Tuesday, March 9, 2010

NIMEKUBALI KUFUATA USHAURI WENU- LAKINI NITAANZAJE KUMUACHA??

(Nashukuru kwa kuparticipate katika blog yangu, Mungu awabariki, pia mawazo na michango yenu ni vya thamani sana, maana vinasaidia watu, na kufanya wawe strong zaidi, sasa kuna hii issue jamani, huyu dada niliepost mkasa wake mara ya mwisho, amenitumia ujumbe, ambao kiukweli, mimi peke yangu siwezi kumshauri, anahitaji ushauri zaidi toka kwenu, kwakuwa tumeshauri, basi ni vizuri pia tukamsaidia kumpatia mbinu ya kufanya ili kumtema huyo mkaka)

UJUMBE
nashukuru sana kwa ushauri wako na pia kwa wadau wa blog yako, namwomba Mungu anisaidie, Maana hapa nililipo hata  ada ya shule ninayosoma analipa yeye bado nusu lakin kutokana na ushauri  nimeamua mwenyewe kumuacha namwomba mungu anifanyie njia  ingine ya kupata ada ya kumalizia, maana mshahara wangu ni mdogo. Dear naomba niambie nifanyeje jinsi ya kumwacha nimwambie live tu! au nitumie simu? maana sina hata ugomvi nae,  japo wakati mwingine huwa naamka hata usiku nalia sana, maana alikuwa akitusaidia sana mimi na mwanangu, nimeanza kumchunia, hanielewi na ananishangaa tu! hata mwanangu pia ananiuliza  mama siku hizi mbona uncle haji nyumbani - msimamo nilionao ni kuachana naye no way, nimefikiri sana ila sijajua jinsi ya kufanya. Asante sana violet, nakupenda
  
 
Jamani, ujumbe huo hapo wapenzi wangu, tumemshauri mwenzetu kutokana na matatizo aliyonayo, wengie tumemshauri aachane nae, nae amekubali kufuata ushauri wetu, sasa ameniuliza, kama ambavyo mmesoma hapo juu, kwamba aanzaje kuachana nae? haelewewi maana hajagombana nae, isitoshe ndie anaewasaidia mahitaji, na ndie anaemsomesha, hivyo sehemu kubwa ya msaada wake ameiweka kwa huyo kaka,
JAMANI HII ISUE NI NZITO, si masikhara, mimi peke yangu kumshauri nimemshauri, naombeni na nyie wanawake wenzangu mumsaidie, kumpatia mawazo, afanye nini, je amuite amwambie, amchunie tu,  au awe anampotezeapotezea, yani hata sijapata jibu lililosimama, hebu tusaidiane wapenzi,
INSHORT YUKO KWENYE WAKATI MGUMU SANA!14 comments:

 1. naomba nianze kukusifia sana sus V,
  aisee umependeza, nimependa ulivyo simple mwaya,
  ushauri wangu kwa huyo dada ni kwamba,BORA KINGA KULIKO TIBA, pia nimshukuru kwa kukubali ushauri wa watu, itamsaidia maishani kwake, tatu nimpongeze kwa kuwa wazi, maana mficha uchi siku zote huwa hazai,
  sasa rafiki yangu fanya hivi,
  TAFUTA SIKU AMBAYO UNA NAFASI WEWE NA YEYE, KWASASA USIMCHUNIE, ONGEA NAE KAMA HAKUNA KITU CHOCHOTE KILE, ILA MWAMBIE SIKU AKIWA NA NAFASI UONGEE NAE, MTOKE MUENDE SOMEWHERE, WEWE NA YEYE TU!, mkifika mwambie lengo lako, usimchunie wala kumtafutia kisa, ukifanya hivyo inaweza kuja kukuletea shida badae, mkawa maadui hadi kufa, mwambie tu, kuachana kwa kuchuniana ni kuachana kwa kisecondary huko, kwa kizamani, wala hakuna maana, siku hizi watu wanaachna na bado wanakuwa marafiki wa kawaida tu,
  mwambie sababu zinazofanya umuache bila kumficha, kwanza hauko tayari kulea watoto watano wote wa wanawake zake,
  mwambie majibu ya ukimwi yananitatiza, kwanini mtoto awe nao na baba hana,
  tatu, kwanin iwake zake wote wanakufa
  nne huwezi kukaa roho juu, mke aliondoka ambae yu hai, atakusumbua, aweza hata kukuuwa, ukamwacha mwanao anateseka,
  wala usikubali akushawishi kwa lolote lile,
  atakuelewa
  huu ni upeo wangu mimi

