Wednesday, March 17, 2010

NILIKUWA MZIMA, NILIPATA ULEMAVU WAKATI NAJIFUNGUA-MUME WANGU HANITAKI TENA

Taarifa ya Mama huyu imenisikitisha sana, imenitoa machozi, kuna watu wanapata shida sana jamani, tumsaidie kwa mawazo, ajuwe nini cha kufanya, inaumiza sana.

Habari yako mdogo wangu Violet, naandika kwa uchungu sana, moyo wangu unaniuma na machozi yananimwagika. Maana sina thamani ya kuishi kama binadamu wengine, naamini nilizaliwa kwa bahati mbaya, Naona bora hata ningekufa nilipozaliwa tu kama alivyokufa mwanangu. alienipa matatizo

Miaka nane iliyopita nikiwa chuoni Tabora, nilizaa na baba mmoja, baada ya kutoka chuo tukaamua kuishi pamoja kwa makubaliano, mtoto akuwe kidogo ndio tubariki ndoa, but since there tukawa busy na kuendelea kufurahia maisha yale, hatukuwa interested tena na kufunga ndoa, (ni kosa ambalo nakubali nililifanya) tulikuwa na maisha ya kawaida sana, ila kwenye upendo hata kama kuna shida huwezi kuona karaha sana, upendo unafunika kila kitu, Nikiwa na Yule baba tulikuwa tumepanga, badae tukajenga kwetu huku Shinyanga. Tukahamia hapa, akanifungulia biashara, nikawa nafuga, Catering, grocery, mambo yakawa safi kabisa,

Mwaka juzi nilipata mimba, tukakubaliana kabisa nizae, na alinihudumia sana hadi naenda kujifungua, nilipofika hospitali wakati najifungua nilipata kifafa cha mimba, nilizaa mtoto ambae alikaa siku tatu akafariki, mwanangu alikuwa wa kike, wakwanza ni wa kiume, niliumia sana,

Kitu ambacho sikielewi hadi sasa, nikwamba baada ya mwanangu kufariki, nilikuwa bado niko hospitali, siku ya nne nikawa siwezi kuamka, yani nikikaa tu miguu haisogei kwenda kokote, ikawa inajaa maji tu, na sehemu ya kiunoni nikawa sihisi chochotekile, nilijua nia maradhi tu na yatakwisha, lakini siku zina kwenda, ikabidi hospitali wanipatie wheel Chair, ili kunisogeza

Nimeumiasana, maana mume wangu amebadilika ghafla, kipnindi cha mwanzo alikuwa ananipendapenda, lakini ss ananichukia ile direct, miradi amempa dada yake ndie awe msimamizi, anasema mimi siwezi, nilijuwa nitapata support yake, roho inauma sana, Napata support toka kwa mwanangu James, nampenda mwanangu, yeye ndie atake nizika,

Kuna watu walinishauri nirudi kwetu, maana ilifikia kipindi akawa ananikashfu, anasema mm ni mzigo, kwanza hatuna vyeti vya ndoa, nimwachie mwanae niondoke, sasa mimi nitaenda wapi na hali hii jamani? Bila yeye kutaka nizae tena ningepata ulemavu huu, Dunia imeniangukia jamani, sina wa kunitetea, mama alishakufa zamani, baba yangu ni mgonjwa nae alikuwa ananitegemea mimi,

Tumechuma mali nyingi sana na baba James, nilimwambia basi nipe nyumba moja(maana ziko tatu) na mtaji kidogo kasha mimi nikakae huko na mwanangu, nitatafuta mtu atakuwa ananisaidia kusimami vibiashara vyangu, anasema atanipa kwa misingi ipi, anasema eti karibia nakufa, hizo mali nitaziharibu tu!, anatamani nife siku yeyote ile anaona kama namchelewesha, inauma sana violet

Kuna dada mmoja , alinipa jina la blogu yako, akanieleza ilivyo, nikaona namimi niandike ili nipatiwe ushauri, nifanye nini? Natamani hata kujiua, lakini moyo unagoma kufanya hivyo, nisaidieni mwenzenu.
10 comments:

 1. WALA USIJIUE, KWANI HUJAFA HUJAUMBIKA, MWOMBE MUNGU SANA SANA TU, NA MIMI NAKUACHIA NENO HILI " YESU KRISTO WEWE ULIYEMFUFUA LAZARO, AKUFUFUE NA WEWE, ANZA KUFANYA MAZOEZI KWANI KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI UTAKUWA MZIMA TENA. Amini hivyo.

