Friday, March 5, 2010

NILIACHANA NA MUME WANGU, NIMEPATA MWINGINE ANATAKA KUNIOA- WANASEMA ANA UKIMWI.


Hi violet, kama nilivyokwisha kukueleza. Mm ni mama wa mtoto mmoja niliolewa miaka 13 iliyopita ndoa ya kikristo, niliishi na huyo mume kwa miaka 5 ndipo alipopata mwanamke mwingine na kuhama nyumbani kwenda kuishi nae.

Nafanya kazi kwenye ofisi moja hivi, Sasa hapa kazini nimepata boyfriend ambaye amefiwa na mke wake, ana watoto 5, kati ya ha 1 alizaa na dada mmoja ambaye hakumuoa, wapili ni wa mwanamke aliyefariki ambaye alizaaga na mwanaume mwingine ndo kamuachia anamlea,wengine ni wamke wake walieachana.

tatizo liko hapa! watu wanasema huyu kaka kaathirika manake amefiwa na wanawake 2 kabla ya huyo wa 1ambaye amezaa naye watoto 2 naye alifariki. Nikamshauri tukapime akakubali tukapima mara 3 angaza wote salama lakini sijui why roho yangu inataka tuende tukachek tena hosp ingine naye amekubali,

kwnn tuliamua kufanya hivyo kwakuwa anataka kunioa. Ila sasa huyo mwanamke wake aliyezaa naye ambaye yuko hai ni mkorofi kiasi kunitisha. Pia baada ya kurumbana sana akaniambia kuwa mke wake wa 2 alikufa kwa HIV na mtoto wao mdogo ameathirika. Violet! niko njia panda kwani nampenda ingawa ana madhaifu yake mengine lakini sometimes nasita kukubali ndoa naye, pia nimepata tetesi kuwa huyu mtoto mdogo ameathirika, sasa niko njia panda yani hata sielewi cha kufanya, nishaurini jamani ili nipate njia ya kutokea maana sielewi nianzie wapi niishie wapi.

ni mengi mpenzi wangu nashindwa kuandika yote.  kwa ufupi huu naomba wanablog wanisaidie kwa ushauri
asante na kazi njema

8 comments:

 1. mh! we dada hujitaki wewe, kwani wanaume wamekwisha? kuhangaika huko unataka nini jamani, halafu ubachela ale na nani wewe uambulie kulea, wako mmoja wa mwenzio rundo, kuna mapenzi hapo, halafu mbona utata mwingi sana, kwanini usiachane nae? i i was you, wala nisingeumiza kichwa changu kabisa, mimi nakushauri achana nae, sivyo utakuja kujutia maisha yako, usikute anafahamina na madr, wamepanga wakudanganye, iweje mtoto awe ameathiria yeye mzima? mtoto kautoa wapi? huo ni urongo, dada kuwa makini katika maamuzi,
  NOTE- USITHUBUTU-UTAKUFA

  ReplyDelete
 2. pole sana dada, mmh! mi naona utulie tu dada yangu achana na huyo mtu,wewe tulia fanya kazi yako umlee mwanao na usiache kumuomba mungu utapata tu mwingine atakaye kufaa, huyo atakuletea shida na mwanamke wake ushasema ni mkorofi ujue hapo unahatarisha maisha yako, fungua macho dada uone mbali usiangalie tu hapa karibu yako, ujue mtoto wako bado anakuhitaji sana, sawa dada! ok take care.

