Friday, June 11, 2010

NIMEMFUMANIA MCHUMBA WANGU, AMETUBU NA ANATAKA TUFUNGE NDOA, NIKUBALI?

Watanzania wenzangu naombeni mnisaidie mwenzenu,

Katika maisha yangu yote hadi sasa nina miaka 24, sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine, zaidi ya huyu mchumba wangu nilie nae, nampenda kuliko kitu chochote

Tumeanza urafiki wetu nikiwa na miaka 21 ila mchumba wangu amebadirika sana, alisema atanioa, amejitambulisha na kwetu, lakini gafla, ameahirisha, anasema kwa sasa mambo yamekuwa mengi sana, na hata maongezi yake si ya kawaida, yani anaongea as if amekasirika, sasa ile hali mimi siipendi, kila nikijaribu kupeleleza ili nijuwe labda nimemkosea, sipati jawabu lolote,


Baada ya kuchunguza sana, nikagundua anatembea na secretary wao, na ninasikia tu kwa watu kuwa anataka kumchumbia, nimelia sana na moyo wangu wala hautaki kuamini hili, nilishawahi taka kunywa vidonge nife, dada alinikuta, na kunisema sana, lakini bado akili haijakaa sawa,

Mwezi uliopita rafiki wa mchumba wangu, alikuja yeye na dada yake, wakaomba kuongea na mimi, I thought kwamba wametumwa na Rick (mchumba wangu), kumbe walikuja kwa mengine,

Kilichomleta ni kwamba, anataka kunioa yeye, anadai alikuwa akiichunguza tabia yangu toka siku nyingi na kudai kuwa mchumba wangu si mwaminifu, lakini kwakuwa hatujafunga ndoa, basi yeye anataka kunioa, na dada yake ni mtumzima amethibitisha hilo, mimi nilikataa kata kata, nikawafukuza kwa hasira,

Nilimpigia sim mchumba wangu kumwambia, alichukia sana, akachukuwa company yake, wakalewa wakaenda kumpiga, walimpiga sana, Yule kaka alinitumia sms hii, ‘’ iko siku utanikumbuka’’ dada, sikuamini siku ambayo nilitoka safari, na kupitiliza kwa mchumba wangu nikamkuta na yule secretary wao, nilikwenda moja kwamoja kwakuwa sikumpata kwenye simu kumjulisha kuwa nakwenda. Na ni wiki ile ile ambayo rafiki yake alipigwa,

Toka siku ile moyo wangu umekufa ganzi nilimchukia gafla na nikaona siwezi kuishi bila yeye. alipoitwa na baadhi ya jamaa zangu, alisema kuwa nibahati mbaya tu shetani alimpitia! Ila Bado ananipenda, na anataka anitolee mahari kabisa ili tufunge ndoa, lakini dada yangu ananikatalia maana ndie alienilea toka mdogo. Sasa nishaurini mdogo wenu nifanyaje? Sijielewi, nimsamehe, au nimkubali Yule rafiki yake


4 comments:

 1. pole mdogo wangu,lakini hadi sasa naona kama vile kichwa chako hakijatulia, na ndio maana huna maamuzi sahihi, unahitaji muda tena mrefu sana, wa kukaa na kuamua ufanye lipi.Kuamua jambo wakati una machungu, always utaishia pabaya tu!, suala la kuolewa wewe kwa sasa lifute kwanza ukae uanze upya,
  KUHUSU MCHUMBA WAKO
  Nikwambie vile nihisivvyo mimi, huyo hakupendi, si alikwambia ana mambo mengi? hawezi kuoa kwa sasa, sasa hizo hela zimekuja baada ya kumfumania? tena umshukuru Mungu kwakukuonyesha mapema, huyo hakufai dear, achana nae, akikuoa huyo ndugu yangu, itakula kwako,
  RAFIKI WA MCHUMBA WAKO.
  Unaweza kuanza kumuingiza kwenye akili taratiibu, uone kama atakukaa, lakini sio kukurupuka kisa umefumania, basi ndio na wewe utake kuolewa, coz nae hujaijuwa tabia yake, wewe kuwa mtulivu, mwambie nae kama anakupenda akupe muda, ili utulize kichwa
  KUHUSU KUTAKA KUJIUA
  Mh! hivi unaanzaje kuchukua dawa, kuweka mkononi, unachukuwa na glass ya maji, DU! ila wanawake wengine majasiri kha! mimi hizo paracetamol 2 tu kumeza isue, kwanini ufe coz of man? why? kwani yeye ndio kakuleta duniani hapa, ana kipi hasa ambacho wanaume wengine wanavyo na wamemzidi kabisa? ah!mimi naomba hilo wazo lako uliuwe kabisa, usirudie
  ukishajiua unaenda mbingu ya nani?? ni bora mateso unayopata hapa au adhabu utakayoikuta kule? haya ukishajiua utamzuia huyo Rick kuoa au ndo utampa nafasi nzuri, HEBU MUWE MNAFIKIRIA KWANZA JAMANI,
  kuhusu kuniona mimi,usijali tutaonana mpendwa wangu, mradi umenipa namba yako, basi nikiwa free tu nitakupigia then tutaongea mengi
  CHA MSINGI, CHUKUWA MUDA, FIKIRIA KWANZA USIKURUPUKE TU!

