Thursday, January 21, 2010

Nisahihi kufunga ndoa na ujauzito kwa madai mtoto akizaliwa atakuwa ndani ya ndoa??

Hebu tuwekane sawa kwa hili jamani, siku hizi imekuwa kama fassion,
mtu kufunga ndoa huku mjamzito,

Pia tuelezane ukweli kabisa, je ni kweli kwamba mtoto huyo atakuwa ndani ya ndoa??


Wewe kama wewe, unaona ni sawa?? na kuna ukweli juu ya hili. .........








                                                             

11 comments:

  1. Helow mama Tracy kwanza hongera mpendwa kwa maendeleo,ujue cku zote mtu lazma uwe na wivu wa maendeleo na c wivu wa kumharbia mwenzio,natumai dina amekupa changamoto hadi ukaamua naww kufungua blog yako,big up mamaa kwa hilo,khs kufunga ndoa na ujauzito kwangu mi naona c sawa,na cpendi initokee,mana mi ktk ndoto zangu nataka nikiolewa nikae km miaka miwili hv nifurahie maisha ya ndoa vizuri na ma huzband pia tupange mambo yetu sawa then ndo taanze kusaka mtoto,ASIA ALAWI

    ReplyDelete
  2. kwa sisi waislamu, mtoto anakua sio wa ndani ya ndoa, anahesabiwa ni wa nje!!!!

    ReplyDelete
  3. Si sahihi kufunga ndoa kipindi cha ujauzito kwa sisi waislam wanasema dini inakataza na hata hivyo ukijazaa huyo mtoto wanasema ni wa kwako ww mwanamke kisheria ila sijui kwa wenzetu wakristo.Na hata hivyo haipendezi kufunga ndoa na mimba kwani kuna wengine zinachagua vyakula haya unaambiwa bi harusi alishwe keki umelishwa na haupendi si unaweza tapika mbele ya hadhara ya watu then ikawa aibu tujitahidi ndugu zangu kwa ili raha ya ndoa ufunge bila kuwa na mimba.Kama maajaliwa ya mungu mtapanda mtoto ndani ya ndoa ila kuna wanaume wenye tabia ya kusema hawezi uziwa mbuzi kwenye gunia mpaka amjaze mimba mwanamke ndio aoe tuache tabia hii jamani km mungu kapanga mtapata tu.

    ReplyDelete
  4. Ni kweli si sahihi mwanamke kufunga ndoa huku anamimba. but mimi naona kama ikitokea akashika mimba kabla ya harusi its better kuolewa nayo tu kuliko wale wanaoamua kutoa mimba hiyo ili tu asionekene kaolewa akiwa na tumbo kubwa.
    Ukweli ni kwamba wengi wetu huwa tunaanza kufanya mapenzi na wapenzi wetu hata kabla hamjaamua kuoana sasa mimba ni matokeo....mie sioni kama ni fashion kuolewa ukiwa na mimba.
    Mimi mwenyewe yamenikuta mana natarajia kuolewa katikati ya mwaka huu na tayari ninamimba changa sasa, sasa ni bora nisiolewe hadi nijifungue au ni afadhari nifunge ndoa na mimba yangu?

    Mdau

    ReplyDelete
  5. Hongera mama Tracy
    pili nikushauri mdau hapo juu, suala la kufunga ndoa huku una mimba kwa mantiki ya mtoto awe ndani ya ndoa, ni uongo mtupu!
    wizi mtupu yani?
    ndugu yangu mimi nakushauri usubiri ujifungue, then ufunge ndoa ukiwa fresh, japo mtoto teyari yuko ndani. kwanza mbona mimi naona aibu sana jamani, kila mtu ataona mmeshindwa kuvumilia hadi mfunge ndoa na mimba? kama mlitaka mtoto mapema si bora mngehalakisha ndoa???
    watoto wote ni sawa, wa ndani ya ndoa na nje ya ndoa, lakini ni vizuri kufunga ndoa ukiwa umeshazaa, uje kuibariki,(kwa wakristo) na sio kufunga ndoa na kitumbo mbele,
    haifai jamani kha!
    shameee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    JOYS

    ReplyDelete
  6. Yani hii tabia imezidi siku hizi..mi sipendi kweli yani.Basi tu!