  ReplyDelete
 2. Achana naye mwambie tuu mimi na wewe basi usijingize matatizoni, kukinga ni bora kuliko kutibu. Mwambie mimi naona siwezi kabisa, labda ni keria,au kama kasuka dili hapo hospitali. bora angekuwa mzima na mtoto ni mzima tungesema mungu kamfanyia muujiza maana wapo waliosevu iweje mtoto mgojwa mke wafe yeye apone.MUELEZE TUU MIMI NAONA SITAWEZA KABISA.endelea kulinda uwaminifu
  Mama DEAR

  ReplyDelete
 3. mh!
  Dada Violet, mi naona hili shuzi sio la kujamba hovyo, ni zito na nilazima litatoa harufu tu, niko natafuta mawazo tofauti tofauti kwa wafanyakazi wenzangu hapa, nitakutumia nini cha kufanya ili uachane nae,
  pole sana dada, naamini unaumia sana, naamini unajisikia vibaya sa,
  but kwakuwa umeamua, utaweza tu! pole sana dada

  ReplyDelete
 4. yanini uzunguke bwana ah!<
  we mpigie hata simu, mwambi usinifate fate tena, sikutaki, mdanganye umepata mchumba anataka kukuoa, asikuletee ukimwi wake, akafe peke yake, achana nae dada yangu, HAKUFAI HUYOOOOO

  ReplyDelete
 5. usikubali kununuliwa tafuta happyness na maisha,Mungu atakusaidia...

  ReplyDelete
 6. jamani dada v we mzuri but why unavaa vicheni mguuni?kwa mama anejiheshimu haipendezi kabisa

  ReplyDelete
 7. hapo pagumu dada yetu,embu piga magoti mombe Mungu akusaidie pengine ww ndio unatakiwa usimame na kumuombea uwe msaidizi wake kwenye kipindi hiki kigumu kwa matatizo aliyo nayo,embu ww jiweke kwenye hivyo viatu vyake alafu amue kukuacha ingekuwa je.pindi unapojua kwanini upo na mtu fulani nayo inasaidia sana tuu ukimwi siku hizi umekuwa ugonjwa kama magonjwa mengine.na labda ww ndio unapaswa kumsaidia,ni vizuri kusikiliza ushauri lakini pia na ww jiulize sio kukurupuka tuu dada yetu unaweza olewa na mwingine na yeye akawa akuupata pia je utamkimbia?au ww uwezi jua utakako pita hapo baadae mtu akakukimbia,tuwe na mioyo ya uruma jamani tusiwe kama wanyama.hapo upendo ndio unatakiwa uwepo zaidi na kikubwa muombe Mungu mshirikishe wote msali hakuna lisilowezekana kwa Mungu wetu dada.nakutakia kila la kheri,

  ReplyDelete
 8. wewe unaesema amuhurumie, unawaza mbali wewe? au ndio nyie mnaoangamia kwa kukosa maarifa? inakuwaje, inakuwaje kuhusu watoto wote watano, au huyo mama anataka kufungua shule ya watoto, kifupi ni kwamba
  HAKUFAI, HANA HURUMA HUYO, HOW COME WAKE WAFE WOTE, NA MWINGINE AMKIMBIE, THERE MUST BE SOMETHING WRONG TO HIM, dada usirudiane nae hata punje,
  NI MTAZAMO TU

