Monday, June 21, 2010

NILIKUWA NAUMWA JAMANI - NILILAZWA, BUT NOW IM GUD
Sijawatupa, tena niliwamisi vibaya mno wapenzi wangu, but nilikuwa mgonjwa, vidonda vya tumbo vinanisumbua sana, nililazwa pale Dar Group, but now namshukuru Mungu niko safi kabisa, na ninaendelea vizuri, Im back dears.


kwenye ward yetu tulikuwa wawili, nikapata na shost humo humo, kitoto hiki kinaitwa Rachel au Nyambura, kilitokea kunipenda sana, hadi kulala kikawa kinataka kulala na mimi hakimtaki mama yake, nikichomwa sindano nikikunja uso, kinaanza kulia chenyewe, huku kinanipapasa,


kwakuwa chakula kilikuwa hakikai tumboni basi, nilipopata nafuu nilikuwa nasikia njaa hadi miguuni, nilikunywa juice kama maji, coz ndio iliyokuwepo kwa kipindi hicho, jamani vidonda vinatesa lo! halafu vinatokeaga gafla tu jamani,


at the end of the day, nilipata discharge na kumuacha shost wangu hospitali, wakati natoka mtoto alinililia sana, mama yake akaniomba nimsubiri ambembeleze alale ndio niondoke, yeye shost alikuwa ana malaria, hata hivyo ni kajasiri sana, yani kalijikaza kweli, basi nilimbembeleza mwenyewe, hadi akalala kabisa ndio nikaondoka, nashukuru Mungu after two days mama yake akaniambia nao wameruhusiwa,

all in all narudisha sifa na utukufu na shukrani za pekee kwa Mungu wangu, kwa kunitetea na kunipa nguvu, uponyaji na afya,6 comments:

 1. pole sana mama, lakini mbona vidonda vya tumbo vinatibika? na ukizembea vinaweza hata kuuwa, nakushauri usiwe unakasirika, usiwe unawaza, upe moyo wako nafasi, na mungu atakuponya, nimempenda recho, msalimie

  ReplyDelete
 2. Pole sana dada Violet....

  ReplyDelete
 3. masikini,
  pole mpenzi wangu, mungu atakusaidia utapona, usiwe unakasirika, hiyo ndio dawa kubwa ya aussas, yani usichukie, ukichukia tu! unaviamsha, pole sana mdogo wangu, Mungu akurehemu
  nimekihurumia kirecho jamani, nahisi kama alivyoamka akakukosa alilia sana. bora kama kimetoka salama.
  zainab

  ReplyDelete
 4. pole dada yangu

  ReplyDelete
 5. Pole sana dear, You just cast your sickness unto God, He is our healer!

  ReplyDelete
 6. Pole mwaya, Almighty God is going to heal you forever, kwakuwa hiyo kitu inatibika!!Masikini Rachael, pole yake ingawa nimekaonea huruma sana. Shost karibu Mbeya mamii,karibu sana nakusuburi kwa hamu kwani pia nitakuwa na kazi na wewe. Stay blessed you and your family.
  Mumy Jnr.

  ReplyDelete