Tuesday, June 22, 2010

MUME WANGU ANANINYANYASA NA HATAKI KUNIPA TALAKA-NIFANYAJE

Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 40, niliolewa miaka 25 iliyopita, lakini hadi sasa na utu uzima huu sina mtoto hata mmoja, baada ya kujiona nina matatizo, nilimruhusu mume wangu azae na mwanamke mwingine, alizaa nae mtoto mmoja ambae sasa ana miaka tisa, lakini baada ya mtoto kufika miaka miwili Yule dada alipata ajali akafariki, hivyo mtoto akahamia kwangu na nikamlea hadi sasa, kama mwanangu na ananipenda sana.

Kuna siku nikiwa nyumbani kwangu  nilipigiwa simu niende buguruni, nikaambiwa wewe mtu mzima ni (dawa) jikaze, mumeo anaoa leo, unalijua hili? Nikawaambia hapana mume wangu ameniaga anasafiri kikazi, wakasema muongo, mumeo anaoa (wakanielekeza eneo la shuhuri ili niende) nilijikaza nikanyanyuka na kwenda, nilipofika hilo eneo nilikuta kweli harusi kubwa, vyakula na taarab inapigwa, nilijibanza pembeni nililia sana, na nilishuhudia kwa macho yangu na kumuona mume wangu,

Kilichoniumiza kwanini mume wangu anifiche kitu kama kile? Kwanini asiniambie tu kama anataka kuoa, kwanini afanye siri? Basi sikufanya lolote, nilikubali matokeo nakurudi kwetu Kisarawe, baba yangu alinisihi nirudi nyumbani kwa mume wangu, hadi anipe talaka ili tugawane mali tulizochuma pamojan, nikarudi. baada ya wiki moja mume wangu akarudi, hakujua kama hata kwenye hiyo harudi nilienda na kushuhudia nikiwa nimejitanda vitenge na nikaondoka, , cha ajabu hataki kunipa talaka, anasema kama unaenda wewe nenda, ila mimi najua kuoa tu! Sijui kuacha

Mimi sikumuuliza kitu, ila hakuwa na amani, nilipoona yupo kimya niliamua kuanza kumuuliza, mwanzoni alikataaa, nilipomshikia kisu na kumtishia, ndio akakubali kuwa ameoa na akaomba msamaha, tokea pale sikumwamini tena,, na chuki zikazidi, mbaya zaidi huyo bi mdogo ni mtoto mdogo sana, ni sawa na mwanawe wa kuzaa,

Huwa anakuja kwangu, eti kumsalimia Yule mtoto ninaekaa nae, kuna siku alikuja na kutaka kuondoka nae, nilimkunja, nilimpiga sana, nilimuumiza, toka siku ile, mumewangu nae hanipendi,

Sasahivi Napata tetesi kutoka kwa watu kuwa anataka kuuza nyumba hii tunayoishi, na isitoshe analeta vitu ndani bila hata kunitaarifu, mimi nayeye tunazaidi ya miaka 25 ya ndoa, yani ananibagua sana, hanishirikishi kwenye chochote kile, sasa na utu uzima huu akiuza nyumba ahamie kwa huyo bi mdogo mimi nitaishi vipi? Na hataki mimi nifanye kazi yeyote ile, toka aliponioa, hataki nitoke,

Tumejenga nyumba mbili pamoja, tumenunua magari mawili na daladala moja, lakini hata mahesabu ya daladala sikuhizi sipewi mimi, yanapelekwa kwa bi mdogo, sina amani wala furaha hata kidogo, nifanyaje?

