani kila mmoja amepangiwa mwenza wa maisha yake.sali sana utapata mwingine anayekupenda kuutoka moyani kukujali wanawake ni wengi sana na bado wanazaliwa mwache huyo malipo nihapahapa duniani

  ReplyDelete
 10. Yawezekana mimi nikawa tofauti na wachangiaji wengine, ktk maisha kunamambo mengi.Maisha ya mwanadamu nayafananisha na kinyonga ambae anauwezo wa kujibadilisha wakati wowote.Huyo dada inawezekana kabisa akawa mke mwema baadae,baada ya kujitambua mwenyewe kuwa aliyofanya ni mabaya,hasa baada ya kukosa amani,mikosi na mambo mbalimbali ambayo si ajabu kunamakubwa aliyokumbana nayo mara tu baada ya kukuonyesha kiburi na zarau, hayo tayari ni mafundisho makubwa kwake,na hatakujasahau maishani mwake, na ninakuhakikishia mtakaporudiana atakuwa na adabu ambayo hujahahi hata kuiona tangu mlipokuwa marafiki.Sasa kwakuwa ameshakutia aibu vya kutosha na ndugu wote wanajua,kabla hujamkubalia kurudiana naye tafadhali usimguse,1.nendeni hospitalini ukamcheki afya yake asijekuletea magonjwa.Akiwa hana tatizo aende akawaombe msamaha ndugu zake pamoja na washenga wenu wote kwa usumbufu na aibu aliyoisababisha na pia awahakikishie kuwa atakuwa mke mwema kwako 3.Baada ya hapo mnaweza kurudiana na kurudisha uhusiano wenu kama mwanzo,ukimpa masharti ambayo wewe hupendi afanye.Ninaimani endapoutaamua kumrudia na kuyatekeleza haya mtaishi maisha mazuri sana,tena yenye furaha tele. Sinahakika kama ukimuacha na kutafuta binti mwingi,je huyo utakaempata atakuwa na tabia zipi,si ajabu akakuletea matatizo makubwa kuliko ya huyu aliyekumbuka kutubu.Toba ni kitu muhimu sana ktk maisha yetu.Nakutakia maaamuzi mema.

  ReplyDelete
 11. sasa anataka kurudi kwako kwa sababu kagundua makosa na anakupenda bado au anarudi kwa sababu mikosi imemuandama? maana simuelewi mimi! mikosi ikiisha atakuacha tena. hana msimamo hata kidogo. usile matapishi, kwani wewe mbwa? endelea na maisha yako. mjibu kua tayari una mwanamke mwingine. kakuaibisha kwa marafiki na wazazi, unahangaika nae wa nini. usionane nae tena. maisha yanaenda mbele, hayarudi nyuma.

  ReplyDelete
 12. Kaka pole sana kwa yaliyokukuta! naomba usithubutu kurudiana naye, hana lolote zaidi ya unafiki. Kwani mabinti wenye tabia nzuri wapo, na Mungu atakupa Mke mwema.
  from Lizy- Kigoma

  ReplyDelete