    ReplyDelete
  7. lo!
    hata wafungishaji wa ndoa wanakosea, baadhi ya madhehebu, ss kwanisani kwetu ukijulikana tu unamimba
    ndoa haifungwi, na unatengwa, inamaana umeshindwa kuvumilia wewe, lo! uroho gani huo???labda ufunge ndo huku unamimba isiyoonekana na ujidanganye wewe na Mungu umdanganye, ni tabia mbaya

    ReplyDelete
  8. Inaeleweka hahihitaji mjadala mrefu,Mimba sio kisingizio.

    ReplyDelete
  9. Mnasema kwa sababu hayajawakuta jamani mimi mwenyewe yalinikuta siwezi kusema chochote kile sikupanga kupata mimba from no were nikakosive kumwambia mpenzi wangu akasema yeye mwenyewe hakuna nini wala nini na usitoe tuwandae harusi, na urafiki wetu ulikuwa una miaka miwili na nusu, ilibidi nikubali lakini cha moto nilikipata kuandaa harusi ukiwa na mimba si mchezo na kama mimba inakusumbua uwende huku na huku hata choice ya kitu kizuri huna bora liishe, lakini maisha yangerudiwa nisingejaribu kufunga ndoa na mimba kwani siku ya harusi mchungaji alipogundua ni mjamzito kilitokea kitu cha ajabu niliingizwa kanisani bila kufunikwa shela usoni mchungaji alisema haina haja ya kufunikwa nimemaliza kila kitu niliingizwa shela iko kwa nyuma kama ndiyo natoka kufunga ndoa kumbe ndiyo naingia lakini mungu ni mwema nandunda na dear wangu ana miaka mitatu sasa, ila sina jibu katika hilo.
    mama dear

    ReplyDelete
  10. Hongera Violet kwa blogs yako nzuri ya kuelimishana na kusaidiana katika jamii... mimi kwa upande wangu nasema tabia ya kuolewa na mimba siyo nzuri kwani hata biblia imekataza, kidini inamaamisha kuwa mmezini nje ya ndoa na ndio maana ukapata mimba ambayo kwa wakristo wazuri wanaosoma bliblia kwenye amri kumi za mungu imeandikwa usizini,,., lakini kwa kuwa wanawake siku hizi tunaona kuwa ukiwa na boyfriend lazima uzini naye kwanza ndio utaona kuwa anakupenda, na atakushawishi mpaka ukubali kufanya hivyo, ukikataa anakwambia umpendi na anatafuta demu mwingine, wakati wewe unakuta unampenda kwa dhati, na hiyo ndio imetupeleka wasichana wengi kuanza mambo hayo kabla ya wakati wake, mpaka mtu aje aambiwe kuwa wewe sasa ni mchumba ndio unakuta anajiaminisha kabisa anajiachia anaona kuwa yeye sasa ni kama mke lakini sivyo ndugu zangu naona kwenda na fashion ndio kinachotuharibu kabisa... na wakati mwingine unakuta mvulana anamwambia mchumba wake usipobeba mimba kwanza mi sikuowi na unakuta mwanamke anakubali badala ya kushaurina ili waende sambamba na maadili ya dini.
    Mi nashauri kwa ndugu zangu wote uwe mwanamke au mwanamme kufunga ndoa na mimba ni dhambi, hairuusiwi na tusifanya kama ndio fashion kama mtu anakupenda kweli utafunga ndoa bila mimba... ina maana huyo mtu akikulazimisha ubebe mimba kwanza hakupendi je ikatokea mkafunga ndoa bila mimba... na ikakutwa kuwa kwa bahati mbaya mtoto wa watu hukufanikiwa kupata mtoto si atakuacha huyo jamani?... maaana nia yake ilikuwa ajaribu kwanza kama utapata mimba ndio akuoe...na nyie mnaosema mnaconceive bila kujijua muache hiyo tabia mana kula kila sababu ya kukufanya usiconceive kabla ya wakati.

    ReplyDelete