Friday, May 28, 2010

POLENI KWA KUWACHUNIA JAMANI, NILIKUWA NAUGULIWA
Jumapili hii nilikuwa hospitali, Twins wangu walikuwa wanaumwa,  walikutwa na malaria, 
but, many thanks to God, coz wamepona na wako shwari kabisa, kazi ya kuzaa wala sio kubwa
kiviiiiiileeee, issue iko kwenye kulea we! usipime,

tena hawa wawili ndio bonge la issue, maana kila nitakachofanya kwa huyu, basi na huyu nae lazima nimfanyie, nilijaribu siku moja kwa makusudi tu!  nikamnunulia Tymon nguo Trace nikamchunia, we! mbona nilijuta kuthubutu!

mtoto alinililia hadi nilijiskia vibaya, tena alivyo mpanaaa  mtoto huyu, akagoma kukaa na sisi ndani akatoka akaenda kukaa nje kwenye kona ya nyumba peke yake, nikamfata nambembeleza aingie ndani akagoma,

anasema ''mama wewe si haunipendi na mimi sikupendi' nikamwambia nakupenda sana mwanangu, ''wewe ndio dada mkubwa, akanibana tena ''mbona mimi hujaniletea nguo kama tyimo? nikamdanganya baba yako kasema anakuletea ndio maana sijanunua. ndio akakubali kuingia ndani, alipofikia tu kaanza kumchimba mkwara Tymo,'' usikae na mimi kakae na mama yako, namimi namsubiri baba yangu''.
 ila ilinibidi nimwambie baba, lete nguo ya Trace mwenzio nimeyakoroga huku.
akaletewa akawa na amani.

hata kuumwa, mara nyingi unakuta kidada kinaumwa, baada ya muda kidogo kaka nae anaanza vilevile, but all in all uzima wao ndio furaha yangu, wakofresh kabisa sasa hivi,
 tupo pamoja dears, nawapenda sanaaaaaa

weekend njema


4 comments:

 1. masikini, usiwe unawatenganisha jamani, mapacha hadi wakishabalehe ndio huwa wanaacha kufanana baadhi ya vitu, kwakuwa kila mtu anakuwa amejitambuwa, maneno aliyotumia mwanao, yatamkaa ndani ya moyo kwamba mama hanipendi, na ni mbaya sana,
  mapacha wanakazi sana, nasema hivi kwakuwa mimi mwenyewe ni pacha, huwa hatupishani kitu hadi yeye alipooa nami kuolewa, na huwezi ammini, siku ya harusi yake, kumfanyia part nyumbani, beg part, mimi ndio nilikaa nae mbele, na siku ya send off yangu, mbele nilikaa nae yeye, tunapendana kupita kiasi,

  ReplyDelete
 2. pole sana dada violet,
  karibu tena, na nashukuru kusikia wamepona,
  mimi nimejifungua wiki mbili zilizopita, mtoto wakiume, nimemwita jina kama la mwanao, tymon! nililipenda sana. na nikibahatika wa kike nitamwita Trace kama wako, majina ni mazuri na hata wao pia wazuri, Mungu akukuzie jamani, nikiwaangalia hapa nakumbuka ile story yako jinsi ulivyopata nao shida.

  ReplyDelete
 3. awwwwwwwww jamani, pole mamii ndo ulezi, i wish u the best, mungu akukuzie.na mungu awajaalie maisha mazuri na kila la kheri twins wako wakiwa nawakua.

  ReplyDelete
 4. Pole sana kwa kuuguliwa na vipacha vyako lakini tumshukuru Mungu kwamba sasa vime-recover. Mimi pia nina mapacha wa kike na kiume sasa ni wakubwa wana miaka 8 na wapo std III. Kwa namna fulani wamefanana sana tabia zao hata kuugua ni kama hao wako, mmoja asbh mwingine jioni! Lakini suala la kuwatimizia mahitaji kwetu ni tofauti kidogo tulivyowazoeza. Mimi hawalalmiki na sijazoea kuwanunulia kama ngua pamoja labda wakati wa sikikuu tukijaliwa ndo wananunuliwa pamoja. Nyakati nyingine za kawaida nikipita nikaona nzuri ya kike nachukua, mvulana naye tena siku nikiona ya kumfaa namchukulia na kwakuwa ndivyo nilivyowazoea hakuna ulalamishi wala nini. Huwa tu nikimletea mmoja namwambia mwingine safari ya mwisho si unajua nilikeleta wewe anakubali. Nikimpa nasema leo nimepata yako, siku nyingine zamu ya mwingine, sawa? Anajibu sawa. Kwahiyo siku nikimletea mwenzie hakuna ugomvi. Mapacha si kwamba ni wa ajabu sana tofauti na wengine, no. Isipokuwa tu ni namna tunavyo wa-handle na kuwa-treat ndo inajengeka akilini mwao wajione special zaidi ya watoto wengine. Kiukweli mapacha ni watoto wa kawaida tu isipokuwa malezi ndio yanawafanya wawe kama walivyo. Wangu na hivi hawafanani ukimwambia mtu kuwa hawa ni mapacha atakataa.. Lakini hawa wangu wanapenda sijawahi kuona, katika huu umri wao mdogo sijawahi kuona wakigombana na mambo kama hayo, wanapenda sana tena kuliko hata hiyo sana yenyewe. Darasani Kulwa hana uwezo kama Dotto (msichana) kwahiyo Dotto anachofanya akimaliza kazi yake anamsaidia kakake! Nilipata hiyo taarifa nikampiga marufuku Dotto kwamba amwache kakake ajifunze mwenyewe ajue hata kama ni kwa kuchapwa na mwalimu. Ya mapacha ni mengi jamani, tutachosheni bure! Mje mtutembelee nyumbani mshuhudie! Mama wawili.

  ReplyDelete