Wednesday, June 30, 2010

NIMEKUTA CHUPI YA KIKE KWA MCHUMBA WANGU, ANASEMA YEYE HAIJUI NIFANYAJE.


Wadau hapa nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni ushauri wenu, nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu Tanga(ndiko kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka nikiwa nimeshavishwa pete.

Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto wake wote tulio mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na kukuta kweli hali ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu kumuuliza yuko wapi, ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba amesafiri kikazi gafla kwa siku moja tu then kesho yake angegeuza, nikamuuliza inakuwaje huniambii, akasema nimesafiri gafla, hata hivyo nilitaka nikujulishe maana nimeondoka leo.Niliumia sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, mbona mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana? Nilijisikia huzuni sana ila nilijipa moyo

nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto wa mwenye nyumba, nikamuuliza kama kweli mchumba wangu amesafiri,(nikajua labda alikwenda supermarket kununua vitu vya safari) akasema mbona yupo? Na asubuhi nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo pale kwake, akasema atachelewa sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho ndio nije, nikamwambia namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni nimekaa namsubiri, aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na kuanza kunifokea kwanini nisingesubiri hadi kesho.

Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi mkubwa,

Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani, itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.

Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri wenu?


6 comments:

 1. Inabidi ufikirie kama unaweza kumsamehe mtu wa namna hiyo amabaye hata akishikwa live bado anakataa anaendelea kutunga stori. Angekuwa anakuthamini hata kidogo angeomba msamaha alivyo kamatwa. Lakini huyo anaendelea kukudanganya na kukufanya mjinga tena wakati wote mmeona evidence ya viatu na chupi. Sidhani kama kweli anakupenda

  ReplyDelete
 2. Pole sana dada. Huyo mchumba si mwaminifu hata kidogo la muhim ni kuachana naye mapema kabisa usije juta baadaye. Wanaume wengi wa siku hizi ni wadanganyifu sana wanavalisha mabinti pete hata zaidi ya watatu. ACHANA NAYE KABISA HANA MAPENZI YA DHATI HUYO.

  ReplyDelete
 3. Mkazi wa G/mbotoJuly 1, 2010 at 4:16 PM

  Huyo mzushiii tena kimbia, huyo ni mtu wa kucheat hata ukija kuolewa naye ataendelea kucheat. Mimi mwenyewe yalinikuta story inafanana kama yako nikaamua kubwaga manyanga.Hivi sasa nimeolewa na mtu mwingine na nina life nzuri tu ya ndoa. Sasa yule bwana alioa naye mwanamke mwingine lakini ninavyoandika hivi sasa ndoa yake ni balaa maana nasikia mwanaume anacheat kwa kwenda mbele hadi mkewe hana raha na ndoa imevunjika. Hivyo dada kaa chini na utafakari, uchumba si ndoa na kama ulivyoona hivyo umeenda field kidogo mwenzako kacheat.Je baadaye akija kukuoa si hata ukiondoka kikazi huku nyuma atacheat tena.Hivyo kuwa makini kama wanaume wapo tu utapata mwingine.

  ReplyDelete
 4. shosti huyo si mwanaume na inaonyesha mapenzi yamepungua na kama angeuwa bado anakupenda ilikuwa ulivyorudi ukamuita angeitika hata kama yupo na huyo mwanamke wake asingetoa sababu lakini inavyoonyesha mwenzio anapendwa zaid kuliko wewe.cha muhimu kata mawasiliano kama anakupenda kwa dhati na anaujua umuhimu wako atakutafuta.

  ReplyDelete
 5. Mpendwa mdogo wangu,
  Kwanza nikupe pole kwa uliyokutana nayo,kkwa upande wetu sisi Wakristo tunaamini kuwa Mungu hafanyi jambo bila kumjulisha Mtumishi wake.Kwa Upande wako binafsi naona Mungu anakupenda sana sasa kazi yako wewe ni kuamua kusuka au kunyoa kwani uamuzi wa mwisho unao mwenyewe.Kikubwa sana ni kwamba uwe na moyo mpana wa kuweza kuyapokea hayo lakini kama moyo wako ni mdogo nadhani ni kuepuka mapema maana ukiolewa nae utakufa kwa bp wakati kila siku unaletewa taarifa hii na ile.kaza buti mume mwema mtu hupewa na Mungu ni mwema,mpole,mwaminifu,mpenda maendeleo,pia anawapenda watu wa nyumbani mwake akiwemo na mke(mchumba)wake,sio msaliti.Dada tulia Dunia tuliyomo sio ya jana imechafuka,magonjwa ni mengi sasa ukiolewa na mtu ambaye sio mwaminifu halafu asiye na toba utajuta mbeleni.tulia mwangalie Mungu atakuonyesha njia.
  Ni hayo tu.Ninakuombea kwa Mungu akupe Hekima ya kufanya maamuzi mema.

  ReplyDelete
 6. dada pole kwa yaliyokukuta...hiyo yote ni mitihani ya maisha unayopewa na mungu na kukupima una uvumilivu kiasi gani ktk moyo wako...cha muhimu ckiliza pia moyo wako unataka nini na sio kusikiliza ushauri wa watu pekeee..ckiliza na moyo wako pia japo ushauri nao ni mzuri ila pima huo ushauri pamoja na moyo wako

  ReplyDelete