Monday, March 22, 2010

RANGI GANI YA GAUNI LA BIHARUSI INAFAA KUVALIWA SIKU YA HARUSI?

Nimekuwa nikuhuduria sherehe za harusi kwa miaka mingi sana na hata yangu pia nilikuwa muhusika. Ni siku watu huwa na furaha na wanapendeza sana kwa mavazi maalum yaliyoandaliwa kwa siku maaluum pia. Lakini kuna jambo nahitaji kujifunza na kuwafunza na wengine ambao pia hawafahamu kama mimi. Huwa najiuliza :Je ni rangi gani ya SHELA inatakiwa ivaliwe na BIHARUSI gani? Hii sina maana ya kuwa ni mweupe/maji yakunde au mtanzania harisi/mweuzi. Ok ina weza kuwa point ila point yangu ni hii. Wanawake anayeolewa akiwa mwanamwali/bikira nasikia ndio anatakiwa avae SHELA jeupe peee na mwanamke ambaye si mwanamwari avae rangi yoyote apendayo.  Hapa mimi bado sijawekwa sawa kabisaa na bado sijafumbua jibu kwanini iwe hivi? Naamini kunawenye upeo mkubwa juu ya hili watatufunza wooote. Naomba maoni yenu.10 comments:

 1. kiukweli mamy nguo ya harusi white ndo inampendeza bi harusi bwana, mmh kuhusu kuvaa mwanamwali sijaisikiaga kwakweli. lakini nyeupe mwake mwake

  ReplyDelete
 2. Wow! violet nimefurahi sana kuona comment yangu. Sarah

  ReplyDelete
 3. hata mie niko nawe dada angu. White inavutia ile siku bwana, na hata picha zake zinapendeza sanaaaaaaaaa. sema kwa cie waislam ndo tuna baadhi ya rangi unatakiwa uvae kwenye kale kasiku unapokula kiapo, na kwa undani sijalifuatilia ni kwanini.

  ReplyDelete
 4. hivi dada violert
  tuongee ukweli kabisa
  dunia ya sasa kuna mtu anaeolewa akiwa bikira?
  teh teh teh, wanaume wenyewe hawafagilii bikira, mh! katika mia utakuta ni mmoja,
  ah , kwanza hakuna,
  nirudi kwenye mada,
  Shela rangi yake ni nyeupe, maana ile rangi inamaanisha vitu vingi, upendo, amani, usafi, na vingine vingi, ila siku hizi sijui ndio fassion, sijui ndio nini, mtu anavaa shela la rangi ya pinki, kha!, au anavaa rangi ya puple, yani kusema ukweli mm huwa inanikera sana hii, shera ni jeupe jamani, mkatae mkubali, kila kitu kinatakiwa kuwa cheupe, huu utaalamu tulionao wa kufoji kila kitu huu mh! yatatushinda

  ReplyDelete
 5. Kwa ninavyojua mimi, rangi zina maana kubwa kikanisa (Katoliki). Ndoa ni sakramenti ya kanisa hivyo ki-litrujia mtu (bibi harusi) anatakiwa avae shela nyeupe. Rangi nyeupe inamaanisha mwangaza, utakatifu, usafi wa moyo, furaha, shangwe, nk. Ukizingatia umuhimu wa siku yenyewe ni ajabu kuona mtu hasa mkristo amevaa shela ya rangi tofauti ukishajua kwamba kila rangi kwa kanisa ina maana kubwa. Hata kama si bikra haijalishi kwani kwa mjibu wa mafundisho, anayekwenda kupokea sakrament ya ndoa sharti awe na moyo safi na mweupe kwa kupokea kwanza sakramenti ya upatanisho (hapo ya kale yote yanafutwa na tazama anakuwa mpya!)ili aanze maisha upya na mapya akiwa na neema ya utakaso.

  ReplyDelete
 6. hakuna lolote, nyie wote mnaosema shela ni rangi nyeupe, mlimuona nani ameanza na vazi jeupe? shela ni vazi kama vazi lingine, unaweza funga ndoa umevaa hata vitenge au panjabi, mnajifanya wanzunguuu,
  na wewe violet unasapoti hilo la kuvaa shela lolote? kazi kuiga wazungu tu, nani kwenye bibilia zenu au kuruani amevaa shela jeupe? msikuze mambo kwa kujifanya mnajua,
  wala msitishe watu, kila mtu anavaa atakavyo hata baibui unavaa ndoa inafungwa, hata ukitaka kuvaa kaniki ndoa inafungwa,

  ReplyDelete
 7. mh! kazi ipo,
  ulieniuliza mimi nasupport kuvaa shela jeupe,
  NI KWELI, nasupport tena kwa nguvu, kwamba shela linapendeza sana likivaliwa jeupe peeeeeeeeee. apart from colour, inapendeza sana rangi nyeupe, hii ya kusema mtu uvae kitenge mh! au bazee au panjabi, DUH! MH! SIJUI, MAENEO HAYO MIMI NI MGENI, NA wala sitasuport, kwa upande mwingine mtu aweza sema hana uwezo wa shela labda, anashona bazee, sasa garama ya bazee si unaweza nunua hata satin nyeupe nzuri, ukashona kiblaus chako simple na skirt yako ndefu iliyokushika kidogo, ukanunua kijiresi cha shilingi 4000 ukachona kile cha kichwani, gharama si nizile zile? ah! tubadilikeni jamani, mama yangu kafunga ndoa miaka ileeeeeeeeeeeee, na alivaa shela jeupe, iweje mie nivae bazee? hiyo wala hainiingiii akilini, wala hainogi kusema ukweli
  lo!

  ReplyDelete
 8. Ki-orijinariti wote hamjui mwanzo wa Shela jeupe na kuvaa rangi yoyote. Hata huyo Violet hajui pia, ingawa katupa sisi wadau tumfunde sawa namfunda sasa, naanza sasa. Hapo mwanzo ulikuwa ukiolewa au siku ya mkesha waharusi BIBI na BWANA mnaandalia chumba na kina bibi au kinashangazi. Kitanda kinakuwa na shuka leupe peee. Halafu kinachofanyika humo kidume lazima akukuruke mpaka shuka ilowe damu ya Bikira, halafu kesho asubuhi kinashangazi wanashangilia binti kaolewa akiwa hajachafuliwa yaani msafi hajachezewa hata kidogo na FATAKI yeyote. Sasa huyo ndiye aliyekusudiwa kuvaa Shela JEUPE akihakikisha yeye ni msafi ki ukweli. Sasa kwa wale waliokutana na kinafataki ndio wanatakiwa wavae lolote tu. aaah nimechoka kuandika.

  ReplyDelete
 9. Mi naona rangi yoyote sawa tu ukisema bikra tu wavae nyeupe bikira wenyewe adimu siku hizi wanaume wenyewe hawa wanataka kuonjeshwa kwanza wanadai hawawezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia hahaha!

  ReplyDelete
 10. Oyooooooooooooo, tushachokana story hizi hizi, vipi?hakuna watu wengine wenye mikasa yao??mi nilidhani angalau baada ya siku moja utapost mikasa ila kila siku ishu ile ile....inakuwaje dada?//

  ReplyDelete