Wednesday, March 3, 2010

NINA MCHUMBA TUNAPENDANA SANA, ILA TUMETOFAUTIANA DINI - WAZAZI HAWATAKI NIFANYAJE


Habari dada Violeth, Mimi ni bint wa miaka 26 nina mpenzi ambaye tumekuwa pamoja kwa miaka 2 na miezi 3 sasa, tunapenda sana, tatizo mimi ni mkristo na yeye ni mwisilam, alimwambia mama yake kuwa anampenzi mkristo, mama yake amepinga hilo amesema anataka binti aliyekulia kwenye mahadili ya kislam, hataki kusikia kabisa ukristo, na mimi binafsi siko tayari kubadili dini, niliongea na mama yangu hakupinga ila aliniambia niendelee kumuomba mungu anionyeshe kama kweli ni yeye aliyenipangia.

sitaki kuishi bila ndoa maana maisha haya hayana heshima? napia raha ya ndoa wazazi wote waridhie, mpenzi wangu hajui la kufanya hadi sasa, niliwahi kumjaribu nikamwambia tuachane kila mtu akatafute wa dini yake, hataki kuachana na mimi kabisa, ananipenda sana, na kwangu pia inakuwa vigumu kuachana na yeye,
kwakweli tupo pagumu ukizingatia tunaheshimiana sana na tunaelewana. kwasasa tuko masomoni nje ya nchi na wazazi wetu wote wapo tanzania, nikifikiria najisikia vibaya sababu sijui nini mwisho wetu, na niliamua kuwa na yeye sababu nilimjua tangia tuko secondary tulisoma shule moja na badae tukakutana tena collage tanzania huko kote hatukuwa pamoja na tumekuja kukutana tena huku,ndio akaniomba tuwe pamoja. naogopa asije akaniacha kwenye mtaa badae sababu ya wazazi, naomba ushauri wenu nifanye nini, nakosa raha juu ya hili, najuwa kuna wakubwa wangu walipitia tatizo kama hili na wakafanikiwa kulitatua, naombeni mnishauri na mimi mdogo wenu, sijui cha kufanya, nina wakati mgumu sana?






8 comments:

  1. pole sana mdogo wangu, mimi binafsi naona mapenzi ni ya watu wawili tu, chamsingi, mkae, muelewane muweke misimamo tu, wazazi msiwape nafasi, maana wanawake tuna gubu sana sisi, kuhusu kugunga ndoa, kama kila mtu hataki kubadili, basi kafungieni bomani, kila mtu na dini yake,
    usizidishe manjonjo, baraka za wazazi za nini, kama hawataki je, siku hizi hayo hayapo maana hao wazazi wenyewe ni waasi namba moja, anaweza kukuchukia tu bila sababu za msingi akataka usiolewe, inakera sana hii, mimi huwa inanikera sana tabia hii ya wazazi wa kuingilia mapenzi ya watoto wao, kama mnapendana amueni kuwa kitu kimoja, lengo moja,
    Tina

    ReplyDelete
  2. ilishawahi kunitokea hali kama hiyo mdogo wangu, tukaforce ndoa, jamani nilipata shida sana, niliichukia ndoa, mama mkwe aliniletea shida hadi kunifanyia uchawi ili mwanae anichukie, na nilichukiwa mimi, nilikuwa napigwa nusu kufa, nilishawahi kuvunjwa mkono, kisa ndoa ya kuforce,
    hadi sasa naishi na mwanume mwingine, wa dini yangu, tunapendana sana, yule niliamua kuachana nae, nakushauri mdogo wangu, usikubali, labda hao wazazi wake waridhie, usikubali mdogo wangu,

    ReplyDelete
  3. msisikilize wazazi, huyo mama yeye alitafutiwa mume au walipendana,
    wazazi wa siku hizi kisema cha huyo aliepita ni kama wachawi, au mmnataka muolewe na watoto wenu, wewe mzazi utaingilieaje mapenzi ya watoto wako, fungeni ndoa ya bomani, mshow love, hao wazazi msiwape nafasi

