Tuesday, June 1, 2010

MUMEO NI MLEVI SANA? NA AKIRUDI TU ANAFIKIA KUKUTWANGA? JARIBU DAWA HII INAWEZA KUMSAIDIA

Nimepata rafiki mpya wadau, kama mjuavyo, wanawake tukikutana tu! Basi katika maongezi yetu lazima tufikie sehemu ya kuongelea waume zetu, iwe kwa mazuri au mabaya, lazima tuwaongelee tu! Basi jana akawa ananieleza matatizo ya mumewe, na jinsi alivyofanya hadi mumewe kuamua kutulia, nikamuomba niitoe ktk blog ili iwasaidie na wengine, amekubali. Na ndio naawapa kama ifuatavyo.

Mm nilimpenda sana mume wangu, kupita maelezo, na tangu anioe sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya ndoa,Ila alibadirika gafla sana, akawa na Company ya ajabu ajabu, akachukia hadi watoto wake,

Halipi ada ya shule, mm hanipendi hata kidogo, nimelia sanasana sana. Nimeshtaki kila mahali, hadi nikaona kama Mungu hanipendi vile, Akirudi ni usiku sana, amelewa chakari, akifika tu mimi naanza kulia kabla sijapigwa, labda atanihurumia, alkini wapi, nikifungua mlango tu! Ninae, yani ananipiga bila hata sababu

Siku moja nilichukuwa picha za harusi yangu, nikazitazama, machozi yalinitoka sana, nililia sana, nikapata wazo ambalo hata sijui ni Mungu alinipa au ni akili zangu tu, Ilikuwa siku ya juma mosi, niliamua kwenda salon, nikawaambie wanipambe mimi ni bibi harusi ila kuvaa nitavalia nyumbani, basi walikubali, wakanipamba vizuri sana, na usoni wakaniremba, nilipendeza kupita siku yangu ya harusi,

Nikarudi nyumbani nikachukuwa shera langu, nikalivaa, na kila kitu, na viatu nikashika na ua langu, nikakaa chumbani kitandani, kusema kweli nilikumbuka mbali sana, nililia sana huku nikiwa na ua langu, ni mwanaume niliempenda kwa moyo wangu woote,

Aliporudi akafungua mlango, akaingia ndani, kapitiliza hadi chumbani huku akitukana, basi kufika tu pale, alipigwa na butwaa sana, na pombe zilimwisha, akaniuliza wewe nani? Nikamwambia mimi ni mke wako? Najaribu kufanya kama bado sijaolewa vile, ni kama ndio najiandaa kwenda kanisani kukabidhiwa mume wangu,  maana haya unayonifanyia si ya mume kumfanyia mke, nahisi kama sikuwa nimeolewa, (nililia kwa uchungu sana)
Mume wangu alipiga magoti huku analia nayeye, akasema mke wangu naomba unisamehe, wewe umeolewa, na mimi nimke wako, nisamehe mke wangu , alilia sana, basi hapo hapo nami nikamuleza ninavyojisikia, nini nataka anifanyie ili nijihisi niko kwenye ndoa, nina mume,

Nashukuru alinielewa, toka siku ile hadi sasa tuna raha, kipigo kimekoma, mikwaruzano iliyopo sasa hivi ni ile ya kawaida tu, ambayo huisha bila hata kipigo.(kiukweli jana wakati ananisimulia, nilisisimkwa, na hivi nina machozi ya promotion, we! Yakaanza kulenga lenga, ni akili ya aina yake jamani, amewaza sana, nimependa na nyie wapendwa mjifunze kitu kupitia hili, hata kama hutovaa shela kama yeye, unaweza kutumia njia ingine tu itakayomvuta karibu yako, )

2 comments:

  1. Nimeupenda sana huu Ushuhuda kweli wanawake tunatakiwa kuwa wabunifu kila siku.

    ReplyDelete
  2. kusema ukweli nimefarijika sana na story hii ya huyo dada, na nitajaribu kwa mume wangu pia, maana anachofanyiwa yeye ndicho nachofanyiwa mimi, inaniumiza sana, inanifanya nitamani hata kuondoka nyumbani, mume masaa yote ni mlevi, hata wekend kukaa na watoto hawezi,
    asante violet, ngoja nijipange nijaribu labda atatulia

    ReplyDelete