  ReplyDelete
 2. Mmmh jamani kuna majaribu duniani..nimesoma ..halafu ikabdi nifikirie kwanza ingekua mimi...
  Dada yangu ,mimi nakuomba kwanza usali sana kwa imani yako Mungu akupe ujasiri na nguvu..halafu kama kuna uwezekano wa kuita wakubwa wa familia yake na yako mkae pamoja na uwaeleze tatizo lililopo haina haja ya kuomba muishi pamoja..ila wakusaidie kama ataweza kukupa mtaji au moja ya nyumba mlinazo uishi uendeleze maisha yako.
  Unaeza kwenda kwenye ofisi kama za Ustawi wa jamii au TAMWA kuomba msaada , ila labda ungeanza kwanza na kuongea na wazazi wake na wako ili usikie nao watasemaje..pengine unaweza kupata msaada , nakuombea hivyo..
  Mungu ni mwema na ahadi zake ni kweli hawezi kukuacha uhangaike.
  Ubarikiwe sana.

  ReplyDelete
 3. Bwana Yesu asifiwe Mama James,

  Usikate tamaa, kama Mume kakuacha Mungu hajakuacha, Mwombe Mungu akusaidie upate watu wazima waseme na huyo mume wako.

  Mi sijui sheria ila, nachofahamu kidogo ni kwamba haijalishi uko na cheti cha ndoa au la lakini kwa muda uliokaa na Baba James unatosha kuitwa Mke wa ndoa.

  Mwombe Mungu, pia tafuta mtu akusaidie au anaweza kujitekeza mwana blog akakusaidia ili akupe haki yako. ila cha muhimu usikate tamaa. Pia nenda kwenye maombi, hakuna lisilowezekana kwa Mungu utashangaa Mungu anakuponya. narudia tena, Mungu aliye kuumba anakufahamu hawezi kukuacha, utapona tu. endelea kufanya mazoezi na Maombi. Mama usikate Tamaa.

  ReplyDelete
 4. Usijiuwe liko tumaini ambaye ni yesu kristo, yesu anajibu, yesu anaweza, yesu anatenda mambo makubwa kuliko tuyaombayo wala tuyawazao, najua ni kipindi kigumu sana unapitia cha kwanza mkubali yesu kama bwana mwokozi wa maisha yako, tafuta watu wa kuombea uombewe soma neno simamia neno mchana na usiku, uponyaji udhihirike, naomba no yako ya simu kupitia dada v tuombe liko tumaini ambaye ni yesu, naandika mail hii naugua ndani yangu. Amini siku moja utatembea na utasimama. kwani yuko Doctor wa madoctor. Usijiuwe kabisa utaingia mbingu ya nani
  Mpendwa

  ReplyDelete
 5. mmh! pole sana dada kweli hayo ni mateso makali sana, nakuomba sana dada utoe hayo mawazo ya kujiua,mwamini mungu yeye ndie muweza wa vyote anaweza kufanya miujiza yake ukatemebea tena, najua maneno ya mumeo ndio yanakukatisha tamaa,haya anayosema yakapate kushindwa kabisa ktk jina la yesu,mi nakushauri kama unachochote ulisave unaweza tu kurudi kwenu ukaanza kabiashara kako, najua inauma sana na ningumu sana kuondoka hapo na kuachana na mumeo ukizingatia huko kote mlipotoka,lkn mi naona bora urudi nyumbani asije akakuua bure,yani kweli tanzania inabidi tuwe na sheria kali, mimi niko canada huku wenzetu hawataki ujinga ukiishi tu na mwanaume miezi 6 mnaesabiwa ni mume na mke hata kama hamjafunga ndoa na mkiachana mnagawanyishiwa nusu kwa nusu na bado mume kila mwezi lzm alete matumizi kama mmezaa wote, hata kama amekuacha,sasa kwa tanzania sijui wanafanyaje, kweli nikiona mambo haya naogopa kuolewa au kuishi na mtu,yani mi sina la kukwambia zaidi, kwa upande wangu bora kurudi nyumbani.

