Friday, June 4, 2010

WATOTO WA MUME WANGU, WANATAKA NIACHWE, MAMA YAO ARUDIWE

Nilikuwa na uhusiano na baba mmoja huku kondoa ambae ni mtu mzima sana kwangu, lakini kwakuwa mapenzi hayachagui umri, basi tulipendana sana, na nilipomuuliza kwa umri ule alionao aniweke wazi kama ameoa, alisema walishaachana na mkewe, ila anawatoto watatu mabinti wakubwa wawili wa umri kama wangu, na wakiume mmoja.

alinipeleka kwao mwanza, akanitambulisha kwao, na ni kweli kwamba waliachana na mkewe, basi tukaanza maisha ya pamoja, yeye ni mfanya biashara! Na mm nina grocery yangu. baada ya miaka miwili nikajaliwa kupata mtoto wa kiume, nilimwambia tumeshachunguzana vya kutosha, sasa tufunge ndoa tuishi kiharari, akakubali, wakati tuko kwenye maandalizi ya ndoa alipigiwa simu huko kwao, kwamba watoto wake wanataka kuja, mimi sikuwa na hofu yeyote, nilimkubalia waje tu!

Violet, toka hao watoto wamefika, ndani hatuna amani hata kidogo, tunaishi kama mtu na wake wenzie, mimi kawaida huwa sipendi kuongea ongea lakini watoto hawa wamefanya niongee, Ugomvi kila siku, na kuna siku nilikuwa nafua nguo zangu, mtoto wa mume wangu wa kiume anamiaka 27, akatoa nguo zake zote mimi nifue, nilikataa kwakweli, ukizingatia hakuwa mgonjwa kusema anahitaji msaada, wale wa kike hawataki kufanya kazi yeyote ile, kukicha tu, sitting room kuangalia CD, kupika nipike mimi, au msichana wangu wa kazi wao wanataka kula tu, mbaya zaidi wanasema umemng’oa mama yetu nawewe jiandae tutakutoa, wakati mimi nilikuta wameshaachana kabisa. Na hapa tunapokaa ni nyumba yangu mimi. Baba yao kanikuta nayo

Kingine Hawampendi mwanangu kabisa, kuna siku nilirudi toka kazini, nikakuta mtoto kavimba mdomo wote, hawezi kuongea, nikamuuliza mschana, imekuwaje, akasema Regina (mtoto wa mwsho)wa mume wangu alimsukuma toka mlangoni hadi chini, akaangukia tofali, mdomo ukachanika kwa chini, nililia sana, nilichukia, nikawafata walikuwa chumbani kwao, alichonijibu akasema mwanao mjeuri, nilimuuliza wewe binti mkubwa miaka 24 utagombana na mtoto wa miaka mine kweli? wakati naongea nao walinirukia walinipiga sana,

Wakat yanatokea haya mume angu alikuwa safari, nilimpigia simu aliporudi nikamueleza, aliwasema sana, ila mimi nilimwambia hawa watoto wameshakuwa wakubwa, miaka 24 na 27 na huyo mkubwa 30. Wajitegemee, kwanini wakae kwangu ? nilimshauri awape mtaji wakafanye biashara, watoto walichukuwa pesa, na kuondoka hawakuondoka, na wamesema hawatoki pale, hadi mimi niondoke aje mama yao, sina amani wala raha hata kidogo, nisaidieni mwenzenu.

6 comments:

 1. LOL! POLE DADA!
  Kua na serious talk na mumeo akupe msimamo wake as unaendelea kukaa nao anazidi tu kukuumiza na kwa mtoto wako ni mbaya sana as inamfanya ajione kwamba akubaliki na ni mbaya sana as mtotot wako atakua na chuki ndani ya moyo wake which is not good for her.

  ReplyDelete
 2. nakubaliana na anoy wa kwanza this is right mwambie huyo dady akupe final solution

  ReplyDelete
 3. pole sana dada hapo ni kwako je hao watoto wanaelewa hilo wmambie mumeo awapangie nyumba yao waondoke wakikataa wape nots waambie hapo ni kwako na co kwa bb yao wakigoma nenda kawachukulie rb polis wapuzi hao hawasitiriki ukizubaa wanaweza hata kukuuwa au kukutilia sumu

  ReplyDelete
 4. kwa kweli nasikitika sana baada ya kusoma hi stori pole sana my dada hao watoto hawawezi kukupenda daima wanadhani wewe ndiyo chanzo kuachwa kwa mm yao sasa ongea na mumeo hao watoto warudi kwao haraka sana la sivyo watakusababishia makubwa zaidi

  ReplyDelete
 5. Pole sana dada yangu ndio maisha mwenyezi mungu atakusaidia, hao watoto wachukulie rb kwa sababu hawana adabu wakati nyumba ni yako, hun asababu ya kumbembeleza hata huyo baba naye akkikuletea za kuleta mrushe aende na watoto awake, wanaume hawana dili dada yangu mama yao mmoja kasoro matumbo tofauti.

  ReplyDelete
 6. Pole sana dada yangu! Ila pia wewe dada mimi naona pia umejiletea haya matatizo, kwanini uingilie familia nyingine? Hata kama wakiondoka kwenye hiyo nyumba sidhani kama utaishi kwa amani in case chochote kimtokee huyo mwanaume! Unafanya maisha yako yawe so complicated kwa kuwa na huyo mwanaume, na ukimzalia watoto ndiyo kabisaaa maana tayari ana watoto wakubwa either way you are not safe. Ningependa kukushauri usijishushe maana maisha yako yatakuwa ni drama tu hata ufanye nini hawawezi kukupenda na hao ni watoto wake hata ufanye nini hawezi kuwakataa. Damu ni nzito jamani.
  My dear, tafuta mtu atakayekupa amani na upendo kuingilia ndoa ( maana ni kifo tu ndiyo kinatenganisha watu hizi njia zingine ni excuses tu kwasababu huyo mke wake wa kwanza hata mbele za Mungu anatambulika). Tafuta ndoa yako na nyumba yako, I hope utapata nafasi ya kusoma hii kabla hujazaa na huyo bwana. Kila la kheri :)

  ReplyDelete