    ReplyDelete
  4. mnaotoa ushauri mfikirie jamani, ndoa yenye baraka ni nzuri sana,hamuoni kama itamletea shida baadae kama akiforce? umri wako bado mdogo sana mdogo wangu, mimi naomba chukuwa muda tena, muongee wewe nampenzi wako, muone mtaamuaje, msikurupuke tu1, mkikubaliana sawa,
    pia kama itawezekana, hata mkifunga ndoa, msikae mkoa mmoja na wazazi, mkae mbali, hii itasababisha kupunguza maneno maneno,
    fikiria kwanza dear, then utapata maamuzi yaliyo sahihi,
    asante

    ReplyDelete
  5. Binti hapo kazi ipo fikiria sana nini unahitaji maishani, huwezi kufanya maamuzi haya mazito kabla hujajua unataka kuwa nani na nini unahitaji maishani. Achana na mambo ya kufikiria short term, fikiria long term. Is the guy potential? esp. intellectually? is it the person you really want to have in your life time? kuna chance nyingine zikipotea huwezi kuzipata tena, na kama sio risk taker itakuwa ngumu kufanikiwa. Mimi nimeona watu wengi sana wanawakimbia wachumba zao kisa dini mpaka kesho uwezekano wa wao kupata hiyo ndoa haupo tena.Na nimeona watu wengi sana wameolewa na dini tofauti na maisha yanaenda bomba, hilo swala la kudanganyana na baraka za wazazi ni issue, kwani unaenda kuishi na wazazi au na mme. Kwanza kitu cha kufurahisha wewe na bf mko nje which means mna exposure na ni wasomi mtashindwa kukaa chini na kuwaelemisha wazazi wenu dunia inavyoenda? think twice! g'd luck!

    ReplyDelete
  6. dada pole sana. nami yalinikuta kama hayo kwani nilipata mchumba wa dini tofauti
    (christian) na baba yangu ndo alikuwa wa kwanza kupinga kuhusu suala la kuoana ikabidi niachane naye, nikapata wa pili naye dini hiyo hiyo ikabidi nimface mdingi mwenyewe na kumwambia unataka nizeekee home? maana sijawahi kupata muislam hata siku moja. na nashukuru mungu alinielewa na hatimaye akaruhusu ndoa, tukaenda zetu bomani na sasa tuna mtoto na kusema kweli nina amani na raha sana. NAKUSHAURI KAA NA WAZAZI ONGEA NAO TARATIBU NINA IMANI WATAKUBALI TUU KUBADILI OR KWENDA BOMANI. na unaweza ukampata wa dini yako lakini ukaishi maisha ya majuto kuliko. SIKU HIZI WATU WANAANGALIA PENDO LA DHATI MPZ.

    Thx - Mama wa Furaha

    ReplyDelete
  7. napenda tu kukukumbusha kua heshima ya mwanamke si kua katka ndoa, ni matendo yako, umejiweka vipi na unajiheshimu kiasi gani. wako wenye ndoa lakini hawana heshima wala kuheshimiwa na mtu hata mmoja kutokana na matendo yao ya kutojithamini na kujiheshimu wenyewe. pili, sioni kwa nini kama mnapendana na huyo mpenzi wako kubadili dini iwe tatizo. kumbuka kua mwanamke hana dini, anachofuata ni dini ya mumewe. kuoana dini tofauti sio vizuri maana mtawapotosha watoto. kama kweli unapenda mwenzio, lipe na kufuata dini yake kipau mbele.

    ReplyDelete
  8. Pole ndugu yangu lakini ki africa sijui ki ulaya mke humfuta mume kuoana kila mtu na dini yake ni kuwacorner watoto mbona issue so simple kama una mpenda badili dini na umfute

    ReplyDelete