Thursday, March 11, 2010

HOW TO CHOOSE A GOOD HUSBUND? (KWA AMBAO HAMJAOLEWA) THIS IS SPECIAL FOR YOU!

Ni vizuri kabla mtu hujaolewa, ukakaa ukafikiria, ni mume wa aina gani atakufaa, madhaifu yako unayajua wewe mwenyewe, kila mtu ameumbiwa wake, kuna wanawake wakorofi kupita kiasi, yani hivyo ndio walivyo, you cant change their behaviour na wanajijua kabisa kuwa ni wakorofi, na kuna wanaume ni wakali kupita kiasi, sasa niambie wanapooana wawili hawa, huko ndani nini kitaendelea? hivyo ni vizuri kufikir ni mwanaume wa aina ipi utaweza kuishi nae kabla hujakurupuka kufunga ndoa,
Neno ndoa kama nilijuavyo mimi ni Nyumbani Daima Ombeni Amani , sasa kama wote mtaamua kuoana mabaunsa amani itatoka wapi? (THINK TWICE)

Ndoa ni tamu jamani asikwambie mtu, ila some time mh! panakuwa parefu sana, kama wote mtataka kuwa juu,  naomba niwashauri wadogo/wakubwa zangu ambao hamjaolewa, niwamegeeni kile ninachokiona mimi kitawafaa ktk harakati za kutaka kujua sifa za mume atakaekufaa, zipo nyingi, zingine wadau mtaziongezea.

1. lazima utambuwe, ndoa ni maamuzi ya kutoka ndani ya moyo wa mtu mmoja. (wewe tu!) ukisha kubaliana na maamuzi yako, ndio unayawasilisha kwa yule ambae unaona atakufaa ili myaunge kiwe kitu kimoja.(ndoa sio lele mama, usione raha kuvaa shela na kurundika pete mkononi, kama  usipojipanga sawa, utajuta)

2.katika maisha ya uchumba, vingi sana vinatokea, vikwazo lazima vitakuwepo, sasa je unavyomuangalia ni mwepesi wa kusamehe, na kusahau? au ni yule mwenye gubu, kosa umefanya leo lakini kila mkipishana analikumbushia?

3. Angalia, ni mtu anaekujali? anakusikiliza? anashaurika? kuna wanaume wengine akisema yeye basi na ukurasa umegungwa, ''No discussion'' hata kama anakosea, hataki kuambiwa, (muhimu kulitazama hili katika uchumba wenu)

4.  Anakupenda kweli? hana tamaa? maana kuna wenawake wengine huwa wanaforce ndoa, mradi tu avae shela atujaze ukumbini tumuone alivyopendeza, kumbe mwanaume wala hakuwa teyari kumuoa, baada ya mwaka mmoja tu! anaanza, najuta kuolewa mimi, wakati alitaka mwenyewe, (fikiria hili pia)

5. Kila binadamu ana mapungufu na madhaifu yake, na kila mwanadamu ameumbiwa wa kufanana nae, ndio maana ndoa ya mke mpole na mume mkali, zinaweza kudumu sana, au ndoa ya mume mpole na mke mkali zinadumu sana, ni kwakuwa kila mmoja amecoup na mwenzie, anajua hapa kapanda sana leo, ngoja mimi nishuke, (yanaisha) na ndoa za wote wanataka kuwa waelevu kila siku mingumi ndani, - sasa chunguza kwa mchumba wako, jitazame na wewe, mnaweza kuvumiliana tabia zenu?
point hizi tano, ni za kwangu mimi ninazoona ni kubwa kuzitazama, zingine wataongezea wachangiaji, hii itasaidia kupunguza matatizo ya ndoa zetu za sasa hivi,  

 next time nitawaambia, kabla hujaingia kwenye ndoa unatakiwa kufanya maamuzi gani ya binafsi, yakwako mwenyewe bila kumshirikisha mtu!




7 comments:

  1. Anonymous said...

    asante sana dada violet kwa darasa lako la leo, real nimeenjoy sana, na hope to get many things from you, thats first,
    second natarajia kufunga ndoa mwanzoni mwa mwezi wa tano, naomba uwe mgeni kwenye harusi yangu, nitakupatia card free ya mwaliko kuanzia kitchen part, send off na harusi pia.

    tatu,
    sifa ulizozitaja zote mchumba wangu anazo, lakini kwenye suala la hasira, da! sijui itakuwaje, maana ni mwepesi sana wa hasira, ila ni mrahisi kusamehe, na huwa harudii, sasa niambie ndoa yetu hii itadumu?

    nakupenda dada violet, na pia ninaomba uniambie mapema maamuzi ya binafsi unayotakiwa kufanya, I wish ungesema leo leo. nahamu yakujua kma maamuzi hayo niliyafanya.siku njema dada, na masomo mema piakaa ukujua nakupenda sana na nahisi kujifunza mengi sana toka kwako
    Maggie