  ReplyDelete
 2. Pole Dada. Huyo mchumba wako hakupendi tena,kakulamba vya kutosha kwa muda mrefu hadi ameshakinai,sasa anatafuta wengine.Wewe ulikuwa na mapenzi ya kweli kwake ndo mana ulimuachia mwili wako apakue anavyotaka,yaani alikuwa kama alishakuoa. Hilo lisikutie shaka kabisa,tena wewe bado mdogo,anza kumsahau kabisa na hata huyo mwingine anaetaka kukuoa nionavyo wala hakufai,huyo alitumia tiketi ya tabia mbaya ya huyo mchumba wako ndo akaanza kukufuata.Waache wote hawakufai utampata mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwako na mtaoana na kuishi kwa amani.
  Acha ujinga wa kufikiria kujiua,hilo si suluhisho la matatizo.

  ReplyDelete
 3. Pole sana mdogo wangu kwa machungu yaliyokupata, lakini pia usijali sana hiyo ni mikasa tu ya mapenzi hamna mtu ambaye hajawahi kupata hiyo mikasa ya mapenzi ni ya kawaida tu wala isikuumize sana, ninachotaka kukushauri hapa ni kuhusu huko kutaka kujiua ndugu yangu, hivi wazazi wako wamekuzaa, wamekulea iwe kwa shida au kwa raha mpaka huo umri uliofikia eti uje kujiua kwa sababu ya mwanaume aliyekukuta mkubwa tu na akili zako asiyejua kuzaa wala kulea wasikie tu umejiua kirahisi namna hiyo. unafikiri itakusaidia nini ndio atasema ulikuwa unampenda sana au acheni hayo mawazo mgando wanaume wapo wengi mwombe Mungu atakupatia aliye mwaminifu sio huyo uliyempata kwa akili zako mwenyewe.Pili usikubali kuolewa na huyo kaka utakuja kujuta baadaye. tatu Mpe Yesu Maisha yako.

  ReplyDelete
 4. Dada kama wewe nimsomaji mzuri wa blog hii utakuwa umesoma kisa cha yule Dada aliyeingia kwenye uke-wenza pasipo kujua,Huyo kijana naweza kusema amejaa tamaa na uharibifu,Dada kataa uke-wenza kwani ni mbaya huta pata Amani,utaishia kujuta wakati wote naweza kusema una bahati kujua tabia ya huyo kijana mapema kabla hujaingia kwake kwa Ndoa.Ushauri wangu kwako ni huu,Tulia mdogo wangu huku ukimuomba Mungu maana naamini Mume mwema mtu hupewa na Mungu,atakupa tu kwani Mungu wetu hawai wala achelewi,mtumaini yeye naye atakufanikisha.
  Ninaamini Mungu atakufanikisha wala usiwe na shaka,wewe ni wa thamani sana mbele za Mungu na Wanadamu kataa mazomeo ya shetani anayokunongoneza kila wakati kwamba kuachwa na mchumba ndio mwisho wa maisha,mwambie shetani mimi ni wa thamani,thamani yangu haipimiki,mwambie shetani mimi ni mshindi,ushindi wa Mungu unanita Nguvu simama kwa miguu yako kudai haki yako kwa Mungu nae Atakupa kisha utamrudishia Utukufu Mungu.

  ReplyDelete