  ReplyDelete
 9. maharifa alitakiwa awenayo tokea anaanza uhusiano naye mwanzoni kabisa sasa mpaka shule ameshakulipia kwanini ukufikia ukuomba ushauri kabla ya kuingia kwenye mausihano na hyo baba na lazima atakuwa alikuambia kwamba anawatoto,na mpaka amekubali kupima na vipimo vimeonyesha hana kapimeni tena na usikilize moyo wako sio kila ushauri unatakiwa kuufata dada tuliza kichwa ufikirie kwa kina kabisa dada yetu kumbuka leo kwake kesho kwako

  ReplyDelete
 10. pole sana dada kwa matatizo hayo!
  ushauri wangu achana nae huyo mwanaume hakufai hata kidogo!

  kujiingiza kwake ni sawa na kujichimbia kaburi mwenyewe embu fikiria wake zake wote wamekufa na wewe si utakufa umwachie watoto ?inavyoonyesha ukifa atatafuta tena mwanamke mwingine alee watoto ikiwa ni pamoja na mwanao sasa vipi hapo?

  ni bora ungekuwa nae tangu mwanzo halafu ukimwi akaupata mkiwa wote hapo utasema umvumilie lakini kaubeba huko akuletee tu from nowhere?hapana!

  ukiongea nae laivu anaweza hata kukudhuru maana najua ataona umevuka mipaka na unamkashifu cha msingi mpigie simu na umwambie umepata mchumba au hata umeamua kuwa peke yako kwa muda kwani masomo yamekuzidi hivyo asubiri mpaka umalize masomo

  halafu mfungie vioo mbaya kabisa!

  ReplyDelete
 11. Dada, mi nakushauri uchague moja mlango mwembamba au mpana au uzima au mauti. hivi kweli ukionyeshwa tanuru la moto hilo hapo mbele yako na ukaona mwenyewe utajipeleka ili uungue!!!!!!!! mbona huelewi? umeambiwa mwache kwani wewe ni malaika! ngoja uende na huyo mke wake aliye hai uone atakachokufanya. Fanya hivi, Mwombe Mungu muulize je! huu ndio ubavu wangu? Mungu atakupa jibu acha kuwa na mawazo mengi. Mungu atakujibu moja kwa moja. ndio ufanye maamuzi. Kama Mungu atakuambia wewe ndiwe ubavu wake, na ni nyama kati ya nyama zake then hakuna atakayepingana na Mungu na kama ana ukimwi ujue Mungu atakuonyesha kitu cha kufanya. Acha kutegemea akili zako.

  ReplyDelete
 12. pole dada, mi nakubaliana na aliye comment wa kwanza kabisa, ila kuanzia sasa sali sana, mwombe mungu hiyo siku mtayopanga muongee maongezi yenu yaende vizuri na uongee nao kwa ustarabu kabisa,mwambie yote hayo chunga sana kauli yako, naamini atakusikiliza, hata akianza kuja juu wewe kuwa mtaratibu tu, mwambie pamoja amekusaidia hayo yote lkn unajiona hatarini na haupo tayari kugombana na huyo mke wake wa zamani, pole sana hapo ni pazito lkn jikabizi kwa mungu atakuwezesha tu. na mi nitakuombea pia.

  ReplyDelete
 13. Pozi lako kama unaona baridi vile. Vazi na shoes umependeza

  ReplyDelete
 14. sissy V umependeza huyo alosema kuvaa cheni mguuni ni vibaya naona ni wa juzi. cheni ya mguuni haina tofauti na mvaa hereni au mkufu ni pambo tu kama mengine, unless kama anaichukulia tofauti, umependeza na mguu mshallah! umependeza mtoto wa kike. huyo mdada ni wale HATERS! ukipendeza lazima akosoe.

  ReplyDelete