    ReplyDelete
  2. Asante Maggie kwa kuapriciate somo hili, usijali, tutaendelea kufundishana zaidi,

    kuhusu mchumba wako, mimi nimefurahi sana kuwakuwa umejua shida yake, hivi unajua kama mtu ukijuwa udhaifu wa mwenzio ni raha sana? coz hatakusumbua wala kukupa shida, utajuwa jinzi ya kutake care, utajua jinsi ya kuepuka utajifunza mengi kupitia udhaifu wake,

    wewe umeshatambua kuwa mumeo mtarajiwa ana hasira, NILICHOPENDA UMEJUA KUWA HASIRA ZAKE ZA MUDA MFUPI NA HUWA HARUDII KUKUKUMBUSHIA KOSA, huyo ni mzuri sana, maana hatakuumiza kwa yaliyo pita. kwakuwa ni mwepesi wa kusahau. thats gud
    BUT na wewe ujitahidi kuepuka vile vya kumfanya achukie, sio utumie udhaifu huo kumuumiza mwenzio au kumkera, jitahidi sana kuepuka, mambo yatakwenda smoothly na utaenjoy ndoa yako mdogo wangu,
    nakupenda pia, na all the best katima maandalizi ya harusi yako,

    ReplyDelete
  3. nimependa mtiririko huo,
    ni ukweli mtupu, ndio maana ndoa za siku hizi kila kukicha ni ugomvi, tofauti na zamani, wazee a zamani wengi wako wawili wawili, kama walivyo kuwa, tofauti na siku hizi, lo! uchafu mtupu, inatuogopesha hata kuolewa, kweli ukitafuta wa kuvumilia shida zako, utaishi kwa vizuri,.

    ReplyDelete
  4. LINGINE LA MUHIMU UMESAHAU,
    MUHIMU KULIANGALIA NA LENYEWE,
    UUME WAKE UNASIMAMA? UNAKUFIT? UNAUFEEL?
    MWENZANGU KAMA HUUFEEL, JIACHIE, MAANA HIYO NDIO NDOA.

    ReplyDelete
  5. hiyo ya uume kufiti kweli hata mimi naona ni muhimu sana!

    mimi na nilikuwa na boyfnd alinipenda sana hata mimi nilimpenda na tulikaa kwa miezi miwili bila kujuana kimwili siku tulivokuja kuduu nilichukia to the maxmum!

    kidudu chake kilikuwa kidodo sana yaani kama cha mtoto wa darasa la pili!

    imagn nilivokuwa nampenda1 nilitamani nifanyaje sijui, lakini baada ya kuduu nashangaa akaniambia uchi wangu mtam na umemfiti vizuri nilitamani kumzaba kibao lakini sikumwonyesha ile chuki

    toka siku ile nikadiside kuachana nae,ilikuwa 2005 mpaka leo bado ananibembeleza niwe nae eti coz hajui kosa nililomwachia!

    so nawashauri kujuana kwanza kabla ya ndoa.

    ni hayo tu dada vai

    ReplyDelete
  6. teh teh teh teh, tumbo langu mie,
    eti kidude kama cha mtoto wa darasa la pili, lo, nimecheka sana
    ila kweli mwenzangu ilo nalo neno, UUME MUHIMU,

    ReplyDelete
  7. Jamani kumjua mwanaume kabla ya ndoa hiyo sio suluisho. mimi nilikaa na mchumba wangu mwaka mmoja na nusu ndo tukaoana na hakuwahi hata siku moja kunitamkia suala la kufanya mapenzi kabla ya ndoa. nilimkuta yuko fresh kila kitu kimekamilika, kitu kinasimama kama kawaida tena kikiguswa tu kinarespond immediately, na mpaka sasa tuna enjoy maisha ile mbaya na wala sijawahi kujuta why nimeolewa naye. hivi ngoja niulize, kuna haja gani ya kwenda honeymoon kama mlishakutana before? mbona mnapoteza maana yake? semeni yote lakini ukweli utabaki palepale kama mkifunga ndoa bado hamjajuana mtaenjoy saaaana kwenye honeymoon yenu kwa kuwa kila mtu anakuwa na hamu na mwenzake. lakini mkifanya kabla mtaona sawa tu kama mwanzo.(yani hamtoufeel ule utamu wenyewe). kitu kinachohitajika wapendwa wangu ni kumwomba Mungu akusaidie upate mume mzuri na ALIYEKAMILIKA. kama utajenga tabia ya kumshirikisha Mungu mambo yako yote hatakuacha hata kidogo na mambo yako yote yataenda sawa sawia.

    ReplyDelete