6 comments:

  1. duuh!pole sana,inasikitisha sn..kwann wanaume hawa makatiri kiasi hiki?mi ushauri wangu
    1)nenda mahakamani ukadai talaka yako kabla hajauza hiyo nyumba.ili mje kugawana sawa ivyo vitu.na kila kitu kitaamuriwa hapo mahakamani kwa haki,
    2)kaa mbali na huyo mke mdogo na usimruhusu kufika kwako hata mara1,mnafki sn huyo huyo ndo alosababisha yote hayo,mtt mdogo kuchukua wazee ka baba ake ndo nn?
    3)usimfikirie huyo mwanaume ingawa inauma sn,inabidi ujikaze na ujipe moypo kuwa unaweza kuishi bila yy
    4)ushajua maovu ya mumeo ss akili kumkichwa,anza kujishughulisha na biashara i hope mda wote mliokuwa mkiishi kwa amani utakuwa unakijiakiba kidogo,other wise naweza kusema hujachelewa kitu chochote unaweza kusimama ww mwenyewe ktk maisha yako na kamwe usikubali kurudi kwenu na begi lako tu km ulivyofika kwa mumeo weka nia nautafanikiwa tu mungu yupo pa1 nawe na anaona jinsi unavyoteseka,malipo hapa hapa duniani watakiona cha moto ipo cku yao ama zao ama zako ila kumbuka kumuomba mungu sn.pole sn ndugu yangu

    ReplyDelete
  2. pole sana my dada sasa nenda mahakamani ukadai haki yako usikubali nyumba ikauzwa mwanamme akikaa na mwanamke miaka mitatu mkiachana mnagawana mali usikubali kirahisi kama mna nyumba mbili akupatie moja aende kwa huyo kimada wake lakini ipo siku atakukumbuka muombe mungu malipo ni hapa hapa duniani

    ReplyDelete
  3. pole mama yangu, Ondoka huyo jambawazi anataka kukudhurumu mali mlizochuma wote, pole sana mama, jaribu kufata alichokushauri huyo mdau hapo juu, nimeumizwa na mkasa wako mama, pole sana

    ReplyDelete
  4. polesaamma yangu mie nina umri wa mika 22 sijaolewa walasijawahi kupendana tkt maisha yg ila huwa nafatilia mambo mengi yamapenzi.so mambokama ayo mama yangu aliwahi kuyapitia ila alikuwajasiri na akayashinda.mimi nacho ona cha 1 chukua hati zote za nyumba zihifadhi sehem cos unaweza kutolwandani ya nyumba bila kujua.afu ndi uende mahakaani pia uwe makin sana na mume wako anawea hata kukuuwa sababuya mali mamaumbamunguatakusadia hayo nimajariu tu ya dni pole sana mamangu

    ReplyDelete
  5. mmmhhh sijui nianzie wapi, kwanza nitoe pole kwa kinachoendelea kwenye familia yenu, mimi naomba nitofautiane na wachangiaji waliotangulia, napata wasi wasi kidogo, pamoja na kutomzalia mtoto huyu mume bado ameendelea kuishi na wewe hii kwangu inamaanisha kuwa anakupenda, ukamruhusu akazae nje akakubali na bado mkawa pamoja hili nalo bado linaashiria upendo wake kwako, lakini wasiwasi wangu umeanzia hapo mama wa huyo mtoto kufariki na wewe kumpiga huyu mke mwenzio hadi kumuumiza, kumbuka yeye hana kosa amependwa kama ulivyopendwa wewe sasa kwanini umpige? mimi nahisi wewe unaukatili fulani na pengine ndio kinachomfanya huyo mumeo akatafute amani kwingine, ushauri wangu kwako ni mmoja tu jichunguze kama wewe ndio chanzo cha huyo bwana kwenda kutafuta amani ya moyo wake kwingine, ukipata jibu lifanyie kazi, kuna sehemu imeandikwa mwanamke mpumbavu hubomoa ndoa yake yeye mwenyewe, sasa angalia usiwe mwanamke mpumbavu, hizo mali unazotaka kupigania si lolote kama huna amani moyoni, wangapi wameachiwa kila kitu lakini wanaishia kujinyonga wenyewe baada ya nafsi zao kuwasuta?

    ReplyDelete
  6. duh,mamaangu kweli roho inaniuma sana niliposoma mkasa wako, mm ni sawa na mtoto wako sina cha kukushauri ila namwamini tu mungu kwamba hakuna lililomshinda, wala huwezi kumuomba mungu mkate akakupa jiwe, piga magoti mlilie mungu mweleze yanayokusibu muombe akufungulie milango yake, akuonyeshe nyia ya kutokea kwenye huo msalaba

    ReplyDelete