Monday, June 28, 2010

KARIBUNI KATIKA CLUB YA NDOA ZAKAYO NA WITNESS

This weekend tulisherehekea harusi ya mtoto wa wifi yangu, Zakayo aliemuoa bibie Witnes, ilipendeza kiukweli, tulienjoy sana, sasa hebu cheki pic hizi, waweza pata some styles

waliingia kwa style yao, walikuwa wenye furaha na kujiamini sana, ''niliipenda hii'', umeona eee, Bi harusi kambebea mumewe Koti

kati kati ya ukumbi akamvalisha,

anamfunga vishikizo, jamani raha sana, nilimpenda huyu Bi harusi, yani always alikuwa anatabasabu,
mie nae sikukosa, ninavyopenda shughuri we!

Mume wangu nae alikuwepo kumpongeza mjomba wake,


Abilia chunga mzigo wako wewe!!!!!!!!!!!!

Wasimamizi wao pia walikuwa wacheshi, wote walikuwa na furaha


shemeji yangu na mimi, Ba trace na mke mwenzangu, was fun sana tu!


hivi ndivyo ilivyoonekana keki kwa juu,

na hapo ndio full,

i like this style, badala ya kupeleka keki kwa wakwe mmezibeba, sasa hivi zinapelekwa na kigari kama hicyo, huku vile vitoto vya mbele vikiwa vinaendeshwa na matroni wao '' ubunifu wenye maana sana huu'' ni baraka tu!

Maids wa kike

wakiume nao hawa

enjoy dears

10 comments:

  1. jamani mmependeza sana, nimependa hiyo picha uliyopiga na mumeo mnatazamana, nimewapenda sana, wewe ni beautful na mumeo ni handsome, nawapenda, na kweli wewe unapenda shughuri, hahahahahaaaaaaaaaa, nafurahi sana mtu akijijua anapenda nini na anachukia nini, maana kuna wengine, hawajui wanachopenda wala wanachochukia,
    kwakweli nimewapendasana, mbarikiewe

    ReplyDelete
  2. ASANTE KWA PICHA
    NAKUPENDA SANA DADA VAI

    ReplyDelete
  3. sio shughuri ni shughuli
    hiyo harusi ilifanyika kijiji gani?maana style ya nywele za bi harusi mmmmmh
    otherwise ninawatakia maisha mema na marefu yaliyojaa upendo

    ReplyDelete
  4. jamani walipendeza sana, hata nyie mmependeza sana, nawatakia maisha mema ya ndoa yao, mungu awabariki wakazae watoto wakike na wakiume, nimekunwa na style yao ya kuingia, ''cute'' nimependa style ya ua lako la kichwani, nimependa pozi za mumeo pia, hahahaaaaa just jokin dear, usiache kuruhusu comment yangu, nimewapenda wooote, kwenye harusi ya mdogo wangu nitakualika violet, nitakupigia simu itakapopangwa tarehe rasmi,

    ReplyDelete
  5. shost uliesema hujapenda style ya nywele za biharusi, hebu piga tengeneza zako (style nzuri ya kimjini mjini) then unitumie ili tuione, tujifunze kutengeneza nywele kupitia wewe, utakuwa umefanya jambo la msingi sana kukosoa huku ukionyesha mfano,

    ReplyDelete
  6. Jamani mmependeza, huyo anonymous aliesema style ya nywele mbaya, ni mshamba tu! hiyo style ndio imeingia sasa hivi, nyuma unashonea waving mbele unabana bomba, usikute yaya hana hata nywele, wabongo bwana kwa kukandia vyetu!, woote mmependeza,
    MAISHA MEMA KWAO

    ReplyDelete
  7. Mambo vai nawapa hongera hao maharusi na wamependeza nanyi pia na mmeo mmependeza.japo kuna vitu ambavyo naona havijakaa sawa natoa ushauri japokuwa hiyo ndoa haitarudia ila ushauri wangu ni kwa wadau wengine wa blog hii.kasoro nilizoona moja ni kuhusu upambaji wa ukumbi sehemu ya high table. ukiangalia hiyo picha waliyosimama wasimamizi wa maharusi sehemu ya katikati kuna mapambo mengi yamekuwa kama kichaka at the same time na pembeni yapo.kwa hiyo nadhani hili ua la katikati lisingekuwepo au linekuwepo dogo tu. hapo ni dhahiri kuwa walipoketi maharusi mtu akiwa mbali inakuwa ni vigumu kuwaona vizuri na wakati siku ya harusi macho yote huelekea kwa hao wapendanao. Jambo la pili ni keki. Imekuwa very complicated sidhani kama kulikuwa na haja ya kuweka dude lote hilo kuhandle keki tu mi naona ni style ya kizamani kidogo. hata kama partition za keki ni nyingi wangetumia stand ndogo ya kawaida na sio hiyo nguzo ndefu kama mnara wa simu. Ni hayo tu dada angu ni mtizamo wangu wadau km ni point ichukue kama ni pumba ipotezee. AHSANTE KWA KUPOST COMMENT YANGU DA VAI

    ReplyDelete
  8. nimependa ushauri wako dear, ukiangalia ni kweli, ndio raha ya kushauriana hii, itawasaidia wengine ambao hawajaolewa kutofanya makosa madogo madogo kama haya, ulichoongea mpendwa ni sahihi, we are a human being, naweza ona sawa kumbe si sawa, naweza ona si tatizo kumbe ni tatizo, kama ambavyo umeona wewe, mimi sikuona kama ni tatizo, lakini baada ya kumention kama hivyo, nimeona ni kweli mbele kulikuwa giza sana, kijani kilizidi, asante nimependa ushauri wako dear!

    ReplyDelete
  9. hongera kwa maharusi but penye ukweli tuseme. bi harusi mzuri japo nguo na mapambo hawakumtendea haki suti ya bwana harusi wangevaa hata waist coat imekuwa too formal kama anaenda mkutanoni na mapambo kama mdau alivorekebisha juu na nguo za maids hakuna hata mapambo kichwani?all in all nawatakia pongezi muhimu ni kufugna ndoa sherehe ni kitu baki.

    ReplyDelete
  10. To be honest, harusi kama ya kijijini, naona Vai ndo ulipendeza.

    ReplyDelete