  ReplyDelete
 3. dada mimi naomba sitisha mahusiano na huyo kaka mapema sana (kama yako)naona unaingia kwenye trouble, ambazo unajitakia wewe mwenyewe, kwani wanaume wamekwisha? halafu kaa ufikirie, wewe ulishaolewa, ukochini ya ndoa, na mwenyezi Mungu anasema ''ALICHOKIUNGANISHA MUNGU, MWANADAMU ASIKITENGANISHE, hata kama mmeachana, as long as he is alive, he is still your husbund, kwanini usikae ukapiga maisha wewe mwenyewe, bila kuwazia kuolewa, hebu delete mawazo hayo, unaweza kuamua kuwa na mshikaji mmoja ambae atakutimizia haja ya kimwili, na ambae hana mrorongo wa matatizo kama huyo ulieangukia kwake, but most of your thinking wekeza kwa mtoto wako, hivi dada,
  ukiangalia kwenye blog ya dada violet, ni wanawake wangapi wanalia juu ya waume zao? yani tanuru la moto wao wanataka kutoka, wewe unataka ukajitumbukize humo? muhurumie mtoto wako, miaka 13 bado hajafika kokote huyo, anahitaji msaada wako ili aishi vizuri, sasa uache kumelea mwanao uende ukalee watoto wengine, inakuingia akilini hiyo?
  sikulaumu mdogo wangu, ila nakushauri tu,
  mimi hapa nina miaka 43, na niliachana na mume wangu miaka kumi na saba iliyopita, akaenda kuishi na mwanamke mwingine, nikaanza maisha peke yangu, hadi leo, sitamani kuolewa tena, niko na wanangu watatu, na namshukutu mungu kwakuwa amenisaidia, wote wanasoma, wanamaisha mazuri, hawana tofauti na wale wanaoishi na baba zao, nakuomba mdogo wangu, achana na huyo mwanaume, huwezi kuamini, lakini mwaka jana, mume wangu alirudi na kutaka turudiane, nilikataa kabisa, nikaitiwa wachungaji, sikukubali, nikaitiwa wazazi(vikao vya familia) nikakataa, kwakuwa sikuona reason ya mimi kurudiana nae wakati alinitupa, amekuwa masikini ndio anataka kuja kufia kwangu,
  sitaki na sitakubali, maisha ya pekeyako mazuri sana, yanakupa nafasi ya kujipanga kupigana na maisha
  USIJARIBU MPENZI WANGU, ''KOMA'' sio tusi, ila naonyesha msisitizo jinsi gani nisivyotaka uingie kwenye shida.

  ReplyDelete
 4. Chonde chonde, kama hujafanyanaye mapenzi tafadhali achananaye. yani ufe kwa ajili ya kupenda na hali unaelewa ni mgonjwa, haiwezekani kwani ulizaliwa nae? jamani muonee huruma mwanamke mwenzako alieiingia labour kukuzaa halafu leo unajiamulia kufa kwa ajili ya mtu ambaye mmekutana tu.fikiria angekuwa mwanao anachukua maamuzi hayo ya kufa kwa ajili ya kupenda ungejisikiaje? KWAKWELI INAUMIZA.

  ReplyDelete
 5. pole sana dada, kama wachangiji wengine walivyosema pia mimi nakazia hapo hapo huyo HAKUFAI KABISAAAAAAAA!! TENA KIMBIA MBIO. hapo hamna mapenzi mtapotezeana muda tu. ebu kaa chini na ufikirie ni kwa nini hao wake zake wamekufa? yawezekana kuna laana inatembea kwenye ukoo wao na wewe wataka kujitumbukiza huko.nakusihi mdogo wangu katika Jina la Yesu tulia mwombe Mungu atakupa wa kwako kwa wakati wako USILAZIMISHE USIJE UKAJUTA.

  ReplyDelete
 6. jamani tuwe wa kweli..ni bora kuachan kama ilibidi na yeye kama binadamu ana haja zake kusema kuwa asiolewe kunaweza mfanya akawa anatenda tendo takatifu na mtu wakati im sure yeye anataka kuingia kwenye ndoa. Kwa sasa hivi hata makanisa yanatenganisha..huwezi lazimisha ndoa . dada ushauri wangu tafuta mwingine kama huyo unamdoubt alafu pia ana watoto wengi mtakwua na majukumu wengi ukipata mwenye atlast watoto wa3 inakuwa rahisi zaidi pia unaweza olewa dada nakussuport

  ReplyDelete
 7. Achana naye mwambie tuu mimi na wewe basi usijingize matatizoni, kukinga ni bora kuliko kutibu. Mwambie mimi naona siwezi kabisa, labda ni keria,au kama kasuka dili hapo hospitali. bora angekuwa mzima na mtoto ni mzima tungesema mungu kamfanyia muujiza maana wapo waliosevu iweje mtoto mgojwa mke wafe yeye apone.MUELEZE TUU MIMI NAONA SITAWEZA KABISA.endelea kulinda uwaminifu
  Mama DEAR

  ReplyDelete
 8. Hivi huyu anataka ushauri kweli au anatujaribu maana majibu yote anayo mwenyewe sis hatuna cha kumshauri otherwise amechoka kuishi maana mambo yako wazi kabisa.

  ReplyDelete