Wednesday, July 7, 2010

NIMEOA MKE MCHAFU SANA- NITAVUMILIA UCHAFUU HUU HADI LINI??

Mke wangu ni mchafu kupindukia, nimesema sana hadi nimechoka, imefika kipindi namsusia hata chakula, maana mazingira anayopikia tu! Unaweza kutapika, lakini wala hajali, na anafuraha kabisa, hali ambayo imenifanya nishindwe kuelewa nimuweke kwenye kundi gani,

Kabla sijamuoa hakuwa hivi, alikuwa akijitahidi sana usafi, baada ya kumuoa tu! Akaanza kudai housegirl, nikamuuliza, housegirl wa nini wakati huna kazi, upo nyumbani tu! Wala mtoto huna? Akawa mtu wa hasira sana, akaagiziwa huko kwao akamleta, nilishindwa kuzuia, nikawa namlipa tu!, alipojifungua ndio kabisaaaaa, uchafu umezidi, housegirl ndio amekuwa kama mama wa mtoto, yeye ni usingizi na kuangalia TV tu,
Jaribuni kumsema nyie wanawake wenzake labda ataelewa, na kweli kwakuwa bado yuko nyumbani, nitaprint comments zoote nitampelekea asome, labda itasaidia, wala sishawishiki kumtafutia biashara, maana hajawahi hata kuniambia nimfungulie hata biashara, yeye ni wakudai mafuta ya gari, ashinde anazungukaa, jioni anarudi, hadi nahisi sijui nimeoa changu doa, mwanamke gani safari haziishi? Hata siku za weekend mimi nipo nyumbani, yeye anaondoka.

Blog hii nimepewa na dada yangu, ndio nimeona bara niombe msaada wa mawazo yenu,

Wakati mwingine mtoto anaweza vikwa pampas akajisaidia, hadi choo kikaganda, bila kusafishwa, kuna siku nilipata hasira sana ,nikamuwasha vi bao, mtoto alinyea shuka asubuhi wakati natoka, nimerudi jioni nakuta vile vile, namuuliza kwanini hujasafisha, eti anajibu alipata safari gafla akatoka nae amerudi jioni, kwanza hajaaga, pia hata usafi tu! Safari gani hiyo hadi usahau usafi wa familia yako,

Huwa najuta kwanini nimeoa, ndio kwanza ndoa ina miaka miwili tu! Ila nimechoka sana utadhani nimeoa mika kumi iliyopita, nilimshtaki kwao, wakasema ndio alivyo, hadi dada zangu wamemsema lakini habadiliki, sijui anashetani gani la uchafu,

Violet na wanawake wenzie, hebu mshaurini huyu kiumbe abadirike.

6 comments:

 1. pole sana kaka wanawake wengine hawaoleweki cha kukushauri mrudishe kwao kwanza akae na umwambie mpaka utakapomfuata ila uwe unafanya utafiti kwa watu wake wa karibu kama amebadilika ila wasiwe ndugu zake wanaweza kumfichia siri hata kwa malipo ya mpelelezi wako lipa tu ili mradi ujue amebadilika, ukiona hajabadilika hata kwa muda atakao kuwa kwao wala kujuta, utaamua wewe mwenyewe ukae naye huku utaendelea kuvumilia na kuchukua msalaba wako ama kuachana naye yote yamo mikononi mwako.

  ReplyDelete
 2. hi kaka
  pole sana kwa yaliyokukuta huyo hana hata chembe ya kubadilika,,, nakuonea huruma, lakini inatakiwa umtafutie mwanamke mwingine akuone naye ajue kwamba umemchoka sana labda anaweza akabadilika...
  pia jaribu kumpa adhabu ambazo akikuona atabadilika tu utakuta usafi upo.