  ReplyDelete
 6. pole mpenzi,pole sana, ni majaribu yatapita dada yangu hasa ukimtegemea yesu yeye atakupa amani ya kweli, cha msingi tafuta mtu akusaidie kwenye sheria utapata tu haki zako, ila hapo kwa mumeo si pakukaa anaweza kukuwekea sumu huyo baba, kashakuwa mnyama kabisa huyo mumeo. wanadamu hatujui kama hujafa hujaumbika leo kwako kesho kwake, mungu akupe amani iliyo dhabiti ndani ya moyo. futa wazo la kujiua. sheria zipo. fuata sheria akupe chako uanze na maisha yako.

  ReplyDelete
 7. Hbr wapendwa! inaniuma kusikia ivi kwani hata mimi ni mwanamke ambae sijui Mungu amepanga nn kwangu, but yote kwa yote nakuomba kwanza muweke Mungu mbele na pili usimuonyeshe James kwamba unamchukia baba ake kwani lazima utambue huyo ni baba ake hata iweje na anawajibu wakumtunza,
  wewe sasa unachopaswa kufanya nikuwa karebu na marafiki wakweli na ndugu ambae huwa uko karibu nae sana.Amini nakwambia utapona tu kwani hicho ni kilema cha ukubwani lazima utapona mama,ili kamwe usimkufuru Mwenyezi Mungu kwani hilo ni jaribu amekupa na unapaswa ulishinde,akikisha unafanya mazoezi kidogokodogo uanapoweza, mali za mume wala usiangaike nazo na wala usigombane nae kwani ipo siku mtaombana radhi na mtarudi kuishi maisha ambayo hukuyategemea,
  wale wasanii wanao act move huwa wako sahihi mpenzikwani huwa wanaonyesha vitu harisi, najua unaumia sana mwili na roho but amini muujiza utatendeka juu ya maisha yako ata kama ni baada ya miaka 10 kwani Mungu wetu hachelewi wala hawai ila huja kwa wakati mama. Nakuomba akikisha James anasoma kwa bidii bila kumpa mawazo yatakayo mfanya ashindwe kufauru darasani kwani ndie nguzo yenu ya baadae, kuhusu kujiua achana na mawazo finyu wewe ni mama wa karne hii hutakiwi kukata tamaa na kumuacha shetani achukue nafasi hakiki unashinda vita hii,naomba maneno haya yakutie nguvu leo na usimamame imala. MUNGU AKUTANGULIE KATIKA KILA JAMBO NASI WANAWAKE WENZIO TUTAKUMBOA,.

  ReplyDelete
 8. Mpendwa pole sana na masahibu haya. Nikuombalo dear Muombe Mungu kwani yeye ndiye mwamba na hashindwi na jambo. Humshusha ajikwezae na kumpandisha aliye chini. Ila ni vizuri pia ukapata usaidizi wa kisheria, maana una haki zako nawe pia. Usiwaze kujiua mpenzi halafu James umuache na nani jamani?

  Dada Violet, nisamehe mpenzi lakini nilichukua hii habari na kuipost kwenye blog ya harusi yangu ili dada apate ushauri zaidi. I hope huta-mind.

  Dada tembelea pia link hii uone ushauri zaidi mpendwa http://www.harusiyangu.com/forumreplies.php?topicid=643

  ReplyDelete
 9. POLE SANA DADA JAMANI NASIKIA UCHUNGU SANA UKIZINGATIA NAMIMI NI MAMA. MPENDWA OMBA NA AMINI YESU ANAWEZA UTASIMAMA TU SIKU MOJA NA KUFANYA SHUGULI ZAKO, KILA SIKU OMBA NA KUMSHUKURU MUNGU KWANI ANA MAKUSUDI NAWE USIKATE TAMAA, TAFADHALI USIJIUE MAMA JAMES, MWANGALIE MWANAO ANAKUPENDA, MWOMBE MUNGU AMBADILISHE BABA JAMES AWE NA UPENDO.KAMA UNA MTAJI RUDI NYUMBANI UFANYE BIASHARA YOYOTE HUKU UKIMWAMINI MUNGU NAYE ATAFANYA. SOMA NENO LA MUNGU NA KULISIMAMIA YEREMIA 33:3 USICHOKE KUMUITA NAYE ATAITIKA MPENDWA. KWANI UNAISHI WAPI?

  ReplyDelete
 10. Pole sana mama james,mtumaini mungu kwa kila jambo kila lenye mwanzo huwa na mwisho wake,mungu hakupi Tatizo bila kukuonyesha ufumbuzi.Nakupenda mama james

  ReplyDelete