  ReplyDelete
 3. Nakupa pole:
  aliyekupa ushauri wa kumtafutia mwanamke mwingine siyo sawa...unaweza kukutana na bomu zaidi ya mkeo... labda kama ulishafanya hivyo.. ila nakusihi acha mara moja kwani umeamua kuomba ushauri inaonekana bado unamthamini...kila mtu ana weakness zake lakini kwamaelezo ya uchafu aliyonayo mkeo si weakness bali ni TABIA.Kitu cha kwanza fanya uchungzi yakinifu,tumia mtu ampeleleze kuhusu kuzurura kwake,vilevile jaribu kupekua simu yake ila uwe tayari kwa lolote utakalolikuta,kama hujaona lolote linalohusu Infedility/cheating basi jua tatizo lake ni UCHAFU na SIYO UHUNI.
  sasa,najua ulimpenda ndio maana ukamuoa,mnachotakiwa mfanye kitu kinaitwa "MAZUNGUMZO" kama ni siku nyingi hamjatoka,sasa huu ni wakati wa kutoka,just the 2 of you,kama kutoka mnaona haifai,basi andaa mazingira mbaki peke yenu nyumbani ili myazungumze..fanya iwe tofauti ili nae ashtuke why this...? mshike mkono nenda nae kukagua maeneo ya nyumbani:jikoni,store,kitandani kabatini hata ikibidi kagua nguo zake za ndani.. nguo za mtoto n.k, mwambie..hujawahi kuona mwanamke mchafu kama yeye..kama ulikuwa na girl friends kabla yake mwambie ni jinsi gani walivyokuwa wasafi...na kunawakati unajuta kwanini ulifunga nae ndoa..mpe muda wa yeye kujirekebisha..tena u have to be serious hapa ili aelewe..mpe adhabu kwamba hutakula chakula nyumbani hadi uridhike na usafi wa jikoni,mashuka kama unaspear ya godoro au chumba kingine hama chumba au lala chini..mwambie ajifunze kuoga au kubadili mashuka ndio utalala nae kitanda kimoja,kama saa mbili ulikuwa unarudi nyumbani anza kurudi saa sita au hata saa nane fanya hivi kwa muda mchache ili uone kama atabadilika,asipobadilika u have to pretend kama u have a girlfriend outside ila usifanye kweli,try to be busy na simu usiku,punguza kumjali kama yupo mature enough ataelewa na kubadilika kama hata badilika basi ujue huo ni msalaba wako na kama ukishindwa kuubeba,wewe sio wa kwanza kudivorce.Ila kabla hujafikia maamuzi hayo,jaribu kumpa muda.

  All the best.

  ReplyDelete
 4. Habari kwanza pole,ni hivi miee nakuomba kwa hisani yako nimfundishe adabu mkeoo kama unataka atabadilika huyo wala usianze kuchelewa nyumbani kama huyo dada anavosema hapooo,maana ukichelewa nyumbani utaenda wapi jamani si ndio utapata vishawishi huko nje??ushauri wangu wewe nipigiee ama ni text miee kwenye number hii 0044 7787030793 sitaki kuwa na uhusiano na mume wa mtu bali nataka tumfundishe mkeoo,then mie nakua nakupigia wala hatuongei mabaya bali maisha tuu umuone ndani ya week naimani atabadilika tuuu huyoo,anakuona bado unamdekeza na wala usimfukuze wala chumba usimtenge hizo ndio raha na shida mlizofungia pingu za maisha kaka yangu.so am waitin,,,,usiwaambie pia watu wengi maana baadae ukija kuya settle atakosa amani mkeoo,hope umenifahamu.pole yataisha

  ReplyDelete
 5. cha msingi jaribu kuongea nae, pia unaweza ukawa unafanya nae usafi,na ikishindikana zaidi unatakiwa uwe unamchapa vibao viwuli vitatu kila unapomuambia kitu anagoma kutekeleza, hiyo ndo dawa pekee,,, na sio jambo la busara ukamwacha awe anazurura kuna leo na kesho kama mna mtoto wewe kama hupo ataweza kwali kumlea kwa tabia hiyo,,, wewe kama mwenye nyumba unatakiwa uwe mkali,,,yes kuwa mkali,, mchape vibao,, asipibadilika mrudishe kwao kwa likizo fupi,, naamini atabadilika, mpangie budget kaka sio kila akiomba pesa unatoa tu kumbuka kuna leo na kesho,,,

  ReplyDelete
 6. huyo mwanamke anabidi arudi kwao akafundwe jinsi ya kuishi na mume kuondoka bila kumuaga mumeo ni utovu wa nidhamu,uchafu ni sumu ya mapenzi inaua mapenzi kabisa pia tabia ya kubweteka kusubiria mume ndio mtafuta riziki atakuja kujuta sdababu hatujui nani atatangulia mbele za haki,sasa akitangulia mwanamume na mwanamke amezoea kubweteka mtoto atamlea vp,MWANAMKE JIREKEBISHE UTAKUJA KUJUTA.

  ReplyDelete